Elections 2010 Jamani Lyatonga Mrema kapatwa na ugonjwa gani?

ukistaajabu ya lyatonga kaa tayari kusikia ya slaa!...mi nafikiri sio njaa ila anajaribu kuwachanganya zaidi wananchi wa tanzania ili wajue maana nyingine ya upinzani!.....labda ifikie mahala watanzania wengi wakajua upinzani sio maana yake kupinga kila kitu cha chama tawala, na kujumuika na upinzani sio dhambi!.....na kama kuna neno mbadala litumike kuliko neno upinzani, nafikiri tukiviita vyama vyenza itakuwa poa zaidi...mrema amefanya kile ambacho kinaonekana ni ukakasi mbele ya macho na masikio ya wengi lakini ni ukomavu na ushujaa wa kuigwa!.....tusiwe kama sera za george bush alokuwa na usemi kuwa....."if youre not my friend then youre my enemy"......

vyama vyenza bado vunaweza kushiriki mikutano ya chama tawala na bado vikabaki na maadili yake na uadilifu wake.....
hebu fikiria ikatokea chadema ndo chama tawala, then watu wa cuf nao wasiendee? mbona bungeni cuf na chadema marafiki?
mrema upo sahihi kufanya unaloamini ni la kweli!
 
The poor fellow is politically bankrupt. Which brings Obama's call " Do you want another 5 years of the same or do you want CHANGE?"
 
Next time serikali itampeleka matibabu Sauzi au Uingereza ,sio India.
Huyu mtu anadisgrace kabila lake,maana inaonekana ni ndumilakuwili
 
Mrema anajua alichokusudia kufanya. Hebu tuangalie kwa jicho la tatu, pale kulikuwa na watu zaidi ya 2000, tena kutoka pande zote za Tanzania, watu walikuwa wanaangalia kwenye TV live kila kona ya nchi including Vunjo, alichoweza kufanya ni pamoja na kutangaza nia ya kugombea ubunge pamoja na kupata jukwaa la kuombea kura kupitia mgongo wa mkutano wa CCM. Katika hali ya kawaida, angepata wapi forum kubwa kama ile tena bure? Ile ni style aliyotaka nayo na ndiyo maana tunamjadili sasa!
 
Jamaa ni mjanja, alikuwa anafanya booking!

Siamini kama ni yule yule Augustine Lyatonga Mrema, ambaye mwaka 1995 pale Dar (viwanja vya Anatoglo) aliweza kukusanya maelfu ya watu na kusema mambo yafuatayo:
  • Kwamba CCM ni wezi na kuwa wengi wa viongozi ndani yake ni wachafu (wala rushwa),
  • Yeye kaamua kujitoa CCM kwavile ni mtu safi na sasa kaamua kuingia NCCR-Mageuzi ili awakomboe wanainji wa Inji hii,
  • Moja ya ufisadi wa CCM ni ushahidi wa dhahabu aliyoikamata pale DIA (sasa Julius Nyerere International Airport).
  • Pamoja na mengi mengine ambayo kwasasa siyakumbuki, japo siku hiyo nilikuwepo pale Anatoglo!
Kwahakika kwa wakati ule ingekuwa ni vigumu kwa yeyote mwenye akili timamu kama nilivyokuwa mimi, kuamini kuwa leo(2010) huyu Mrema angerudi na kuifagilia CCM, ni ajabu na kweli ila kwa siasa za Bongo inawezekana na sasa tunaona.

Nakumbuka pia kwenye kinyang'anyiro cha urais CCM 1995, baada ya Lowasa na JK kutokuteuliwa na chama wakati huo yeye Lyatonga alidai kuwasikitikia na kuwataka waje wajiunge na NCCR-Mageuzi. Hii inatisha nadhani sasa baada ya kuona umri ndo bye bye, afya nayo mgogoro kaona hana budi kujikomba kwa JK ili walau aambulie japo Ubunge wa viti maalumu mkoa wa Ikulu. Kwa leo yatosha.:lie:
 
ukistaajabu ya lyatonga kaa tayari kusikia ya slaa!...mi nafikiri sio njaa ila anajaribu kuwachanganya zaidi wananchi wa tanzania ili wajue maana nyingine ya upinzani!.....labda ifikie mahala watanzania wengi wakajua upinzani sio maana yake kupinga kila kitu cha chama tawala, na kujumuika na upinzani sio dhambi!.....na kama kuna neno mbadala litumike kuliko neno upinzani, nafikiri tukiviita vyama vyenza itakuwa poa zaidi...mrema amefanya kile ambacho kinaonekana ni ukakasi mbele ya macho na masikio ya wengi lakini ni ukomavu na ushujaa wa kuigwa!.....tusiwe kama sera za george bush alokuwa na usemi kuwa....."if youre not my friend then youre my enemy"......

vyama vyenza bado vunaweza kushiriki mikutano ya chama tawala na bado vikabaki na maadili yake na uadilifu wake.....
hebu fikiria ikatokea chadema ndo chama tawala, then watu wa cuf nao wasiendee? mbona bungeni cuf na chadema marafiki?
mrema upo sahihi kufanya unaloamini ni la kweli!


Umeielewa thread??
 
jamani huyo MRema, si akatulie kwao atunze afya yake, siasa ya nini sasa au ndio njaa? nahisi kwapatwa na kirusi cha akili
Legend
Umshukuru mungu sana kwa kutokuwa mheshimiwa. Ugonjwa wa hadhi hii ukiuzoea ni mbaya kama ukimwi.
Ndiyo maana wazee wengi[waheshimiwa] wakisikia mtu katangaza nia ya kugombea jimbo upesi huanza kulia pesa za mafisadi.
Lakini ukiangalia kwa undani ni kuwa wanajijua kuwa wamechuja hivyo na ndiyo maana wanalia lia ovyo.
Na ikifika kipindi cha kampeni huamkia hata wajukuu zao ili mradi wapenye kwenye uheshimiwa [unamkumbuka yule mlinzi aliyefukuzwa kazi kwa kutomtambua mheshimiwa??]
si unajua utamu wa asali???? Na inafikia mahala hawa wazee wanaamini kabisa kuwa nchi hii haiwezi kwenda bila wao
 
Mrema anajua alichokusudia kufanya. Hebu tuangalie kwa jicho la tatu, pale kulikuwa na watu zaidi ya 2000, tena kutoka pande zote za Tanzania, watu walikuwa wanaangalia kwenye TV live kila kona ya nchi including Vunjo, alichoweza kufanya ni pamoja na kutangaza nia ya kugombea ubunge pamoja na kupata jukwaa la kuombea kura kupitia mgongo wa mkutano wa CCM. Katika hali ya kawaida, angepata wapi forum kubwa kama ile tena bure? Ile ni style aliyotaka nayo na ndiyo maana tunamjadili sasa!

Kyachakiche
Kumbe umemuelewa mzee wa Kiraracha. The guy is crafty
 
...Hivi huyu Lyatonga ameugua ugonjwa gani au ni kweli kuwa alipandikiza ili aue upinzani
Lyatonga Mrema, kwani ameacha kazi lini uko UWT? Sidhani kama aliwahi kuwa mpinzani wa kikweli, zaidi ya kutimiza matakwa ya kazi aliyotumwa.
 
Mrema anajua alichokusudia kufanya. Hebu tuangalie kwa jicho la tatu, pale kulikuwa na watu zaidi ya 2000, tena kutoka pande zote za Tanzania, watu walikuwa wanaangalia kwenye TV live kila kona ya nchi including Vunjo, alichoweza kufanya ni pamoja na kutangaza nia ya kugombea ubunge pamoja na kupata jukwaa la kuombea kura kupitia mgongo wa mkutano wa CCM. Katika hali ya kawaida, angepata wapi forum kubwa kama ile tena bure? Ile ni style aliyotaka nayo na ndiyo maana tunamjadili sasa!

Heshima kwako Kyachekiche.

