Je, Huu ndio mwanzo wa Mwisho wa Barcelona?

Wamepoteza michezo mitatu iliyopita....
Wameondolewa kwenye UEFA champions league...
Wamezidiwa Point nyingi na dalali za kuvuliwa ubingwa wa la liga ni dhahiri...
JE HUU NDIO MWISHO WA BARCELONA??

Ndiyo tafsiri ya ushindani, vinginevyo mantiki ya ushindani itakufa!!!!
 
hakuna aliyechukua ubingwa Wa UEFA Mara mbili mfululizo tangu mashindano haya mapya yaanze, na hakuna timu iliyowahi kuchukua ubingwa kutoka kundi alilokuwa Barcelona hata Mara moja tangu mashindano haya yaanze..
JE HISTORIA INASEMA NA INAWEZA KUTUONGOZA KTK HILOOO????
NEXT SEASON, ingawa bila mabadiliko ktk safu ya mbele na Kocha bila kuachac watu muhimu nje na kumweka Tello mmmh itakuwa bado mpaka abadilishe pale mbele apate TALL STRIKERS

we unasema nini inter milan msimu 2010 alimtoa barca na kuchukua ndoo
 
Hii ndio timu tamu damu na Mkulu wetu wa magogoni, aliialika kuja kuzindua uwanja mpya, dau lao kubwa lilimvunja mbavu hadi akaizila, lakini upenzi hajauacha.
 
Bongo tumezoea Simba na Yanga tu, mpira haukui, ushindani ni wa timu mbili. Ulaya kuchukua ushindi mara mbili mfululizo ni bahati, hakuna mteremko. Barcelona imetolea mkukumkuku na timu inayochechemea liki kuu ya Wabritish. Njomba, unafikiri mchezo nini? Bah!
 
Barca bado ni timu nzuri, ila kwa mechi ya chelsea waliishiwa mbinu ukiachilia mbali habari ya club kutorudia ubingwa misimu miwili consecutive. Kwa ujumla barca huwa anapata shida sn kwa the blues kila wanapokutana. Pia kila xavi na iniesta wanapobanwa wakashindwa kucheza mpira wao wa kawaida mechi hiyo pia inakuwa ngumu kwa messi. Seems mwaka huu unaweza kuwa mzuri kwa CR7 kwa kumpiku messi uchezaji bora.
 
Barcelona wameprove kuwa tactics zao hazina maana, wanashindwa kuifunga timu ya watu 10, wanashindwa kuifunga timu ambayo haina central defenders (baada ya kutolewa Cahil na Terry), wanshindwa kufunga kupitia penati, wanafungwa na mfungaji asiyefunga (Torres)
 
usiseme hivyo mkuu.

waliofurahia ushindi wa Chelsea ni wale wanaoshabikia "voice for voiceless", "power to powerlessness"!
Fikiria mtu kama De-Mateo alikuwa benchi tu na watu wengine wanalipwa mshahara mkubwa zaidi lakini ameweza kubadilisha huo mtazamo. Hiyo ni pamoja na sifa zote zinazoambatana na takwimu chungu mzima lakini kinachocheza mpira sio takwimu mkuu, ni watu na imedhiirika hivyo!
 
Barca hawana plan b,plan-A yao ya kumiliki mpira na kupenetrate ilishindwa kabisa jana coz chelsea walidefend mwanzo mwisho...kifupi ni kwamba walicho onyesha jana ndo mwisho wa uwezo wao..
 
Barca hawana plan b,plan-A yao ya kumiliki mpira na kupenetrate ilishindwa kabisa jana coz chelsea walidefend mwanzo mwisho...kifupi ni kwamba walicho onyesha jana ndo mwisho wa uwezo wao..

Like us Gunnerz (I'm sorry to say this)
 
Nilependa filosofia ya DiMateo , na hasa pale aliposema " we need two perfect performances against barca" , it worked.
 
Wabongo wenye kusikilizia nini watu wengine wamesema ili mkariri na kukirudiarudia mna kazi! Tatizo la Barça kwa sasa ni mabeki wazuri wenye kasi, basi.. Hiyo habari ya Barça kutokuwa na plani b tulianza kuisikia mwaka ule man u walipopaki basi huko Camp Nou halafu wakawatoa kwa goli la Scholes huko OT. Wanaokariri wakaibuka tena mwaka juzi Inter chini ya Mourinho ilipowatoa. Cha ajabu ni kuwa kila Barça inapotolewa ikirudi inarudi na style ileile na inazikandamiza tena vibaya timu pinzani! Wazee wa kukariri tuambieni, ni kweli kuwa timu zitakazopangwa na Barça CL ijayo zitakuwa na mteremko kwa sababu 'tactic zao hazina maana' na 'zama zao zimeisha?' Timu yoyote itakayocheza mfumo wa 10-0-0 na baadaye 9-0-0 lazima itaisumbua timu pinzani hata ikiwa bora kuliko Barça.
 
Tatizo la Barça kwa sasa ni mabeki wazuri wenye kasi, basi.. Hiyo habari ya Barça kutokuwa na plani b tulianza kuisikia mwaka ule man u walipopaki basi huko Camp Nou halafu wakawatoa kwa goli la Scholes huko OT. Wanaokariri wakaibuka tena mwaka juzi Inter chini ya Mourinho ilipowatoa. Cha ajabu ni kuwa kila Barça inapotolewa ikirudi inarudi na style ileile na inazikandamiza tena vibaya timu pinzani! Wazee wa kukariri tuambieni, ni kweli kuwa timu zitakazopangwa na Barça CL ijayo zitakuwa na mteremko kwa sababu 'tactic zao hazina maana' na 'zama zao zimeisha?' Timu yoyote itakayocheza mfumo wa 10-0-0 na baadaye 9-0-0 lazima itaisumbua timu pinzani hata ikiwa bora kuliko Barça.

Mkuu punaine-red. hapo kwenye red hata mimi naona ndio penye tatizo kwa Barca. Ukiangalia goli la pili la Ronaldo siku walipocheza na RM Ronald aliweza kufunga kwa sababu aliwazidi mbio mabeki wa Barca. Na sio kwamba Barca walizembea ku overcome counter attacks za RM.
 
Poleni saaana wana Barca huo ndo mpira unadunda mlishazoea kuwafunga wenzenu safari hii zamu yenyu bana
 
Back
Top Bottom