je kati ya watz 45 million kuna Mwakyembe mmoja tu?

Tewe

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
1,101
813
Heshima kwenu wana jamvi.

Tokea kuteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi, mheshimiwa Mwakyembe ameonesha utendaji na uzalendo wa hali ya juu ikiwa ni dhamira kufufua hata huduma zilizokwisha sahaulika kama reli ya kati, usafiri wa tren jijini dar, shirika la ndege ATCL na leo hii ameahidi kuifanya bandari ya Dar es salaam kuwa kivutio cha huduma za bandari kwa kuondoa wizi wa bidhaa, kuondo ucheleweshwaji wa kupata mizigo bandarini na kuifanya bandari kuweza kuchangia vizuri pato la taifa.

Hayo aliyasema wakati akikabidhiwa ripoti iliyochunguza kwanini bandari yetu imedorora kuliko bandari kubwa 36 barani Afrika. Mwakyemba ameahidi kuwashughulikia wote wanaojihusisha na vitendo vya wizi, uzembe na kuifanya bandari kupoteza mvuto kwa wasafirishaji wa bidhaa.

My take; hivi katika taifa la zaidi ya watu milioni45 kiongozi mzalendo mwenye kujali maslahi ya taifa ni mmoja tu? Mawaziri na viongozi wa idara zingine tafadhalini igeni mfano wa utendaji wa Mwakyembe ili angalau taifa letu lisonge mbele
 
usafiri wa treni dar?really?
umeanza lini?

Si kwamba umesha takeoff ila uko kwenye hatua za mwisho za utekelezaji hadi safari ya majaribio imeshafanyika. I stand to be corrected
 
Mwakyembe ni MSANII.

Ni mtu msomi na uwezo MKUBWA sana ila ndiyo hivyo tena. Ukiwa CCM, usitegemee utafanyakazi kama MSOMI.

Mchungaji Msigwa anasema, Wasomi wanaongea kama darasa la pili.

Nina imani angelikuwa chini ya Chama Imara, basi Tanzania ingelifaidika sana na usomi wake kama Mwanasheria.

Last edited by a moderator:

Unamaanisha nini kumuita msanii? Binafsi naamini kati ya majembe ya nguvu yaliyokosa shamba lenye rutuba mwakyembe ni mmojawapo. Angehamishia shughuli zake kwenye shamba lililo tumaini kubwa la watz tungenufaika kwa kiasi kikubwa na elimu yake. Hatahivyo mnyonge mngongeni jakiyake mpeni
 
Last edited by a moderator:
Kwani hadi leo hii KAFANYA nini?

Yaani kitu alichofanya na unaweza kukionyesha kuwa KIMEFANYIKA na bado kinafanya kazi.

Wee nunua tu MATAIRI ya gari na uanze kujisifu kuwa UMESHANUNUA GARI.
Unamaanisha nini kumuita msanii? Binafsi naamini kati ya majembe ya nguvu yaliyokosa shamba lenye rutuba mwakyembe ni mmojawapo. Angehamishia shughuli zake kwenye shamba lililo tumaini kubwa la watz tungenufaika kwa kiasi kikubwa na elimu yake. Hatahivyo mnyonge mngongeni jakiyake mpeni
 
Mbona wako wengi tena wazuri sana ila wako benchi!! Kocha ana visasi kagoma kuwapangia namba!!!
 
Kagasheki,mwakyembe,magufuli ndio mawaziri pekee tz wenye uzalendo na nchi yao wengine wanasubiria madili wapige wajilimbikizie aka jumba la mbezi beach nk
 
Asante kwa kutukumbusha maneno yenye MASHIKO YA UZALENDO NA C USHABIKI WA KISIASA
 
Heshima kwenu wana jamvi.

Tokea kuteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi, mheshimiwa Mwakyembe ameonesha utendaji na uzalendo wa hali ya juu ikiwa ni dhamira kufufua hata huduma zilizokwisha sahaulika kama reli ya kati, usafiri wa tren jijini dar, shirika la ndege ATCL na leo hii ameahidi kuifanya bandari ya Dar es salaam kuwa kivutio cha huduma za bandari kwa kuondoa wizi wa bidhaa, kuondo ucheleweshwaji wa kupata mizigo bandarini na kuifanya bandari kuweza kuchangia vizuri pato la taifa.

Hayo aliyasema wakati akikabidhiwa ripoti iliyochunguza kwanini bandari yetu imedorora kuliko bandari kubwa 36 barani Afrika. Mwakyemba ameahidi kuwashughulikia wote wanaojihusisha na vitendo vya wizi, uzembe na kuifanya bandari kupoteza mvuto kwa wasafirishaji wa bidhaa.

My take; hivi katika taifa la zaidi ya watu milioni45 kiongozi mzalendo mwenye kujali maslahi ya taifa ni mmoja tu? Mawaziri na viongozi wa idara zingine tafadhalini igeni mfano wa utendaji wa Mwakyembe ili angalau taifa letu lisonge mbele

pole yake na pole yako wewe unayemshabikia, kwa taarifa yako anafanya majungu zaidi kuliko kazi. Kwasasa TRC ndo imekuwa mbaya zaidi kuliko ilivyowahi kuwa, ATCL ya sasa inalipia gharama kubwa za kukodi ndege kuliko kipato, hapa huyo Mwaky wako amefanya nini?
 
"Kuna mambo kamati teule imeyaacha ili kuokoa serikali iliyo madarakani" Dr. Mwakyembe

Kama Mzalendo ni mwenye kutetea serikali ilojaa ufisadi isianguke basi itakuwa ulimaanisha gazeti la MZALENDO...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom