Jaji Warioba: Huwa kunatokea changamoto kwenye uchaguzi ila siyo kama za mwaka 2020. Yalikuwa mambo mapya hapa Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Bado watu hawajamsahau Jiwe 😁😁

Sasa kama alikuwa kipenzi Chao Wanyonge Kwa nini inaonekana alipora uchaguzi?

Kwani hayo mambo mapya anayoyasema Babu Warioba ni yapi Hadi amechafukwa na kukerwa?

johnthebaddest Mzee wa Shujaa wa mchongo 🤣🤣
---
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Joseph Warioba, ameonyesha kukerwa na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, huku akisema mambo hayo yalikuwa mpya katika histori ya chaguzi nchini.

Jaji Warioba ameyasema hayo leo Jumanne Septemba 12, 2023, wakati akitoa mchango wake kwenye mkutano wa wadau wa demokrasia nchini, ulioitishwa na Baraza la Vyama Vya Siasa, na kufunguliwa jana na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita, Jaji warioba amesema alitarajia kuona zikifanyiwa kazi na Serikali, na hasa kisheria kwa sababu mambo yaliyofanyika yalikuwa wazi na watu wote waliona.

“Mwaka 2020, pamoja na mafanikio, kulikuwa na changamoto nyingi sana na kwa vyovyote vile, hata kama isingekuwa sasa, mimi nilitegemea angalau ndani ya Serikali, changamoto zile zilionekana na hatua zingechukuliwa ama kisheria au kikanuni au utaratibu kuepusha zisije zikatokea mwaka 2024 na 2025," amesema na kuongeza;

“Wote tunajua kilichotokea mwaka 2019 na 2020, ilikuwa mara ya kwanza, Watanzania wamezoea kupiga kura, huwa zinatokea changamoto lakini siyo kama ilivyokuwa mwaka 2020, ilikuwa mara ya kwanza kwa wagombea wengi kuenguliwa kwenye uchaguzi, tuliona matumizi makubwa ya fedha katika kila hatua kuanzia kwenye uteuzi hadi kampeni.”

Jaji Warioba amesistiza: "Kama wanataka kuepusha hayo yaliyotekea huko nyuma, basi ni vema wakajiandaa kwa kuangalia sheria, kanuni na hasa taratibu za kusimamia uchaguzi ili wasipate matatizo kwenye uchaguzi ujao."

Jaji Warioba anaamini kuwa hayo yasipofanyika, yatasababisha watu wasiende kupiga kura kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mwananchi
 
Bado watu hawajamsahau Jiwe 😁😁

Sasa kama alikuwa kipenzi Chao Wanyonge Kwa nini inaonekana alipora uchaguzi?
...
ccm walipora uchaguzi ndio manaa wanaiba na kugawa mali zetu kwa wageni tujipange vizuri kuwakabili.

Lissu alishinda uraisi na wabunge wengi walishinda,mzee Warioba ni kweli sio mnafiki,maana yake kila mtu ajiwakilishe mwenyewe.
 
Bado watu hawajamsahau Jiwe 😁😁

Sasa kama alikuwa kipenzi Chao Wanyonge Kwa nini inaonekana alipora uchaguzi?

Kwani hayo mambo mapya anayoyasema Babu Warioba ni yapi Hadi amechafukwa na kukerwa?

johnthebaddest Mzee wa Shujaa wa mchongo 🤣🤣


View: https://www.instagram.com/p/CxGFrgQN17T/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Hizo anazozizungumzia Mzee Warioba, kuwa "Changamoto" za chaguzi mabilimbali, hazina tofauti kubwa sana na huo "uchafuzi" uliotokea 2020, kama matokeo yake ni yale yale ya kuwabakisha madarakani CCM.

Kinachotakiwa sasa ni kupambana na hizo "changamoto" na kuzikataa kabisa katika chaguzi zinazofuata, 2024 na 2025; iwe ni chini ya katiba hii mbovu iliyopo sasa, ambayo ndiyo inayozisababisha changamoto hizo, au hata ikiwepo katiba mpya ya mapambo anayoitengeneza Samia kwa kutumia ujanja.

CHADEMA inao wajibu wa kuwaongoza wananchi kukataa hizi changamoto.
 
Back
Top Bottom