Heshima kwenu wana jamvi.
Tokea kuteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi, mheshimiwa Mwakyembe ameonesha utendaji na uzalendo wa hali ya juu ikiwa ni dhamira kufufua hata huduma zilizokwisha sahaulika kama reli ya kati, usafiri wa tren jijini dar, shirika la ndege ATCL na leo hii ameahidi kuifanya bandari ya Dar es salaam kuwa kivutio cha huduma za bandari kwa kuondoa wizi wa bidhaa, kuondo ucheleweshwaji wa kupata mizigo bandarini na kuifanya bandari kuweza kuchangia vizuri pato la taifa.
Hayo aliyasema wakati akikabidhiwa ripoti iliyochunguza kwanini bandari yetu imedorora kuliko bandari kubwa 36 barani Afrika. Mwakyemba ameahidi kuwashughulikia wote wanaojihusisha na vitendo vya wizi, uzembe na kuifanya bandari kupoteza mvuto kwa wasafirishaji wa bidhaa.
My take; hivi katika taifa la zaidi ya watu milioni45 kiongozi mzalendo mwenye kujali maslahi ya taifa ni mmoja tu? Mawaziri na viongozi wa idara zingine tafadhalini igeni mfano wa utendaji wa Mwakyembe ili angalau taifa letu lisonge mbele