Elections 2010 Jamani Lyatonga Mrema kapatwa na ugonjwa gani?

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
Wadau nimepata hii habari kutoka kwa blog ya Michuzi. Hivi huyu Lyatonga ameugua ugonjwa gani au ni kweli kuwa alipandikiza ili aue upinzani?

Mwenyekiti wa TLP Mh. Augustine Lyatonga Mrema akishangiliwa na wana CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho Kizota, Dodoma

Uzuri wa ndege manyoyaaaaa
Uzuri wa CCM seraaaaa
Huu ni ujumbe wa Khadija Kopa akimfagilia Mheshimiwa Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa Chama Cha TLP alipofungua moyo wake akimmwagia sifa kede kede Mwenyekiti wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete.

Hapa sasa hivi Lyatonga Mrema anatoa salamu rasmi kutoka chama cha TLP na kuwasema wale wanaosingizia katumwa na wana CCM wakome.

Anashangiliwa na wana CCM kwa nyimbo na vigelegele, anasema kwamba CCM haikamatiki. CCM Chama Kubwa, amesalimu amri. Kwani mwaka 1995 alishindwa, mwaka 2000 aligaragazwa na Mh. Mkapa, na mwaka 2005 ndio kabisaa Kikwete akammaliza. Hivyo CCM ni chama imara, hakishikiki. "Kweli CCM inagaragaza upinzani".

Mheshimiwa Mrema aliongeza, "Kila mwaka wa uchaguzi inakula kwangu, sasa nimechoka" anasema Mrema kwa hamasa huku akiendelea kusifia CCM na uongozi wake.

Kwa maneno yake amesema, hana sababu ya kuacha kumsifia Rais Kikwete kwani ndiye Rais pekee anayemjua. Amefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka mitano hususan katika harakati za kupambana na ufisadi na mafisadi nchini.

Amekiri ya kuwa katika marais wengi waliopita , Kikwete ni mthubutu na mtekelezaji. Anaumia roho sana kusikia kuna watu wanaombeza ati hajafanya lolote hivyo wamtose.

Mrema amewasuta wote wanaobeza maendeleo ya serikali ya Rais Kikwete na amewaomba wana CCM waendelee kumsaidia ili afanye vizuri zaidi. Hapo Mrema alishangiliwa sana kwa nyimbo za CCM na kusindikizwa na bendi ya TOT.

Mrema amemaliza kwa kusema ya kwamba anafuata wosia wa baba wa Taifa na hivyo atagombea ubunge Vunjo kupitia chama chake cha TLP.

Mwenyekiti wa CCM amemshukuru kwa kuwa mkweli lakini amemuhakikishia ya kwamba hata wana CCM watakwenda huko VUNJO na watakutana tena.

Mambo moto moto hapa Kizota, salamu zinaendelea. Picha zinakuja
 
Nimefikia mahali ambapo namuonea huruma zaidi kuliko kumtazama kama mshindani wa kisiasa!
 
Anatafuta huruma ya kurudi bungeni hana jingine jipya kwa mantiki hii basi awaeleze wanachama wenzake kuwa yeye ni CCM B na wote wafanye hivyo ili tujue wapinzani ni nani na wanafiki ni wapi.
 
Mrema kafulia, anajua hata huko vunjo hachaguliki tena kwani watu wote wameshamshitkia kuwa ni vuvuzela la kikwete,anachofanya sasa ni kuzengea vile viti kumi vya wabunge wa kuteuliwa na rais, na hivyo atapata.Ni aibu iliyoje mwenyekiti wa chama cha siasa ambacho kina mgombea urais akampgie debe mgombea wa chama kingine? Ama kweli njaa haina adabu,adui yako muombee njaa, yaani leo Mrema anakubali kuwa comedian wa CCM.
 
Mrema is a used man a.k.a scaper, what do you expect to come out from his empty head? he is completely finished
 
Mrema bana!!!
Leo anameza matapishi yake.....!!!

Hi ndo bongo bana, ama kweli adui yako muombee njaa!!
 
Mrema bana!!!
Leo anameza matapishi yake.....!!!

Hi ndo bongo bana, ama kweli adui yako muombee njaa!!

kumbuka katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu. time will tell. lets just wait and see.
 
Anatafuta huruma ya kurudi bungeni hana jingine jipya kwa mantiki hii basi awaeleze wanachama wenzake kuwa yeye ni CCM B na wote wafanye hivyo ili tujue wapinzani ni nani na wanafiki ni wapi.

Kama Fundikira aliteuliwa kuwa mbunge, nadhani Mrema naye atateuliwa ndicho anacholilia kwa JK. Kushinda Jimbo la Vunjo dhidi ya CCM na Chadema bado ni ndoto kwa sasa labda wagombea wengine wote wawekewe pingamizi apite mwenyewe
 
You Guys should read between the lines.
The old man of Kiraracha is a cunning fox and a realist.
He knows for sure that Jk's popularity this time round is higher than ever and as such it will be very difficult for any candidate to beat him to the high chair.
Old Kiraracha's dream is now to go the big house in Dodoma through his home district.
Even for him that seat is not a guarantee so he did what he does best 'play both ends against the middle''.
My belief is that his gimmick may pay and off and i will not be surprise to see him in Dodoma after October.
 
Its roumored that BWM is fianacing him to get rid of the incumbent over the Kiwira saga......Kimaro let all hell break loose...even to himself
 
jamani huyo MRema, si akatulie kwao atunze afya yake, siasa ya nini sasa au ndio njaa? nahisi kwapatwa na kirusi cha akili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom