SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
Wakuu,
Wala sina mpango wa kubadili headline kwa sababu wanaokumbuka akiwemo Zittto mwenyewe wanajua kuwa niko sahihi kabisa!
Sakata la kufukuzwa Zitto Kabwe linaanzia kwa msimamo wake binafsi aliouanzisha bungeni. Yeye hakutaka kuzama zaidi kwenye malumbano ya kwamba ama posho ni sahihi au si sahihi. Zitto aliamua kukataa kuchukua posho ile.
Mtego uliotaka kumnasa Zitto ni ule utaratibu kwamba attendance form ndiyo inayotumika kulipa wabunge posho zao (seating allowances).
Bado hili halikuwa kikwazo kwa Zitto na mwishowe akaamua kuacha kusaini kabisa forms hizo ili kukwepa kuingizwa katika list ya wachukua posho.
Spika Anne Makinda alikuja na kauli kwamba kwa attendance form ndiyo ushahidi wa mhudhurio ya mbunge basi Zitto akikosekana mara tatu basi atakuwa amejifukuza ubunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Ni kweli Katiba ya nchi Ibara ya 71(1)(c) inasema hivi:
Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika
Sijasikia Anne Makinda au bunge zima likisema limeacha kutimiza mpango wa kumfukuza Zitto ubunge. Hivyo, binafsi nimekuwa nikifanya countdown na hatimaye muda uumefika.
Zitto alianza kuacha kusaini mahudhurio kwenye Session/Mkutano wa NNE. Mkutano wa SITA unaanza Tuesday, January 31, 2012. Matokeo yake ni nini?
Matokeo yake ni kwamba siku bunge linaahirishwa basi Zitto Kabwe atakuwa amekamilisha MIKUTANO MITATU huku karatasi ya mahudhuriao haionyeshi jina lake!
Kama alivyoeleza Spika, basi Spika huyohuyo Anne Makinda itabidi atimize kauli yake kutekeleza kifungu cha katiba kinachomtaka Zitto afukuzwe ubunge.
Sijajua bunge linaloanza wiki ijayo litaisha lini. Lakini tunatarajia kuwa saa ya kuliahirisha yaani kuuahirisha MKUTANO WA SITA basi ndiyo saa ya kutangaziwa pia kufukuzwa kwa Zitto kabwe ubunge wake.
Hatuhitaji kujua Makinda atatumia ushahidi gani wakati yeye mwenyewe alinukuliwa akifafanua kuwa kutosaini attendance form kunamfanya Zitto mbunge yeyote akabiliwe na adhabu ya kufukuzwa ubunge.
Nafahamu kuwa kuna thread humu Zitto mwenyewe alieleza kwamba process ya kumfukuza anataka aone itakuwaje, kwa sababu ni kweli attendance forms hajazi lakini TV zinamuonyesha yumo bungeni, hansard zinamuonyesha anashiriki vikao.
Je, wadau mna la kuongeza?
Wasalaam.