Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
WENGI WANAOTAKA WAKE ZAO WASIFANYE KAZI WANAUPEO MDOGO WA KUFIKIRI ALAFU NI WABINAFSI
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Chizi sio lazima uokote Makopo, kuna Chizi Fresh ambao ndio wengi wapo kundi hili tena wengine wasomi. Alafu kuna ambao ni Chizi Maarifa hawa wengi ukiwaona kwa mbali unaweza kudhani wako timamu lakini ukiwatazama kwa ukaribu ni wendawazimu.
Unakuta kajamaa kametoka familia Maskini, kameoa kutoka Familia Maskini. Kanafanya kazi iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri lakini pato lake kwa mwezi hata Milioni moja halifiki.
Lakini ukikasikiliza mawazo yake kuhusu uchumi na mahusiano utabaki kuona kalivyo na upeo mdogo.
Yaani kisa umenunua mwanamke kwa bei ya jumla(kutoa mahari) labda shilingi milioni nne. Basi Mwanamke huyo ambaye sasa ataitwa mkeo unasema asifanye kazi kisa umemuoa.
Ukiulizwa kwa nini asifanye kazi? Huna hoja ya maana hata moja zaidi ya kutokujiamini, ubinafsi na ukandamizaji kama sio unyanyasaji.
Unamwambia mkeo asifanye kazi au asimiliki kipato kingi tena inafikia hatua kwa uzuzu wako unamhujumu mkeo na kumuwekea vikwazo ili asifanikiwe. Ati unaogopa atakunyanyasa ati atakuwa jeuri. Chizi weeeh!
Mkeo asifanye kazi, unapesa za kumhudumia mahitaji yake yote?
Alafu wengi wenye mtazamo kama huu unakuta Wake zao hata mafuta ya kupaka hawana, nguo wanazovaa mtumba, tena bora mtumba lakini ziwe nyingi. Lakini hata pesa ya kuwanunulia wake zao nguo walau kila mwezi nguo moja au mbili hawana. Mke kapauka, kazeeshwa. Yaani hatamaniki tena. Kila siku kumlisha mkeo Maharage kazi kujambajamba. Alafu unakuta jitu linasema linahudumia mke. Alafu halitaki mkewe afanye kazi. Ili angalau pesa ya kubadilisha chakula hapo nyumbani iwepo sio kila siku ugali na mchicha au maharage. Nyama na samaki mpaka sikukuu. Familia inapitisha Wiki hata maziwa hakuna. Alafu ulivyo chizi unaona sawa tuu. Alafu ukijaribu mtandaoni huku ooh! Mwanamke asifanye kazi utadhani umemudu mahitaji yake. Mwehu wewe!
Watoto wako ada zenyewe zinakusumbua, lishe yenyewe hawali. Utapiamlo na kifaduro kinawasumbua. Watoto mpaka imefikia hata uwezo wa kufikiri hawana Kwa sababu kila siku unawalisha chakula kingi cha wanga kama ugali, mihogo, maandazi na maujiuji ya nafaka. Ilhali kiafya watoto chini ya miaka 20 wanatakiwa kula protein nyingi kuliko kundi jingine la chakula ili miili yao ijengwe vyema. Vyakula vya protini ambavyo vinatakiwa viwe vingi katika mlo wenu hapo nyumbani ni Samaki, nyama, maharage, maziwa, mayai n.k.
Lakini kwa vile kipato chako ni duni huwezi kuhudumia hivyo. Alafu kwa vile tayari unakifaduro cha ubongo huoni kama unahitaji usaidizi na kwa ubinafsi wako unataka watoto wako nao wakose lishe kama wewe ulivyokosa. Ati mke asifanye kazi au asikusaidie majukumu. Kwa huduma gani unazotoa mwehu wewe!
Haya, mshahara wako wenyewe haukutoshi kutunza Wazazi wako.
Alafu hutaki mkeo asifanye kazi. Hivi unafikiri wazazi wake mwanamke watahudumiwa na kutunzwa na nani kama sio huyo mke wako. Mbuzi wewe.
Pesa yako hata milioni moja haifiki kwa mwezi. Unataka wadogo wa mkeo wahudumiwe na nani?
Unataka ile nyumba ya wazazi wa mkeo ifanyiwe ukarabati na nani kama sio mkeo.
Alafu haya machizi Fresh hapohapo unayasikia yakisema, usijenge Ukweni, mara Usitoe pesa Ukweni. Alafu hapohapo unayakuta yanazuia Wake zao wasifanye kazi. Hivi kama sio Ushetani na laana hizo ni kitu gani? Hivi kuna ubinafsi na ukatili wa kutisha zaidi ya huo?
Bado umfulishe na kumfanyisha makazi mengi bila kumpa lishe bora. Zaidi ya hapo umpige kisa ameona mambo sio mambo na umemgeuza msukule wake hapo.
Embu acheni Upumbavu wenu.
Ni mara elfu Mwanamke asioelewe au awe single Mother alee Watoto wake kitabutabu kuliko kuishi na mwanaume mwenye Ushetani wa namna hiyo.
Mwanaume elewa kuwa kama wewe unavyopenda na kuhitaji kuhudumia Wazazi wako ndio hivyohivyo mkeo naye anataka wazazi wake wahudumiwe.
Na ndio maana Watibeli Hawatoi Mahari kwa sababu inaharufu ya manunuzi au biashara ya binadamu kwa visingizio vya kishetani.
Hutaki mkeo afanye kazi alafu ukiombwa pesa ya kuwasomesha wadogo zake unapiga yowe na kulalamika. Wewe mwehu nini.
Na mimi nawaambia Wanawake hasa Watibeli ni lazima wafanyekazi. Kufanya kazi ni amri ya kila kiumbe ili kiwe huru na kujitegemea chenyewe. Binadamu asiyefanya kazi ni mfu.
Mtu mwenye akili na Mwanamke kamili na mke mwema hujisikia aibu na fedheha kumtegemea mumewe kwa kila kitu.
Mimi nimemaliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam