Je, Bandari ya Bagamoyo na uwanja wa ndege wa Msalato ni miradi isiyo na faida?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
Tanzania tumejariwa utajiri wa rasilimali madini,gesi asilia na mafuta,utajiri huu ni kinyume na maisha halisi ya wananchi wa Tanzania, nje ya mipaka ya Tanzania kuna soko kubwa la bidhaa mbali mbali zinazozalishwa nchini, tunahitaji uwanja wa kimataifa kwenye mji mkuu wa nchi ili kuweza kufanya biashara za kimataifa, tunahitaji bandari ya Bagamoyo ili kuongeza ufanisi na pato la Taifa,kadiri nchi yetu inavyoendelea kufanya biashara za kimataifa tunahitaji miundo mbinu ya uhakika kuweza kuaccomodate biashara za kimataifa, kuhusu bandari ya Bagamoyo.

Watanzania hawajui kuhusu China Merchant, wanachojua ni kuwa Mkataba ulikuwa na masharti mabovu, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA aliyeondolewa na kwa taarifa ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano,Hayati Rais John Magufuli,masharti ya fedha na ujenzi wa mradi ndio jicho la Watanzania lilipo, key angle ya Watanzania sio nani anajenga huo Mradi,tunaweza kujenga kwa uadilifu na discipline kubwa ya matumizi ya kodi za Watanzania.

-Kwa nini viwanja vyetu vya ndege vinatumika chini ya 20%

Tanzania tumejaaliwa bidhaa zote ambazo zinahitajika kwa wingi duniani kuna non perishable goods

Baobab Fruit Powder (unga wa ubuyu)

Green cardamom (iliki za kijani)

Yellow maize (mahindi ya njano)

Chickpeas (njugu mawe)

Sunflower seeds ( mbegu za alizeti)

Organic soybean meal

Peanuts

Red kidney beans

Dried green peas

Red skinned peanut

Pine wood shavings

Cashew nuts

Tamarind

Dried ginger

Wheat

Sesame seeds

Raw honey

Cotton yarn

Rasilimali Maji iliyopo Tanzania kwa ajili ya kilimo.

1. Ziwa Victoria ambalo linakwenda kumwaga maji katika mto Nile na kuhudumia nchi ya Kenya,Uganda na Misri huku Tanzania ikiwa hakuna inachofaidika nalo hususani kwenye kilimo.

2. Mto Ruvu

3. Mto Wami

4.Mto Pangani

5. Mto Rufiji

6. Ziwa Tanganyika

7. Ziwa Nyasa.

8. Ziwa Manyara.

9. Ziwa Eyasi

10. Ziwa Rukwa

-Rasilimali Samaki

Eneo la uvuvi la bahari ya Hindi, kilomita 223,000, Nile perch, Sardines, prawns ambao wanapatikana kwa wingi na wamekuwa wakisafirishwa ikiweza kuchangia 1.6% GDP kama juhudi ikifanyika tunaweza kufanya rasilimali samaki wakachangia 30% GDP na kutengeneza ajira kwa asilimia 30%.

-Aina ya Samaki wa kuuza nje ya nchi.

1. Nile perch(Lates niloticus)

2. Tilapia(Oreochromis niloticus)

3. Dagaa (Lake Sardine) Rastrineobola argentea wanaopatikana Ziwa Victoria.

-Samaki wa Ziwa Tanganyika.

1.Dagaa (Stolothrissa tanganicae and limnothrissa miodon)

2.L.Stappersii, L.Marie na L.Microlepis.

-Samaki wa Ziwa Nyasa

1.Tilapia

2.Haplochromis spp

3.Lake Sardines Engraulicypris sardella.

Kwa makisio Serikali inaweza kuvuna tani 730,000 za samaki kutoka Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, makisio yakiitoa EEZ ambayo haijafikiwa kiuvuvi.

Rasilimali ya dhahabu, almasi, tanzanite, ruby, rhodolite, sapphire, emerald, amethyst, chrysoprase, peridot, tormaline, chrysoberyl, spunels, garnets, zircons, coal, uranium, soda, kaolin, tin, gypsum, phosphate, rasilimali hizi zote zinazomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 zinahitaji uwanja wa ndege mkubwa kama wa unaotarajiwa kujengwa msalato na bandari ya kisasa kama inayotarajiwa kujengwa Bagamoyo.

