Je, Maggid Mjengwa ndiye Mwanakijiji kama ilivyoelezwa na BBC?

Status
Not open for further replies.
hii niliipa BBC-Swahili jana wakati wakijadili mambo ya mauwaji ya Norway. Mtangazaji wa BBC alimtambulisha mmoja wa wachangiaji wa mjadala kama (namnukuu) "...Maggid Mjengwa, yeye hupenda kujiita Mwanajijiji...".

Mwenye kujua ukweli atujuze, au kama vipi mtu na aseme kama Mwanakijiji na Mzee Mwanakijiji ni mtu mbili gafauti.
 
Hata mimi nilishangaa sana jana Charles Hilal alipomtambulisha kama ndiye Mwanakijiji! I really appreciate Mwanakijiji's threads and I never miss reading his Ndoto ya Mwanakijiji.
 
Majid Mjengwa na Mzee Mwanakijiji ni member humu JF kwa hiyo tuwasubiri tu, wakiiona hii thread watajieleza.
On the side, mtangazaji akiliposema kwamba Majid hupenda kujiita mwanakijiji sidhani kama alimaanisha hii hoja. Majina kama mwanakijiji, mkulima, babu, dogo, mkuu, boss, huwa yanatumika mara nyingi bila ku reflect uhalisia wake. Kwahiyo inawezekana Majid anapenda kuitwa mwanakijiji kama Mzee Mwanakijiji na haina uhusiano wowote!
 
Jina Halisi la M.M Mwanakijiji ni Benjamini G. Mwalukasa, kwa wanaokumbuka, siku za nyuma alikuwa akiandika sana kupitia kijarida chake cha cheche akijitambulisha kama Benjamini G. Mwalukasa Mhariri. M.M Mwanakijiji ni ufupisho tu wa Mhariri Mkuu, hiyo mwanakijiji ni a.k.a katika kujidhihirisha kwake kuwa yeye ni mtu wa kawaida.
Si kweli kuwa Majid Mjengwa ndiye M.M Mwanakijiji kwa kuwa Majid Mjengwa hakuwahi kujitambulisha kama M.M Mwanakijiji, lakini pia, kupitia kijarida cha cheche, M.M Mwanakijiji amekuwa akitumia picha yake bila kificho, kwa wale watakaohitaji nakala ya kijarida hicho waseme tuwatundikie humu
Ndugu soma vizuri kanuni na sheria za JF, una ruhusa ya kutaja jina la mtu bila ridhaa yake na kwa kosa hili unastahili ban ya atleast one week. pili MM maana yake ni Mzee Mwanakijiji.
 
Nawapa picha hii........mjue nani MAGGID na nani MMMJ

sp6.jpg
 
And now gentle ladies and gentle men, on my own behalf and on your own behalf let me invite his Excellence MZEE MWANAKIJIJI to officially close this discussion!! "karibuMeeku o Parasa"
 
Ndugu yangu Mayasa,

Ahsante sana kuwaonyesha wengine njia. Uko sahihi kwa asilimia mia moja. Kwa vile Mjengwablog niliamua kuiita ' Kijiji' ambamo watembeleaji ni kama 'wanakijiji' wa Mjengwablog, basi, kuna walioamua kuniita ' Mwenyekiti' wakimaanisha Mwenyekiti wa Kijiji. Kaka yangu Charles Hillary ni mmoja wa ' Wanakijiji' wangu na alielekea huko katika kunitambulisha.

Sikuona umuhimu wa kuanza mjadala kwa kukanusha redioni ( BBC) utambulisho ule wa kuitwa ' Mwanakijiji'. Ni kwa vile yaliyokuwa mbele yetu katika mjadala ule yalikuwa ya muhimu zaidi. Kila dakika ilikuwa na umuhimu zaidi kuliko kuipoteza kwa kuwachanganya wasikilizaji juu ya "Oh, mimi sio ' Mwanakijiji' ni ' Mwenyekiti' na blah blah nyingine. Kwani kama ' Mwenyekiti' wa kijiji anaishi katika kijiji anachokiongoza kuna kosa gani kuitwa mwanakijiji?

Hivyo basi, niliyoyaandika hapa ndio yachukuliwe kuwa usahihi wa jambo zima na mengine mliyosoma yachuliwe kama ' Porojo za kuchangamsha kijiwe!"- Hata mie zimenichangamsha, ahsanteni sana!

Maggid
( 'Mwenyekiti' na 'Mwanakijiji' wa Kijiji Cha Mjengwablog. Unakaribishwa kijijini kwetu!)
PS: Mzee Mwanakijiji pia ni 'Mwanakijiji' wangu na mie ni ' Mwanakiji' wake, mwenye kubisha akamwulize!

pole sana mzee, naamini umejieleza vya kutosha na umeeleweka na hata mleta thread yeye alikutaka uje utoe ufafanuzi,(.....hakukanusha kwamba yeye si Mwanakijiji. Ina maana kwamba yeye kweli ni Mwanakijiji??

Labda atakuja kutupatia ufafanuzi kwanii mimi nijuavyo, Majid siyo Mwanakijiji wa JF a.k.s Mzee Mwanakijiji!
) umekuja na umefafanua lakini cha ajabu wapo watu wanaondelea kuandika upuuzi usio na msingi!!!
majina hayana ufungamano na mtu!! nyerere aliitwa JK na kikwete aliitwa JK , mbona kile kipindi cha mwanzo mwaka 2006-7 hamkusema kuwa kikwete hana hakimiliki ya jina la JK?

kila mtu ana ufahamu wake na upeo wake na yafaa tuheshimiane kwa hayo, hali kadhalika mm mwanakijiji ana upeo wake na ukomo wa upeo wake, na haina maana kuwa mm mwanakijiji ndiye mwenye uono bora zaidi, kwani si ni hapahapa JF mlipomponda kwa maelezo yake na nia yake ya kutaka kujiunga na CCJ mwaka jana? si ni hapahapa alionekana kama kichekesho kwa kujaribu kuwa kigeugeu??? huu ni unafiki, nakiri maggid ana upeo wake na mapungufu yake, hali kadhalika mm mwanakijiji ana uzuri wake na mapungufu yake
tatizo kila anayeandika kwenye kompyuta au simu, hufikiri yeye ana busara zaidi kuliko wengine, kweli nyani haoni ***** lake na MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!!!
 
Mods wamekuwa wapole sana safari hii naona wako busy wanafuatilia bunge kwani watu mnatafuta ban kwa nguvu lakini naona wao wanawacheka tu kwa kutukanana!!
 
01%2Bcopy.jpg


Nimeshtushwa sana na taarifa na uvumi unaoendelea sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii na blogs nchini Tanzania juu ya Maggid Mjengwa, hivi nani kasema Maggid sio rafiki wa Dr Slaa? nani kasema Maggid sio Mwanakijiji? nikipewa nafasi nitaeleza mengi zaidi......uhusiano ulioko kati ya Mzee Mwanakijii na Maggid!
 
Mkuu nilikuwa sijui kama Majid ndiye MMM Mwanakijiji lakini jana nikasikia kupitia BBC Mtangazaji bwana Charles Hilary Nkwanga akimtaja Majid Mjengwa kwamba kwa jina lingine anaitwa mwanakijiji! Hivi ni kweli Majid Mjengwa ndiye MMM Mwanakijiji?
 
Ha ha ha ha....dah watu bwana.kwani kama ni kweli kuna tatizo gani?je,alisema Mwanakijiji wa JF?
 
Ha ha ha ha....dah watu bwana.kwani kama ni kweli kuna tatizo gani?je,alisema Mwanakijiji wa JF?

Ben unajua jina la Mwanakijiji ni kubwa sana hapa JF na Tz kwa ujumla. Sasa jana watu tulishangaa Hilary aliposema kuwa Majid Mjengwa kwa jina lingine Mwanakijiji na akarudia mara mbili ama tatu hivi na Majid hakukanusha sasa tukadhani yeye ndiye MMM Mwanakijiji. Kama si hivyo basi Majjid Mjengwa MM amelitumia vibaya jina la Mwanakijiji!! Kwani Majjid Mwenyewe amekanusha?
 
Mjengwa namkubali sana... Yeye ni miongoni wa ma-Blogger wa Mwanzo kabisa hapa Tanzania... sio Bogus japo kuna Kipindi anakumbatia Magamba....
 
Wandugu, Mjengwa na mimi ni watu wawili tofauti; tunaofahamiana na kushirikiana kwa karibu katika shughuli zetu mbalimbali. Nadhani mchanganyo haukutokea katika Maggid kujibu bali katika C. Hillary kuuliza zaidi. Nadhani maelezo ya Maggid yanatosha kumaliza huu mjadala na nimeyakubali.
 
wabeja sana. Kiongozi wangu MM unajua ni rahis kwa ibilisg kujifanya Mungu kuliko Mungu kujifanya ibilisi.
 
Ben unajua jina la Mwanakijiji ni kubwa sana hapa JF na Tz kwa ujumla. Sasa jana watu tulishangaa Hilary aliposema kuwa Majid Mjengwa kwa jina lingine Mwanakijiji na akarudia mara mbili ama tatu hivi na Majid hakukanusha sasa tukadhani yeye ndiye MMM Mwanakijiji. Kama si hivyo basi Majjid Mjengwa MM amelitumia vibaya jina la Mwanakijiji!! Kwani Majjid Mwenyewe amekanusha?

Amekanusha,ametoa ufafanuzi ambao Mwanakijiji naye ameunga mkono....tatizo watu wanafikia hatua kwa sababu ya mihemko au sijui ni nini wanaanza kuwachambua watu kwa kebehi na kudhalilisha wengine.maggid na Mwanakijiji ni waandishi na wachambuzi wazuri kabisa.Watu sasa wawe na staha,inapendeza!
 
ana mjua kibonde tu but to be honest mzee mwana kijiji sie maggid hapo mtangazaji alitumia kama ni kisifa but mwanakijiji hawezi kuwa juha .
Conquest-kiwahisli bado kufukia kueleweka hata kama ni asili yetu.
 
Wandugu, Mjengwa na mimi ni watu wawili tofauti; tunaofahamiana na kushirikiana kwa karibu katika shughuli zetu mbalimbali. Nadhani mchanganyo haukutokea katika Maggid kujibu bali katika C. Hillary kuuliza zaidi. Nadhani maelezo ya Maggid yanatosha kumaliza huu mjadala na nimeyakubali.

Ndugu yangu Mwanakijiji mwenzangu Mzee Mwanakijiji,
Asante sana kwa kuchangia kwenye kuliweka wazi suala lililojitokeza na kuzua mjadala mkubwa ambao pia umekuwa wa manufaa kwa kutusaidia kupata maarifa mapya. Nawashukuru pia wachangiaji wote wengine, bila kuwasahau walionitukana na kunikebehi. Wengine tumekuwa kama makuli wa bandarini, kebehi na matusi tumeyazoea!
Maggid
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom