Jana Leo na Kesho, mstari mrefu wa mafanikio kwa mtanzania.

Jun 8, 2016
83
648
Jana Leo na Kesho, mstari mrefu wa mafanikio kwa mtanzania /muafrika mweusi.

“I write nikiwa inspired” niliandika kwenye makala yangu ya kwanza.

Kuna swali ime ni inspire, imenisikitisha, imenipa uzuni, kwa jinsi gani mtu mweupe, the white man, amefanikiwa kuua uwezo wa wengi sana kujiamini na kuweza kwenda mbele, swali linauliza: Je, mungu kaumba baadhi ya wanadamu kwa upendeleo wa akili na maarifa?

Nikiisoma nakaribia hadi kutapika, kwa kua mtu mweusi kaandika hii. Na anazidi danganya na kupeleka mbele mfumo uliotengenezwa na watu weupe, wa kuua, kurudisha nyuma, kuchochea na kufanya wanadamu wadhani kwamba ukizaliwa na ngozi ambayo ni nyeusi we si mwanadamu kamili na inabidi utawaliwe.

Kwanza nikajua kama utani flani hivi, ila nikaingia kwenye comments na wengi wanakubaliana nae.

Mimi sio mwana historia, kuna mengi sijui bado na najifunza kila siku, kama kuna fact nimekosea ntakubali kuelezewa Zaidi na kukosolewa.

Soma Hii Polepole na Kwa makini sana, systems(mifumo ya dunia) hazitaki ujue Zaidi. Rudi usome tena, click link zote kuthaminisha (ni ndefu kidogo).

Jana

Ninaposema jana namaanisha historia, the past, vitu gani ambavyo vimetuleta hadi kufikia hapa tulipo, maana hauwezi, akili haitokuja kufunguka kama hujaisoma historia.

Kwenye report yangu ya form 4, history ndo somo pekee ambalo nilipata F. Sikua na hamu nayo, sikuipa a second thought, nilifikiri tu kwamba mambo yashapita, mimi kukariri miaka na majina na matukio itanisaidia nini. Fast forward miaka kumi mbele, hamna kitu ninachopenda kisoma kama historia. Natafuta vitabu vya researchers wa african history, natafuta makala, video, audio kuelewa kwanini leo ipo hivi ili kesho niifanye tafauti, na huu ndio umuhimu wa jana, umuhimu wa historia.

Mifumo inakwambia kwamba, ohh we ni maskini, na vyote ni juu yako, fanya kazi kwa bidii, usipofanikiwa, ukifa bila kufanikiwa, vyote ni juu yako, ambacho hawataki kukubaliana nacho ni kwamba kilichofanyika jana, ndicho kinachowafanya watu wawe hivi leo, ndicho inachofanya kesho yetu isije kwa manufaa.

Tuchukulie mfano, jana mtu alikuja na tofali akakuvunja miguu, alafu leo mnaanza kwenye mstari mmoja kushindana kukimbia, mnaanza wote, wewe unajivuta kwa nguvu zako zote, yeye anakimbia haraka alafu anakucheka, “muone huyo mtu hawezi kukimbia vizuri” anasema.(ngoja nikuchoree mstari wa kwanza).

Unaweza usiamini kwamba hicho ndo sababu mamilioni ya watu weusi ni maskini hadi leo na watazidi kua maskini kesho, lakini ngoja niendelee, ngoja nikuchoree mistari, let me connect the dots.

FACTS
  • Takribani miaka 200 tu iliyopita, kama generation tatu tu hadi kufikia tulipo hapa, nchi Tajiri zilikua zinautajiri mara tatu tu Zaidi ya nchi maskini.
  • Baada ya miaka ya ukoloni kuisha kwenye miaka ya 1960 hivi, miaka ambayo wazazi wetu wengi walikuepo nchi tajiri zikawa tajiri Zaidi ya mara 35.
  • Na hivi leo Nchi Tajiri zimepita nchi maskini kwa Zaidi ya mara 80.
Kwahiyo ni kipi kilichotuleta tuwe hivi leo, ni jana, ni historia, na kivipi tutaepuka mifumo inayotaka watu weusi wabaki maskini kesho, ndo swali ambalo inabidi tujiulize?

FACTS

Jana, Mwaka 1960 Congo ilipopata uhuru kutoka kwa Belgium, wananchi wa congo waliomaliza chuo kikuu walikua 16 tu kati ya watu milioni 14. Leo congo ipo vitani, Belgium uchumi wake unafanya vizuri tu. (Tukumbuke kwamba walidai wanakuja leta maendeleo na kuwekeza mifumo yao)

Jana tarehe 29 february mwaka 1906, miaka 112 tu iliyopita, nkosi mputa gama, magodi mbano, njorosa mbano, zinanimoto gama, fratera gama, mtepa hawayi gama, mtekateka tawete, majiyakuhanga komba, moambalioto soko, songea mbano na mputa mkuzo gama walinyongwa pamoja na watu zaidi ya laki 3 kuuwawa kwaajili ya kupigania uhuru wa watanganyika kutoka kwa wajerumani.

Hawa watu walijua kwamba wazungu hawa ambao muuliza swali amesema basically ni wametengenezwa tofauti na mungu na wemepewa vya ziada ni waongo, ni watu wabaya ambao wanaua na kubaka, na kuchukua rasilimali, na kudanganya kua wanafanya mazuri huku watu wanaowafanyia mazuri maisha yao yanaenda chini, ukiwasifia wajerumani kwa ku invent chochote kabla ya Mtanzania, hawa watu wote waliokufa kutupigania wanakugeuzia mgongo huko walipo.

Kosa kubwa tunalozidi fanya ambalo mimi mwenyewe personally najaribu kuachana nalo ni slave mentality ama akili za utumwa ambazo bado zinaendelea kututawala.

SLAVE MENTALITY ni nini? Akili za utumwa ni nini?

Akili za utumwa ni kukubaliana na kusheherekea kitu chochote ambacho tulipewa jana kipindi cha utumwa, na kuchukua na kukubaliana navyo kama vyetu. Sito taja ni vingapi ambavyo tumepewa, maana vitu vingine ni nyeti sana na vimeshatuingia na kua foundation za wengi, so ili kuepuka na akili za utumwa, jiulize sasa hivi ni kitu gani unachokubaliana nacho ambacho tulipewa na mkoloni.

