Chigwiyemisi
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 531
- 225
Siku za hivi karibuni tumeshuhudia migogoro kadhaa ndani ya vyama vya siasa. Migogoro mikubwa ilikuwa kwenye vyama vitatu, CCM, NCCR-Mageuzi na CUF. Yaliyotokea wote tumeyaona. NCCR wamemfukuza Mbunge wao David Kafulila na CUF wamemfukuza mbunge wao Hamad Rashid. Sina uhakika kama migogoro ndani ya vyama hivyo itafikia mwisho ama laa ikizingatiwa kuwa wote waliofukuzwa wameshitaki mahakamani. Lakini kwa mtazamo wangu nimeona nia na uthubutu walionao viongozi wa vyama hivi viwili katika kushughulikia matatizo yao! Sitaki kuzungumzia kama wameonewa au hawajaonewa lakini uthubutu ni ishara ya ukomavu kiuongozi.
Kwa upande wa CCM, wadau wote wanaofuatilia siasa wanajua jinsi ambavyo chama hiki kimepata shida kutekeleza falsafa yake ya kujivua gamba. Kila kinapojaribu kung'ata kiungua moto mdomoni na kutema! Mwenyekiti wake ameshindwa kabisa kuchukua hatua dhidi ya wale wanaoitwa mafisadi kwenye chama chake! Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa kiongozi mkubwa katika chama chochote kikubwa cha siasa. Ameruhusu watu kuwa maarufu zaidi ya chama! Failure, failure, failure!
Kwa misingi hiyo nimelazimika kuona kuwa Mbatia na Maalim Seif wana uthubutu kuliko JK!
Jadili!