Takasa na safisha vitu na mambo yako kwa usalama wako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Vita ya Maisha ni baina ya makundi hasimu mawili. Nuru na Giza, Juu na chini, Uchafu na usafi, Wema na Ubaya, Inuko na anguko, Mng'ao na mfubao.

Kwa watu makini wanajua wazi kabisa kuwa ili mambo yako yaende lazima yasafishwe, yatakaswe, na ili mambo yako yaende mrama, kuyumbayumba lazima yachafuliwe.

Ni katika uchafuzi ndiko Ujinga, Umaskini na Maradhi huishi huko.

Adui yako ili akumudu na akushinde ni lazima akuchafue, akufubaze, ili uanguke na kushindwa. Mchafue, kisha afubae, halafu mshinde na kumuangusha. Hiyo ni kanuni ya kivita inayotumika tangu kale na kale.

ili familia yako ishindwe, ianguke na iwe familia iliyofeli. Basi maadui zako huanza kukuchafua na kukufubaza. Wataanza na wewe, kisha mkeo halafu mwisho watoto na wajukuu zako.

Mbinu zitumikazo kukuchafua na kukufubaza;

1. Kukupa jina lenye sifa mbaya
Mfano, huyu jamaa mlevi huyu, au malaya, mchawi, mshirikina, au kubwa jinga, kibarua, au kibaraka
Utasikia; kwa yule mzee wa totozi, au fulani ni mshirikina ajabu. Kitakachofuata hapo ni familia yako kutambulika kwa utambulisho wako, ile familia kwa uchawi haijambo.

Usikubali mtu akuchafue kwa jina baya. Anakumaliza kwa uhakika sio wewe tuu bali mpaka watoto wako ambao labda bado hujawazaa. Hata kama unatabia mbaya vipi usikubali mtu akutaje kwa tabia hizo huko nyuma kukuchafua na kukufubaza.

2. Kukupa Uhusika mbaya wa kiumbe au mtu mbaya

Mfano, nyani, mbwa, nguruwe, kibwengo, msukule, mende, n.k, Wazungu waliwaita Waafrika nyani, na mara kwa mara wamekuwa wakifanya hivyo. Usikubali mtu akapewa uhusika wa kiumbe au mtu mwenye uhusika au sifa mbaya.

3. Kukupa vitu vyenye uchafu au sifa duni
Kwa mfano kukupa vitu used visivyo na heshima, kukupa vyakula au vitu duni. Mtu akikupa vitu vya namna hiyo vikatae na mkatae. Unaenda kwa mtu anakuambia, kuliko nitupe ni bora umekuja nikupatie vikorokoro hivi. Halafu ukiviangalia vimeharibika au vimeisha. Huko ni kukuchafua na kukufubaza.

Mtu akupe vitu tena vyenye hadhi na thamani ikiwa anahama na hana uwezo wa kuvichukua vitu vyote na alikuwa anavihitaji sema hali ndio imesababisha tuu.

4. Kukufanya mtu wa burebure
Usipende kupewa vitu vya bure. Huo ni uchafuzi na ufubazaji. Iwe wewe ni mwanaume au mwanamke usikubali kupewapewa vitu vya bure, huko ni kuchafuliwa na kufubazwa ambako kwa hakika utaleta kudharauliwa.

Elewa kuwa kwenye maisha hakuna kitu cha bure. Usipokilipia kwa heshima basi utakilipia kwa dharau. Mtu akupe kitu kama umemfanyia kazi, mtu akupe kitu kama Ahsante (isiwe Rushwa lakini).

UTAKASO
Kitu chochote kilichotumika na mtu mwingine ambaye sio wewe kinahitaji ukisafishe na kukitakasa. Hiyo ni kanuni ya Usafi. Kitu chochote ambacho umekitumia wewe mwenyewe halafu kikachafuka kitahitaji ukisafishe na ukitakase. Hiyo ni kanuni ya Afya.

Ukienda hospitalini Madaktari watakuambia kile nilichokisema, vifaa, zana na vitu vilivyotumika lazima vifanyiwe usafi ili vitumike tena. Ingawaje vipo vitu ambavyo sharti vitumike mara moja tuu.

Usipofanya usafi na utakaso kunatokea madhara ikiwemo magonjwa ya kimwili na kiroho. Yapo pia magonjwa ya kihisia ambayo mengi yanatokana na matokeo ya uchafu wa kimwili.

Damu safi na damu chafu, moyo safi na moyo mchafu, mwili safi na mwili mchafu, akili safi na akili chafu.