Mkuu afadhali wewe umemwelewa Mzee wa Kiraracha.wengine wanajaribu kumwona mjinga wakati hata Mtu huru katangaza kugombea ubunge Hai.Mtu wa kumshangaa ni Lipumba asietaka kusoma alama za nyakati.Ukweli ni kwamba CCM iatshinda tena ingawa sipendi hii hali lakini mpaka sasa sijaona juhudi za dhati za vyama vyote vya upinzani kutaka kuongoza dola.

Najua wako baadhi ya wachangiaji wasioamini Mzee wa Kiraracha atakuwa mbunge wa Vunjo lakini mtashanga sana jinsi atakavyopita kwa kishindo huko Vunjo kama hamuamini mulizeni Mheshimiwa Kimaro alivyogaragazwa kwenye uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji hadi akafikia hatua ya kuwarubuni wenyeviti walioshinda.
 
Naamini pia wananji wa Vunjo watakuwa wamwpata somo hapa ni ipi hasa sura halisi ya ya Mheshimiwa huyo. Amepata jukwaa kujitangaza lakini pia amejiweka wazi yeye ni mtu wa aina gani. Swala ni je, wana Vunjo watamchagua?
 
katika siasa za nchi , kuna wagonjwa kabisa wa akili wawili , Lyatonga Mrema na Kingunge Ngombare mwili.
Kingunge huwa namsamehe kwa sababu maradhi anayougua ni yauzee, sasa hivi uwezo wake wa kutambua na kutatua mambo ni sawa na mtoto wa miaka mitatu[3] tu.
Mrema maradhi yake ya sukari na ninini sijui , nafikiri imemshambulia hadi kwenye ubongo wake, sasa hata kupewa nafasi yakuongea kwenye hadhara kubwa vile ni dalili pia kwenye chama cha CCM kuna watu ni wajinga pia.
Mrema anaumwa , maradhi yameleta aina ya ukungu kwenye Ubongo, uwezo wake wakuprocess mambo uko chini sana na ni wataratibu mno.
Dalili moja kubwa ya jambo hilo ni ukosefu wa misamiati yakutosha wakati anaongea majukwaani, hawezi tena kutafuta neno jipya, anarudia maneno yaleyale, vitu vilevile, anajikanyaga katika kujenga hoja, anaropoka, anajikana na kujikosoa, hajiwezi tena.
Mrema uwezo wake wakuyatatua matatizo ama kuyatizama macho uko chini ya uwezo wa mtoto wa miaka MINNE[4]
nI MGONJWA HUYU.
 
HTML:
Urais kwa wagombea wa TLP moto Send to a friend Monday, 12 July 2010 08:56
James Magai

WAKATI wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) wakitarajiwa kumpitisha mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, kuna taarifa za kuwepo mvutano baina ya pande mbili zinazovutana, mmoja ukidai kuwapo kwa njama za kumuengua mmoja wa wanachama walioomba kuteuliwa katika nafasi hiyo, huku mwingine ukipinga.

Habari zilizolifikia Mwananchi kutoka katika vyanzo vya kuaminika ndani na nje ya chama hicho zinasema kuwa uongozi wa juu wa chama hicho umepanga kumwengua mmoja wa wanachama waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa, Macmillan Lyimo.

Habari kutoka katika vyanzo hivyo zinadai kuwa uongozi huo wa juu wa chama hicho unapanga kumwengua Lyimo na kumwacha Mutamwega Mgahywa apite moja kwa moja.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zinadai kuwa kuna baadhi ya wanachama ambao wanapinga mpango huo kwa madai kuwa Mgahywa ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mwibara wilayani Bunda mkoani Mara kwa muda wa miaka 10 hana sifa za kugombea nafasi hiyo.

Hata hivyo akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kuhusu madai hayo ya kutokuwa na sifa ya kielimu kugombea nafasi hiyo na vyeti alivyoviwasilisha kwa katibu mkuu, Mgahywa alisema madai hayo hayana msingi wowote.

Kuhusu kiwango chake cha elimu Mgahywa ambaye alilieleza Mwananchi kuwa ataweza kulitolea ufafanuzi wa kina na kwa vielelezo leo ikiwa ni pamoja na kutangaza msimamo wake, alisisitiza kuwa yeye ni msomi wa kutosha na kwamba hana wasiwasi na madai hayo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa TLP Hamad Tao alikanusha madai ya Mgahywa kuwasilisha vyeti vya sekondari wakati akirejesha fomu huku akisisitiza kuwa ni msomi mwenye shahada ya udaktari.

Alisema hata hivyo katika katiba ya chama chao hakuna kipengele cha kiwango cha elimu kwa mgombea wa nafasi hiyo wala kwenye katiba ya nchi bali hiyo iko kwa CCM tu.

Kuhusu mpango wa kumuengua Lyimo Tao alisema hakuna mpango huo na kwamba waombaji wote watapigiwa kura na kwamba taarifa hizo ni woga wa aliyezitoa akidhani kuwa kuna mmoja atapendelewa.

Habari zaidi kutoka ndani ya chama hicho zilidai kuwa uongozi wa juu wa chama hicho umeapa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa hapitishwi na kwamba mpango huo una maslahi binafsi.

Wakimweleza Lyimo, baadhi ya wanaTLP hao ambao hawakutaka majina yao kutajwa walidai kuwa ingawa hajulikani sana katika anga za siasa, lakini ndio mgombea anayeweza kutoa upinzani mkubwa kwa CCM

“Mimi namfahamu Lyimo, nimekuwa nikifuatilia vitabu vyake anavyoviandika, ana mawazo na mtizamo mzuri ambao unaweza kuleta mabadiliko katika nchi,” alisema mmoja wa wana TLP hao na kuongeza;

“Ndiye mgombea ambaye akisimama kuelezea sera zake atatoa upinzani mkubwa kwa wagombea wengine na nina imani wananchi wengi wanaweza kumuunga hata mkono maana watu wameshachoka na CCM”.

Kwa upande wake Lyimo alipoulizwa kuhusu madai hayo ya mpango wa kumuengua, alisema yuko kwenye mkutano lakini alijibu kwa ufupi tu kuwa hawezi kuzungumza zaidi kwa sasa bali anasubiri kuona kitakachotokea leo.

Hata hivyo habari zilizolifikia Mwananchi jana kutoka katika chanzo kingine cha habari cha kuaminika ndani ya chama hicho muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilisema kuwa uongozi wa chama hicho umesalimu amri katika mpango huo.

Chanzo hicho kililidokeza Mwananchi kuwa uongozi wa chama hicho umeamua kusitisha mpango huo wa kumwengua Lyimo, kwa hofu ya kusababisha mtafaruku ndani ya chama, baada ya kuona kuwa kuna nguvu kubwa iliyo nyuma yake ndani na nje ya chama hicho
HTML:
Mwenyekiti-Augustino Lyatonga Mrema
Katibu Mkuu-Hamad Rajab Tao
Wote choka mbaya, kuna chama hapo kweli?
 
Wakuu zangu labda nilisahau kuwafahamisha mchezo wa kisiasa unaofanyika Tanzania.

sasa hivi kumezuka Upinzani mpya na sio wa kifalsafa au Itikadi isipokuwa Chaguo la Mtandao. Wabunge wengi kama sii wote wanaogombea kiti cha Ubunge wanapitia CCM kupata baraka zao. Sasa ikiwa unagombea jimbo ambalo inajulikana huwezi kushinda au kuna mshindani wa CCM ambaye atapita lakini sio Mtandao wagombea huingia jimbo hilo na tiketi ya chama cha Upinzani ili mtandao umwezeshe mgombea kupata ushindi.

Mrema na Seif hamad hawa walikuwa CCM toka wakati wa Nyerere..Ni wapinzani waliochomekwa kuleta ushindani ili nchi yetu ionekane ina demokrasia ya kweli lakini baada ya kuonekana dalili za wao kuchukua madaraka wakaingia tamaa na kuasi kabisa.. Matokeo ya Mrema ni pamoja na kuasi kwake, kufikiria kwamba angeweza kuleta ushindani wa kweli hali mamlaka hayo yalikuwa yamepangwa ndani ya mchezo wa sinema. CCM wakamtema na kwa bahati mbaya mzee wetu ana laana pia juu yake.. Haya anayajua vizuri na hakika itaendelea kumhunt maisha yake yoote kama mzee Mwinyi na Mkapa! - Damu za watu zinafanya badr.

Kwa hiyo Mzee wa kiraracha anarudi kwa chama kubwa na taratibu anamrudia Mungu wake kwani sidhani kama kiafya yuko fit. Nilimwona Bongo mtaani hakuwa ktk hali nzuri kiafya nadhani anayo matatizo ya maradhi au ndio jua kali (waya) limefika nyuzi 100 za kimaisha.
Tumwombee Mungu apewe uzima, lakini kisiasa he is done!
 
Hamna chama tena ndugu yangu! Kiongozi mwenyewe choka mbaya, fika pale Sinza umkute maskani yake....anatia huruma!!
 
When the "most popular" member of your party endorses a presidential candidate from another party that means your party is done for. Mrema kabaki jina tu lakini hana nguvu yoyote ya kisiasa na TLP ina fifia pamoja na nyota iliyo kuwa ya Mrema. Ndiyo tatizo ya kujenga vitu around personalities. TLP ili sikika kwa sababu ya uwepo wa Mrema na kwa vile sasa hivi Mrema ana fuata falsafa ya "if you can't beat them then join them" basi TLP ni aidha iwe kitengo cha CCM au ikubali kumtema "personality" wao na kujijenga kutoka chini.
 
Sipingi watu wanaosema inawezekana Mrema anajua anachokifanya, ila kama amekubali kuwatumikia basi awatumikie ila asifanywe zezeta lao (the comedian) la kutungiwa mashairi na kina Hadja Kopa, au kuwa kama mwanaume aliyelishwa limbwata.

Hatari zaidi inakuja kama yeye Mrema hajijui kama anafanywa ndondocha la CCM na kutushangaa sisi tunaomshangaa, ni sawa na kichaa aliye uchi kuwashangaa waliovaa nguo.
 
Akili ni kitu cha muhimu sana ambacho Mrema anapungukiwa. Kama Mrema angekuwa na akili za kutosha akasikiliza ushauri aliokuwa amepewa wa kutokuingia kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 bila mabadiliko ya Katiba, basi leo hii CCM isingekuwa madarakani kutokana na shinikizo la mageuzi lililokuwapo kwenye jamii wakati huo, na huenda baadaye yeye mwenyewe ndiye angekuwa rais wa tatu wa Tanzania.

Leo hii analia njaa tu hasa baada ya chama chake kukosa ruzuku kwa kutokuwa na wabunge. Baada ya kupewa huduma ya matibabu huko India na Kikwete, basi hawezi kusahahu fadhila hiyo, na hilo linamuacha kwenye njiapanda ya kisiasa: kuwa mpinzani na kuwa shabiki wa CCM. Angefanya jambo la maana kama ataachane na siasa kabisa kwa vile hana njia tena; akirudi CCM atachekwa kuwa anakula matapishi yake, na akiendelea huko TLP atakufa njaa kwa vile hakuna mafanikio yoyote ya kisiasa tangu aanze kuongoza chama kile.
 
kama ni mimi ni Mwanachama wa chama chake cha TLP ningemuomba huyu Mwenyekiti wa TLP Mh. Augustine Lyatonga Mrema Ajiuzulu kwa kukisifia Chama cha CCM. Ama kweli Waswahili husema Ng'ombe akivunjika mguu hurudi zizini kwake Ndugu Mrema hafai kuwa Kiongozi wa chama cha Upinzani amesema utumbo kama huo? na Wafuasi wake bado wana imani nae?Mzee Mrema ameshakuwa Mzee hafai hata kugombea Ubunge jimboni kwake atakwenda kuwasaidia kitu gani watu wa jimboni kwake akiwa kama yeye ni Mbunge muwakilishi wa Watu wake bungeni? Mzee Mrema umesha zeeka na kuchoka mambo ya siasa bora jiuzulu ibaki heshima yako kwa kizazi kijacho asanteni.
 
Back
Top Bottom