Jana Wakoloni walikubaliana (walidanganyana) kwamba muafrika hajielewi, muafrika hana uwezo wa kuendelea, muafrika hana akili, muafrika inabidi atawaliwe ili achangie na aweze endeleza mifumo ya dunia. Na wakaja na dini zao, vitabu vyao, na kuua, kubaka, kutesa kwa mda mrefu, hapa tanzania wakoloni kutoka magharibi kwa miaka zaidi ya 500, generation/ vizazi zaidi ya 8 vili chukuliwa kwamba sio watu, hawana uwezo, hawa ni babu na bibi zetu(hapa hatujaongelea wakoloni kutoka mashariki).

Kipindi chote hiki wakoloni nchini kwao wanajenga, wanasoma, wana innovate, wana tunga, wanafundishana, wanafanya kazi pamoja ili kukuza uchumi wao.

Wajerumani ndio waliofanya ukatili mkubwa sana kipindi cha maji maji rebellion, Tanganyika, na mengine mengi tu walifanya kwenye nchi zingine afrika.

August 4, 1905, kinjekitile alinyongwa ili kutishia mtu yoyote kujifanya kwamba anapigania haki za wa Tanganyika. Sijui kwanini hatuna siku ambayo tunapumzika na kusherekea ujasiri wake, alionganisha watu wote waachane na tofauti zao na kupigania uhuru wa Mtanganyika, na kuanzisha maji maji rebellion.

Walichokifanya jana ndicho kimetuweka hapa leo.

Makala ninayoijibu imeandikwa na mtu ambae bado ana akili za utumwa.

Kutoka miaka ya 1400 hadi kuja kufikia 1961, nchi hii yetu ilipokuja kupata uhuru tulikua tupo kwenye kipindi cha ukoloni, tulivunjwa miguu kwa miaka Zaidi ya 500, na leo wanatwambia tukimbie, tushindane tuone nani ambae anaweza fika mwisho wa kwanza. Tusisahau historia, msatari wa kwanza huo nimekuchorea kutoka jana hadi leo.
jana vs leo.jpg

Leo

Uongo mkubwa wa leo ni kwamba mtu yeyote anaweza akawa tajiri kwenye mifumo hii, uongo mkubwa wa leo ni kwamba akifanya kazi kwa bidii mtu yoyote anaweza kujikwamua kutoka kwenye umaskini, uongo mkubwa wa leo ni kwamba watu ambao ni maskini ni maskini kwa kua hawajafanya kazi kwa bidii. uongo mkubwa wa leo ni kwamba mimi na wewe tulikua, na wengi wetu wenye ngozi kama zetu watazidi kua maskini kwa ajili hatuna uwezo wa kufikiria kama watu wenye ngozi tofauti na zetu.

Hela ni nini? Zinapatikanaje? Zinatengenezwa vipi? Mtu akifa anamuachia nani? Hela zipo ngapi duniani? Benki zinafanya vipi kaizi? kwanini thamani ya hela inapanda na kushuka? kwanini hata kama nchi ina rasilimali nyingi wananchi wake bado maskini?

Ukifanya uchunguzi unaweza jibu maswali yote hayo juu, na ukishayajibu, ujiunge kwenye upande wa kushangaa ni jinsi gani mifumo ya dunia ilivyowekwa kumfanya mtu mweusi abaki maskini.

Leo hii kuna lodge ngorongoro, ambayo ina milikiwa na watu wenye ngozi nyeupe ili watu wengine wenye ngozi nyeupe wakija kufanya utalii hela zao zinazunguka kati yao, serikali inakata makato lakini majority of pesa inarudi kwao, haiendi kuzunguka kwa wananchi ambao hali zao ni za kati, wala wenye maisha ya chini. Kwenye pita zangu nmekutana na watu wawili ambao budget yao ya wiki hapa nchini ni takriban milini 20 za kitanzania.

Leo hii, nchi tajiri zinakuja kusaidia africa na kutangaza kwamba wanasaidia Nchi za Afrika, wanaleta bilioni kadhaa, lakini kwa mifumo walioiweka rasilimali wanazozitoa kwenye nchi za Afrika zina thamani ya Trilioni kadhaa, lakini kupitia mifumo kama Trade mispricing, kwamba receipt ambazo zinalipwa sio za kweli na haziendani kabisa na maliasili ambazo wanachukua, na kulipia bei ndogo sana kwa ajili ya maliasili za kutengeneza mabilioni, jiulize ni mfumo gani ambao una panga bei ya thamani za rasilimali?

Na swali lingine la kujiuliza ni kwamba leo hii thamani ya hela ni nini? Dollar za kimarekani 9,400 ni sawa na million 20 na za kitanzania, tumefikaje hapa leo hii?

Leo ni maswali tu sana sana, kwa kua leo hali iliyopo inabidi itufanye either tubadili mifumo ili mtu mweusi aweze fanikiwa, ama tukubaliane na mifumo.

Turudi jana Tena (tutafika kesho ngoja kidogo).

-Tunaambiwa jana kwamba muafrika hakua na uwezo wa kufikiria, tunaambiwa. Tunaambiwa uongo, what are the facts, ukweli ni nini? Jana ilikuaje? Turudi nyuma, kabla ya ukoloni, turudi nyuma Zaidi, historia ambayo hata mashuleni kufundishwa ni ngumu, hivi jiulize kabla ya ukoloni, wa afrika walikuaje, waligundua nini, walikua wanafikiria nini, Afrika mashariki ilikuaje, kabla hawajachora mistari kugawana vipande vya afrika ambavyo leo tunaita mipaka, kabla hawajaanza kutujaza na akili za utumwa ilikuaje?

Industrial revolution, yaani kipindi cha viwanda kuanza, kimejengwa na damu na jasho la mtu mweusi, kila nchi ambayo ilianza kufanikiwa kwenye miaka ya 1760 kwenda 1800 hivi ni nchi za wakoloni. Ni nini Kilichokua kinaendelea Tanganyika kipindi ambacho industrial revolution kinaanza kwenye nchi za magharibi?

Kipindi cha miaka hiyo, kiliitwa the scramble for afrika yaani nchi za afrika zimefanywa kama biskuti hivi ambazo wamepewa watoto wa darasa la kwanza kugawana, Germany, british, france, Belgium, Portugal, Italy nchi zote hizi na zingine zimefaidika kwa damu na jasho la watu weusi, kisha leo tunashindana kwenye uwanja mmoja.

