Kwanini mahakama zetu bado zina kigugumizi kuandika hukumu za wananchi kwa lugha ya kiswahili?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
Pamoja na Jitihada za Bunge letu kubadili sheria zinazo husiana na taratibu za utoaji haki lakini mpaka leo bado haki za wananchi zinaandikwa kwa lugha ya kigeni na kusomwa kwa lugha ya Taifa!!!

Isipokuwa Mahakama za mwanzo tu, ukienda mahakama za wilaya ha mahakama kuu, lugha za uandishi wa haki za watqnzania ni kiongereza tu!!!!

Ukitembelea kwenye tovuti inayo hifadhi kesi mbalimbali zikizo amuliwa yaani Taazilii hukumu zote zimeandikwa kwa kiingereza!!! Sasa lengo la mahakama kufanya hivyo ni nini?!! hivi kweli tunawajali wananchi?!!

Kwanini thamani ya lugha ya kiswahili inapuuzwa katika kutoa haki za wananchi?!!

Kweli hadi leo bado tunaishi kwenye fikira za kitumwa kwa kiwango hiki? tunakumbatia lugha ya kiingereza na kupuuza lugha yetu?!!!

Mbona Bunge letu tukufu linaendesha shughuli zake kwa lugha yetu ya taifa na sisi wananchi tunafuatilia mambo mbalimbali na tunaelewa, kwanini mahakama iwe kivyake?!!!

Ama suala hili la matumizi ya kiswahili nalo linasubiria Katiba mpya?!!!

Kwanini haki zinazo wahusu watanzania hadi leo zinaendelea kuandikwa kwa lugha ya kigeni wakati asilimia 99 ya watanzania wanazungumza na kukielewa kiswahili??!! Kuna siri gani imejificha kwenye jambo hili?!!

Tunataka kujua ni Mahakama ndio haitaki au Serikali?!!

Tunamuomba waziri wetu wa Katiba na Sheria Dr. PINDI CHANA afuatilie jambo hili kwa masilahi ya wananchi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom