Je, DOWANS wameshalipwa?

Mi nadhan malipo yalifanywa kipindi kile cha babu wa loliondo ilpopamba moto. Ndo alikuwa man of the moment na serikali nzima na vyombo vyote vya habari vikahamia huko. Taarifa zinasema lilikuwa lengo maalum la magamba ili wananchi tusikumbuke Dowans na wakalipa kipindi hicho.

Pia siamini kama RA angekubali kujivua gamba kabla hajachukua mpunga wake wa Dowans
 
Mbunge wangu kokote uliko, tafadhali ninaomba ktk maswali yapapo kwa papo kwa PM, fuatilia sakata hili.
 
Wah. Zitto Kabwe & John Mnyika najua mpo kwenye hii forum, tupeni majibu sahihi juu ya hili.
Najua Nape ana majibu ila naogopa atayachakachua
 
Tusimuhukumu EL peke yake kwenye hili, mi nafikiri Samwel Sita, na Bwana Shelukindo walipe hizi hela wao ndo waliokomaa wakati ni wanasheria, sometimes waTZ tunakuwa mashabiki zaidi kuliko kuangalia uhalisia, Zito aliposema mitambo safi tuinunue watu wakasema keshanunuliwa, sioni chembe ya sababu ya kulalamika, wajinga ndo waliwao waliotuingiza mkenge kina Sita kuhusu hili la Dawans wasimung'unye maneno. Hawa ndo wametulipisha hizi hela, watu wanaenda mahakamani we unaenda kanisani kulaani mafisadi unaandikwa kwenye magezeti na hayo magazeti tunasoma halafu tunafungia maandazi, wenzetu wanakomaa mahamani na kuchukua chao.
 
Back
Top Bottom