_83946256_berlinconference_alamy.jpg

Ukisema mtu mweusi hana akili ya kufikiria kama mtu mweupe, mamilioni ya watu, waliokufa na kuuliwa ambao labda wangekuja kua madaktari, wana sayansi na vingine vingi ambavyo watu ambao maisha yao yamekatwa wanakugeuzia mgongo.

Textile, nguo hizi ndio ilikua viwanda vya kwanza kufanikiwa, na vilifanikiwa vipi? Kwa kuwaweka watu weusi kwenye mashamba yao ili kuwapatia pamba na vitu vingine, mashamba ya kwenye colony zao, mashamba ambayo wamechukua watumwa kuwarudisha kwao, mashamba ambayo damu zimetoka za watu weusi.

Kutoka Wikipedia:

“The Industrial Revolution marks a major turning point in history; almost every aspect of daily life was influenced in some way. In particular, average income and population began to exhibit unprecedented sustained growth”

Facts

Hii video ndefu sana, ila ukiiangalia yote utafaidika sana na historia.

Robin walker ni mwana historia, ambae ana institution inayo fanya uchunguzi wa historia ya afrika, na wanagundua vitu vipya kila siku, historia ya kweli sio ambayo tunaambiwa na wakoloni kila siku.

Ndani yake kwenye dakika ya 21 hivi, Robin walker anasema kwamba

“Kilwa was considered one of the most beautiful and well constructed cities of the world” anasema

Mji wa kilwa ulijengwa karne ya kumi, yani 900 AD na kisha kuongezewa karne ya 15, miaka ya 1400 hivi, kabla ya wakoloni kuja, kabla hawajasema kua wa Afrika wote wanaishi kama wanyama tu hawana maendeleo, na inabidi kutawaliwa, miaka Zaidi ya 400 kabla hawajaanza kuja kuua na kufanya watu wawe watumwa.

kilwa-750x500.jpg

Miaka ya 1200 hivi, karne ya 13, east Africa walikua wamejenga vyoo, na majengo ambayo Miaka Zaidi ya 600 kabla wakoloni hawajaja, civilization ilikua inafanya kazi vizuri kabisa, tulikua na majengo ambayo magharibi wanayaota. Mji wa lamu, ambao upo Kenya, unasemekana ulijengwa miaka ya 1370.

w1055.jpg

Waswahili walikua watu mahiri sana, Swahili settlement zilijenga na ku innovate mambo mengi sana ambayo yanafichwa na historia, historia inayofundishwa ni version ya mkoloni, kwamba civilization afrika ilianza kipindi ambacho walikuja wao, miaka ya 1700-1800 hivi. Ni uongo mtupi. Jana haikua hivyo jana na juzi yetu wameifuta ili kutengeneza leo ambayo tunaamini ka mtu mweupe ana uwezo Zaidi yetu, tupilia mbali mtu yoyote ataewaza hivi, mgeuzie mgongo leo kabla hatujaenda kukutana na mababu zetu waliokua na akili kuliko hawa watu waliokuja kuwauwa na kuwalzimisha kujiunga nao na kuwapa rasilimali kwa kutumia mdomo wa bunduki.

Leo

Leo tunakubaliana kwamba ngozi nyeupe ina uwezo wa kufikiria kuliko watu wenye ngozi nyeusi, kweli akili za utumwa zimefanikiwa kujengwa na wakoloni.

Leo nusu ya cobalt, maliasili ambayo inatumika kutengeneza simu hizi, ambazo dunia nzima tunatumia inatoka congo, inatoka afrika, na wananchi wa congo ni maskini wanaambiwa kwamba hawana uwezo wa kufikiria kama mkoloni, DRC inabidi iwe kama sio nchi tajiri namba moja basi iwe kwenye top 3, maana ndipo wenye upatikanaji mkubwa wa cobalt, copper, diamond, tantalum (inapatikana kwenye simu, computer, dvd player, video games na vingine) na tin, kwanini na vyote hivi Congo sio tajiri, Mifumo ama systems.

cobalt reserve.PNG

Leo tunajaribu na tunakubaliana kwamba tunaweza kua kama Steve Jobs, Mark zuckerberg, Bill Gates ana wengine wambao ni watu wenye ngozi ambazo sio nyeusi, wakati apple inazidi kua tajiri, wakati wakiingi congo wananyonya maliasili ambazo wanaenda kutengenezea Iphones kisha wanarudi kutuuzia hukuhuku afrika, wakati most computers ambazo zinatumia windows zinatumia mali asili za afrika, na badala ya kulipa thamani yake kweli wenyewe wanalipa visenti ili kwenda kuuza bidhaa zao mamilioni. Wamefanikiwa kutengeneza thamani kwa ajili ya kipindi cha ukoloni, na leo vitu vinavyotoka kwa vina thamani kuliko vinavyotoka kwetu.

Leo Hii ukoloni haujaisha, na tusipo amka, kesho haitakua nzuri kabisa.

Uwongo mkubwa wa leo ni kwamba hela ikienda kwa mtu mmoja, hiyi hiyo inaweza kwenda kwa mtu mwingine na yeyote akifanya kazi anaweza kua tajiri kama billgates, thamani haipo hivyo huu ni uongo.

Hivi apple, iphone? jana babu zenu wamebaka, wameua, mmechukua watu weusi kwenda kutengeneza mifumo yenu kurahisisha na kuendeleza uchumi, jana mmefanya watu wawe watumwa, jana mme fanya watu waishi chini ya ukoloni, leo hii mnalipa vi centi ili kupata maliasili, watoto wadogo wanachimba haya madini mnayotumia, na nyie mnatengeneza mabilioni kuuza simu, na kweli dunia nzima tunaangalia apple kama watu wanaotengeneza hela kimaadili?

drc10.jpg

Na hizi sio siri, ukisearch google ama youtube unaona yanayoendelea. Sio siri, yote yapo wazi.

Hivi battery za simu zote zingetengenezwa Congo, na magari yanayotumia battery yange tengenezwa Congo, alafu nchi ambazo zingenunua hizi simu na magari walipe thamani yenyewe kabisa, congo ingekua maskini, hivi kama kampuni kuchukua cobalt kuweka kwenye battery zake ingebidi ilipe thamani kubwa, la sivyo ijenge viwanda vyake nchini humo ama iwekeze nchini, kuna mtu angepigana unadhani, kuna vita ingetokea?

Hakuna vita Afrika ambayo haijasababishwa na wakoloni kuanzisha, au kusababisha na kuchochewa na mmarekani, and that is fact.

Misaada wanayofanya ni ujinga mtupi.

Watu milioni 13 wanahitaji misaada congo leo, ndio vichwa vya habari vinavyosema leo, lakini hatu address lasirimali wanazochukua, walizochukua, na watazozidi chukua kila siku, aisee mkolini amefanikiwa kusukuma hoja zake kwenye akili za watu.

Eti leo, wanataka okoa wakongo kutoka vitani, vita ambazo wamezitengeneza wenyewe.

Hela zozote wanazotoa wasiziite msaada, nchi yoyote ambayo imeshirika kwenye ukoloni inahitaji kusema kwamba wanalipa walivyoiba, sio msaada.

Ukinivunga miguu leo, alafu kesho unaambia ndugu zangu kwamba eti ohh, namsaidi kwa kumpeleka hospitali, hapana, haunisaidii, unalipa ulichofanya, na nikipona, tutaonana kesho.

Main Thing/kitu muhimu cha kujua na kuelewa kabla ya kwenda kesho.

Na nili comment hili kwenye makala nnayoijibu, everything is gradual, inabidi tuanze A ili kufika B, ndipo tutapoweza fika K, hadi W.

Sio Mtu mmoja ambae anaweza kufikiria kila kitu, mark zuckerberg alitumia PHP kutengeneza facebook kwa idea ambayo aliiba kutoka kwa watu walioitunga, PHP ilibidi itengenezwe kwanza na watu wengine, na lugha ambayo miaka mingi sana imejengwa polepole, je ni kweli wa afrika tulishindwa kutengeneza lugha za programming kabla ya wakoloni?

Hapana, PHP imetengenezwa mwaka 1994, na watu ambao baba zao na bibi zao hawajapitia utumwa na ukoloni.

jana php.jpg

Hivi watu wote waliouliwa na kuteswa na kubakwa, unadhani hata mmoja wao alikua hana uwezo wa kuja kupata mtoto au mjukuu ambae angekuja kutengeneza lugha ya programming?

unadhani kama mda wote huo watu wangekua hawakimbii na hawaogopi kuuliwa, wanapeleka watoto wao shule, na wanafundishana na kufanya kazi pamoja, na ukiweka rasilimali zote tulizonazo, mkoloni angetufukia? Hapana, na wote wanajua hili ndio maana mifumo bado ipo na inafanya kazi hadi leo, na wamefuta historia kabla ya ukoloni.

Lugha ya kwanza ya kutengenezea program (programing languages) iliyotumika na ilitengenezwa mwaka 1954, unajua nini kilikua kinaendea Tanganyika mwaka huu? Mwalimu Julius Nyerere na Oscar Kambona ndipo walipo igeuza TAA(Tanganyika Afrika Assosication) kua TANU (Tanganyika African National Union), hapa hata uhuru bado.

“Leo hii tunajaribu kukimbia the same race, baada ya historia yote hiyo, tunataka watu wetu washinde OSCARS ama watengeneze kitu cha kushindana na facebook, ama washinde miss world, tunataka watu wetu waweze shindana na mtu mweupe kwenye mifumo ambayo imejengwa kumfaidisha mtu mweupe”.

Swali la kijinga ambalo watu watauliza ni hili hapa

Kama mifumo imejengwa kumfaidisha mtu mweupe kwa nini kuna dangote na matajiri wengine weusi?

Jibu la kwanza -> Ili wachace wawe matajiri, wengi inabidi wawe maskini, na kuna matajiri wachache sana weusi, ambao wanafaidisha mifumo bado, dunia imekubaliana kwamba wachache wengi inaobidi wawe maskini ni watu weusi.

Jibu la pili – Hela za matajiri weusi wote zinaenda wapi? Mtu akinunua Ford, Audi, Porsche, Volkswagen, BMW, Mercedes benz na magari mengine mengi,wanatengeneza hela kutoka kwa watu weusi, wanaende kuwarudishia hela watu ambao babu zao waliuwa watanganyika Zaidi ya laki tatu na kuiba maliasili nyingi sana ili wenyewe waweze kwanza fika kipindi ambacho wantengeneza magari haya.

So ukiota kua tajiri ili ununue Mercedes, ujue watu laki tatu na Zaidi waliouwawa wana kugeuzia mgongo huko walipokua.

Wajerumani walianza kutengeneza automotives magari na vingine, kwenye miaka ya 1860, unafahamu nini kilikua kinaendelea Tanganyika/ east Afrika mwaka 1860? Watu walikua wanagombania na kugawana hii mipaka ya east afrika, wa Portugal waka nyanganywa na Waarabu, Germany na British wanagombania kugawana na kuchora mipaka ili watawale kila mtu na sehemu zake.

Tuzoom kidogo msatari wetu

jana magari.jpg

MATAJIRI WEUSI WACHACHE WAMETENGENZWA ILI KWANZA TUAMINI KWAMBA WOTE TUNA UWEOZO SAWA NA MIFUMO IPO SAWA, PILI ILI WAKUSANYE HELA VIZURI NA KUWARUDISHIA WENYE NGOZI NYEUPE.

ILI KUTENGENEZA HELA INABIDI UTENGENEZE THAMANI, ILA UKIWA MWEUSI THAMANI YAKO HAITHAMINIWI NA WATU WALIOTENGENEZA MIFUMO INAYOELEZEA THAMANI NI NINI.

Aisee, watu wamepotea sana, comment kama hii hapa chini.

swali.JPG

Na ukizingatia Tanzania ndipo mifupa ya binadamu wa kale kabisa ilipopatikana, inasikitisha.

Kama mungu unaemtaja hapo na unamuamini kweli yupo, ni kweli wenye upendo na Amani, basi amesha walaani sana wakoloni kwa waliofanya, na yupo upande wetu tuweze fanya kesho ambayo hawakuwai iwaza.

