Je, naweza kupata Laptop nzuri kwa budget ya laki nane?

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Heshima kwenu watalaamu wa jukwaa hili,

Nina Budget ya 800K ninahitaji laptop. Majukumu maalum ni kama Kutumia Softwares kama AUTOCAD, CIVIL 3D, STAAD PRO, MATLAB na program baadhi za Engineering ambazo sijazitaja.

Nahitaji laptop bora kwa hio gharama kikubwa iweze kurun hizo programs smoothly.

Pia kukiwa na machine bora ila bei imezidi slightly unaweza ku suggest.

Ningefurahi zaidi kupata na specifications na aina ya mashine ili niiweke katika shortlist.

Cc: Chief-Mkwawa Behaviourist Extrovert
 
Dell Latitude 5491 (hii ni around 700k to 800k)
Thinkpad T470 (hii ni around 800k)
Thinkpad T460 (hii ni around 700k)
HP ProBook 450 G5 (hii inaendaga mpk 1M)
HP ProBook 840 G3 (hii ni around 900k)

Hizi ni baadhi ambazo nimeziona madukani hapa karibuni. Ila kwa program za 3D unaweza pata tafuta hata laptop ya 5th or 6th gen yenye dedicated graphics za Nvidia or AMD.

Mm kuna jamaa yangu anatumia hzo software kwenye Thinkpad T440p yenye Nvidia graphics na anasema kwake iko vizuri tu ila hii ni PC kubwa kidogo sio hzo slim na alichukua kwa 600k.

Pia hzo nilizotaja hapo ni bei za refurbished nzuri sio bei za mpya na uhakikishe ni ya 8GB RAM or 16GB sio chini ya hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dell Latitude 5491 (hii ni around 700k to 800k)
Thinkpad T470 (hii ni around 800k)
Thinkpad T460 (hii ni around 700k)...
Barikiwa sana Mkuu! Je ni used/refurb au mpya
 
Heshima kwenu watalaamu wa jukwaa hili.

Nina Budget ya 800K ninahitaji laptop..
Majukumu maalum ni kama Kutumia Softwares kama AUTOCAD, CIVIL 3D, STAAD PRO, MATLAB na program baadhi za Engineering ambazo sijazitaja.

Nahitaji laptop bora kwa hio gharama kikubwa iweze kurun hizo programs smoothly.

Pia kukiwa na machine bora ila bei imezidi slightly unaweza ku suggest.

Ningefurahi zaidi kupata na specifications na aina ya mashine ili niiweke katika shortlist.

Cc: Chief-Mkwawa Behaviourist Extrovert
Kama unaweza ongeza kidogo 900k mpaka 950k go with i3 10th gen unapata mpya.

Hizi Cad softwares zinataka core 1 yenye nguvu badala ya core nyingi hivyo it doesn't matter kama ni dual core ama core 8.

Kupata dedicated Gpu ni bonus japo kwa budget yako labda used,

Display ya 1080p Pia wameieka kama recommendation, unaweza tumia Pia monitor ya nje, Sema ni vyema display ya laptop ikawa na hii resolution.

Kwa used gen ya 8 unapata hii budget na low end nvidia kama 930mx ama 940mx hivi. Naziona i5 8th gen kwa hii bei zoom Tanzania.
 
Mkuu ni vitu gani huwa vinafanya core kuwa na nguvu,yaani nitajuaje kuwa core hii ina nguvu na core ile haina nguvu?Nilikuwa sijua kuwa unaweza kuwa na core nyingi ambazo hazina nguvu!
 
Core ni kma procoessor iliyopo ndani ya CPU. Hizi core ndio zinafanya hzo instructions zinazohitajika kurun program flan. Nguvu ya core inakuwa determined kwa kupima Instructions per cycle (IPC), hii ni idadi ya maelekezo core yako inaweza fanya kwa mzunguko mmoja wa CPU (mzunguko mmoja wa CPU clock speed). IPC ndio muhim sana, core mbili tofaut kutoka processor mbili tofaut zinaweza kuwa na clock speed sawa (mf 1GHz) ila moja ikawa na 2000IPC na nyingine ikawa na 1000IPC ile ya 2000 IPC ndio yenye nguvu. Lakini kumbuka kuwa clock speed bado ni muhimu, kma CPU zote ni za class moja na generation sawa ile yenye clock speed kubwa ndio itakuwa na nguvu zaidi.

Sasa je ni kitu gani kinachangia core/processor kuwa na IPC kubwa kuliko nyingine?

Cha kwanza ni number ya transistors, kila processor ina transistors ndani yake ambazo ndio zinarun hzo instructions. Core moja inaweza kuwa na transistors nyingi kuliko nyingine. Yenye transistor nyingi itakua na IPC kubwa.

