Je, Bunge litamfukuza Zitto kwa "kutokuhudhuria" vikao; hasaini kupokea posho!?

Wakuu,

Wala sina mpango wa kubadili headline kwa sababu wanaokumbuka akiwemo Zittto mwenyewe wanajua kuwa niko sahihi kabisa!

Sakata la kufukuzwa Zitto Kabwe linaanzia kwa msimamo wake binafsi aliouanzisha bungeni. Yeye hakutaka kuzama zaidi kwenye malumbano ya kwamba ama posho ni sahihi au si sahihi. Zitto aliamua kukataa kuchukua posho ile.

Mtego uliotaka kumnasa Zitto ni ule utaratibu kwamba attendance form ndiyo inayotumika kulipa wabunge posho zao (seating allowances).

Bado hili halikuwa kikwazo kwa Zitto na mwishowe akaamua kuacha kusaini kabisa forms hizo ili kukwepa kuingizwa katika list ya wachukua posho.

Spika Anne Makinda alikuja na kauli kwamba kwa attendance form ndiyo ushahidi wa mhudhurio ya mbunge basi Zitto akikosekana mara tatu basi atakuwa amejifukuza ubunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Ni kweli Katiba ya nchi Ibara ya 71(1)(c) inasema hivi:

Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika

Sijasikia Anne Makinda au bunge zima likisema limeacha kutimiza mpango wa kumfukuza Zitto ubunge. Hivyo, binafsi nimekuwa nikifanya countdown na hatimaye muda uumefika.

Zitto alianza kuacha kusaini mahudhurio kwenye Session/Mkutano wa NNE. Mkutano wa SITA unaanza Tuesday, January 31, 2012. Matokeo yake ni nini?

Matokeo yake ni kwamba siku bunge linaahirishwa basi Zitto Kabwe atakuwa amekamilisha MIKUTANO MITATU huku karatasi ya mahudhuriao haionyeshi jina lake!

Kama alivyoeleza Spika, basi Spika huyohuyo Anne Makinda itabidi atimize kauli yake kutekeleza kifungu cha katiba kinachomtaka Zitto afukuzwe ubunge.

Sijajua bunge linaloanza wiki ijayo litaisha lini. Lakini tunatarajia kuwa saa ya kuliahirisha yaani kuuahirisha MKUTANO WA SITA basi ndiyo saa ya kutangaziwa pia kufukuzwa kwa Zitto kabwe ubunge wake.

Hatuhitaji kujua Makinda atatumia ushahidi gani wakati yeye mwenyewe alinukuliwa akifafanua kuwa kutosaini attendance form kunamfanya Zitto mbunge yeyote akabiliwe na adhabu ya kufukuzwa ubunge.

Nafahamu kuwa kuna thread humu Zitto mwenyewe alieleza kwamba process ya kumfukuza anataka aone itakuwaje, kwa sababu ni kweli attendance forms hajazi lakini TV zinamuonyesha yumo bungeni, hansard zinamuonyesha anashiriki vikao.

Je, wadau mna la kuongeza?

Wasalaam.

Hivi kama hakusaini lakini akaongea hansard si itaonyesha kuwa alikuwemo kwenye session!
 
Hakuna wa kumfukuza Zitto! Wanamwogopa! Walilazimishwa na Mh Rais wamchague Zitto kuwa M/kiti wa kamati ya bunge! Watakuwa wanamfanya mkuu wao punguani!! Hawawezi maana pia wanafaidika na uwepo wa Zitto pale!
 
Sheria,utaratibu,kanuni n.k. zinawekwa kwa kuzingatia mantiki yaani logic hivyo hapa sio suala la kusaini au kutosaini kwenye kitabu cha mahudhurio au cha malipo bali ni kutekeleza wajibu wa kibunge kuzingatia wakati na mahali palipopangwa.
 
Hivi kama hakusaini lakini akaongea hansard si itaonyesha kuwa alikuwemo kwenye session!

Mwanamayu,

Hata mimi nimeshindwa kujua kinachojadiliwa hapa. Zitto ni mchangiaji mahiri wa hoja bungeni, na hansard hurekodi kila kitu, sasa mjadala wa kufukuzwa kwake kwa kukataa kusaini mahudhurio sijui hata unaanzia wapi. Utaratibu ule uliwekwa kuwadhibiti wabunge ambao ilidhihirika kuwa lengo lao ilikuwa kujipatia posho tu na si wabunge aina ya Zitto. Hadi anakufa, Sumari hakuhudhuria vikao zaidi ya vitatu mfululizo, labda tujadili kwa nini sheria haikufuatwa kumfukuza Sumari? Tukizingatia kuwa tunapaswa kufuata utawala wa kisheria.
 
Labda twende mbali kusaini attendance forms ni kuna nguvu kisheria? Maana sheria iliyotajwa hapo juu iko silent as to whether signing the respective forms is just only a proof kuwa mbunge kahudhuria. Ni changamoto kati ya mambo ambayo Watazania kokote walipo na hasa walioshika nyadhifa mbalimbali wanatakiwa kuangalia baadhi ya taratibu zilizokaa kama mchezo wa kuigiza au ushirikina na kuzihoji na hatimaye kuzibadilisha.

Halafu na wenye madaraka wanatakiwa wakomae na watoe nafasi kwa wanaowaongoza wakomae. Hivi mtu anayefikia kupata wadhifa wa ubunge na akawa na diplomatic passport, akaapa kwa misaafu na katiba mtamwekea vikwazo mithili ya mwanafunzi wa chekechea? Kama kuna mbunge ambaye anakacha kuhudhuria bila sababu ya msingi basi hajui wajibu wake. Na ili abadilishwe apewe semina elekezi na ushauri wa kitaalamu ili aelewe wajibu wake. Ikishidikana mshitaki katika mahakama ya umma-wananchi waliomchagua wamkatae na wachague wajumbe wengine. Hivyo kufikiri kumfukuza Mh.Zitto kwa kutosaini form na hali anahudhuria na anachangia na hana sifa ya kusinzia na kukoroma bungeni itakuwa ni Makinda hypothesis
 
mkutano wa tano zitto hakuhudhuria alikuwa india, kwa hyo kifungu hicho kitaanza kutumika ktk mkutano wa saba
 
mbona wote mnaochangia sijawahi kuona majina yenu!???

Kweli hii ya leo kali, manake mpk wewe mwenyewe sijawahi kukuona.

Tukirudi kwenye mada, Zitto hajakiuka kifungu chochote cha katiba. Ukisoma vizuri hicho kipengele cha katiba, utaona kuwa kimesema mbunge atapoteza wadhifa wake kama hatahudhuria vikao na sio kama hatosaini karatasi la mahudhurio.
 
mkutano wa tano zitto hakuhudhuria alikuwa india, kwa hyo kifungu hicho kitaanza kutumika ktk mkutano wa saba

Mkuu Gwota,

Mimi kama mleta mada nakiri kwamba hili jibu lako ni moja ya majibu yanayoifanya JF ijulikane kama Think Tank.
Jibu fupi, straightforward. Nilisahau kuwa Zitto alikuwa India kipindi kilichopita.

Mkuu saluti mara mia and Keep it up JF!
 
Wakuu, I salute you,

Nilileta thread nikirejea jinsi inavyowezekana Mh. Zitto Kabwe akafukuzwa ubunge wake mara mkutano wa bunge uanzao wiki ijayo utakapoahirishwa.

kwa urahisi waweza kuirejea thread hiyo hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...okuhudhuria-vikao;-hasaini-kupokea-posho.html

Mmechangia kama kawaida yetu na wengine wengi zaidi ya 1,000 wamesoma thread hii. Great.

Kumewahi kuwa na hoja kwamba waandishi wa Tanzania wanaitumia JF kama source. Baadhi ikaelezwa kuwa hili si tatizo japo wengine hawaonyeshi appreciation kwamba JF ndiyo source ya habari zao ambazo zinanunulika.

Sikushangaza thread hii kutoka kwenye magazeti. Magazeti ya leo yaani HABARI LEO na THE AFRICAN wametoa kama nilivyo-post humu.

HABARI LEO wametumia maneno "mdadisi au wadadisi " kila waliponukuu . sina matatizo na hili kama tunaleta hapa thread halafu tunaitwa wadadisi, ni kweli sisi ni wadadisi na tunastahili sifa hiyo. Sasa sijui kwa nini mwandishi wa HABARI LEO asiitaje Jamii Forum kama moja ya chanzo, maana asilimia kubwa ya wanavyosema hao wadadisi wake ni kilekile nilichosema kwenye thread ile.

Pamoja na hayo sina tatizo sana na hao HABARI LEO kwa hiyo intended or inadvertent overlook. Shida yangu kuu ni jinsi THE AFRICAN walivyoiandika. THE AFRICAN wamekopi vilevile lakini kilichonishangaza ni wao kutoitaja kabisa JAMII FORUM na badala yake wanataja kwamba imejadiliwa na "WANABIDII FORUM" .

Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba msomaji asiyeijua JAMII au WANABIDII basi kwa kusoma gazeti hili anapata akili kwamba kumbe WANABIDII kumefurika vichwa vinavyjua kufikiri hata kama mwanzoni alikuwa anapuuzia Social media. Kwa namna moja WANABIDII imepigiwa marketing or campaign stratergy na JAMII FORUM tulioleta post hii tusiposhtuka bai sifa zetu zitaenda kusiko.

Nimeleta thread hii ili wenzagu tuione concern hii na tunaweza kupata mawazo zaidi ya kupambana na hali hii.

Sina upenzi wa kudumu wa chama chochote. Lakini ni mara nyingi JF imekuwa ikibezwa kuwa ni "mtandao wa CHADEMA". Moderators wanajua zaidi walivyohangaika kukanusha hilo na baadhi humu mkafikia kutaja majina ya wana CCM wengi tu waliomo humu, tena long living members.

Sijui mmilikia wa HABARI LEO lakini hasa THE AFRICAN ni watu gani na wana muelekeo gani. Lakini nawasihi tuwe macho na jinsi magazeti yanavyohabarisha kuhusu JF kwa kuiponda lakini vilevile zinapotoka brilliant posts unashtukia magazeti hayoayo yanaikopi post nzima tena front paga lakini yanataja mtandao mwingine kabisa.

African The-01.jpg Habari Leo-01.jpg
 

Attachments

  • African The-03.jpg
    African The-03.jpg
    93.3 KB · Views: 521
  • African The-02.jpg
    African The-02.jpg
    87.2 KB · Views: 532
  • Habari Leo-02.jpg
    Habari Leo-02.jpg
    356.1 KB · Views: 551
...mkuu waandishi wa habari tulionao hapa nchini ni wataalam wa ku-copy na ku-paste,mi ndo maana lishaamua JF kuwa chanzo changu cha chabari tena naiamini sana JF coz habari zinazo patikana hapa zinakuwa bado hazija chakachuliwa kama za magezetin zinavyofanyiwa usani na hao wapoke basha za kaki.Huo uhuni unaofanywa na hao waadishi uchwala wa magazeti,wa ku-copy leo JF na ku-paste kesho kwenye magezeti yao usikukatishe tamaa mkuu(SubiriJibu)...
 
ni magazeti machache sana ambayo huwa naweza nikanunua, nikakaa chini na kusoma. waandishi wahabari wa tz wanauwenda wazimu vichwani mwao.
 
Hili suala la waandishi kuja kuiba story humu na kwenda kuzipaste kwenye magazeti yao mimi nalipinha kwa nguvu zote cuz linacreate uvivu kwenye newz room,jamaa watakua wanalipwa mishahara ya bure kwa kazi zinazofanywa na watu wengine,waache uvivu waumizwe vichwa,walichagua kuwa waandishi wao wenyewe mbaya zaidi hata magazeti yanayojiita ya uchunguzi wa kina kama mwanahalisi nao wameanza kamchezo hako ka kuja kukwiba story humu,mfano ni ile story ya zitto kumshauri au kumsuta jussa na cuf kuhusu suala la mpiganaji Hamad Rashid na wenzake kufukuzwa CUF..
 
Hili suala la waandishi kuja kuiba story humu na kwenda kuzipaste kwenye magazeti yao mimi nalipinha kwa nguvu zote cuz linacreate uvivu kwenye newz room,jamaa watakua wanalipwa mishahara ya bure kwa kazi zinazofanywa na watu wengine,waache uvivu waumizwe vichwa,walichagua kuwa waandishi wao wenyewe mbaya zaidi hata magazeti yanayojiita ya uchunguzi wa kina kama mwanahalisi nao wameanza kamchezo hako ka kuja kukwiba story humu,mfano ni ile story ya zitto kumshauri au kumsuta jussa na cuf kuhusu suala la mpiganaji Hamad Rashid na wenzake kufukuzwa CUF..

Unaweza kuwa sahihi juu ya uvivu (kwa baadhi yao), lakini huwezi kueteta plagiarism aisee...Mwanahalisi walitoa credit kwa sources zote, kuanzia facebook mpaka hapa JF sasa huwzi kuwafananisha katika hilo na hao ambao ama hawataji kabisa vyanzo au wanataja vyanzo ambavyo si sahihi! Maana hata hiyo ya huko Wanabidii si ilianzia hapa?
 
Back
Top Bottom