KESHO

Mfumo wa capitalism (ubepari) ndio imetuleta hapa tulipo.

leo na kesho.jpg

Kesho ya hivi tunaifanyaje? Kesho ambayo afrika ndio bara la kwanza kwa kila sector, kesho ambayo nywele na ngozi za watu weusi za watoto wetu zinapendwa na kukubalika kama zilivyo, kesho ambayo afrika inarudi kua wakwanza kama ilivyotakiwa iwe, Sina majibu yote, nitaandika nyingine kujaribu address kesho lakini kama umeisoma na umeelewa na una cha kuchangia, tafadhali changia, nakubali nikosolewe ila tafadhli weka link kama unasema kitu, usichangie kama hauna facts, hiyo ndio njia nyingine wametushika akili, kukubaliana na vitu bila kuwa na ukweli, bila kua na facts.

Kesho ni kuangalia makosa yote yaliyofanyika. Kujadili na kuweza kukua, bila hivyo sidhani kama tutaweza epuka vikwazo ambavyo hatuvioni vilivyowekwa na wakoloni.

We have to reckon with our history, there is no other way around it.
 
Tulianza kupokonywa kupitia bunduki,asaiv tunapokonywa kupitia hela naamin ipo siku hawata tupokonya tena.
mkombozi wa africa karne hii ni alikuwa ni GADAFI namsubir mwingine.
 
Naomba ni some tena na tena ndio nichangie japo kidogo, lakini hii mada ni fikirishi sana ambayo nadhani mwisho wa siku hakuta kua na lakufanya.
 
napuita zangu tu

sory nime qoute "" nilikuwa nataka kutoa heshima kwa mtoa mada """

mtoa mada kama ningekuwa na Dada aiseee ningekupa umuoe tu""" wewe Jamaa NI genius nimependa uchambuzi wako na reference unazozitoa....kwakweli naweza kusema umeiapsua pasua akili yangu vibaya mnoooo"" umefanikiwa kunisaidia kujibu maswali mengi sana ambayo huwa najiulizaga mimi mwenyew"""
hakika sidhani kama patakuwa na wakuipinga hoja yako zaidi na zaidi na imani patatokea watu wakukuunga mkono haswaaa"""
niwe muwazi kwenu wadau kila navyojitahidi kusoma hizi article zinazoihusu historia ya mtu mweusi huwa najikuta nazidi kuichukia dunia ...nazidi kuuchukia ulimwengu ..maaana naona ulimwengu umejaa maovu mengi nambay zaidi muathirika mkuu akiwa nimtu mweusi ....kwakweli Mungu kabla hajanileta huku alipaswa kuniuliza kama Nipo Tayari kuishi katika ulimwengu wanamna hii uliojaa dhulma kiasi hiki .....

nimalizie kusema tu ....kwa Mara ya kwanza nimejikuta nalengwa na machozi baada ya kumaliza kuisoma hii thread .......

naichukia DUNIA KWAKWELI
 
nimejaribu kuipitia vyema hiyo pictr ya mji wa lamu ....nimeona hao watu wakiwa wamevaa kanzu na bagarashia ""nimejikuta najiuliza maswali mbona aina hiyo ya mavazi ni mavazi ambayo yanatokana na desturi ya waarabu ..na hata hilo jengo ambalo lipo kwenye pictr muonekano wake nikama majengo ya kale ya nchi za uarabuni "" hoja yangu ni hii palikuwa na uhusiano ipi baina ya waatmrabu na watu waafrica mashariki kwa wakati huo mpka kufikia hatua yakuchukua ustaarabu wawaarabu na kuutumia katika maisha yao "" je walipata kutawaliwa na hao waarabu katika hiyo miaka uliyoitaja""? na kama ndio hivyo "" je kabla ya sisi kutawaliwa hatukuwa na ustaarabu wetu wenyew ambao ulikuwa una tutangaza sis kama sis ""? au ndio tulikuwa wavaa ngozi ""??

maana mpka leo sis watu weuis niwatu tunaoishi katika ustaarabu wawatu wengine hatuna ustaarabu unaotu tambulisha kama watu weusi ..hapa nazungumzia kama ilivyo kwa China na India ama waweza jionea kwa mataifa kama uingereza nakadhalika
 
"Kesho ni kuangalia makosa yote yaliyofanyika. Kujadili na kuweza kukua, bila hivyo sidhani kama tutaweza epuka vikwazo ambavyo hatuvioni vilivyowekwa na wakoloni".

nimependa kuanzia hapo ulipoishia. kwa ujumla makala (siyo nakala) yako ni nzuri. Ni fikirishi, na inafundisha. Hta hivyo, nimeona dhana yako iko katika kutizama kwa nje. Nje yetu kama Waafrika au Watanzania. Tukijitazama hivyo, hatukosei. Lakini pia kuna namna nyingine ya kujitazama na kuwatazama walio nje yetu.

Kwa mfano: dunia imekuwa ikiwagawa watu katika maeneo mawili makuu: watumwa na mabwana. Afrika na Waaafrika iliangukia katika kundi la watumwa. Waafrika walitwaliwa, kwanza na waarabu (kuanzia karne ya 9), halafu na wazungu (kuanzia karne ya 15). Utumwa wa Waaafrika katika Arab World hujaugusia. Madhara ya utumwa wa Waafrika katika Arab World hujauzungumzia. Je, utumwa huo ulikuwa wa kiwango gani? Ulileta madhara gani katika bara la Afrika? Utumwa wa Waafrika kwa Warabu ulidumu kati ya karne ya 9 na 19 (jumla ya karne 10). Pamoja na biashara ya watumwa, Waarabu walishiriki katika ujangili. Miji ya Pwani iliyostawi wakati wa mahusiano ya Afrika na Waarabu ilijengwa na nani? Je, ubunifu wa majengo walifanya Waafrika weusi? Majengo yalikuwa mji wa Kilwa, au Lamu au Mombasa yalimilikiwa na Waafrika weusi?

Eneo jingine la mgawanyo linahusu watawala/wakoloni na watawaliwa/makoloni. Hii dhana ya mgawanyo ilianzishwa na wazungu kama ulivyoelezea. Sababu za kutawala au kukolonize ni za kibinafsi. Kwa mfano, wakati wazungu wanatukolonize walisema wanataka kustopisha biashara ya utumwa iliyokuwqa ikiendelezwa na Waarabu. Lakini tunafahamu sababu ya msingi zaidi ilikuwa ni ya kiuchumi, kama ulivyoelezea kwa ufasaha juu ya raslimali zilizopo katika ukanda wa Black Afrika.