Pili ni size ya core hyo. Core kubwa inamaanisha kuwa inaweza beba transistors na nodes nyingi zaidi. Ndio maana zile Xeon processors za kwenye servers zinakuwa na core zenye nguvu sana

Kingine pia ni kwamba fabrication method (njia inayotumika kutengeneza processor) inachangia uwepo wa transistors na nodes nyingi. Kma ukicheki kwenye processor specification utakuta hchi kitu kimenadikwa: 10nm or 7nm or 5nm. Hichi ni kipimo cha udogo wa components (transistors and nodes) zilizopoa kwenye processor. Uwepo wa components ndogo inawezesha kuweka transistors and nodes nyingi kwenye processor yako na kupandisha IPC kwa kila core.

Pia processor zenye clock speed ndogo zinaweza kuwa na IPC kubwa sababu ya joto linalotengezwa. Processor zenye clock speed kubwa zinatengeza joto jingi na hii inalimit ufanyaji kazi wa transistors hvyo kuwa na IPC ndogo. Ila ukiwa na clock speed ndogo unaweza pandisha IPC yako sababu joto sio jingi sana. Ndio maana unakuta 10th gen i3 yenye clock speed ya 1.4ghz inaikalisha 3rd gen i7 yenye clock speed ya 2.7ghz kwenye single core performance.

Ukitaka details zaidi soma hizi sehemu mbil:

1.

2. Instructions per cycle - Wikipedia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni vitu gani huwa vinafanya core kuwa na nguvu,yaani nitajuaje kuwa core hii ina nguvu na core ile haina nguvu?Nilikuwa sijua kuwa unaweza kuwa na core nyingi ambazo hazina nguvu!
Njia rahisi Ni kuangalia benchmarks, benchmark nyingi maarufu kama cinebench, geek bench, passmark etc zinatofautisha score za single thread benchmark na multithread.

Vitu vinavyo fanya core kuwa na nguvu kushinda nyengine ni
-clock speed, yenye GHz kubwa ina nguvu kushinda GHz ndogo (factor nyengine zikiwa sawa)
-cache memory, zile l2 na l3 cache zikiwa kubwa na zenye speed na nguvu ya cpu inaongezeka
-architecture iliotumika (hizi generation)
-IPC ambayo ni kiasi gani cha instruction cpu inaweza fanya kwenye kila cycle (hizo GHz)
-manufacturing process ambayo jinsi inavyokuwa ndogo Ndio jinsi wanavyo jazia transistor nyingi kwenye cpu.
 
Shukrani mkuu!
 
Shukrani mkuu,haya mambo ni too technique!
 
Kaka mambo ya cores pamoja na clock speed kwa sasa hivi nayapata vizuri lakini IPC bado.Je mpaka sasa hivi IPC kubwa kuliko zote kwa laptop ni ngapi na ndogo kupita zote ni ngapi ili niwe na average kichwani?
 
Natumia Hp pavillion ikiwa na Ram 4GB, Processor 2.4 , 1TB , Nvidia Geforce, core i5 nime install hzo program zote na zinarun fresh bila tatzo

Nunua Pc yenye properties kama hzo ila Ram na processor zikiwa kubwa uta enjoy pia zaid

Huu mwaka nafunga mwaka wa nne sasa prota, civil 3d, archicad, autocad hakuna kinachosumbua na games ndo penyew

Kaa humo mhandisi
 
Kaka mambo ya cores pamoja na clock speed kwa sasa hivi nayapata vizuri lakini IPC bado.Je mpaka sasa hivi IPC kubwa kuliko zote kwa laptop ni ngapi na ndogo kupita zote ni ngapi ili niwe na average kichwani?
ngumu kuiweka kwa exactly namba fulani na kila benchmark inatumia namba zake. na ipc haina cha laptop ama simu ama desktop,

mfano gen ya 9 ama 8 ama 10 etc ya intel ipc ni ile ile, kinachotofautisha nguvu ni ghz tu, kwa desktop zitakua na nguvu sababu ghz kubwa na laptop ghz ndogo itapitwa nguvu.

na ipc kubwa sasa hivi ni ya AMD kwenye zen3, processor za AMD zinazoanziwa na 5000,
 
Dedicated Gpu ni graphics card ambayo ipo separate na processor, mara nyingi inakuwa ya Amd Radeon ama Nvidia,

Wanabandika sticker kwa juu ikiwa laptop inazo hizo graphics.
Mkuu Hp probook G5 napata? Kwa 800K
 
Back
Top Bottom