Ili maisha yako yaharibike ni lazima ukutane na vitu, mambo na watu wachafu au waliofubaa. Huwezi upata UKIMWI (uchafu) kwa mtu ambaye hana UKIMWI. Hiyo haiwezekani.

Huwezi pata maradhi kwa viumbe wasio na vimelea vyenye kudhuru. Mambo yako ya kiuchumi hayawezi kuharibika kama haujakutana na watu wachafu, hiyo haiwezekani.

Maisha yana njia zake. Ili wewe uharibikiwe basi elewa kuwa kuna mhusika fulani lazima ukutane naye ili akijaribu. Huwezi kuharibika from nowhere. Huwezi kuwa maskini na mpumbavu from nowhere.

Hiyo inaenda sambamba na kufanikiwa au kushinda. Huwezi ukashinda bila kukutana na watu safi au viumbe visafi, hiyo haiwezekaniki.

Ndio maana unapaswa uwe makini unapokutana na mtu usiyemjua (stranger). Unapofanya usajili wa marafiki na watu wanaokuzunguka lazima uwe makini sana. Kuanzia mke/mume pamoja na marafiki na jamaa zako utakaoamua wawe karibu yako.Lazima ufanye Usafi.

Fikiria umeenda kupanga katika nyumba au chumba ambacho alikuwa akiishi mtu mshirikina na mchawi. Fikiria uchafu wote alioufanya na kunajisi nyumba au chumba ambacho umekodisha. Unafikiri eneo hilo litakusafisha au litakuchafua?

Au umepanga nyumba au chumba ambacho aliyetoka alikuwa ni mtu anayeingiza wanawake au alikuwa shoga au msagaji. Je, eneo hilo litakusafisha au litakuchafua?

Fikiria umenunua gari ambalo lilimgonga mtu kwa makusudi na limemwaga roho ya mtu kwa makusudi, unafikiri gari hilo litakusafisha au kukuchafua?

Elewa kuwa kama mwili na vitu vinavyoonekana kama nguo au chumba unavyokisafisha kwa sabuni na kemikali ndivyo hivyohivyo kwa upande wa roho.

Kama vile kwa upande wa Physicians walivyotengeneza madawa ya kusafisha mwili ndivyo hivyohivyo kwa upande wa roho.

Ili wewe ukutane na Riziki yako kuna mchakato fulani ambao lazima uupitie ili uipate hiyo unayoiita riziki, na mchakato huo mara nyingi lazima uhusishe vitu na watu. Halikadhalika na ili ujikute kwenye mkosi lazima mchakato fulani ufanyike ambao utahusisha vitu na watu.

Chochote utakachokipata au ambacho kipo chini ya miliki yako lazima ukisafishe na kukitakasa, ili kiwe safi. Hiyo ndio namna pekee ya kuyapa maisha yako furaha na kuwa nje ya mfumo wa mikosi na mabalaa.

Unaweza pia ku-date na mwanaume au mwanamke ambaye ni mchafu wa kiroho akakuchafua. Mambo yako yakaanza kwenda ndivyo sivyo. Yakaanza kuharibika.

Elewa kuwa Maisha hayahitaji mambo makubwa sana. Ila ukiwa mchafu au ukitumia kitu kichafu utahitaji nguvu na mambo makubwa sana kuishi.

Acha nipumzike sasa. Nawatakia Sabato Njema.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Mfano Mtu kanipa simu used je nafanyaje kujitakasa na kama mtu alikuwa anatomba mademu katika Gheto je nifanyeje kusafisha Hilo Gheto ufafanuzi mkali wa hizi naweza jitakasa vipi?
 
Mfano Mtu kanipa simu used je nafanyaje kujitakasa na kama mtu alikuwa anatomba mademu katika Gheto je nifanyeje kusafisha Hilo Gheto ufafanuzi mkali wa hizi naweza jitakasa vipi?

Hiyo ni mada ya siku nyingine Mkuu.

Kwanza kiusalama kununua au kupewa simu used ni hatari. Lakini kama haikuwahi kufanya uhalifu kwa mujibu wa sheria lakini muda huohuo ilikuwa inatumika kudanganyia mademu au kuibia Madanga. Itahitaji uitakase.

Halikadhalika na vyumba.
 
Wapi huko kusiko na vicheche ututajie mheshimiwa?!!
Sifa yenu ndo iyooo ndo maana nyerere aliwapa vitengo nyeti vya kushikaa ela akijua hamuwezi kuibaaa ila mwamkee hata mtongani to azizaly hafiki mshamlaaa kichwaaaa.......
 
Back
Top Bottom