Shajara Yangu Mpambano wa Maalim na Komando Uchaguzi Mkuu Zanzibar 1995

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
SHAJARA YANGU UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR MPAMBANO WA MAALIM NA KOMANDO 1995

Miaka 29 sasa imetimu toka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 baada ya mapinduzi na muungano mwaka wa 1964.

Niko Zanzibar na fikra zangu zimerejea nyuma juma la mwisho mwezi October 1995 kuelekea siku ya kupiga kura tarehe 22 siku ya Jumapili.

Jumamosi jana yake tarehe 21 nimefika Zanzibar asubuhi siku ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu na boti yetu maarufu miaka ile Flying Horse, yaani Farasi Arukaye.

Wala hakuwa farasi anaeruka.

Farasi huyu akijikokota kati ya Zanzibar na Dar es Salaam.

Boti za kasi zilikuja baadae.

CUF ilikuwa inafunga kampeni yake kwa mkutano mkubwa Kibanda Maiti na Maalim Seif na Lipumba walionguruma katika viwanja hivyo.

Nalitumia neno hili "ngurumo," kwa makusudi kwani kwa hakika viongozi hawa siku ile waliunguruma.

Lipumba kwa kipindi kifupi na kwa namna ya ajabu alikuwa amefanikiwa kuingiza mtazamo mpya katika siasa za Tanzania kwa kuwaongoza Watanzania hasa vijana wa rika lake kutoka Tanganyika katika siasa za Zanzibar.

Katika kundi hili la Watanganyika walioingia CUF na kujihusisha na CUF na kumuunga mkono Maalim Seif lilikuwa kundi la vijana kutoka Tanganyika waliokuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana wenzao visiwani.

Lakini vijana hawa walikuwa na agenda yao ya ziada na maalum.

Hii ilikuwa silaha ambayo CUF na Maalim waliitumia vizuri na ndiyo iliyojenga msingi wa ngome ya chama Tanzania Bara.

Ushindani baina ya CUF na CCM ulikuwa mkubwa sana ukikumbusha siasa za miaka iliyopita Zanzibar ilipokuwa inapigania uhuru wake kutoka kwa Waingereza.

Zile zilikuwa enzi za ZNP na ASP na ukipenda unaweza ukaichomeka ZPPP.

Mgombea wa CCM Dr. Salmin Amour maarufu kwa lakabu ya Komando na Maalim Seif mgombea wa CUF wanahitaji kitabu kizima kuwaeleza.

Dalili zilikuwa wazi kuwa mabadiliko makubwa yatatokea katika uchaguzi huu na taarifa za kitaalamu za wajuzi wa somo la uchaguzi walibashiri hivyo halikadhalika.

SAMAHANI
Katika video nasema uchaguzi ulikuwa 1997.
Ulimi umeteleza ni 1995.

View: https://youtu.be/quT0CfTkC_s
 
Mzee Mohamed, Salaam!kwa nn Salmin Amour aliitwa Comandoo??
 
Back
Top Bottom