tabibumtaratibu
JF-Expert Member
- May 29, 2011
- 2,405
- 1,181
Kwenye sarufi kuna kitu kinaitwa VIYEYUSHO,hiv ni vitu gani na aina zake ni zipi?
kwahyo Y ni kiyeyusho na pia ni kipashio? Kipashio nacho ni nini?Naomba nijaribu hapo VIYEYUSHO ni KONSONANTI ambazo zinazotamkwa kama IRABU. katika kiswahili kuna aina mbili za VIYEYUSHO navyo ni: "W" na "Y" vipashio hivi viwili katika kutamka huweza kutamkwa kama IRABU. Kipashio "W" hutamka kama IRABU "U" Mfano: "Wanacheza" inatamkwa "Uanacheza" utakubaliana na mimi kama utaweza kutamka vema neno hilo, lakini pia kipashio "Y" kinatamkwa kama IRABU "i" mfano: "Yale" inatamka "iale"Sababu hiyo ndio inayofanya vipashio hivi kuitwa VIYEYUSHO. Vilevile katika lugha ya kiingereza vinaitwa SEMI-VOWEL ambavyo ni "W" na "J" Hii ni kwa mujibu wa uwezo wangu. Sijui kama nimekuelewesha kidogo au nimekuchanganya