Elections 2010 Jamani Lyatonga Mrema kapatwa na ugonjwa gani?

angekuwa jimboni kwangu LYATONGA ANGEPATA KURA YANGU BILA UBISHI.....sasa bunge litarajie mpambanaji wa ukweli ambaye matunda yake kwa wananchi wa TANZANIA yalionekana na TUTARAJIE MENGI ZAIDI.....VIVA LYATONGA
 
pumbavu kabisa...niko marangu na mrema alikuwa anamkutanao jana jioni marangu mtoni...hivi nyie mnatokeaga watu mnakurupuka tu....kwa taarifa yako Mrema anashinda hata augue ukurutu wa milele wachaga huwaambii kitu..CCM wako hoi katika jimbo hilo for you information

Heshima kwako Kigogo,

Mkuu wangu niliwahi kuwaambia watu hapa jamvini Mzee wa Kiraracha anakubalika Vunjo kuliko wapiga debe wa chama fulani wanavyofikiri/wanavyotaka.
Taarifa za uhakika Mheshimiwa A Kimaro mbunge aliemaliza muda wake anamsaidia Mrema hata CCM mkoa wa Kilimanjaro wanjua hilo bila ubishi wowote.
 
Watu wengine roho mbaya , Jimbo la Vunjo linaenda na Mrema, CCM kaeni mkao wa kulia. Hata mkimtakia kifo, kama maulana ajapanga afi.

na hata wananchi wanasema wananchagua Mrema akafie huko huko bungeni...nilisikia hiyo kule marangu nilicheka sana
 
Heshima kwako Kigogo,

Mkuu wangu niliwahi kuwaambia watu hapa jamvini Mzee wa Kiraracha anakubalika Vunjo kuliko wapiga debe wa chama fulani wanavyofikiri/wanavyotaka.
Taarifa za uhakika Mheshimiwa A Kimaro mbunge aliemaliza muda wake anamsaidia Mrema hata CCM mkoa wa Kilimanjaro wanjua hilo bila ubishi wowote.

correct!!!! Kimaro anamsaidia Mrema vibaya sana.CCM wanahaha kila wanakopita wanazomewa hahaaaa
 
Mkuu wangu mimi nilikuwa Marangu J4 kwenye msiba wa mfanyakazi mwenzetu nilishanga sana jinsi watu wa kule wanavyompenda na kumsifu nikajisemea moyoni laiti wangepata nafasi ya kuingia JF wangeshangaa jinsi mtu wao anavyopigwa madongo.

Taarifa za uhakika ni kwamba Mzee wa Kiraracha siku hizi anaitwa Laigwani ole Mrema baada ya wamasaai wa kahe kumsimika kuwa kiongozi wao wa kimila.

wachaga bwana sasa si wachague CHADEMA huyu Lyatonga Mrema hana jipya

na hapa hasa ndipo mlipokuwa mkitaka mufike kwa mjadala huu, chadema acheni hizo, nyinyi mnadai mnataka upinzani ukue bungeni halafu mna roho mbaya kwa wapinzani wenzenu na kuwazulia mabalaa, hapa haya, kule ubunge kwa wa CUF yaani mnahisi nyinyi tu ndio mnao haki kuliko yeyote yule ?

ogopa chama kama hiki kikipata madaraka kitapiga marufuku hata mfumo wa vyama vingi
 
Mhhhhhhh

Sasa basi bwana, tukaelimishe vijijini ama tujielimishe wenyewe?? Hata miezi miwili haijapata kuisha humuhumu watu wale wale, kwa staili ile ile walikaririwa wakisema Mrema sio mpinzani ni kibaraka wa ccm. Leo hii , kwi kwi kwi kwi eti ccm wana haha kwa sababu ya kibaraka wao.Teh teh teh.

