Elections 2010 Je Dr. Slaa akitupa jalamba, ushindi utakuwepo 2010?

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
140
Ni maswali mengi yayoelea vichwani mwa Watanzania kwa sasa, na bado majibu ni Kitendawili.

(a)Ni nani maarufu kati ya Dr Slaa na Kikwete kwa sasa?

(b) Je ni kweli Dr slaa anafahamika hadi huko kwenye grassroot?

(c) Na kama Watanzania watamuamini Dr slaa, je yawezekana akatusaliti huko mbele?

Kwa kweli hapa vichwa vinauma jamani, sijui tunafanyeje kwa hili
 
ndiyo, ushindi dhidi ya ccm utakuwepo. tatizo ni kwamba hatafanya hivyo...sijui ni kwasababu ya vyeo, au mbowe unajua mimi huwa sielewi ni kitu gani kinamzuia?
 
Mpeni sifa Yesu

Unamaanisha kwamba CCM (Kikwete) atashinda au?
 
ndiyo kikwete atashinda. ila tukimweka Dr.slaa kwenye vyama vya upinzani, kikwete atashindwa....tatizo ni kwamba, Dr.slaa hatakubali kugombea urais, sijui tatizo lake ni nini wakati watu kibao wana tumaini juu yake. au hajiamini?
 
IsayaMwita,

Mwacheni Dr. Slaa aendelee kugombea ubunge huko Karatu maana hana uwezo wa kumshinda Kikwete. Sio kwamba hana sifa au hafai, hapana, tatizo ni chama chake ambacho hakijafika vijijini na pia CCM wakitumia mabavu yao hasa kwa wananchi wa vijijini, itakuwa ngumu sana kwa Dr. Slaa hata kupata asilimia 30 ya kura.

Kuliko kumpoteza huyu mpiganaji, ni bora aendelee kuendeleza mapambano kule bungeni. Ninaamini hata Slaa analijua hilo na kafanya maamuzi mazuri ya kuendelea kubaki bungeni.
 
muheza2007

Ukija Dar niletee Machungwa toka pale segera, ndugu yangu umeongea naye Dr Slaa
 
usipende kusema twafa sema nafa , mwache mzee wa watu akawapiganie wananchi wake wa karatu mageuzi nchini bado kitendawili mifumo ya kusimamia chaguzi haijatulia hivyo upinzani kutangzwa washindi si rahisi . Nenda zako karatu mzee/ laa
 
ashinde kwa kura zipi achana na watanzania wamelogwa na ccm

drphone

Ndugu yangu umekata tamaa sana, tena kwa msomi kama wewe, nadhani uje na alternative hapa tunafanyeje, je tumlilie(tumlazimishe) Dr Slaa asimame na Kikwete?
 
hapana, watz siku hizi wanasikiliza hata radio tu huko vijijini...hivyo wanaelewa namna alivyopambana na ufisadi...wanamjua sana...ccm vijijini watu wanaanza kuikataa kwasababu maisha yanazidi kuwa magumu...vijiwe vya kijijini sasahivi vijana wengi hawataki ccm, na ni wazee wanywa pombe peke yao ndo wanahongwa izo pombe...hivyo kama tukijipanga, kura za ccm vijijini zitapungua sana... anaweza kushinda. kwani akipata kura karibia zote huku mjini kwa watu waliochoka kuonewa, vijijini peke yake unafikiri kutamwangusha? zaidi ya yote, siku hizi kuna simu hadi vijijini, ni swala la watu kupiga tu simu kijijini kumwambia bibi na kina shangazi wasipigie ccm kwasababu ccm inakufanya wewe uliye mjini ukose hela ya kuwatumia kijijini....wataelewa tu...si unajua wanavyopenda pesa za vijana waloko mjini..hahaha.
 
ndiyo kikwete atashinda. ila tukimweka Dr.slaa kwenye vyama vya upinzani, kikwete atashindwa....tatizo ni kwamba, Dr.slaa hatakubali kugombea urais, sijui tatizo lake ni nini wakati watu kibao wana tumaini juu yake. au hajiamini?

Mpeni sifa Yesu

Ndugu yangu huu utabili wako mbona umekuwa haulidhishi, na tena hauna mshiko Mkuu?
 
muheza2007

Ukija Dar niletee Machungwa toka pale segera, ndugu yangu umeongea naye Dr Slaa

Sawa IsaMwita. Ila machungwa yetu yanaoza kwasababu ya kukosa viwanda huku Dar mnanunua juice za kuchanganya madawa kutoka SA.

Hawa CCM wamerogwa sijui ugonjwa gani. Huku Tanga tumebahatika na kiwanda cha maziwa na kinasaidia sana wananchi wafugaji ingawaje bei yao ndio inaua kabisa, lakini nafuu angalau hayaozi majumbani.
 
