Jamani mtu huyu kalikosea nini Taifa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Kwa nini kila analofanya linaonekana baya machoni mwa watanzania
Nyerere alimwambia kuwa nchi haiwezi kuongozwa na bepari kama yeye, kwani kuwa tajiri ni kosa?
Kikwete akamwambia asante kwa msaada wako lakini naomba ujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa, hivi taifa ni nani.
Kama hiyo haitoshi sote tunajua yeye na JK walivyohangaika pamoja hadi kutokea kuitwa Boyz 2 Men sasa anaambiwa hatakiwi kwenye chama wala sura yake haitakiwi kuonekana nec wakati yeye ni waziri mkuu mstaafu,sawa.
Kama vile tena haitoshi wanataka kumpokonya kadi yake ili akose hata ubunge alioutolea jasho, jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.
 
Kuwa tajiri sio kosa, ila tajiri anayejipatia utajiri wake kwa njia zisizo sawa ni makosa. Ni wizi. Tajiri mwizi hafai kuwa kiongozi wa nchi, ataendelea kuwaibia hao anaowaongoza.

Msaada unaoingizia hasara kubwa taifa-richmond- ni ufisadi kwa taifa aliloapa kuliongoza.
Kwa tuhuma hizo na nyingi ni sahihi kuondolewa kwenye vyombo vya maamuzi vya chama kama NEC na CC. Nadhani hiyo ingekuwa adhabu tosha kwake.

Suala la kunyang'anywa kadi ili akose na ubunge, lipo mikononi mwake. Kwa busara yake tu anapaswa kujiuzulu kuwatumikia watu wa jimbo lake hata kama atabaki kuwa mwana CCM. Kama hakufaa kuongoza watanzania, ambao wanaMonduli ni sehemu yake, hata faa abaki kuwaongoza wana Monduli.

Nasema haya kama hizo tuhuma ni za kweli. Kama sio za kweli basi na asonge mbele na maisha kama mtanzania yeyote, tujenge taifa pamoja.
 
hawawezi kumfanya chochote ...hayo ni makelele tu wa utaona subiri ..kwanza si alisema JK huyu bwana kapata ajali ya kisiasa tu
 
Kosa la Edward Lowassa unayejaribu kumtetea ni kuwa ana utajiri usiolezeka (unexplained wealth) kwa kiongozi wa umma. Sheria za rushwa Tanzania zinataka viongozi wa umma wenye unexplained wealth wachunguzwe na wafikishwe mahakamani kwa ufisadi. Sote tunajua kama WikiLeaks walivyosema kuwa JK amewazuia PCCB kuwachunguza vigogo.

Lowassa ni dhahiri kuwa siyo kiongozi mwadilifu. Alihusika na kashfa ya ufisadi ya Richmond inayomilikiwa na swahiba wake Rostam Aziz. Alipata utajiri mkubwa usioelezeka akiwa waziri wa ardhi na madili ya viwanja. Amepora kiwanja cha Nyumba ya Sanaa karibu na Movenpik na anajenga gorofa la 70 billion shillings.

Amenunua jumba la kifahari London la thamani ya 1 billion shillings na anachunguzwa na Metropolitan Police ya UK kwa money laundering (rejea stori ya Raia Mwema).

Ana assets nyingi na kubwa sana za multi-million dollars ndani na nje ya nchi. Ni dhahiri kuwa huyu si kiongozi mwadilifu na hafai kuwa madarakani. Kwa ufupi, kosa la Lowassa ni kuwa yeye ni mwanasiasa fisadi.

Need we say more?
 
Kuwa tajiri sio kosa, ila tajiri anayejipatia utajiri wake kwa njia zisizo sawa ni makosa. Ni wizi. Tajiri mwizi hafai kuwa kiongozi wa nchi, ataendelea kuwaibia hao anaowaongoza.

Msaada unaoingizia hasara kubwa taifa-richmond- ni ufisadi kwa taifa aliloapa kuliongoza.
Kwa tuhuma hizo na nyingi ni sahihi kuondolewa kwenye vyombo vya maamuzi vya chama kama NEC na CC. Nadhani hiyo ingekuwa adhabu tosha kwake.

Suala la kunyang'anywa kadi ili akose na ubunge, lipo mikononi mwake. Kwa busara yake tu anapaswa kujiuzulu kuwatumikia watu wa jimbo lake hata kama atabaki kuwa mwana CCM. Kama hakufaa kuongoza watanzania, ambao wanaMonduli ni sehemu yake, hata faa abaki kuwaongoza wana Monduli.

Nasema haya kama hizo tuhuma ni za kweli. Kama sio za kweli basi na asonge mbele na maisha kama mtanzania yeyote, tujenge taifa pamoja.
Tajiri mwizi hafai ila kutumia pesa zake kuingia madarakani sawa.
 
Ni muhimu sana kwangu kumpima umakini wa Kikwete na kama anamaanisha anayosema akiwa anatabasamu au ni usanii

Alisema ni mtu safi na mchapakazi na alikutwa tu na ajali ya kisiasa....sasa ngoja tupate taarifa za kikao nipate kipimo kingine cha umakini wa JK na maneno yake au ni uropokaji wa kawaida ......ndipo nitakapojua kuna la kuskiliza kwa JK au ni maneno tu akiwa hata haelewi anavyosema

Kwangu, Lowassa ni kipimo cha umakini wa JK
 
Nani kamfanya awe tajiri wa kiasi hicho cha kumuita unexplained Wealth?.Je ni mtu,watu,mfumo au kitu gani kilichomsababisha awe na Utajiri huo.Mimi nafikiri tusimlaumu sana yeye,ila tuangalie ni mfumo upi mbaya uliyompa yeye nafasi ya kutenda yote hayo na ni nani alikuwa ana uwezo wa kumzuia asifanye hayo ila yeye hakuwajibika kwa kufanya kazi ilivyompasa.
 
Bahari imechafuka! Meli(ccm) inayumba sana. Mizigo mizito inatoswa baharini! Dhoruba ikizidi usishangae kusikia hata nahodha anajirusha baharini!!
 
Tatizo nyerere alimkataa, na nyerere ni nabii, JK alipuuza unabii wa nyerere akampa Lowasa madaraka makubwa yaliyotokea ni historia. Viongozi wote ambao nyerere aliwanyooshea kidole kwamba hawafai hawawezi kupata uongozi wa juu wa nchi wakadumu, mfano malecela japo siyo fisadi ila alinyooshewa kidole na nyerere kuwa hafai kuongoza, mzee wa watu kajitahidi apate uongozi wa juu wa nchi ila wapi kaishia kulalamika kwamba sasa yeye amekuwa ni buldozer anatengeneza njia ikikamilika haruhusiwi kupita.Kwa hiyo hata kama Lowasa akipita njia anazojua mwenyewe na akaukwaa urais, naamini hatakaa sana kwenye urais atajikuta katolewa either kwa kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye au kwa kujiuzulu mwenyewe kwa litakalotokea.Jamani, lazima tukubaliane kwamba nyerere hakuwa mtu wa kawaida, amekufa ila bado yupo mioyoni mwa watz wengi, ndio maana viongozi wetu wanamrejea sana nyerere katika kuhalalisha mambo yao, lakini kwa kuwa wanamrejea nyerere bila kuwa na dhati moyoni bali kwa nia ya kuwavuta tu wananchi ndio maana hawafanikiwi. Akitokea kiongozi yeyote tz akamrejea nyerere kwa dhati na kufuata nyayo za nyerere kiongozi huyo ataiweza tz, nje ya hapo ni matatizo tu kama sasa. Siyo kwamba nyerere hakuwa na makosa, la hasha alikuwa nayo ila makosa yake yanasameheka kwa kuwa hakuyafanya ili ajinufaishe yeye bali aliyafanya ili taifa linufaike na wala haikuwa dhamira yake kufanya makosa hayo.
 
Kwa maoni yangu,mfanyabiashara yoyote hawezi kuwa rais wa nchi ya kisoshalisti.
 
acheni kujifurahisha
el ndio next presida...
tujadili jinsi ya chedema kupata viti viiingi vya ubunge.
 
Maneno ya Nyerere yalikuwa ni LAANA tosha kwa Lowassa na laana hiyo itaendelea kumtafuna mpaka dakika ya mwisho ya uhai wake.
 
Usipate shida kuelewa maana ya hizi mbio za sakafuni CCM bado tunazisoma kwa kina na kuja kuyatolea maelezo zaidi. Acha wapoteze muda wao!!!!!!!
 
Back
Top Bottom