Je, Joseph Mbilinyi (Sugu) anaweza kufungwa?

Godbless J Lema,
Utii wa sheria na nidhamu ya kizalendo unatafasiriwa kama uoga na wanasiasa wenye uchu wa madaraka.Madhara ya kutotii sheria na maandamano yasionatija yana madhara makubwa kwa maisha ya watu na uchumi wa nchi.Ikumbukwe kuna wananchi walitopeza maisha kwenye siasa hizi uchwara na zenye ulaghai zinazohasisiwa kwenye nchi za maghari.Leo hii wachochezi wanaponda maisha na familia zao huku zile familia zilizoangamia zikibaki zinalia na kusaga meno.
 
Kama kweli CDM ni waungwana ni vyema kwanza wangekemea viongozi wao kuporomosha matusi makali bila ya sababu za msingi, inafaa ile clip ya Sugu iwekwe pia humu ili tuone jinsi tulivyo na viongozi wa ajabu. Kama mbunge unaongea matusi, kejeli na uongo na unatetea huo ndio uhuru basi hamna faida yoyote kwa jamii. Uhuru usio na mipaka ni vurugu.

Hakuna hata Kiongozi mmoja wa CDM atakayekemea ujinga aliofanya Sugu, hii inachochea viongozi wengine wa mizuka wa CDM kuja kufanya makosa hayo hayo. Kama wakati ule Lijuakali anawafanyia fujo Polisi hadi kufungwa ingekemewa Sugu asingefikiria kufanya ujinga na yeye. Endeleeni kutetea ujinga ila hakuna mwananchi atakaye ingia barabarani ili kutetea uovu wa Sugu.
aliyoongea sugu ni ya uongo thibitisha tu hilo, mtu na akili zako huwezi ukazusha uwongo, watu wote tunaona na kusikia, na hakuna lolote linaloshughulikiwa, mtu ananyooshea mwenzake bastola kutishia kuua, hamjatupa majibu mpaka leo, katokea nabiii tito, hao ndio mnatoa matamko ya kumkamata, sawa lisu mtasema wasiojulikana na aliyomnyooshea nape nae hajulikani kweli? unajua kuna mambo ukifikiria yanavyotendekea unajikuta unakufuru kuwa kwanini mzazi wangu asingenichomoa tu nikiwa tumboni au baba angevaa soksi wakati ninatafutwa na unajikuta kwanini umekuja duniani,
 
Hata hawa wanaoshtakiwa walipaswa kutumia busara na Hekima kwenye matamshi yao wakati wa Mkutani
Ukiwa mtu mzima huwezi kubishana na watoto. Kiongozi lazima awe mfano, tumeona Raisi Mstaafu, alikua hana muda na mambo ya kipuuzi kama haya. Kiongozi unapaswa kushughulika na mambo makubwa zaidi ya haya, huu ni mtazamo wangu tu i stand to be corrected.
 
Narudia kujiuliza, ni kwanini siasa inataka kutugawa watanzania badala ya kutuunganisha? Kama vyama vya upinzani havihitaji pamoja na wabunge wake kwanini visifutwe?? Hii chuki yote ambayo inaonekana kuanza kujengeka ndani ya Taifa letu ni nini hatima ya umoja wetu?? Na wanaoshangilia leo juu ya haya yanayoendea ni nini matamanio yao juu yamustakabali wa nchi yetu?? Eeee mungu wa mbinguni ninakuomba ulitizame taifa lako, utuepushe na nguvu ya chuki, uovu dhidi ya wtu wengine ambayo imeanza kujiinua na kuonekana ndani ya nchi yetu.
Labda cha kujiuliza ni kwa nini siasa zinatugawa leo .......... watu wale wale, siasa zile zile............ tatizo liko wapi!!?
 
Wananchi nao wamejaa ujinga,mambo ya ajabu yanaendelea nchi hii wako kimya tu. Wanasubiri Lema,Mbowe na Msigwa wawasemee. Eti siku hizi wanamtumia Mange Kimambi "Hide my ID" this is shithole country
Unafikiri wananchi waleo wanadanganyika na siasa za kijinga,
Japo wengi wao huwazania hawana elimu lakini wamejifunza kupitia mataifa yaliyo uza amani kwa wanasiasa wajinga.
 
Kama kuna wakati tunapaswa kutafakari hatima ya Nchi yetu ni sasa. Tatizo la msingi ambalo tunapita kama Taifa ni uoga , kwa maoni yangu uoga unaweza kuwa ndio dhambi kubwa na mbaya kuliko zote Duniani , hata hivyo kuwa jasiri ni kuwa na nia ya dhati kabisa ya kusimamia haki na kukataa uonevu.

Kila jambo linalotokea ktk maisha yetu ni ruksa inayotokana na hiari ya maamuzi yetu, kwani kushindwa au kushinda kwa jambo lolote hakutokani na uwezo wa maadui zetu bali maamuzi yetu na mtazamo katika mambo mbali mbali.

Sasa tuna kilio kikubwa cha demokrasia kukandamizwa , uhuru wa vyombo vya habari na mambo mengine mengi yanayofanana na haya.

Kwa sasa karibu Wabunge wote wa Upinzani wana kesi mbali mbali katika mahakama Nchini na wengine wana vitisho mbali mbali kama kuuwawa na wengine kuharibiwa mali na kufilisiwa kabisa pia Mbunge wetu Mh Tundu Lissu anauguza majeraha ya risasi Nchini Ubelgiji baada ya kukaa Nairobi takribani miezi minne.

Wakati tunapita kwenye nyakati kama hizi unaweza kusikia watu wanasema kwa kweli Chadema wanapita kwenye wakati mgumu sana , ni kweli tunapita kwenye wakati mgumu sana lakini haya ni mawazo na fikra potofu kufikiri kuanguka kwa demokrasia ni anguko la Chadema. Demokrasia na haki inaposhindwa ni Taifa linashindwa kwa hiyo wajibu wa kupigania haki ni wajibu muhimu wa kila mtu anayependa Nchi yake na wajukuu zake.

Kwa kweli kwa sasa , hatujui hatima ya maisha yetu sana kwani Siasa Nchini zimekuwa na uadui mkubwa sio kwa sababu tumevamiwa na Nchi jirani lakini ni kwa vile hadhi ya madaraka na utawala imekuwa muhimu kuliko HAKI na UTU .

Maisha yetu yamekuwa magumu sana , tunawezaje kukosa mashaka kwenye hali kama hii ya sasa,tunafundishwa uoga kila leo na tunaweza tu kushinda hali hii kwa kudharau tunavyojisikia kuhusu hofu na uoga kwani pasipo kudharau kwa ajili ya malengo ya haki ya Nchi yetu basi dhamira zetu zitapaswa kulaaniwa na vizazi vinavyokuja.

Unapoona kauli ya Jaji Mkuu kuhusu uhuru wa Mahakama , tunapoona Wabunge wanateswa kwa kutengenezewa mashitaka ya aina mbali mbali , tunapoona Mbunge anapigwa risasi mchana nyumbani kwake mioyo yetu inatazama na kulia kwa uchungu,sio fahari wala sifa kuvumilia mateso ila kwa sasa ni wajibu muhimu ambao haupaswi kukimbiwa hata kidogo , kwani thamani ya maisha yetu haijengwi na hadhi zetu na mali zetu za leo na vyeo vyetu bali msingi imara tunaoweka kwa ajili ya vizazi vinavyokuja baada yetu na msingi huo ni haki , tabia njema , usawa , kuheshimiana , utu na hadhi ya utawala wa sheria na demokrasia , kama tukifikiri hivi ni dhahiri kuwa tutakuwa tunaonyesha Upendo kwa watoto wetu na vizazi vinavyokuja.

Kwa bahati mbaya mashabiki wa mpira wamekuwa na hekima ya ushindani kuliko mashabiki wa demokrasia , hakuna Uchaguzi unaopita bila maumivu na mateso na hii inaonyesha busara mbaya ya mwekekeo wetu kama Nchi.

Tutafanya nini sasa Kurekebisha hali hii ? Ni muhimu kujua msingi wetu wa fikra katika haki na utu , kama Watanzania wataendelea kufikiri na kutenda na kuamua mambo ya Nchi yao kwa hofu na uoga basi ni wazo hata mfumo wa vyama vingi hautakuwa na maana kwetu, ni lazima Wananchi wajue Serikali inawajibika kwa ajili yao na ni lazima sana Wananchi wasiruhusu hata kidogo Nchi kuendeshwa bila utaratibu wa sheria na Katiba ,sasa ikiwa Wanamchi watafikiri kazi ya kulinda haki ni kazi ya vyama vya siasa basi Wananchi sisi tutakuwa tunafanya makosa makubwa ya kuangamiza Taifa. Ukiukwaji wa mambo ya msingi unaoendelea unasababishwa na aina ya tabia ya Wananchi katika Nchi, wakati Nchi nyingine mkate ukipanda bei watu wanaandamana huku kwetu Mbunge anapigwa risasi na wanao kusanyika kumuombea wanakamatwa na kushitakiwa na hakuna hatua yoyote inayo chukuliwa na Wananchi kuonyesha kuchukizwa na mambo haya,kipimo hiki kinathibitisha uoga wa kina kabisa ktk jamii.

Tabia hii ya uoga isipo koma nafikiri hata ikatokea Chadema kuongoza Nchi hakutakuwa na tofauti kubwa sana kati yetu na ccm kwani mlinzi wa Nchi bora sio sera na rangi ya Chama cha Siasa bali ni tabia na fikra za wanaotawaliwa (Attitude ) dhidi ya Nchi yao .

Kuishinda hofu sio tu ni faida katika Nchi bali ni msingi mzuri wa kujenga kizazi cha ubunifu sehemu mbali mbali za maisha yao ya kila siku. Hofu haiwezi kujenga uwezo ubunifu (innovations) kwa sababu hofu ni ugonjwa mbaya sana wa akili.

Kabla ya kusema kwamba Bunge letu haliko huru ni muhimu kujiuliza kama hao Wabunge wenyewe wanajua thamani ya uhuru ? Na wako huru ?

Kabla vile vile ya kusema Mahakama zetu haziko huru ni vyema tukajiuluza kama vile vile hawa watumishi wa Mahakama wanajua vyema thamani ya uhuru ? Na wanathamini haki kwa kiwango gani ? Hatuwezi kujenga Taifa imara bila kubadilisha mfumo wa fikra katika kufikiri (from Negative Mentality to Positive mentality ) huu ndio msingi mkuu wa kushinda katika Nchi.

Hivyo wajibu wa kupigania haki ni wajibu unaopaswa kuanzia kwenye familia , badala yake wajibu huu muhimu kama ibada umeachwa kwa Viongozi wa kisiasa peke yao. Hata makanisa makubwa na Misikiti zimeacha kabisa kuhubiri wajibu huu wamebaki wakipambana na uzinzi na konyagi katika ibada zao , wako wachache wanaojitahidi nao hawapaswi kupongezwa kwa kazi zao lakini kwa sababu ya fikra ya kizazi hiki kukwepa wajibu wake basi tuseme ni muhimu kuwapongeza.

Wakati naamka kuandika waraka huu, Mh Sugu yuko magereza pamoja na Kiongozi mwingine Masonga, safari yao itakuwa ndefu kidogo, uhuru wao wa kisheria kuhusu dhamana umedharauliwa na kuonewa , ninajaribu kuhisi tu ikiwa atafungwa mkakati wa Sugu kupoteza Ubunge unaweza kuwa hivi , baada ya hukumu Hakimu anaweza kuchukua likizo kwa hiyo kukataa rufaa kunaweza kuchelewa wakati huo tume itakuwa imeshaandikiwa na kutaarifiwa kuwa Jimbo liko wazi, naendelea kuona maono.... baada ya Tume kuharifiwa, Tume itaitisha Uchaguzi mara moja na Uchaguzi utafanyika na Mbunge atapatikana lakini baadaye Sugu atakuja kufanikiwa kukata rufaa au kumaliza kifungo chake na Ubunge wake utakuwa mwisho....ni nasema haya ni maono tu na sasa ni saa nane usiku sijui kwa nini naona maono haya....

Nini kifanyike kwa kweli nikiri kuwa sijui kwa sasa lakini tukitafakari na kumuomba Mungu tutapata njia..

