Je nimpe talaka au nifanyaje

Asee habari yako ni ndefu na imejaa kiswahili cha kizaramo asafishi,anisikii ani ani,ulichagua mwenyewe au au walikutumia kwenye mabasi ya AKIDA ukampokea,endelea kunuka swala la kumuacha liko akilini mwako mbona game hulielezei na unashiriki vipi wakati mnakulana akiwa hajaoga
 
Mwenzangu anisikii kabisa, amekuwa mbishi umwambii kitu akifanye; anajibizana nami kama watoto,mwana mke wangu ni mchafu sana ina bidi wakati nikichoka nikubali kuwa mchafu kidogo, asafishi nyumba, jiko ni chafu, bafu chafu, ukiweka glass chini sebuleni inaweza kukaa wiki anaipita anaipiga teke na haikoti, si glasi tu kitu chochote, ukinunua vyakula na groceries ukaleta nyumbani anachofanya ni kuyachukua vitu na kutupa ndani ya makabati ukimuhuliza alipoweka kitu ajui. Na akisha weka kitu hakumbuki nini kaweka wapi hata mwaka unapita kitu hakijaguswa mpaka nifanye campeni ya kukagua kila kitu na kuweka nje ili nijue vilipo.
Fridge ni chafu, haipangwi vitu vinatupwa tu ndani yake bila hata kuoshwa vikitoka kwenye store. Chakula akipika nimemwambia siku nyingi inabidi kuya toa kwenye sufuria na kuweka kwenye makopo madogo ndo yawekwe kwenye fridge. Yeye akisha kula ana acha sufuria hapo hapo juu ya jiko bila hata kufunika na vijiko alivyotumia kuchotea chakula anaweka juu ya jiko hapo alafu anakwenda kulala, uki msema anachukua sufuria anaingiza ndani ya fridge na afuniki ingawa zipo wraping-makaratasi ya kufunika vyakula. Vyombo vina lala hapo kwenye sink mpaka kesho yake asubuhi.

Afui shuka mpaka ichafuke kweli au umwambie na akifua nguo au mashuka apigi pasi analundika hapo chini au popote pale alafu ana chambua mmoja baada ya nyingine na kupiga pasi akitaka kwenda sehemu alafu baada muda anarudi kuyafua tena unakuta ngua nyingine wala hazija valiwa zinafuliwa tena; Nimejaribu kuongea na kufundisha lakini asikii, aelewi au hajifunzi
Akilala nimeisha mwambia afunike nywele kwani anaweka dawa lakini afanyi hivyo mashuka na mito yote ina utomvu wa curls, watoto wanashindwa kupumua kwa sababu ya hewa nzito. Nimemnunulia cover ya nywele ya kulala lakini hajui alipo ziweka na ata kama ipo mpaka nimwambie kwa force ndo aweke.

Nnguo zake zina toa harufu mbaya nimemwambia kwa muda mrefu lakini asikii wala hafanyi jitihada kubadilika. Kupika ndo hajui kabisa anajua kupika chakula cha aina mmoja chakula cha mchuzi. Kupika Kuku wa mchuzi na nyama ya mchuzi hajui kupika hata andazi akipika vhapati utavunja meno ngumu kama jiwe. Nimeangalia kwenye internet siku mmoja nikiamka asubuhi nikapika kama mandazi 60 na yakawa mazuri kama ya mama nitilie na watoto wakayapenda lakini ukimwambia apike tena ingwa nimeandika kila kitu hawezi.Anayo internet 24 hours nyumbani
Nikitoka nje wala anipokei wala ani tengei chakula mezani labda kama wote tuko nyumbani ndo anapika alafu anaweka chakula mezani.
Wakati watu wakila yeye akai na watu mezani anakula peke yake, asubuhi namwacha analala wakati nakwenda kazini wala anipikii chai, napika mwenywe. Nawa ogesh watoto kabla ya kuwapeleka shule na kuwa tengea chai. Yeye akiamka anakwenda kwenye nywele za motto ndo anacho jua. Hamsaidii motto na assignment mpaka motto analia nikiingia kuwa mama hanisaidii. Hata kuwasomea watotoneno nalo ni shida nawakuta watoto wana nisubiri niwaombee ili walale yeye wakati huo analala.

Nimemwambia mke wangu awe incharge wa nyumba ajue matumizi yetu ya kila siku lakini hadi leo hajafanya na hajui tunatumia kiasi ghani au tunalipa bill kiasi gain kwa mwezi hajui
Nina ka imani kidogo kabla ya kwenda kulala nataka tisome biblia na kuomba lakini yeye kila siku akisha kula yuko kwenye TV mkitaka kuomba yeye anakwenda kulala.
Sijawahi kumwona mke wangu ameshika kitabu anasoma kitu ambacho ni kibaya sana
Siku nimetoka kazini ghafla nilisahau kitu nyumbani nikarudi nikakuta amekaa chumbani n a chai niliyo mwandalia Baba yangu anaye tutembelea hajamtolea sukari na kikombe anywe hivyo ikabidi nimpe Baba yangu chai. Kusudi baba asione tunashirikiana kumfanyia ubaya nikamuuliza kwa sauti kabisa kwanini hujampa baba chai?

Najua Biblia imeandika uache mke kwa Uasherati tu je hii si zaidi ya uasherati?

Mke wangu afanyi kazi ni mimi ndo naleta kila kitu sasa ni miaka mitano ila naelekea ukingoni. Nilikuwa msafi lakini naelekea kuwa mchafu. Mtoto akitoka shule amwambii akaoghe anamwambia utaoga kesho, dawa akipewa au ya watoto anakunywa mara mmoja tu alafu anatupa hapa mezani – Nifanyaje –Kukwepauchafu nemetoa nguo zangu zote kwenye makabati na kuyafungia kwenye sanduku na nimebadilisha namba ili niwe na nguo hata mmoja ya kutokea, kwani yeye hana nguo ya kutoka zote ni za sokoni na za kutokea


Inategemea ulikutana naye wapi hadi mkaamua kuoana tukijua hilo ndiyo tunaweza kuanzia hapo hapo kukupa ushauri.
 
vitu vingine unaweza usiamini kabisa, hivi mwanamke utakuwaje wa hivi kweli?
 
pole majuto. wapo wanawake kama huyu wa kwako. kaka yangu alikua na kituko kama hiki, lakini alishatwangwa talaka siku nyingi. mwanamke kama huyu wa nini ndani ya nyumba sana sana atakuharibia watoto. huyu wa kaka yangu aliamua kubadilika baadae kwa sababu zake mwenyewe. jitihada ya kumrudisha kwenye tabia yake nzuri ya mwanzo zilishindikana, ikabidi apigwe talaka, ya nini kujipa ma presha watu mmekutana ukubwani.
 
vitu vingine unaweza usiamini kabisa, hivi mwanamke utakuwaje wa hivi kweli?

unaweza kukuta na yeye ni memba hapa maana jamaa kasema ananetweki masaa 24 na akatoa mchango kwa mumewe kuwa he huyu mwanamke ni waajabu sana maana nafikiri hajitambui kama yuko hivyo huo ni ugonjwana. na pia wakinamama wanaowadekeza mabintiu zao wanachangia kuwaharibu maana utakuta libinti likubwa tu liko nyumbani kwao linasubiri kuolewa lakin hapo nyumbani linapikiwa na kufuliwa na mama yake au hausgirl, wengine mpaka kuliswa nimemwona mmoja eti wazazi wake alikuwa wanamlazimisha kula akiwa na miaka 20 anashindwa wanaenda kumchemzhia maziwa na kuanza kumbembeleza anywe baada ya hapo wanamlisha chakula hapo sio mgonjwa wala nini na hakuna kazi yoyote anayofanya hapo nyumbani nguo zake zinafuliwa yeye atoke kuwatembelea marafiki zake na kurudi nyumbani sasa si ndio taipu hiyo
 
Aisee !!!hv unajifunza kutunga Hadithi za Filamu au?maana naona kama hiyo ni story tu!!!!!
 
na wakwangu hivyo hivyo na akrobatiki hanipi vilevile (ila heri mimi siajasema)
Basi kumbe kuna wanaume mna shida jamani, poleni! kweli kuta za nyumba zinaficha mengi lol. inavoelekea uko ulaya, mrudishe bongo asote mwaka hivi akijifunza uanamke na akiwa tayari arudi.
 
........This is terrible wife!! Huyu mdada anahitaji kufundwa kwa mara ya pili.

Vile vile mtu wa kulaumiwa hapa ni mama yake kama alilelewa na mama yake mzazi. Uchafu aliokuwa nao ni kwamba kapitiliza. I'm so sorry for u, I know u love your wife ndio maana hadi leo mpo pamoja. Muhimu hapo tafuta wamama watu wazima wakae naye chini na kumueleza A to Z kuhusu mwanamke na usafi. Vp usafi wa mwili wake upoje?

Pretty; huyu dada hajawahi kufundwa hata kidogo... inabidi aanze upya...

Ndugu Majuto, nakushauri kama wazazi wa huyu binti wapo, basi itisha kikao, mrudishe na uwajulishe sababu ulizoeleza hapo juu zote, then uwaambie wamfundishe na arudi kwako pale tu atakapokuwa amefuzu and yuko tayari kuhudumia familia yake.....

Kama hilo ni gumu, basi tafuta mfanyakazi. Itakupunguzia aibu
 
Majuto hii si story yako niliisikiliza Leo tena kwa kina Dina nadhani ilipostiwa kwenye Blog ya Dina Marious au wewe ndo mhusika? But ungeifupisha kidogo inatia uvivu kuisoma yote.

Pole
 
bwana majuto
ushauri wa ziondaughter na pretty ni mzuri, vile vile wengine wametoa ushauri mzuri kama kumshirikisha mama mchungaji au washauri wa ndoa wazuri kama Chriss Mauki
kwa upande wangu sahau kuhusu talaka. umeongea jambo ambalo kwangu ni zuri na linajenga ndoa nalo ni IMANI NA KUSOMA NENO LA MUNGU. inaonyesha una hofu ya Mungu, mtegemee yeye kwa sana na usichoke kusali na kuamini kuwa Mungu anaweza kukuvusha katika mtihani huo kama alivyowavusha wana wa Israel walipukuwa wanafuatiliwa na jeshi la Farao.
weka huasigeli mzuri akusaidie kazi ila sio kazi zote ( kazi ya bed rum hausgel asipewe pse)
 
Wanawake ni kiumbe cha ajabu,sometimes wanafanya mambo ya ajabu hata kama anajua ni makosa/si vizuri.Kama mwanaume hutokua makini na kukemea tabia hiyo itaendelea na siku utakapo mwambia utashangaa,anaweza kukuambia mbona siku zote nilikuwa nafanya hivyo hukuniambia.Kwakuwa tayari hali hiyo ilishajengenga,anza taratibu na kwa msimamo,usianze kwa ukali sana maana naye antakiwa kuelimishwa.NADHANI BADO HUJASHINDWA BALI HUKUWA NA MUDA MZURI KUONA UDHAIFU WAKE WAKATI ANAANZA,LAKINI SASA UNAO MUDA.TEKELEZA WAJIBU WAKO.
NAOMBA NIFAHAMISHE KAMA NDOA YENU IPO KWA MUJIBU WA DINI NA KAMA WOTE MPO DINI NA DHEHEBU MOJA KTK IMANI.
 
Majuto hii si story yako niliisikiliza Leo tena kwa kina Dina nadhani ilipostiwa kwenye Blog ya Dina Marious au wewe ndo mhusika? But ungeifupisha kidogo inatia uvivu kuisoma yote.

Pole
Samahani kuwachosha ila nilitaka niwape watu undani wa kitu chenyewe,sija soma habari hii mahala. Mzigo wangu nachekecha kutua mzigo au lah! haya ni ya kwangu tu
 
Jamani nakuhurumia sana majuto ..
1. Ulimtoa wapi?
2. Anafanya kazi?
3.mna watoto /mtoto?
Huyo anahitaji msaada hebu jaribu kumchukua hata ndugu yako wakae nae waanze kufundishana mambo ya usafi ,nini maana ya mme na kwa nini aliolewa ..
Lakini na wewe wakati wa uchumba kwani alikuwaje?
1. Alikuwa msafi na makini amekuja kubadilika sasa
navyochukia uchafu mie jamani naweza kuikimbia nyumba yako hata maji ya kunywa siombi ng'o
 
samahani kuwachosha ila nilitaka niwape watu undani wa kitu chenyewe,sija soma habari hii mahala. Mzigo wangu nachekecha kutua mzigo au lah! Haya ni ya kwangu tu

pole majuto mie nimeisoma yote naomba unijibu hayo maswali yangu kwenye ile post ..
 
pole majuto mie nimeisoma yote naomba unijibu hayo maswali yangu kwenye ile post ..
Mtoto yupo, kazi hafanyi kwa sasa ingawa ataanza Feb. Ilikuwa si rahisi kujua kama anayo uchafu kwani kuna watu kwenye nyumba, nani kasafisha hujui? Haya akija kwako kajiandaa, atajitahidi kila kitu aweke sawa, sasa yuko mwenyewe, lo! tatizo - usafi! Mie msafi sana
 
Uhitaji kupaniki ndugu yangu, hili ni tatizo dogo sana na wewe mwenyewe unaweza kulitatua. You have to make sure kuwa mkeo anapata challenges kutoka sehemu mbalimbali ndio aweze kufanya yale ambayo wewe unataka otherwise hatokuwa na mwamko na kutaka kumsukuma ndio unachemka zaidi kaka
 
Umesahau kutuambia kitu kimoja, huyu inawezekana hata pedi zilizotumika anazirundika bafuni hata wiki nzima....,Inawezekana hakufanyiwa Kitchen Party huyo,kama hili ni kweli basi jaribu kuwasiliana na ndugu zake hususani mashangazi ndio huwa wazuri sana kwa hili, waeleze huo mlolongo wa kero zako na uwaombe wakae nae chini wamfunde upya bibie na akikushinda hata baada ya lecture ya mashangazi basi vuta kitu ingine mzee mbona wako wengi tu hao..
 
Back
Top Bottom