Ndugu yangu vita yetu ni kuhakikisha tunajikomboa sisi wenyewe, TUMTAFUTE YESU WETU ILI ATUTETEEE, nadhani muheza2007 hapa ndipo tunakosea, hatuna malengo ya siku zinazokuja, kwetu sisi tukila basi tunasahau na kesho.
 
Mpeni sifa Yesu

Ndugu yangu huu utabili wako mbona umekuwa haulidhishi, na tena hauna mshiko Mkuu?

haulidhishi kivipi mkuu, na kivipi hauna mshiko, unamaana watz hawamkubali Dr. au? silaha ya ufisadi ni tosha kabisa kuidondosha ccm kama awareness ikipelekwa vijijini kwa njia za mikutano, kwa njia za vipindi vya radio, kwanjia mbalimbali....na Dr angepita...hivi unafikiri Lipumba kwa mfano mwingine... na usomi wake ule, akama angekuwa anakubalika na watu wengi, si tungeshashinda...lakini watu baadhi wanaogopa ile sera yake ya ngunguli, jino kwa jino na watu wanaoandamana kuwa wengi wao wamevaa kanzu...isingekuwa hivyo, nakwambia ccm ni raisi sana kuing'oa either kwa njia ya CHADEMA au kwa njia ya CUF. siku iyo ipo tena inakuja mbioooo
 
Lakini Mpeni sifa Yesu unanitia shaka sana, vipi kuhusu wewe, Mama yako , baba yako, na pia wadogo zako wanauwelewa juu ya kupiga kula?
 
Labda jambo lisilofahamika ni kuwa watanzania hawamchagui mtu kwa umaarufu. Pia, matokeo ya washindi kwenye uchaguzi ambayo yanatangazwa si lazima yawe yanayotokana na kura zilizopigwa. Therefore, there is no way Slaa anaweza kumsinda Kikwete, especially kwa uchaguzi wa mwaka huu
 
Mpita Njia

Mpita Njia kama jina lako lilivyo, inawezekana kuwa sisi watanzania hatumchagui mtu kwa umaarufu, ila hapa tunataka Mtu bora na si umaarufu Mpita Njia.
 
usipende kusema twafa sema nafa , mwache mzee wa watu akawapiganie wananchi wake wa karatu mageuzi nchini bado kitendawili mifumo ya kusimamia chaguzi haijatulia hivyo upinzani kutangzwa washindi si rahisi . Nenda zako karatu mzee/ laa

superfisadi,

Ama kweli Tanzania ina watu wa ajabu sanaa..., sielewi watu hawa waoga, awsiojiamini ni nani kawazaa...., superfisadi; sisi hatupigani na kivuli chao, tunapigana na physicacal body, Tazama kama Dr Slaa akiendelea kuwa wa Karatu basi ni nani mtetezi wetu?

Ama tumpe Lipumba
?

Sote tunajua hii ni mara ya Pili Lipumba anagaragazwa, sasa safari hii hata kama tutampa kura zetu ni bure ndugu yangu.

unaposema mageuzi nchini bado kitendawili mifumo, unadhani kuna siku tutaamka tukute tayari imerekebishwa?
Nadhani kuna kila sababu ya kumpata au kuendelea kumshauri Dr slaa asimame,
 
Dr. Slaa hawezi kushinda ikiwa wewe na wengine wote hamtampa kura zenu...Lakini Chadema na Dr.Slaa kama chama watakuwa wametimiza wajibu wao kumsimamisha mtu ambaye anaweza kuweka upinzani na kuiongoza nchi kwa sababu nyingi za msingi.

Dr.Slaa anazo sifa za - Opposition Leadership ambazo huanza na Tabia kuwa ni pamoja na 1. stubbornness na disagreeableness pale pasipokuwa na haki pasipo kupoteza loyalty to his superior.
2. He is Visionary na assertiveness 3. Tender minded - with great concern for the less fortunate 4. Hardworking na persistent 5. Open minded 6. Attentive to his emotions 7. Imaginative 8. Exceptional ability to tolerate stress and adversity, and many many more one can think of....

Yote haya tumeyaona hapa JF..Mungu atupe nini zaidi jamani, gunia la chawa?
Mtu yeyote mgombea aliyeshindwa kusimama na kuukosoa Utawala wenye mapungufu au makosa ya wazi hawezi kuwa Great President. Sii swala la sisi kujiuliza umaarufu wake auanaweza kutuongoza ila sisi kumuomba mtu huyu asimame dhidi ya JK kwa sababu tunamhitaji. Na hata kama atashindwa uchaguzi mkuu bado atakuwa ametimiza wajibu wake mkubwa tokana na sifa alizokuwa nazo, kazi itakuwa kwetu sisi WAJINGA sio yeye tena..

.
 
Mkandara;

Sijajua hebu akiukosa Urais anaweza kuteuliwa kuingia bungeni?

Mkandara; nauliza hivyo ili kuwa na tahadhari ama wewe hilo unalionaje?
 
Back
Top Bottom