Ushauri:Baada ya Makonda kumaliza Back to Back ya kuwashambulia Watumishi aanze Back to Back ya kuelezea Mema waliyoyafanya pia.

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
550
786
Nchimbi ni akili kubwa sana aliposema Watumishi wa Umma siyo maadui wa chama tafsiri yake ametumia hekima ya wazee wanaosema Mkeo akikosea anasemwa chumbani siyo hadharani,Kuku wako Manati ya nini wakati jioni anaingia Bandani.

Anachokifanya Makonda kwasababu ni populist kinawezekana kikampa umaarufu ila kina gharama pia kwa chama cha Mapinduzi kwasababu kinachonganisha Chama chake na Watumishi wa Umma ambalo ni kundi lenye wapiga kura linalohitajika kwao.

Ninafahamu zipo Sheria,Kanuni na Miongozo ya Watumishi wa Umma ikiwemo ya kuwawajibisha hawa Watumishi wanapokosea najiuliza kwanini havitumiki kinaanzishwa kitu kingine cha kudhalilishana kwenye majukwaa ya kisiasa tena mbele ya vyombo vya habari Dunia nzima inaona.

Makonda anachotaka kuwaaminisha watu ni kwamba Matatizo yote ya Wananchi yamesababishwa na Watumishi wa Umma pekee Wanasiasa hawahusiki kabisa,je hii ni kweli?

Ninafahamu hata yeye alipokuwa Kinondoni baadae Jiji zima la Dar es salaam hakuweza kumaliza Kero sasa kwanini leo aone wenzake wote hawana wanachokifanya wala wanachokijua ndiyo maana kero zipo,kwanini asikiri mfumo una shida itafutwe namna bora ya kutatua kero hizo hata kama yeye hayupo.

Inavyoonekana Watumishi wa Umma wakifanya Mema ni ya Wanasiasa wakifanya Mabaya ni ya kwao,sasa kwanini asishauriwe kutenda haki akapiga Back to Back nyingine ya kupongeza Mema yaliyofanyika?

Ni Mtazamo tu,mawazo tu masela msijenge chuki,Naruhusu POVU.
 
Acha mpigwe spana mnaleta undezi sana kwenye ofisi za uma! Ccm iliomba kura kwa kuwaahidi wananchi kuwafanyia mema.

Ccm wameajiri watumishi ili kufanya implementation ya yale waliyoyaahidi halafu watumishi wanarelax! acha Makonda awanyoe hadi akili zikae sawa.
 
Back
Top Bottom