Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Waziri wa Nishati, January Makamba amelaani tabia za baadhi ya wanasiasa wanaodai kwamba Mwenge wa Uhuru umepitwa na wakati na ni mzigo kwa Taifa.
Makamba akipinga hoja hiyo amesema Mwenge ni tunu na nembo ya Taifa ambayo inapaswa kuheshimiwa hivyo, kusema kuwa unasumbua wananchi ni kuitusi nchi.
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ameitoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 14, 2023 katika Jimbo lake baada ya Mwenge kukimbizwa kwenye jimbo hilo na kuzindua na kukagua miradi tisa yenye thamani ya Sh779.1 milioni.
"Mwenge ni tunu na heshima kubwa kwa Taifa letu, tukiwa na mawazo na mtazamo kuwa hauna maana ni sawa na kuitusi nchi yetu. Wakati tunapata Uhuru hotuba ya kwanza ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alisema sasa tunawasha Mwenge ili uangaze nchi nzima," amesema.
Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ni kielelezo cha uhuru, utaifa na ndoto hivyo, ni kiunganishi cha Watanzania na ni kielelezo cha Mtanzania.
Pia Soma:
- Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
- Kwa Sasa, Mwenge una Madhara kwa Jamii Kuliko Faida.Ufutwe.