Nimalizie kwa kusema kuwa tunapaswa kuingia kwenye wajibu mkuu sana wa kutafuta haki na kulinda haki kuliko wakati wowote wa maisha yetu.

Mungu alishasema katika vitabu vyake kuwa USIOGOPE , maana yake alijua kuwa kutakuwepo na vitisho lakini MSIOGOPE...sasa kama huu ndio msimamo wa Mungu kuhusu hofu basi nami naomba ubaki kuwa msimamo wangu na familia yangu.

MSIOGOPE....

Godbless Lema (MB )
Hayo ni maono au ndoto?
Siasa za matusi hazina nafasi kipindi hiki
.Na siyo kwamba watanzania ni waoga, hapana
Siyo wapinzani au wananchi, sote tulimuomba Mungu tupate Rais jasiri, asiyependa rushwa
Asiye mzururaji
Mwenye kiu ya maendeleo,Naam tulipigia kura mabadiliko!

Ushauri kwa upinzani
Hubirini maendeleo, hizi person attack ni siasa za kishamba, mmepewa halmashauri, ni kipi cha maana mlichofanya kama mbadala wa ccm?
Msipobadilika, nature itawabadilisha
Tukutane 2020
 
Acheni kulialia kasikilize ile audio ya dakika 39 ikiyowekwa mahakamani live Jana halafu utwambie nani anamuonea nani?,tatizo mlizoea kuchukulia mambo kirahisirahisi awamu zilizopita, zamu hii mambo yamebadilika na msipobadilika mvua zitewanyeshea kweli. Hakuna demokrasia ya kuongea bila break duniani.Demokrasia Ina mipaka yake, JPM alipoingia madarakani alisema "Nimeamua nchi isonge na itasonga tu", na kweli inasonga tu mtakaoamua kuwa walalamishi endeleeni Kama itawasaidia, wengine tunaendelea na Maisha Kama kawaida, wananchi wanataka maendeleo sio porojo za demokrasia, sijui mikutano ya siasa na malalamishi kila siku.
Hivi nchi inasonga kwa kuwafunga wapinzani? Hivi nchi inasonga mbele kwa kuleta hofu kwa watu unaowaongoza? Hivi nchi inasonga kwa hakimu kuweka sheria pembeni na kufuata maagizo toka juu? Hivi nchi inasonga kwa kuwa na kesi nyingi mahakamani? Hivi nchi inasonga kwa kutofuata sheria zilizopo? Kama hivyo ndivyo, tuendako ni pabaya zaidi.
 
Tupe option Kama kiongozi siyo kulalamika lalamika, halafu nawashauri mbadirishe aina ya siasa kwa nyakati tuliyojayo , coz wakati siyo wa jk , huu ninwakati wa undava undava ..!!
Mawazo ya Lema ni food for thought. Tujadili na tupate a way forward pamoja sio yeye aseme tu.
 
Hapo nimedaka neno:-
Demokarisa inaposhindwa ni Taifa limeshindwa.
 
Kila jambo linalotokea ktk maisha yetu ni ruksa inayotokana na hiari ya maamuzi yetu, kwani kushindwa au kushinda kwa jambo lolote hakutokani na uwezo wa maadui zetu bali maamuzi yetu na mtazamo katika mambo mbali mbali.
This too shall pass
 
Pole Sugu walikutafuta sana sasa wamekupata lengo jimbo liwe la Tulia hilo!! Jipange omba Mungu kinachokuja sio kizuri!! Nimeliona hilo
 
umefika wakati wa kuweka uoga pembeni na kupambana mpaka kieleweke. Watanzania tunapelekwa kwenye mapambano bila kutaka wala kupenda. lakini hatuna kingine cha kufanya. tujiandae kisaikolojia.
 
MUNGU ndiye aruhusuye matukio yote kwa makusudi maalumu... Yesu aliwaambia mahakimu watoe hukumu kwa haki bila upendeleo... RAISI wangu atakuwa na maswali mengi sana ya kujibu atakapokutana MUNGU maana hafuati haki...
 
We as a nation will survive!

Time only.

Time will tell.

No permanent situation. Never!
 
Back
Top Bottom