Kidini, hapa napo kuna mgawanyiko mkubwa. Kwa Waarabu na Uislamu wao, Waafrika ni makafiri na washenzi. Kwa Wazungu na Ukristo wao, Waafrika ni wapagani na washenzi. Hata hivyo, tujuavyo leo, Jumla ya Wakristo na Wasilamu katika Black Afrika ni kubwa kuliko idadi ya makafiri, wapagani na washenzi waliobaki. Why? Hakuna aliye tayari kuitwa mshenzi. Katika upande wa lugha, Ali Mazrui anasema kwamba karibia asilimia ishirini (20%) ya maneno ya Kiswahili yanatokana na Kiarabu.

Je, Waarabu, hata walio katika Bara la Afrika ni wema kwetu? Kuna mchangiaji mmoja ametaja uzalendo wa hayati Kanali Muammar Qaddafi. Kiongozi aliyewahi kuitawala Egypt katika karne ya 20, Gamal Abdel Nasser, alifanikiwa kuiweka nchi yake katika nafasi yenye umuhimu wa pekee katika ulimwengu wa Kiarabu, dini ya Kiislamu, na katika bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Profesa Mazrui, Nasser aliwahi kutamka kwamba: "we cannot, in any way, stand aside, even if we wish to, from the sanguinary and dreadful struggle now raging in the heart of the continent between the five million whites and two hundred million Africans. We cannot do so for one principal reason - we ourselves are in Africa".

Je, Africa ni moja? Hapana. Kuna Africa ya Kiarabu na Afrika ya weusi. Kuungana kwao hawa ni kwa sababu moja tu: ubeberu wa Wazungu. Hakuna kingine. Hata sasa tunawatazama Waarabu kwa jicho la wenzetu, kama tunavyowaona Wachina, Wasingapore na wengineo wanaohasimiana na wazungu. Nasser aliamini kwamba kama mazungu yanawashughulikia Waafrika weusi ndani ya Bara la Afrika ambalo Waarabu nao wanaishi humo, basi nao hawatakuwa salama - interdependence.

Je, tunawezaje leo kuyaepuka ili tusonge mbele? Kumbuka, wakoloni wazungu wa Kijerumani waliwapiga kirahisi akina Kinjekitile kwa sababu ya kusaidiwa na Watanganyika waliokuwa maadui zao. Hata vita kuu vya dunia (1 & 2) Waafrika walikuwa wakitumika kama maaskari. Ulihitimisha kwa kusema "kesho ni kuangalia makosa yote yaliyofanyika, kujadili na kuweza kukua". Vema. umetusaidia kwa kiasi kuona makosa yaliyofanyika.
 
sisi hatukua wajinga tulikua na akili ila tulishindwa kugundua nguvu ya state katika jamii zetu.

weupe walichotuzidi ni kuanzisha strong system hicho ndicho kilimaliza maisha ya mweusi na itakua hivyo milele mpaka tutakapokua na strong states.

Syatem zipo wapi na zinafanya nini leo zaidi ya karne ya ishirini kuna zaidi ya waafrika million 600 usiku hawajui kitu kinaitwa umeme.

State zetu bado hazipo imara tangu wakati wa kinjekitile mpaka leo na hata miaka 50 itayokuja hatuna purpose

Walter Rodney aliwahi kuandika kwamba

if there is no class stratification in a society,
it means that there is no state,

because the state arose as an instrument to be used by a particular class to control the rest of society in its own interests.
 
"Kesho ni kuangalia makosa yote yaliyofanyika. Kujadili na kuweza kukua, bila hivyo sidhani kama tutaweza epuka vikwazo ambavyo hatuvioni vilivyowekwa na wakoloni".

nimependa kuanzia hapo ulipoishia. kwa ujumla makala (siyo nakala) yako ni nzuri. Ni fikirishi, na inafundisha. Hta hivyo, nimeona dhana yako iko katika kutizama kwa nje. Nje yetu kama Waafrika au Watanzania. Tukijitazama hivyo, hatukosei. Lakini pia kuna namna nyingine ya kujitazama na kuwatazama walio nje yetu.

Kwa mfano: dunia imekuwa ikiwagawa watu katika maeneo mawili makuu: watumwa na mabwana. Afrika na Waaafrika iliangukia katika kundi la watumwa. Waafrika walitwaliwa, kwanza na waarabu (kuanzia karne ya 9), halafu na wazungu (kuanzia karne ya 15). Utumwa wa Waaafrika katika Arab World hujaugusia. Madhara ya utumwa wa Waafrika katika Arab World hujauzungumzia. Je, utumwa huo ulikuwa wa kiwango gani? Ulileta madhara gani katika bara la Afrika? Utumwa wa Waafrika kwa Warabu ulidumu kati ya karne ya 9 na 19 (jumla ya karne 10). Pamoja na biashara ya watumwa, Waarabu walishiriki katika ujangili. Miji ya Pwani iliyostawi wakati wa mahusiano ya Afrika na Waarabu ilijengwa na nani? Je, ubunifu wa majengo walifanya Waafrika weusi? Majengo yalikuwa mji wa Kilwa, au Lamu au Mombasa yalimilikiwa na Waafrika weusi?

Eneo jingine la mgawanyo linahusu watawala/wakoloni na watawaliwa/makoloni. Hii dhana ya mgawanyo ilianzishwa na wazungu kama ulivyoelezea. Sababu za kutawala au kukolonize ni za kibinafsi. Kwa mfano, wakati wazungu wanatukolonize walisema wanataka kustopisha biashara ya utumwa iliyokuwqa ikiendelezwa na Waarabu. Lakini tunafahamu sababu ya msingi zaidi ilikuwa ni ya kiuchumi, kama ulivyoelezea kwa ufasaha juu ya raslimali zilizopo katika ukanda wa Black Afrika.

Kidini, hapa napo kuna mgawanyiko mkubwa. Kwa Waarabu na Uislamu wao, Waafrika ni makafiri na washenzi. Kwa Wazungu na Ukristo wao, Waafrika ni wapagani na washenzi. Hata hivyo, tujuavyo leo, Jumla ya Wakristo na Wasilamu katika Black Afrika ni kubwa kuliko idadi ya makafiri, wapagani na washenzi waliobaki. Why? Hakuna aliye tayari kuitwa mshenzi. Katika upande wa lugha, Ali Mazrui anasema kwamba karibia asilimia ishirini (20%) ya maneno ya Kiswahili yanatokana na Kiarabu.

