SIRI: Mwanamke ambae hajui Mapishi (Kupika) hafai, na hapaswi hata kuolewa

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,563
10,547
UCHAMBUZI wa KUSTAWISHA JAMII.

Baada ya kufanya tafiti, upembuzi na ulinganifu nikaja na jibu kwamba MWANAMKE ambae hajui Mapishi/Mapochopocho/ kukaangiza basi huyo Mwanamke hakufai kimbia.

Ndio maana sisi Watanzania mtu akioa tunasema "Jamaa kavuta JIKO" eeh.

Hiyo kauli ina maana kubwa sana na sio Jiko tu la Kupika, Jiko la Maamuzi, Jiko la kuandaa mtazamo.. Jiko la kuandaa watoto wazuri na wenye maadili, pia Jiko la kumpikia Chakula kitamu(Cha Usiku) MUME wake..

Naomba nideal na JIKO la CHAKULA kama CHAKULA

1 Wengi wao si WASAFI

Mwanamke ambae hajui kupika ukienda mahali alipopika utakuta Maganda ya vitunguu, Manyanya.. yaan vyombo na maji machafu yametapakaa hapo.

Na kutokana hawajui kanuni ya MAPISHI, kukuta Nywele ktk chakula ni jambo la kawaida.

2 Wengi wao Wanasababisha Maisha ya Mwanaume kuwa Mafupi
Mwanamke ambae hajui kupika, hatoweza kukupikia Chakula cha Afya, NEVER. Atajaza Chumvi, Mafuta ktk Chakula mpk upate shinikizo la Damu, yaan mpaka uumwe kisukari. Ila yule anaejua Mapishi anajua makadirio ya kila kiungo na kwa kila kiwango. Tuwe serious na Afya zetu HAKUNA kuoa Mpuuzi ambae hajui Kupika.

2.1 NGUVU za Kiume:

Mwanamke ambae hajui kulitendea haki JIKO la Chakula, ni rahisi sana kukuharibu hizo nguvu zako za kiume ambazo zinaishia ishia.. kwanini?

Hajui chakula tiba kinachoongeza madini ya Manii bora.

Kutokana na Mafuta na Masukari anakumaliza kabisa.

Unapata Mtihani wa kwenda kununua Chakula cha haraka mara kwa mara (Fast foods/Junk Foods). Limwanamke la hivi ni adui na sio mpenzi, ndio maana watu wanajiuliza kwanini Wanaume wanakufa mapema? Kuna sababu kama hizi.

3 Huongeza Gharama za Maisha bila ya wewe kujua:

Mfano mdogo tu, mtu mafuta ya kutumia wiki 1 ila atatumia siku mbili (2). Em piga mahesabu hapo, kwa sukari, etc..

Kutokana hajui kupika, kuunguza viungo vya Mapishi na kuanza UPYA kupika ni jambo la kawaida, anaongeza gharama zisizo za msingi. Na mbaya zaidi kama hajui na hataki kujifunza hakuna MABADIRIKO wapo hivyo hivyo.

Wewe au Mtu kama Mimi ambae sipendi kula Chakula kibaya, siwezi kuvumilia mapishi mabovu nitajaribu kwenda kununua chakula ktk mahoteli au migahawa huko kitu ambacho unatumia fedha ya ziada wakati uliacha hela nzuri na mahitaji yote nyumbani.

HINT: Kutokana na hayajui kupika, huwa hiyo kazi wanaiona ni nzito mnoo hivyo usishangae ukarudi kutoka kazini ukakuta kakukaangia Mayai (yenye mafuta na chumvi nyingi) na mkate hapo pamoja na Chai ndio ule ulale.

4 Anakuaibisha kwenye Familia:
Kuna matukio mbali mbali ya kifamilia yanayotaka Wanawake kujumuika na kupika pamoja, BRO kama umeoa Mpumbavu ambae hajui kupika hutoona anachangamana na Wenzie, yupo busy na simu au mambo ya kijinga jinga, hii inakupa sura mbaya wewe kama Mwanaume wake uliyemuoa.

Kuna Wageni pia kutembelea nyumbani: mtu hajui kupika wageni wanalishwa chakula kibichi unafkiri watakuchukuliaje?.

NIMALIZIE KAMA IFUATAVYO
1- Mwanamke hana pa kujitetea et kwanini hajui kupika hana hoja ya kujitetea yenye mashiko.

2- Mwanaume anavutiwa na Jambo dogo sana: Mwanamke mara nyingi hana cha ku offer kikubwa tofauti na Mwanaume ipo wazi, basi jitahidi hata ktk Mapishi umkonge moyo Mumeo/Mwanaume wako, atleast akiwa zake katulia anajivunia nina Mwanamke mzuri anaejua kunipatia ktk Mapishi.

Mie ubovu wangu ni CHAKULA.. yaani nikila chakula kizuri umenimaliza siangalii hayo mengine, kuna Dada mmoja yupo Instagram huko mara nyingi anapost video za mapishi, yule Dada kwa kweli nilikuwa namtamani sana.. yaan unapata hisia nae hata kama Sura hujaiona.

Sasa Wanawake wajinga wajinga, wao wanafkiri kujipamba mawanja na makeup nyingi ndio kumvutia Mwanaume hapana.

MWANAUME anaejua kupika ni HATARI kwa MWANAMKE ambae hajui kupika:

Wifi yenu huwa ananiogopa sana nikisema nataka nipike leo, huwa anajishtukia na atafanya kila linalowezekana nisipike maana anajua nikitoa kitu kinatoka haswa.

Bahati nzuri anajua kupika nje ya hapo siku nyingi ningeshafunga Mkataba.

Naomba kuwasilisha MADA hii.
 
Bonus Tip: Mwanamke ambae hajui kulitumia JIKO la CHAKULA huyo hamna kitu katika JIKO la KITANDA.

Ubunifu huwa hawana: em fikiria Mwanamke anaejua Mapishi ya kitasha na michanganyo kama ya MOCKTAILS, COCKTAILS, MILKSHAKES etc..

Huyu hata katika Kitanda anajua Michanganyo na Mambo mazito mazito ambayo yatanogesha JIKO lake.

Nimewaibia Siri tu.
 
Hii siri tupo nayo!

Tuongeze siri nyingine mkuu
Siri #2:

MWANAMKE naejua kupika ni Mvumilivu sana.

Em fikiria mtu anapika CHAKULA Kizuri anatumia masaa 3 kupika au zaidi na ndani mpo wawili tu. Unafkiri Mwanamke wa hivi utamsumbua na vitu vidg vidg? Wengi hawapendi Kupika na hawajui kupika kwasababu HAWANA Uvumilivu.

Siri #3: WENGI WAVIVU.
 
Siri #2:

MWANAMKE naejua kupika ni Mvumilivu sana.

Em fikiria mtu anapika CHAKULA Kizuri anatumia masaa 3 kupika au zaidi na ndani mpo wawili tu. Unafkiri Mwanamke wa hivi utamsumbua na vitu vidg vidg? Wengi hawapendi Kupika na hawajui kupika kwasababu HAWANA Uvumilivu.

Siri #3: WENGI WAVIVU.
Sidhani ni wavivu!

Ninavyoona, mabinti na vijana wa "kisasa" kuna jambo wamedaganywa kuhusu mahusiano!

Ndio maana hata furaha yao haina raha
 

Attachments

  • Screenshot_2023-08-17-16-20-00-45.jpg
    Screenshot_2023-08-17-16-20-00-45.jpg
    45.7 KB · Views: 5
Hahaha kwa hiyo akaipika nyumba hahahaha
Ila mwanamke asiyejua kupika ni bure kabisa ni ngumu sana kuamini yuko hodari kwenye jambo lolote …
Mwanamke asiyejua kupika huhesabika kama roboti tuuu hii kitu inamuondolea mwanamke sifa zote !

Mwanamke kujua kupika ni jambo muhimu na muhimu sana sana…
 
Back
Top Bottom