Leo ndio Leo, Asemaye Kesho......

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,726
5,442
Habari za Jumapili wapendwa wachangiaji na wasomaji wa mada mbalimbali zinaletwa na wadau hapa Jf kila siku.
Twende moja kwa moja kwenye mada.....
Linapokuja suala la kufanya mabadiliko ya mfumo wa maisha, kutoka hasi kwenda chanya, kutoka kwenye ubaya kwenda kwenye wema;- wengi hupenda kusema ipo siku nitabadilika tu. Kwamba hiyo siku isiyojulikana itafika ambayo mhusika atabadilika.

Tukumbuke kwamba sisi wanadamu tumepewa siku TATU za kuishi..... JANA, LEO na KESHO. Jana tayari imeshapita. Zimebaki siku mbili tu, LEO NA KESHO. Tufahamu pia kuwa KESHO haina uhakika sana, kwa kuwa haipo mikononi mwetu. Kwa hiyo siku pekee tuliyo nayo ni LEO.

MUNGU ametupatia LEO. Hakuna unachoweza kufanya kuhusu JANA yako. Imeshapita. KESHO pia inaweza isiwe yako. Lakini LEO unapoendelea kusoma ujumbe huu, iko mikononi mwako. Unaweza kufanya badiliko la kweli LEO. Kama kweli umeamua kubadilika, badilika sasa. Na Mungu aliyekuumba na kuendelea kukupa uzima na afya atakusaidia kubadilika SASA katika Jina la Yesu Kristo.

2 Wakorintho 6: 2b........ "tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama SIKU ya WOKOVU ndiyo SASA."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom