Je, Joseph Mbilinyi (Sugu) anaweza kufungwa?

[HASHTAG]#MBEYA[/HASHTAG] KESI YA SUGU'
Washtakiwa Joseph Mbilinyi (Sugu) na mwenzake wamemkataa Hakimu anayesikiliza shauri lao kwa madai kuwa hawana imani naye baada ya kuwanyima dhaman kinyume cha sheria.
Kesi hiyo imeaihirishwa kwa saa kwaajili ya kusubiri uamuzi iwapo Hakimu huyo ataendelea nayo ama laa.
 
Udikteta wa Sizonje hauna tofauti na yule dikteta wa zamani wa Misri (Hosny Mubarak). Kama yule wa Misri alikumbana na vikwazo akafika mwisho, basi naye Sizonje siku zake zinahesabika.
 
Acheni kulialia kasikilize ile audio ya dakika 39 ikiyowekwa mahakamani live Jana halafu utwambie nani anamuonea nani?,tatizo mlizoea kuchukulia mambo kirahisirahisi awamu zilizopita, zamu hii mambo yamebadilika na msipobadilika mvua zitewanyeshea kweli. Hakuna demokrasia ya kuongea bila break duniani.Demokrasia Ina mipaka yake, JPM alipoingia madarakani alisema "Nimeamua nchi isonge na itasonga tu", na kweli inasonga tu mtakaoamua kuwa walalamishi endeleeni Kama itawasaidia, wengine tunaendelea na Maisha Kama kawaida, wananchi wanataka maendeleo sio porojo za demokrasia, sijui mikutano ya siasa na malalamishi kila siku.
....Kwa hiyo kwa akili yako ya kipimbi pimbi unaona kwamba all JF members walikuwa huko mahakamani kusikiliza hiyo audio? Si uiweke hapa?
 
CCM wana mwisho mbaya, wale wanaoweza kufikiri hili liko wazi.. Mwisho mbaya wenye aibu kuu
 
Bandiko zuri mh. Godbless J Lema, hakika demokrasia ya nchi yetu inapitia majaribu makubwa sn mungu pekee ndiye anayejua tunapoelekea kwa ss, lkn mm kwa ninavyoona mh. sugu au mbunge yeyote yule wa upinzani asiogope kupoteza jimbo lake kwukuwa hiyo itabaki kuwa ni option ya mwisho ktk kupigania demokrasia ya kweli.Nelson Mandela aliyewahi kuwa rais wa Africa kusini aliwahi kupoteza Uhuru wake kwa muda usiopungua miaka 27 lkn mwisho wa siku nchi yake ilipata Uhuru wa kweli. Mimi nashuri wabunge mupaze sauti zenu ktk kuleta nafuu ya mkwamo huu wa kidemokrasia tunaopitia kuliko kufikiria ubunge, Mandela hakuwa mbunge wakati anaenda gerezani wkt wa revonialtrial.
 
hii kitu imeshapangwa kua sugu apigwe mvua 2 na kuendelea ,baadae anafuatia msigwa,hii yote ni kuua ngome za upinzani,hata kama katiba ikibadilishwa ya miaka 7, kusiwepo na reaction yeyote ,time will tell
Mkuu hili sasa ni wazi pamoja na kuwa wengine tulikuwa tunalikataa hilo sasa 'linakwenda kutimia', 'Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendae hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe, na utakapokwisha kutenda kwa hila. wao watakutenda wewe' (Isaya. 33:1)
 
Chadema walikosea kualisha UKUTA hapo ndo mlipo feri mazima Tungekua Tunaeshimiana Mpaka leo Viongozi wa Upinzani waoga sana
 
Eti uoga? Hizo siasa za majitaka mnazofanya ndizo mnazotaka watanzania wazifuate? Nadhani Godbless J Lema na wenzako wenye tabia kama zako mnapaswa kubadilika na kuelewa ukomo wa kuropoka ropoka ni wapi. Hamuwezi mkaongea vitu bila evidence halafu mkataka muachwe tu. Hizi siasa za chuki mnazotaka kuziita demokrasia hazina nafasi kwa Tanzania. Mambo ya kulishana chuki halafu tuanze kuuana wenyewe hilo halipo. Demokrasia ya kweli ni pamoja na kuheshimu sheria na mamlaka zilizopo. Huwezi kubaki unamchafua mtu mwingine halafu eti ukaita demokrasia. Hayo matukio mnayoyahubiri kila siku kama mna ushahidi wa kutosha kwa nini msipeleke kwenye vyombo husika badala ya kukaa kuyatumia kama agenda ya kisiasa? Hivi kama ni watu mnaofuata sheria iweje mvuruge uchunguzi wa tukio la Lissu halafu mnabaki kupita kwenye majukwaa na kuipaka matope serikali? Lengo lenu ni nini kama siyo kutaka kushinikiza chuki kwa wananchi?
 
Dalili ya mvua ni mawingu. Huyo hakimu ameshaonyesha wazi kabisa kumfunga Sugu. Mimi nilifikiri jaji mkuu angekemea pia hii tabia ya mahakimu kuwaogopa viopngozi wa CCM na kutafuta kila namna ya kuwapendeza. Hakimu huyu nimeshamuona kwamba atajisikia yupo salama sana akimdhalilisha Sugu maana kwa kufanya hivyo ataonekana yupo upande wa mzee na serikali yake. Uliwahi kusikia wapi hakimu anasema sikupi dhamana kwa sababu nataka hii kesi isikilizwe mfululizo.
 
Godbless J Lema,
Narudia kujiuliza, ni kwanini siasa inataka kutugawa watanzania badala ya kutuunganisha? Kama vyama vya upinzani havihitaji pamoja na wabunge wake kwanini visifutwe?? Hii chuki yote ambayo inaonekana kuanza kujengeka ndani ya Taifa letu ni nini hatima ya umoja wetu?? Na wanaoshangilia leo juu ya haya yanayoendea ni nini matamanio yao juu yamustakabali wa nchi yetu?? Eeee mungu wa mbinguni ninakuomba ulitizame taifa lako, utuepushe na nguvu ya chuki, uovu dhidi ya wtu wengine ambayo imeanza kujiinua na kuonekana ndani ya nchi yetu.
Nakumbuka msemo wa Mwl Nyerere...Watanzania ni watu wamoja.
Sioni umoja kwenye haya yanayoendelea, kama unaweza kuwafungulia kesi wabunge wa upinzani zaidi ya 30, na wafuasi wao zaidi ya 150, tumefikia kuwa wawili na sio wamoja tena. kwa sauti ya Lissu.
 
Duuuhh inahuzunisha sana.
Ingawa sio wote waoga lakini majority ni waoga sasa sijui ni elimu au kutojitambua ndio maana watu wanaburuzwa kama man'gombe
Mkuu samaki mmoja akioza hayumkini wote watakuwa wameoza, msigi wa woga tumejengewa toka mashuleni na vyuoni mwetu, hivi sasa mpinzani ni adui, msaliti hafai katika jamii. Haya aliye jasiri na asimame alianzishe nasi tufuate
 
Kama kuna wakati tunapaswa kutafakari hatima ya Nchi yetu ni sasa. Tatizo la msingi ambalo tunapita kama Taifa ni uoga , kwa maoni yangu uoga unaweza kuwa ndio dhambi kubwa na mbaya kuliko zote Duniani , hata hivyo kuwa jasiri ni kuwa na nia ya dhati kabisa ya kusimamia haki na kukataa uonevu....
Kafungwa Luiz Inácio Lula da Silva ndio ije kuwa Sugu? Kama atakutwa na hatia afungwe tu.
 
Siasa hazijawahi kuwa mchezo mwepesi, ina gharama kubwa sana, huwezi kufanya siasa peke yako kama huna watu nyuma yako walio tayari kupita kwenye nyao zako hata ikikubidi kupitia kwenye tanuru la moto. Wanasiasa ni watu wasiokuwa na silaha za moto ila wanaotegemea silaha ya watu walioeleweshwa kipi wafanye wakati gani, wapi na kwanini. Chadema watu hao mnao? au uko kama nyumbu wanaotaka kuvuka mto kutoka Serengeti kwenda Masaimara Kenya? Bila kuwa na watu waliotayari akina Mandela, Nyerere, Jomo Kenyatta, nk wangeuwawa na wakoloni.
 
Kama kweli CDM ni waungwana ni vyema kwanza wangekemea viongozi wao kuporomosha matusi makali bila ya sababu za msingi, inafaa ile clip ya Sugu iwekwe pia humu ili tuone jinsi tulivyo na viongozi wa ajabu. Kama mbunge unaongea matusi, kejeli na uongo na unatetea huo ndio uhuru basi hamna faida yoyote kwa jamii. Uhuru usio na mipaka ni vurugu.

Hakuna hata Kiongozi mmoja wa CDM atakayekemea ujinga aliofanya Sugu, hii inachochea viongozi wengine wa mizuka wa CDM kuja kufanya makosa hayo hayo. Kama wakati ule Lijuakali anawafanyia fujo Polisi hadi kufungwa ingekemewa Sugu asingefikiria kufanya ujinga na yeye. Endeleeni kutetea ujinga ila hakuna mwananchi atakaye ingia barabarani ili kutetea uovu wa Sugu.
Msukuma, Kibajaji wako upinzani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom