Jamani mtu huyu kalikosea nini Taifa

Kwa nini kila analofanya linaonekana baya machoni mwa watanzania
Nyerere alimwambia kuwa nchi haiwezi kuongozwa na bepari kama yeye, kwani kuwa tajiri ni kosa?
Kikwete akamwambia asante kwa msaada wako lakini naomba ujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa, hivi taifa ni nani.
Kama hiyo haitoshi sote tunajua yeye na JK walivyohangaika pamoja hadi kutokea kuitwa Boyz 2 Men sasa anaambiwa hatakiwi kwenye chama wala sura yake haitakiwi kuonekana nec wakati yeye ni waziri mkuu mstaafu,sawa.
Kama vile tena haitoshi wanataka kumpokonya kadi yake ili akose hata ubunge alioutolea jasho, jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.

Laana inamwandama.
 
Jamani baba wa taifa alishamlaani kwa kumuuliza mali zote alizipataje na mpaka anafariki hakumjibu hilo swali na ndio ikawa laana asubiri labda baba wa taifa atafufuka ndio amwondolee laana
 
jaribuni kumchukua nyinyi CHADEMA(MKASKAZINI MWENZENU) LABDA ATAWASAIDIA KUPATA URAISI 2015 BAADA YA SLAA KUANGUKIA PUA
 
Kosa la Edward Lowassa unayejaribu kumtetea ni kuwa ana utajiri usiolezeka (unexplained wealth) kwa kiongozi wa umma. Sheria za rushwa Tanzania zinataka viongozi wa umma wenye unexplained wealth wachunguzwe na wafikishwe mahakamani kwa ufisadi. Sote tunajua kama WikiLeaks walivyosema kuwa JK amewazuia PCCB kuwachunguza vigogo.

Lowassa ni dhahiri kuwa siyo kiongozi mwadilifu. Alihusika na kashfa ya ufisadi ya Richmond inayomilikiwa na swahiba wake Rostam Aziz. Alipata utajiri mkubwa usioelezeka akiwa waziri wa ardhi na madili ya viwanja. Amepora kiwanja cha Nyumba ya Sanaa karibu na Movenpik na anajenga gorofa la 70 billion shillings.

Amenunua jumba la kifahari London la thamani ya 1 billion shillings na anachunguzwa na Metropolitan Police ya UK kwa money laundering (rejea stori ya Raia Mwema).

Ana assets nyingi na kubwa sana za multi-million dollars ndani na nje ya nchi. Ni dhahiri kuwa huyu si kiongozi mwadilifu na hafai kuwa madarakani. Kwa ufupi, kosa la Lowassa ni kuwa yeye ni mwanasiasa fisadi.

Need we say more?

Simtetei Lowasa, ila kuhusu unexplained wealth, viongozi wengi ndani ya CCM na Serikali wana utajiri usioelezeka wala kumithirika. Wote wakifuatiliwa itakuwa aibu! Kwa Lowasa ni kwamba zimeonekana kama ulivyoziorodhesha baadhi lakini hali ni kama hiyo tu kwa viongoozi wote ndani ya CCM na Chama
 
Lowasa ana matatizo yake lakini mengi sana lakini siyo hatari kwa taifa hili kama boss wake wa zamani ambaye anaipeleka nchi hii pabaya sana naomba nirudie pabaya sana! bahati mbaya aliyonayo Lowasa ni kwamba watu wa dini yake wanaona ufisadi ni ufisadi na hawalindi mwovu!
 
Tatizo nyerere alimkataa, na nyerere ni nabii, JK alipuuza unabii wa nyerere akampa Lowasa madaraka makubwa yaliyotokea ni historia. Viongozi wote ambao nyerere aliwanyooshea kidole kwamba hawafai hawawezi kupata uongozi wa juu wa nchi wakadumu, mfano malecela japo siyo fisadi ila alinyooshewa kidole na nyerere kuwa hafai kuongoza, mzee wa watu kajitahidi apate uongozi wa juu wa nchi ila wapi kaishia kulalamika kwamba sasa yeye amekuwa ni buldozer anatengeneza njia ikikamilika haruhusiwi kupita.Kwa hiyo hata kama Lowasa akipita njia anazojua mwenyewe na akaukwaa urais, naamini hatakaa sana kwenye urais atajikuta katolewa either kwa kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye au kwa kujiuzulu mwenyewe kwa litakalotokea.Jamani, lazima tukubaliane kwamba nyerere hakuwa mtu wa kawaida, amekufa ila bado yupo mioyoni mwa watz wengi, ndio maana viongozi wetu wanamrejea sana nyerere katika kuhalalisha mambo yao, lakini kwa kuwa wanamrejea nyerere bila kuwa na dhati moyoni bali kwa nia ya kuwavuta tu wananchi ndio maana hawafanikiwi. Akitokea kiongozi yeyote tz akamrejea nyerere kwa dhati na kufuata nyayo za nyerere kiongozi huyo ataiweza tz, nje ya hapo ni matatizo tu kama sasa. Siyo kwamba nyerere hakuwa na makosa, la hasha alikuwa nayo ila makosa yake yanasameheka kwa kuwa hakuyafanya ili ajinufaishe yeye bali aliyafanya ili taifa linufaike na wala haikuwa dhamira yake kufanya makosa hayo.

Kuna mtu aliambiwa na Nyerere kuwa bado hajawa tayari kuwa kiongozi na mpaka sasa anapeta. Unasemaje kuhusu utabiri huo wa mzee kuhusu huyo jamaa ambaye kwa sasa ndiye kinara wa chama alichokianzisha Nyerere?
 