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya viwanda ambavyo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipenda aivushe nchi yetu iwe na uchumi wa kujitegemea bila kuwa ombaomba,hatukuwa na Bandari ya Bagamoyo wala Uwanja wa ndege wa Msalato lakini sasa tunakwenda kuwa navyo,

1. Tanganyika packers - usindikaji, upakiaji na usambazaji wa nyama ya ng'ombe. Kiwanda hiki kilikuwa kawe na kingine kule mkoni Shinganya.

2. Urafiki,Mwatex Kilitex,Mutex, Polytex,Polystee- Nguo, vitenge

3. Morogoro Canvas - Magunia na maturubai

4. Morogoro shoes- Viatu

5. Morogoro Tannerie- Ngozi

6. Mwanza Tanneries- Ngozi

7. Bora Shoes- Utengenezaji wa viatu

8. Kibo match- Viberiti

9. National, Matsushita, Philips- Utengenezaji wa batteries, radio na radio cassete.

10. Pamba Engineering- Uchongaji wa vipuri vya mashine za uchambuaji pamba.

11. SIDO - Shirika la kuhudumia viwanda vidogo

12. Kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara

13. Viwanda vya kusindika na kubangua , Kahawa, Alizeti, Pareto, Karanga na Miwa.

14. Kiwanda cha vipuri vya mashine cha Mang'ula

15. Kiwanda cha vipuri za mashine cha Kilimanjaro

16. Kiwanda cha malori (kuunda mabasi na malori) cha Scania

17. Kiwanda cha magari cha Nyumbu cha jeshi Kibaha

18. Tanalec- kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme.

19. Kiwanda cha karatasi cha Mgororo Mufindi mkoani Iringa.

20. Kiwanda cha kusindika na kusambaza maziwa cha Utegi mkoani Mara.

21. Kiwanda cha usindikaji wa nafaka cha National Milling Corporation cha Dar-es-Salaam

22. Tanga Steel Rolling Mill- vyuma, saruji na mabati.

23. Viwanda vya saruji vya Tembo Cement, Twiga Cement, Simba Cement pamoja na vile vya ALAF na GALCO.

24. Kiwanda cha zana za kilimo - UFI

25. Kiwanda cha madawa ya binadamu cha KPC - Keko Pharmaceutical Company.

26. Viwanda vya Bia vya Dar, Ndovu na Pilsner Arusha

27. Kiwanda cha Mvinyo Dodoma

27. Kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha

28. Kiwanda cha katani cha Amboni mkoani Tanga.

29. TIPER - kiwanda cha kusafisha mafuta machafu, kusambaza mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa

-Bandari ya Bagamoyo na Uwanja wa ndege wa Msalato ni vichocheo vya Uchumi wa Tanzania.

Kuna mambo mengi yakufanya nchi hii ambayo ukiyafanya yanachochea vingine.

Mfano 1.Waziri wa Nishati alisema bungeni njia za umeme nyingi zimechakaa kiasi cha kushindwa kusafirisha umeme mkubwa,kama hii ni kweli, tunapaswa kufanya ukarabati wa njia hizi ili Bwawa la Umeme la Rufiji ikiisha tuweze kusafirisha umeme tutakaozalisha vinginevyo na wenyewe utakuwa white elephant project kwa sababu umeme hautawafikia Wananchi.

Mfano 2.Tunapitia kipindi cha nishati ya mafuta kuwa ghali,tunayo gesi asilia tayari na ipo ya kutosha. Kwa nini tusiviwezeshe karakana za UDSM, UDOM, DIT,Arusha Technical na za VETA kuweza kufunga mifumo ya gesi asilia kwenye magari na majumbani Ili kujinasua na extensive fuel importation costs? Vinginevyo na hii gesi ya Mtwara ni White elephant kwa sababu haimfikii mwananchi.

Mfano 3.Tuna shida kubwa sana ya upatikanaji wa Maji kwenye wilaya nyingi mno,hali ni mbaya zamani ilikuwa uko Hanang, Monduli, n.k.lakini leo hii maji tatizo hadi Dar es Salaam,tukichimba visima tutawafanya wananchi wapate maji safi na salama ambayo kwa kiasi kikubwa yatapunguza gharama za madawa na vifaa tiba kwa magonjwa yatokanayo na utumiaji Maji yasio salama,lakini pia mifugo itapata Maji hivyo kuinua per capita income ya wafugaji,lakini tukiamua kuchimba visima vikubwa tunaweza kutumia maji kwa umwagiliaji Ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini, vinginevyo miradi yote ya maji iliyogharimu mabilioni ya pesa Tanzania nayo ni white elephant kwa sababu miradi yote inasubiri mvua zinyeshe.

Kwa kumnukuu Rais wa Awamu ya tano,Hayati Rais John Magufuli,Tuchague vyema cha kufanya hatuna mjomba wa kutusaidia*Mchina au Mzungu *hawezi kukuchagulia kitu kitakachokunasua kwenye umasikini,tuchague kimkakati bora,tuchague mipango bora itakayoturudisha tena uchumi wa kati,tatizo lilikuwa China Merchants Group..sasa hawapo watanzania wana Amani hawataki ya Sri lanka yatokee Tanzania,Bora kuchukua mikopo na kujenga wenyewe kuliko kuleta wawekezaji wanachukua documents za miradi kisha wanaenda kukopa wao na wanakuja kuwekeza baada ya kuchukua mikopo bora tukope na kujenga wenyewe
Kuliko mwekezaji kwenda kukopa yeye kisha kuja kujenga na mradi kuwa mradi wake binafsi,Jambo la kufurahisha ni kwamba hadi sasa 100 % ni TPA hakuna tena wale toleo jipya la wachina la China Merchant Group waliokuwa wanataka kutufanya kama walivyofanya Djibouti Sierra Leone SRI LANKA na kwingineko duniani ni vizuri serikali kuhakikisha kuwa kama ilivyo kwenye SGR basi na Bandari ya Bagamoyo 100 % Umiliki ni Tanzania

Utakubaliana nami ndugu msomaji kuwa utajiri tulio nao hauendani na kiwango cha maendeleo ya nchi yetu,nia ni kujipa changamoto za kitaaluma na kufanya uchambuzi na tathmini ni nini kifanyike kama ni kujenga miundo mbinu iliyo bora ikiwamo Bandari ya Bagamoyo na Uwanja wa ndege wa Msalato,Maoni yangu ni kuwa tukifanikiwa kufanya hivyo basi mabadiliko ya kweli yanawezekana,ni wazi fikra za watanzania tulio wengi zinahitaji kubadilika na kuwa katika mtazamo chanya,jitihada kubwa sana inatakiwa kufanywa na viongozi wenye dhamana kulitambua hili na kulifanyia kazi kwa vitendo badala ya nadharia, uchumi wetu tumeukalia pengine shida yetu kubwa ni akili, exposure,kama tuna akili na tumesoma na nchi yetu inaendelea kuwa masikini basi asilimia themanini ya wasomi wana vyeti feki, Watanzania tuamke.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Bandari ya Bagamoyo ijengwe tu. Lakini daraja la Busisi, makao makuu Dodoma na uwanja wa ndege Msalato hapana visitishwe.
 
Bado mambo ya ukakasi kwa kweli na pia pangekuwa na petition ...Ushiriki wa watu mfano ijengwe basi pawe na sababu ila naona bado Kuna mushkeri....kwa mantiki kubwa mi natambua bandari iko hatua ya kuanza kilichopo sasa kupata hizo pesa ila ni swala lipo kabisa katika hatua ya awali..

Ooh !! Nchi yetu Haina taasisi kamil Bali ni mfumo wa mtu Lin tutaendelea ,akija huyu ana yake anaanza upya yule ana yake kwa nn ivi...better watu wakakubaliana yote kama ni uwakika basi mkataba upelekwe hata bungeni ila bado ...Tatizo ni sugu kila mradi naona unafaa ukipewa hints zake kadhaa ishu ni vile je unapewa kipaumbele ...maana shida ni kila mhali Kuna mahitaji ...


Naona hata ishu ya stendi ya Arusha jiji bado watu washarukia huku yaani balaa juu ya balaa kwa nn tusipende moja baada ya moja
 
Uwanja wa ndege Msalato Dodoma haukwepeki. Unataka wageni waje Dar kisha wapande ndege ndogo hadi uwanja wa Area C?
 
Ni wakati wa kuimarisha viwanja vilivyopo tuache upendeleo watu wataisha kwa ajali hasa viwanja vya kando ya maziwa.
 
Msalato airport mahitaji yake ni miaka 30 ijayo, bandari ya Bagamoyo inahitajia kuanzia juzi
 
Back
Top Bottom