Jakaya Mrisho Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu!!!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Wakati wanajeshi wanakula kiapo cha utii mbele ya Rais, tafsiri yake ni kwamba wanasema hawatafanya jambo lolote lile lililo kinyume na matakwa ya Rais ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Amiri jeshi Mkuu ndiye "Bosi" wa majeshi yote ya ulinzi na usalama na ikiwa majeshi hayo yatakwenda kinyume cha matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu basi majeshi hayo yatakuwa yameasi. Kwa hiyo uasi siku zote huwa ni dhidi ya Amiri Jeshi Mkuu na wala si dhidi ya nchi anayotawala Amiri Jeshi Mkuu.

Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kama ukikuta Polisi mitaani wanakong'ota watu au kutaka rushwa, basi juwa hayo ni matakwa ya Amiri jeshi Mkuu, Kama Polisi wanazuia Maandamano au "mikesha" ya wanasiasa juwa kabisa wasingefanya hivyo kama si matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu. Kama unasikia Polisi wanasema Al shababu wataingilia maandamano ya wanaharakati, basi juwa Amiri Jeshi Mkuu naye anaamini Hivyo!!

Hoja yangu hapa tusiwachukie maaskari kwani nao pia wapo kazini na wako kwenye kutimiza kiapo chao cha kumtii Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa nini tusishughulike na Amiri Jeshi Mkuu ambaye hawa Askari wanaotupiga virungu wanamtii yeye??
 
Back
Top Bottom