Simtetei Lowasa, ila kuhusu unexplained wealth, viongozi wengi ndani ya CCM na Serikali wana utajiri usioelezeka wala kumithirika. Wote wakifuatiliwa itakuwa aibu! Kwa Lowasa ni kwamba zimeonekana kama ulivyoziorodhesha baadhi lakini hali ni kama hiyo tu kwa viongoozi wote ndani ya CCM na Chama

Ndio maana inabidi nchi ijiondoe gamba hili linaloitwa CCM ili tufuatilie kwa karibu kujua vyanzo vya utajiri wa watumishi wa umma ambao waliapa kutumia raslimali za nchi kwa maendeleo yetu na wakaishia kujitajirisha wao na familia zao.
 
Kwa maoni yangu,mfanyabiashara yoyote hawezi kuwa rais wa nchi ya kisoshalisti.

Naunga mkono hoja yako. Mfanya biashara mkubwa kama EL aendelee na biashara zake na nina imani hakuna atakaye muongelea. Nadhani Bakhresa ni tajiri pia lakini yuko nje ya siasa na yuko na amani tele.
 
Kuna mtu aliambiwa na Nyerere kuwa bado hajawa tayari kuwa kiongozi na mpaka sasa anapeta. Unasemaje kuhusu utabiri huo wa mzee kuhusu huyo jamaa ambaye kwa sasa ndiye kinara wa chama alichokianzisha Nyerere?

Huyu bwana kwa maoni yangu hapeti kama unavyosema bali yuko taabani anateseka! Angeweza kukimbia angeishakimbia ndani ya siku 100 za awamu ya pili. Utabiri wa mzee nadhani uko uko pale pale.
 
Kwa nini kila analofanya linaonekana baya machoni mwa watanzania
Nyerere alimwambia kuwa nchi haiwezi kuongozwa na bepari kama yeye, kwani kuwa tajiri ni kosa?
Kikwete akamwambia asante kwa msaada wako lakini naomba ujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa, hivi taifa ni nani.
Kama hiyo haitoshi sote tunajua yeye na JK walivyohangaika pamoja hadi kutokea kuitwa Boyz 2 Men sasa anaambiwa hatakiwi kwenye chama wala sura yake haitakiwi kuonekana nec wakati yeye ni waziri mkuu mstaafu,sawa.
Kama vile tena haitoshi wanataka kumpokonya kadi yake ili akose hata ubunge alioutolea jasho, jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.

Quinine,
Let's make it clear, this way. Lowasa hakustaafu uwaziri mkuu, alifukuzwa (kwa ustaarabu tu tunasema alijiuzulu). Hadhi ya Lowasa si sawa na Sumaye wala Salim, wala Mhe. Malecela, katika cheo cha waziri mkuu.
Clear?
 
Kwa nini kila analofanya linaonekana baya machoni mwa watanzania
Nyerere alimwambia kuwa nchi haiwezi kuongozwa na bepari kama yeye, kwani kuwa tajiri ni kosa?
Kikwete akamwambia asante kwa msaada wako lakini naomba ujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa, hivi taifa ni nani.
Kama hiyo haitoshi sote tunajua yeye na JK walivyohangaika pamoja hadi kutokea kuitwa Boyz 2 Men sasa anaambiwa hatakiwi kwenye chama wala sura yake haitakiwi kuonekana nec wakati yeye ni waziri mkuu mstaafu,sawa.
Kama vile tena haitoshi wanataka kumpokonya kadi yake ili akose hata ubunge alioutolea jasho, jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.

Crime does not pay in the long run. Muda wake wa kuiba umeisha. Atapotelea mbali kama Carlos , the Jackal. Ni sheria ya maumbile na asili. .......hakuna aliyemwonea ila wakati wake , kama ilivyo kwa Gbagbo, umefika. Mark my words
 
Politics is all about timing na wakati huu ni wrong timing kwake amechafuka mbele ya raia wote wa TZ na busara kuheshimu mitazamo na misimamo ya wengi
 
Lowasa tatizo lake ni vision yake..anataka always awe juu ya wote,amejaribu kwa pesa amegundua money and wealth does not bring what he needs thats why anafight kwa kila namna apate ufalme
 
...jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.

  • Tunajua waziri mkuu anaenda upokea masurufu hata anapokoma kuwa waizri mkuu.
  • Waziri mkuu anaenda kutibiwa nje hata anapokoma kuwa waizri mkuu
Sasa tunashanga mtu mwenye nafasi ya waziri mkuu bado kuendelea kula dili kwa manufa yake binafisau ya familia au ya rafiki zake. nadhani mtu kama huyo hata kwenye mafaili ya TISS ya ukweli ni danger kwa usalama wa taifa.

Mtu kama huyo anaweza kuuza hata nchi na watu wake.
 
Crime does not pay in the long run. Muda wake wa kuiba umeisha. Atapotelea mbali kama Carlos , the Jackal. Ni sheria ya maumbile na asili. .......hakuna aliyemwonea ila wakati wake , kama ilivyo kwa Gbagbo, umefika. Mark my words

Nyumbu your argument have a lot of sense in it........that is nature at its best course......
 
Haya mbio za kumsafisha Lowassa zimeanza. Nasikia na sarakasi zinazoendelea huko dodoma ni strategy za kumsafisha jamaa kwa ajili ya 2015. Wamteue tu Lowassa ili Chadema, Cuf washinde kwa ulaini Kama kuua tembo kwa ubua
 
Back
Top Bottom