KWA HERI.
 
habari ndio hiyo
 
Eti nasikia mrema ngozi inawasha kila wakati mpaka kashindwa kuzindua kampeni za mgombea wake wa uraisi na huko vunjo ndo kashabwagwa na mrema mwingine wa CHADEMA halafu analalamikia rafu CCM eti Kikwete amsikie na kumuonea huruma kwamba arudi chamani. Anataka msaada wa JK kama alioutoa kwa Wasira maana na Wasira alisota mpaka JK alipomuibua

mi simo
 
na hapa hasa ndipo mlipokuwa mkitaka mufike kwa mjadala huu, chadema acheni hizo, nyinyi mnadai mnataka upinzani ukue bungeni halafu mna roho mbaya kwa wapinzani wenzenu na kuwazulia mabalaa, hapa haya, kule ubunge kwa wa CUF yaani mnahisi nyinyi tu ndio mnao haki kuliko yeyote yule ?

ogopa chama kama hiki kikipata madaraka kitapiga marufuku hata mfumo wa vyama vingi
=====

We mtu wa Pwani au wa Lugoba?
 
ikona wamenyamaza ujue wanahesabia maumivu maana kwa majisifu, wala usingefika kuuliza tungona kashkash zao humu

Duu, kama ni maumivu itakua balaa kweli kweli. Hawa jamaa wanaweza kua kama tlp kwenye buge baada ya oct. Ni wasiwasi wangu tu.
 
wameisha hawa, kwenye uwanja huko sio mchezo, wanaleta siasa za alsahaf yule waziri wa habari wa iraq.

wanadanganya watu waone huko mambo shwari ila kiukweli vijana wao wanamalizika maana wanakimbilia CCM kujisalimisha.

Vita si lelemama.
 
Mkuu wangu mimi nilikuwa Marangu J4 kwenye msiba wa mfanyakazi mwenzetu nilishanga sana jinsi watu wa kule wanavyompenda na kumsifu nikajisemea moyoni laiti wangepata nafasi ya kuingia JF wangeshangaa jinsi mtu wao anavyopigwa madongo.

Taarifa za uhakika ni kwamba Mzee wa Kiraracha siku hizi anaitwa Laigwani ole Mrema baada ya wamasaai wa kahe kumsimika kuwa kiongozi wao wa kimila.

kule huwaelzi kitu kuhusu Mrema...i like that spirit bana
 
wameisha hawa, kwenye uwanja huko sio mchezo, wanaleta siasa za alsahaf yule waziri wa habari wa iraq.

wanadanganya watu waone huko mambo shwari ila kiukweli vijana wao wanamalizika maana wanakimbilia CCM kujisalimisha.

Vita si lelemama.

Duu, sasa ngoja waje kusikilizia maumivu, posho mwakani makao makuu litapungua ohooooo.
 
angekuwa jimboni kwangu LYATONGA ANGEPATA KURA YANGU BILA UBISHI.....sasa bunge litarajie mpambanaji wa ukweli ambaye matunda yake kwa wananchi wa TANZANIA yalionekana na TUTARAJIE MENGI ZAIDI.....VIVA LYATONGA

Mrema huyu wa 2010 au yule wa zamani?
 
Katika mdahalo unaofanyika katika Jimbo la Vunjo unaoendeshwa na TBC1 Augustine Lyatonga Mrema aliulizwa kuwa kwa sasa amezeeka na anaumwa atawezaje kuhimili mikiki Bungeni?

Kujibu swali hilo alisema kwamba mtu kuumwa sio tatizo, mbona Dkt Slaa alianguka bafuni na kuvunjika mkono, kwa hiyo asigombee?

Pia akadai kwamba Bungeni hawaendi kubeba zege na yeye yuko fiti, aulizwe mke wake kwa kuwa "anajua!"

Mambo hayo!
 
Ananikumbusha kauli ya Mzee Malecela mwaka 2005

Urais siyo kazi ya kubeba zege kwamba inahitaji mtu awe na nguvu, bali ni akili iwe timamu

Mzee Kenyatta (RIP) zama za uhai wake aliwahi kusema kwamba:

"Wanaosema kwamba mimi ni muzee, wamuulize Mama Ngina". Mama Ngina alikuwa ni mke wake

Sasa naona Mzee Mrema ameamua kuunganisha zote mbili kwa mpigo.
 
inaekea kweli yupo fit, Mzee punguza kibano kwa mama, ufit wako haupimwi kwa style hiyo bwana, tunataka ufit wa afya katika siasa.
 
Back
Top Bottom