Je, Waarabu, hata walio katika Bara la Afrika ni wema kwetu? Kuna mchangiaji mmoja ametaja uzalendo wa hayati Kanali Muammar Qaddafi. Kiongozi aliyewahi kuitawala Egypt katika karne ya 20, Gamal Abdel Nasser, alifanikiwa kuiweka nchi yake katika nafasi yenye umuhimu wa pekee katika ulimwengu wa Kiarabu, dini ya Kiislamu, na katika bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Profesa Mazrui, Nasser aliwahi kutamka kwamba: "we cannot, in any way, stand aside, even if we wish to, from the sanguinary and dreadful struggle now raging in the heart of the continent between the five million whites and two hundred million Africans. We cannot do so for one principal reason - we ourselves are in Africa".

Je, Africa ni moja? Hapana. Kuna Africa ya Kiarabu na Afrika ya weusi. Kuungana kwao hawa ni kwa sababu moja tu: ubeberu wa Wazungu. Hakuna kingine. Hata sasa tunawatazama Waarabu kwa jicho la wenzetu, kama tunavyowaona Wachina, Wasingapore na wengineo wanaohasimiana na wazungu. Nasser aliamini kwamba kama mazungu yanawashughulikia Waafrika weusi ndani ya Bara la Afrika ambalo Waarabu nao wanaishi humo, basi nao hawatakuwa salama - interdependence.

Je, tunawezaje leo kuyaepuka ili tusonge mbele? Kumbuka, wakoloni wazungu wa Kijerumani waliwapiga kirahisi akina Kinjekitile kwa sababu ya kusaidiwa na Watanganyika waliokuwa maadui zao. Hata vita kuu vya dunia (1 & 2) Waafrika walikuwa wakitumika kama maaskari. Ulihitimisha kwa kusema "kesho ni kuangalia makosa yote yaliyofanyika, kujadili na kuweza kukua". Vema. umetusaidia kwa kiasi kuona makosa yaliyofanyika.

Ahsante sana, dhumuni langu ni kufanya watu kua na mjadala juu ya haya mambo, mimi sio mwana historia kama nilivyosema hapo mwanzo, na pia sijagusia slave trade ya waarabu kwa kua aliyenifanya niandike haya anasifia sana mzungu.

Waarabu hapa kwetu ndio ambao wamekubalika kama wenzetu kumbe nao babu zao walifanya mabaya sana, hivi leo kati ya matajiri wakubwa 10 kutoka tanzania, labda wawili tu hawana damu ya kiarabu/kihindi.
Mtu yeyote ambae anaishi hapa mwenye ngozi nyeusi anajua bila hata kuambiwa kwamba kuna racism na classism inaendelea kila kukicha, tunaelewa jinsi gani mtu mweusi hapa anachukuliwa kama wa chini kabisa, tunaelewa establishment za wahindi wanavyo treat watu weusi, tunaelewa waarabu walivyojitenga, na kupeana nafasi kwenye kampuni zao, bila hata kua na mjadala tunaelewa, hata msafisha vyoo kwenye hoteli za wahindi anaelewa kwamba racism ipo na inacheza nafasi kubwa kwenye opression ya mtu mweusi.

Hii mifumo imejipanga, imekubaliana, mtu mweupe kwanza, the white man, waarabu, wengine wote wanafuata, kisha mtu mweusi anakua mwisho kabisa.

Historia ina matobo mengi sana upande wa Africa kabla ya ukoloni na utumwa, picha wanazotuonesha kutoka egypt enzi za 3100 BC inaonesha kwamba wa egypt walikua kama waarabu flani hivi, lakini hiyo pia ilikua uwongo, na proof inatoka kila siku kwamba egypt walikua ngozi nyeusi na nywele kama zetu waafrika weusi, egypt kulikua kuna civilization kipindi ambacho kote kwingine bado, ma pharaoh walikua na wana sayansi, wakandarasi, wanahesabu na mengine mengi.

Civilization zilianza kwa kua watu waliweza ku settle sehemu ambapo hali ya hewa ni nzuri na wanaweza kujenga ili kujilinda na sources za maji zipo, na wanaweza kulima vizuri chakula, afrika hali ya hewa shemu nyingi haikuruhusu watu ku settle sehemu moja ili kujijenga, east west south kulikua hakuishiki , so walikua wanahama hama sana, ila watu weusi waligundua hili wenyewe kabla ya explorer yoyote kuja kuweka mguu wake kwenye hili bara, na civilization za egypt zilikua watu weusi, egyptian civilization ilikua 3150 BC, roman empire za wa magharibi zimeanza 100 bc, maka mingi sana baada ya egyptian empire kua zimeshaanza.

Binadamu wote wanataka kutafuta kua na nguvu kuliko binadamu mwingine, ni nature ya ubinadamyu ambayo bado hatuja overcome, hiyo ndio sababu ya vita vyote duniani, power. So kabla ya wote kuja hapa wafalme na ma pharaoh walikua wanakula faida za maliasili za Afrika, waarabu walikuja kuomba msaada kutoka kwa wafalme weusi, kabla ya kuamua kuanza kuja kutawala na ku-colonize afrika.

Mansa musa kutoka mali,ndiye tajiri ambaye hajawahi kutokea duniani tena, na alikua ana ngozi nyeusi ila waarabu walikua wameshaleta uislamu, mansa musa alikua muislamu. Sifahamu mengi ila ninachofahamu ni kwamba afrika ni ya mtu mweusi na historia kabla ya wazungu kuiandika upya iliandikwa upya na waarabu, maana tunasoma historia version zilizo achwa na wanahistoria wakiarabu walioleta uislamu huku .

Kitu ambacho kiko wazi ni kwamba hapa ndipo maliasili zote zilizopo na wote wamejaribu kuja hapa ili wafaidike nazo wao. Na wamefanikiwa kuvunja uwezo wa wengi kujiamini, miaka elfu kadhaa ya watu ambao sio weusi kuja kuua na kuiba kimetu affect akili sana.
 
nimejaribu kuipitia vyema hiyo pictr ya mji wa lamu ....nimeona hao watu wakiwa wamevaa kanzu na bagarashia ""nimejikuta najiuliza maswali mbona aina hiyo ya mavazi ni mavazi ambayo yanatokana na desturi ya waarabu ..na hata hilo jengo ambalo lipo kwenye pictr muonekano wake nikama majengo ya kale ya nchi za uarabuni "" hoja yangu ni hii palikuwa na uhusiano ipi baina ya waatmrabu na watu waafrica mashariki kwa wakati huo mpka kufikia hatua yakuchukua ustaarabu wawaarabu na kuutumia katika maisha yao "" je walipata kutawaliwa na hao waarabu katika hiyo miaka uliyoitaja""? na kama ndio hivyo "" je kabla ya sisi kutawaliwa hatukuwa na ustaarabu wetu wenyew ambao ulikuwa una tutangaza sis kama sis ""? au ndio tulikuwa wavaa ngozi ""??

maana mpka leo sis watu weuis niwatu tunaoishi katika ustaarabu wawatu wengine hatuna ustaarabu unaotu tambulisha kama watu weusi ..hapa nazungumzia kama ilivyo kwa China na India ama waweza jionea kwa mataifa kama uingereza nakadhalika

Historia imefutwa, historia imefutwa kupitia dini zilizoletwa, kupitia kudanganywa.

Roman empire ndio civilization za mwanzo zilizokua documented kwa magharibi, afrika civilization zilikuepo miaka zaidi ya elfu 3 kabla ya rome, sijafuatilia sana waarabu ilikuaje.

Kwa research yangu, waarabu na waafrika walianzisha Trade kwanza, na wakawa hadi wanasaidiana. Wafalme wa kiafrika walikua na nguvu sana, dhahabu na maliasili zingine zote zilikuepo afrika, inasemekana waarabu wakiwa na migogoro hadi walikua wanakuja kuomba misaada kutoka kwa majeshi ya kiafrika.

mansa-musa.jpg

ila baada ya hapo kuna utata kidogo ikija kwenye nini kweli kilitokea, maana kuna wana historia wanasema waarabu wakaanza ku danganya na colonize Afrika kwa nguvu, na kuchukua maliasili na kulazimisha dini juu ya waafrika ikabidi ikubalike. Wengine wanasema watu wakaanza kukubali dini ndio maana wengi wao wakaanza kuwa fuata waarabu kwa kua wameleta uislamu, ila historia imeandikwa na mwarabu pia, wasomi kama ibn batutah ni descendent ya waarabu ambao wameanza kuishi afrika.

ibn batutta.jpg

"The study of the Arab slave trade, like the Atlantic slave trade and the continental trade, are not just historical events, they are also political tools, and maneuvered around as such. It has become increasingly important to deal with both the historical as well as the political in any treatment of these subjects in our contemporary moment." quote kutoka hapa

Fanya research, mi sio mwana historia, ila nasoma tu wana historia wanachosema, naweza nikakosea facts mbili tatu.
 
View attachment 722624

mkuu nimekuelewa vyema ...tena sana tu nikitulia nitaipitia vyema hiyo link""ili niende kupata ufumbuzi zaidi""" ila kma hutojali naomba uniwekee hapa baadhi ya vitabu/source mbali mbali ambazo zitanisaidia kuweza kuifahamu vyema historia ya mtu mweusi ""
 
Wasalaam aiseh Mr Michael Mkwanzania@, mada yako imenivuta na kunivutia sana haswaa mpangilio wa mada,matukio nk.

Lakini yote ya yote waswahili wanasema, "mwenye mali hana akili na mwenye akili hana mali "
hivyo ni wakati sasa wa kila mmoja wetu kutambua uwepo wake duniani maana hakuna kilichoumbwa bila sababu
 
mkuu nimekuelewa vyema ...tena sana tu nikitulia nitaipitia vyema hiyo link""ili niende kupata ufumbuzi zaidi""" ila kma hutojali naomba uniwekee hapa baadhi ya vitabu/source mbali mbali ambazo zitanisaidia kuweza kuifahamu vyema historia ya mtu mweusi ""
anza na link hizi hapa

Crash course - hii kwa historia kwa ufupi (zipo nyingi, ila tafuta za afrika kwenye hii YouTube channel)

page za facebook
Real African Writers
Afrikan Centered Education

nitaongeza link polepole.
 
Asante kwa makala inayohamasisha kufikiri.
Lakini kuna upande wa pili wa kwetu watu weusi unaotufanya tutiliwe shaka kuhusu utimamu wetu na uwezo wetu wa kufikiri.
Inakuwaje mtu mweupe ameweza kututawala kwa mabavu hapo mwanzoni halafu akaendelea kutulaghai na kutuhadaa mpaka kesho ...?
Kwa nini kosa tulilofanya jana bado tunalirudia kila leo na hatimae kutugharimu kesho yetu. .?
Ninaposema ndani yetu inatia shaka na kuwapa nguvu wale wasemao kuwa tuna uwezo mdogo wa kufikiri huwa ninajaribu kurejearejea kichwani mwangu juu ya tunachofanyiwa na watu weupe ambacho sisi tunashindwa kulipiza kwao
Inakuwaje tulishindwa kuwatawala badala yake wakatutawala na kutufanya vijakazi na watumwa. ..?
Inakuwaje tunashindwa kuwalaghai au walau twende nao sawa kwenye mgawanyo wa rasilimali zetu ili nasi tufaidike,sijapatapo kusikia mkataba wowote uliosainiwa baina ya mweupe/mzungu na mweusi ambamo kwenye mkataba huo mweusi amemlalia mzungu
Lakini pia ni vp tumeshindwa kumshawishi mtu mweupe/mzungu amuangamize mwenzie badala yake ni wao ndio vinara wa kutufarakanisha na kusababisha tuane wenyewe kwa wenyewe, mf Congo, Angola nk
Huoni kwa uchache wa hayo niliyoyataja ukijumlisha na maendeleo mengine ya kimazingira walio nayo kwamba ni kweli mtu mweusi ana tatizo fulani kwenye ubongo
 
Video hii inaelezea zaidi utata kati ya historia tunayoifahamu yenye utata kidogo kwa sababu waarabu wameibadili.
"All societies select what they want to remembered, but only Africans have been totally denied a history or their own for so long."

Kuna vinchi viko hapo North Africa tu vinajibaraguza kwamba wao sio Waafrika.
Vipi unaweza pata maendeleo wewe kwa kuwakataa na kuwakana watu wa Damu yako kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom