Salaam, shalom.
Baada ya kumsikiliza Kwa makini Mzee WARIOBA akihojiwa katika kipindi Cha Dakika 45 kituo Cha ITV, Kuna mambo nimeyatambua Mzee anajaribu Kutoa angalizo na umuhimu wa Serikali kutathmini kilichojiri 2020 Ili kuepuka KURUDIA changamoto zile zile.
Mzee Warioba amejaribu kuongea jambo zito Kwa Ulimi wa BUSARA kubwa sana kuisaidia Serikali na chama chake kuwa makini na uchaguzi ujao ili jambo muhimu la Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi lizingatiwe kabla ya kuingia uchaguzi wowote ujao.
TATHMINI HIYO ILENGE KUJUA YAFUATAYO.
1. NINI HASA KILITOKEA 2020.
Kuhusu HOJA hii, ni Rahisi kupata majibu sababu zipo hatua kadhaa zimefanyika kujaribu kuondoa sintofahamu Ile ,japo hapakuwa na Nia ya dhati.
2. FAIDA ZA KUINGIA UCHAGUZI 2024/2025 BILA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA.
Ikiwa zipo faida, naamini zitakuwa chache sana Hasa Kwa wananchi japo UKWELI ni kuwa Kila jambo Lina pande mbili.
3. HASARA ZA KUINGIA UCHAGUZI 2024/2025 BILA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA.
HASARA Kwa nionavyo Mimi, ni nyingi kuliko faida.
- KISIASA
Imani ya wananchi kushiriki uchaguzi Iko chini sana, tumeona mwitikio wa wananchi kushiriki uchaguzi Ukiwa chini sana, inahitajika TATHMINI ya kina nini kifanyike kuleta ongezeko la wananchi kuhusu kushiriki shughuli za kisiasa.
Kasoro na Matukio ya kura fake zilizoripotiwa Bado limeweka Imani ya wananchi kushiriki uchaguzi kuwa chini sana.
- KIUCHUMI
Uchaguzi wa HAKI, una mchango mkubwa sana Kwa wananchi katika kuinua Uchumi,
Ikiwa yaliyojiri 2020 yatajirudia, tutegemee kuona Uchumi ukidorora zaidi.
- KIJAMII
Muungano na ushirikiano wa wananchi ndani ya JAMII ulitatatizika sana Kwa yaliyojiri 2020, hivyo kuingia tena uchaguzi wa 2024/2025 kama vipofu Si sawa.
- KIUSALAMA
Si sawa kuwekeza katika kununua silaha na mabomu ya machozi nk nk nk, kuminya DEMOKRASIA.
4. ZIPI ZITAKUWA FAIDA ZA KUSOGEZA MBELE UCHAGUZI WA MITAA 2024?
Iwapo uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika 2024 utasogezwa mbele, tutafanikiwa kukata cost ya Uchaguzi Kwa 50% sababu uchaguzi utakuwa mmoja tu 2025 , unachagua mkt, diwani, mbunge Hadi Rais.
HITIMISHO.
Ni muhimu kuhakikisha changamoto zilizojitokeza 2020 zikatatuliwa tukaingia tukiwa na Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi Ili pasiwepo kitisho kikubwa Cha USALAMA, maana uchaguzi katika Nchi nyingi imekuwa chanzo Cha kutetereka Kwa USALAMA na Amani.
NB: Wazee wa Aina ya Mzee Warioba ni hazina ya Taifa letu. Kuwapuuza ni kujichimbia mashimo ambayo hatokuwepo Jirani wa kutusaidia ikiwa tutajitumbukiza.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen.