Jamani mtu huyu kalikosea nini Taifa

Kuna mtu aliambiwa na Nyerere kuwa bado hajawa tayari kuwa kiongozi na mpaka sasa anapeta. Unasemaje kuhusu utabiri huo wa mzee kuhusu huyo jamaa ambaye kwa sasa ndiye kinara wa chama alichokianzisha Nyerere?
Yaelekea Wewe sio mtu wa kuelewa vizuri, una hoja nzuri ila hauwezi kuzifafanua.

Umesema vizuri jk aliambiwa bado hajawa tayari, ni sawa kabisa kipindi hicho alikuwa na age ya 40 bado kijana kuongoza kwani rafiki zake wote walikuwa masharobalo aliambiwa asubiri akue kwanza.

Na ikapita after 10 years akawa tayari hadi sasa yupo lakini alitahadharishwa kuwa EL hafai, yeye hakufuata yakamkuta hadi anaitwa Kilaza.

Umeongea kwa makini kumbe Huelewi fresh.....
 
Nani kamfanya awe tajiri wa kiasi hicho cha kumuita unexplained Wealth?.Je ni mtu,watu,mfumo au kitu gani kilichomsababisha awe na Utajiri huo.Mimi nafikiri tusimlaumu sana yeye,ila tuangalie ni mfumo upi mbaya uliyompa yeye nafasi ya kutenda yote hayo na ni nani alikuwa ana uwezo wa kumzuia asifanye hayo ila yeye hakuwajibika kwa kufanya kazi ilivyompasa.

Huwezi kumsifu mwizi aliyekuibia kisa eti ulisahau kufunga mlango...
 
Maneno ya mwalimu dhidi john samwel malecela yalitamkwa hadharani bila kutafunwa, akayaandika na ndio ulikuwa utamaduni ulotukuka wa mzee wetu huyu.

Nawaomba wana jf na watz kwa ujumla ni taarifa ipi,wapi, na andiko lipi lililomuhusisha mwalimu nyerere na edward lowasa?

Nawaomba sana mnipatie hili ili tuachane na gossips ambazo hazina tija kwetu zaidi ya siasa mpya za fitina .

Kosa pekee ambalo mimi nalikumbuka na kama mtarejea magazeti ya uhuru 1995 ccm primaries dodoma kuna picha na taarifa direct za edward lowassa na j.j. Guninita wakilia kwa huzuni baada ya b.w.mkapa kuwa ndie mteule na siyo j.m.kikwete...
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni........
 
EL mungu kamjalia kila kitu kilichobaki ni kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania,na njia ya kufika huko ni kumtumia swahiba wake wa kufa na kuzikana jk na ufisadi alionao,watanzania wanatakiwa kuwa makini nae kama alivyosema baba wa taifa
 
Kwa nini kila analofanya linaonekana baya machoni mwa watanzania
Nyerere alimwambia kuwa nchi haiwezi kuongozwa na bepari kama yeye, kwani kuwa tajiri ni kosa?
Kikwete akamwambia asante kwa msaada wako lakini naomba ujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa, hivi taifa ni nani.
Kama hiyo haitoshi sote tunajua yeye na JK walivyohangaika pamoja hadi kutokea kuitwa Boyz 2 Men sasa anaambiwa hatakiwi kwenye chama wala sura yake haitakiwi kuonekana nec wakati yeye ni waziri mkuu mstaafu,sawa.
Kama vile tena haitoshi wanataka kumpokonya kadi yake ili akose hata ubunge alioutolea jasho, jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.

kwasababu ni mmoja wapo kati ya watu wasio na uchungu wa nchi yetu.
 
Yaelekea Wewe sio mtu wa kuelewa vizuri, una hoja nzuri ila hauwezi kuzifafanua.

Umesema vizuri jk aliambiwa bado hajawa tayari, ni sawa kabisa kipindi hicho alikuwa na age ya 40 bado kijana kuongoza kwani rafiki zake wote walikuwa masharobalo aliambiwa asubiri akue kwanza.

Na ikapita after 10 years akawa tayari hadi sasa yupo lakini alitahadharishwa kuwa EL hafai, yeye hakufuata yakamkuta hadi anaitwa Kilaza.
JAKAYA ALILIPINGA HILO KTK HOJA ZAKE AKI QUOTE HATA NYERERE ALIPEWA NCHI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 39 WAKATI YEYE YUKO 40S NA AMEKAA MADARAKANI NA KUPATA UZOEFU KITU AMBACHO MWALIMU HAKUWA NACHO.... NENDENI MKAICHECK SPEECH YAKE YA KUUTAKA URAIS 1995.......

UKWELI UTABAKI UKWELI JAMANI KUNA NINI LOWASSA KAWAKOSEA WATZ? NI MCHAFU HIVYO? AU NI KITENDO CHA KUWA RAFIKI WA UKWELI WA JMK 2005 ?

CCM INAJIVUA GAMBA WACHA TUYATAFAKARI HAYA...........
 
tatizo la el alivyokuwa pm alikuwa much know alikuwa anataka kumpiku boss wake
ndio sumu aliyolishwa jmk na watu wa karibu sana na yeye kuliko alivyo enl......, matokeo yake ni haya.... Nadhani lowasa alipaswa kujua beyond urafiki wao kabla ya ku team up naye na zaidi kujishusha yeye ili rafiki aende salama.....

Siasa ni hatari sana .... Leo namuona gbagbo ktk michuzi inanitia kichefuchefu hata kuisogelea sana
 
Kumbuka alisema yeye na JK hawakukutana mitaani. Kile chuma ni kazi ngumu sana kukiondoa, ingawa ni kilaza tu kama Kikwete so hata akiondolewa katika chama chao Taifa halitapata hasara yoyote. Nina uhakika na yeye hawezi kuondoka hivihivi, anaweza kuleta uasi ambao utakiua kabisa chama cha mapinduzi. Kumbuka JK naye anakaribia kuondoka kwa hiyo atatafuta watu wa kumsitiri akitoka Ikulu, na hawezi kuwaamini watu aliokutana nao mitaani....
 
Kosa la Edward Lowassa unayejaribu kumtetea ni kuwa ana utajiri usiolezeka (unexplained wealth) kwa kiongozi wa umma. Sheria za rushwa Tanzania zinataka viongozi wa umma wenye unexplained wealth wachunguzwe na wafikishwe mahakamani kwa ufisadi. Sote tunajua kama WikiLeaks walivyosema kuwa JK amewazuia PCCB kuwachunguza vigogo.

Lowassa ni dhahiri kuwa siyo kiongozi mwadilifu. Alihusika na kashfa ya ufisadi ya Richmond inayomilikiwa na swahiba wake Rostam Aziz. Alipata utajiri mkubwa usioelezeka akiwa waziri wa ardhi na madili ya viwanja. Amepora kiwanja cha Nyumba ya Sanaa karibu na Movenpik na anajenga gorofa la 70 billion shillings.

Amenunua jumba la kifahari London la thamani ya 1 billion shillings na anachunguzwa na Metropolitan Police ya UK kwa money laundering (rejea stori ya Raia Mwema).

Ana assets nyingi na kubwa sana za multi-million dollars ndani na nje ya nchi. Ni dhahiri kuwa huyu si kiongozi mwadilifu na hafai kuwa madarakani. Kwa ufupi, kosa la Lowassa ni kuwa yeye ni mwanasiasa fisadi.

Need we say more?

Lowasa hana kosa Lolote maana hakuna mtu ambaye ameshawahi kulalamika kuwa ameibiwa au kuombwa rushwa na Lowasa. Utajiri wa Lowasa ni wakurithi kutoka kwa Baba yake, hii ndiyo maana kwa wanaomjua vizuri kwenye miaka ya 1966 Lowasa alikuwa anamiliki Gari. Nisingethubutu kumtetea Lowasa kama kungekuwa na taarifa kuwa alishawahi kufikishwa mahakamani kwa wizi au ubadhilifu. Tatizo la Watanzania ni kuwa ukiwa mtafutaji ukafanikiwa unaambiwa umeiba au fisadi, kwa hiyo kwa nyie mnaohoji mtaji wa Lowasa mnaweza kutuambia ni kiasi gani cha utajiri mngetaka awe nacho? hivi kati ya watu matajiri wakiitwa Lowasa naye atatokea? Je mnaweza kutuambia vyanzo vya utajiri vya watu wengine? Acheni wivu na majungu ya kiswahili.
 
Quinine,
Let's make it clear, this way. Lowasa hakustaafu uwaziri mkuu, alifukuzwa (kwa ustaarabu tu tunasema alijiuzulu). Hadhi ya Lowasa si sawa na Sumaye wala Salim, wala Mhe. Malecela, katika cheo cha waziri mkuu.
Clear?

Well coppied na wasirudie kumuita mstaafu huwaga napata kideri kama cha kuku nikisikiaga jina hilo aisee.
 
Tajiri mwizi hafai ila kutumia pesa zake kuingia madarakani sawa.

Hadi sasa hivi watanzania wote tunataabika na tatizo la umeme sababu yake, halafu unasema anatumia pesa zake. Mtu tuliyemfahamu tangu akiwa AICC Arusha sio huyu wa sasa na siku zote alikuwa mtumishi wa uma. Atueleze ni lini alifanya biashara hadi akafika hapo alipo na athibitishe kuwa alitajirika kialali. Kwajinsi alivyo tajiri anatushawishi vipi kuwa haingii ikulu kujilimbikizia mali??????
 
Kosa la Edward Lowassa unayejaribu kumtetea ni kuwa ana utajiri usiolezeka (unexplained wealth) kwa kiongozi wa umma. Sheria za rushwa Tanzania zinataka viongozi wa umma wenye unexplained wealth wachunguzwe na wafikishwe mahakamani kwa ufisadi. Sote tunajua kama WikiLeaks walivyosema kuwa JK amewazuia PCCB kuwachunguza vigogo.

Lowassa ni dhahiri kuwa siyo kiongozi mwadilifu. Alihusika na kashfa ya ufisadi ya Richmond inayomilikiwa na swahiba wake Rostam Aziz. Alipata utajiri mkubwa usioelezeka akiwa waziri wa ardhi na madili ya viwanja. Amepora kiwanja cha Nyumba ya Sanaa karibu na Movenpik na anajenga gorofa la 70 billion shillings.

Amenunua jumba la kifahari London la thamani ya 1 billion shillings na anachunguzwa na Metropolitan Police ya UK kwa money laundering (rejea stori ya Raia Mwema).

Ana assets nyingi na kubwa sana za multi-million dollars ndani na nje ya nchi. Ni dhahiri kuwa huyu si kiongozi mwadilifu na hafai kuwa madarakani. Kwa ufupi, kosa la Lowassa ni kuwa yeye ni mwanasiasa fisadi.

Need we say more?

Hafaii na si kwamba watu wanamuonea tu anstahili kupigwa risasi hadharani:rip:
 
jaribuni kumchukua nyinyi CHADEMA(MKASKAZINI MWENZENU) LABDA ATAWASAIDIA KUPATA URAISI 2015 BAADA YA SLAA KUANGUKIA PUA

Ulikosea njia kuja JF wewe, una IQ ndogo sana hadi kuanza kufikiria ukanda. Kwani Kaskazini ndio hawaathiriki na aliyoyatenda? Tena kwa taarifa yako huko Arusha ndio wanataabika zaidi sababu ya kupinga chama tawala. Nani asiyejua kuwa EL alikuwa na mkono wake kuhakikisha jimbo la Arusha mjini linabaki CCM?
Ningekujua ningekulabua viboko ukamwonyeshe mkeo
 
lowasa hana kosa lolote maana hakuna mtu ambaye ameshawahi kulalamika kuwa ameibiwa au kuombwa rushwa na lowasa. Utajiri wa lowasa ni wakurithi kutoka kwa baba yake, hii ndiyo maana kwa wanaomjua vizuri kwenye miaka ya 1966 lowasa alikuwa anamiliki gari. Nisingethubutu kumtetea lowasa kama kungekuwa na taarifa kuwa alishawahi kufikishwa mahakamani kwa wizi au ubadhilifu. Tatizo la watanzania ni kuwa ukiwa mtafutaji ukafanikiwa unaambiwa umeiba au fisadi, kwa hiyo kwa nyie mnaohoji mtaji wa lowasa mnaweza kutuambia ni kiasi gani cha utajiri mngetaka awe nacho? Hivi kati ya watu matajiri wakiitwa lowasa naye atatokea? Je mnaweza kutuambia vyanzo vya utajiri vya watu wengine? Acheni wivu na majungu ya kiswahili.

bora useme vilaza wanaleta hoja zimajungu majungu humu hawakawii huko mbele mtoto wa mengi naye akiingia kwenye siasa wakaja mwita fisadi
 
Back
Top Bottom