Je ni haki kwa Mali ya Wananchi kutumika katika mikopo ya Biashara Binafsi

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Nimekutana na hii habari katika Michuzi Blog na kujikuta nikijiuliza maswali kadhaa:
1. Ni haki kwa mfanyabiashara binafsi kutumia Mali ya Umma kukopa benki?

2. Kama hii kampuni ikifilisika, hiyo 'mali ya umma' si itabadilika kuwa mali ya benki?

3. Na ikiwa kama mali ya benki, si ina maana benki itaweza kuiuza popote kwa ajili ya kulipia huo mkopo?

4. Kama mtiririko wote huu ukitokea, kwa kusudi la kurudisha hii mali kuwa ya umma, si itabidi serikali inunue hiyo mali upya kutoka kwa benki?...kwa maneno mengine, si itabidi serikali i-bailout hii kampuni binafsi?

5. Je hii ni haki kwa mlipa kodi wa Tanzania?

michuzi blog said:
HOJA ya kuipa hati Usu ya miaka 33 kampuni ya Discovery Tanzania Heritage (DTH),kumiliki uwanja wa Uhuru Park mjini Moshi, leo ulizua tafrani baada ya madiwani CHADEMA kufanya vurugu katika kikao cha baraza la madiwani kwa kuwapiga Meya na mkurugenzi wa manispaa hiyo kwa kutumia majoho na kofia zao.

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilitoa hati ya eneo la Uhuru Park kwa kampuni hiyo ili iitumie hati hiyo, kukopa Shilingi Bilioni 1.5 benki kwa ajili ya kuendeleza eneo hilo.

Huku wakitoka nje ya kikao cha baraza hilo,Madiwani hao sita wakiongozwa na diwani wa kata ya Mji Mpya, Bw. Abuu Shayo alikuwa akirusha joho, kofia na koti lake la suti katika meza kuu ya viongozi huku wakisema wamechoshwa na vitendo vya kuburuzwa.

Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa kwa dharura ili kutengua uamuzi wa awali wa baraza hilo kumpa nusu hati mwekezaji kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam,kilitengua rasmi uamuzi wake wa awali wa Machi 31 mwaka huu.

Tafrani katika kikao hicho na kuibua malumbano na baadaye madiwani hao kutoka nje ilitokana na kitendo cha diwani wa kata ya Rau kusoma agenda nyingine badala ya mwenendelezo wa agenda kuu iliyotolewa na diwani wa Kaloleni, Michael Mwita ambaye aliomba kubatilishwa kwa uamuzi wa awali.

Wakati akisoma hoja iliyohusu ujenzi wa shule za msingi katika baadhi ya kata,madiwani hao akiwemo wa kata ya Pasua,Japhary Michael alianza kupinga kitendo hicho kwa madai kuwa agenda ilikuwa ni moja ya kubatilisha uamuzi huo na si vinginevyo na hata hivyo kanuni hairuhusu.

Kauli hiyo iliunga mkono na madiwani wa Kiborloni Vicent Rimoy, viti maalum Hawa Mushi na mbunge wa viti maalum Lucy Owenya ambao walisema hawakubaliani na baraza hilo kuleta hoja juu ya hoja.

Kutokana na kitendo cha diwani Lyimo kuendelea kusoma taarifa hizo,madiwani Shayo na Michael walisimama na kutaka meya wa manispaa hiyo kuwapa nafasi ya kutoa taarifa lakini walipoona hawasikilizwi waliamua kutoka nje ya kikao.

“Mheshimiwa Meya nini mnatufanyia hapa……agenda ilikuwa ni moja ya Uhuru Park, hili suala la ujenzi wa madaraja na madarasa linatoka wapi,
Aliongeza”Umesikia yaliyotokea nchini Ukraine!! Acha kusoma hiyo taarifa yako nenda kaisomee katika vikao vya CCM, hamuwezi kutuchezea hapa, hii hoja si mliipitisha ninyi wenyewe, leo yamewafika mnataka kutunyima nafasi ya kuijadili”.

Kutokana na hali hiyo Meya Kaaya aliagiza madiwani Shayo na Michael kutolewa na askari nje ya ukumbi na askari wa manispaa,ambapo walikuja askari Dismas Raphael na Mwasiti Shabani ambao kwa maelekezo ya mwanasheria,Kisa Lyimo waliwatoa nje ya ukumbi madiwani hao huku wenzao wakiwafuata.

Wakati wakitoka nje ya ukumbi,diwani Shayo alivua joho lake na kumtupia meya Kaaya huku akivua kofia yake na kumtupia mkurugenzi Kinabo kwa madai kuwa wanayumbisha na madiwani wa CCM hivyo kushindwa kufuata kanuni na sheria zilizopo.

Kufuatia vitendo hivyo,Meya Kaaya alitangaza madiwani hao kufikishwa katika kamati za maadili huku diwani Shayo akisimamishwa kutohudhuria vikao vitatu vya baraza hilo.

Mapema mwezi Machi kampuni ya DTH iliyokuwa na mkataba wa mika 10 iliomba kupatiwa hati Usu ya kumiliki eneo hilo ili waweze kuomba mkopo huo wa Bilioni 1.5 ili kuendeleza bustani hiyo.

Baadaye wadau mbalimbali wakiwemo wananchi walipinga uamuzi wa madiwani hao huku wengine wakitishia kufanya maandamano ili kupinga hatua hiyo .
mwisho.

source:http://issamichuzi.blogspot.com/2010/04/ya-ukrane-nusura-yatokee-kwenye-baraza.html#comments
 
Tatizo kubwa ni kuwa hao tunaowaita viongozi wako so shortsighted kiasi kuwa madhara ya kitendo kama hiki hawakielewi. Wao wanadhani kwa vile wamechaguliwa basi wao wanajua kila kitu. Dawa ni kuwapeleka mahakamani na kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao hawaoni ndani. hizi njaa zitatuua. Au zimeshatuua, tumebaki wafu tunaotembea?

Amandla......
 
Mkuu hata mie jana usiku niliiona na ikanishangaza sana. Nawashukuru sana walioikomalia na kwa waandishi kuiweka ndani ya vyombo vya habari. Viongozi wahusika na hasa Wabunge inabidi waingilie kati. Pia Mkuu wa Mkoa (ingawa huyu na mkuu wa Wilaya unaweza kuwaelewa kwani wamewekwa na mtu ambaye ..........) ila wangelikuwa makini, wangelifutilia mbali hili wazo. Na kibaya zaidi eti miaka 33, heee!?? Mambo mengine yanatisha. Kesho watakuja kudai MKATABA hatuwezi kuuvunja maana TUTAPATA HASARA.

Hongera kwa madiwani walioshupalia hili swala.
 
Huu ni wizi wa mchana kweupe kwani ni haohao CCM wanaendeleza ufisadi wa kila siku na huenda kwakuwa jimbo la Moshi limeshikwa na mbunge wa CHADEMA Mh. Philemn Ndesamburo basi ujue hapo kuna dalili za kuvuna kitu ili mapesa hayo yafanye kampeni chafu. Sio bure kupindisha sheria kwa manufaa ya mtu mmoja. Nasema hapo kuna harufu ya ufisadi ambayo haiwezi kwisha bila ya kuiondoa CCM na nawaomba wananchi wa Moshi mjini mkaze buti mhakikishe CCM haipati kitu na badala yake Halmashauri nzima ichukuliwe na CHADEMA ili kuondoa uozo huo.
 
Lakini Ndesamburo si ni mjumbe wa baraza la madiwani pia? Alikuwa wapi wakati wanafikia uamuzi kama huo?

Au tatizo ni lile lile la wabunge kudharua vikao vya madiwani na matokeo yake madiwani wanachukua maamuzi ya kijinga shauri ya uwezo mdogo.
 
Tatizo hakuna mwekezaji wa kweli hapo, hivi itakuwaje kama huyo jamaa akikopa hizo pesa bank na kisha kukimbia nazo, hiyo plot si itakuwa mali ya bank na itapigwa mnada na kuwa mali ya mtu binafsi
 
Tatizo hakuna mwekezaji wa kweli hapo, hivi itakuwaje kama huyo jamaa akikopa hizo pesa bank na kisha kukimbia nazo, hiyo plot si itakuwa mali ya bank na itapigwa mnada na kuwa mali ya mtu binafsi

Si ndo hapo! Je wananchi wanapewa uhakika(guarantee) gani kuwa watarudishiwa hii ardhi/plot?
 
Tatizo kubwa ni kuwa hao tunaowaita viongozi wako so shortsighted kiasi kuwa madhara ya kitendo kama hiki hawakielewi. Wao wanadhani kwa vile wamechaguliwa basi wao wanajua kila kitu. Dawa ni kuwapeleka mahakamani na kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao hawaoni ndani. hizi njaa zitatuua. Au zimeshatuua, tumebaki wafu tunaotembea?

Amandla......

Tuwepeleke mahakamani kwa sheria ipi?
 
Back
Top Bottom