Jaji Mutungi ateuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, achukua nafasi ya John Tendwa

CHADEMA hatuna sababu ya kufurahi hadi tutapoona utendaji na weledi wa huyu bosi mpya.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.

Mwenyekiti wa CCM ana mteua msajili wa vyama! Lazima ataipendelea CCM tu!
 
Karibu uraiani babu Tendwa. Sasa imebaki story. Utaishia kuota kuifuta CDM. Mamlaka yako ni ya ukuu wa kaya tu sasa.
 
Tuone na msajili mpya ata tenda vipi kazi aliyopewa. Je, kukandamiza vyama vya upinzani au kutenda haki?
 
Magaidi wako Chadema, mnatumia nguvu kubwa na fedha nyingi kuwahonga Mahakama wawe upande wenu lakini wananchi wanajua kila kitu, nani alimwagia MUSA TESHA Tindikali huko Igunga?

Unaemuita wewe Gaidi kwa wengine wengi wanamuona Mpigania Uhuru by Jaji (Mahakama kuu Tabora)
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.

Mzee bado yupo Zimbabwe akisimamia ulaji wa Mzee Mugabe. Sasa yanayotokea huku nyumbani sijui ameshayapata?????????
 
JAJI TENDWA?GOOD RIDDANCE!Lushoto kwenu?fika salama ,jaribu uwe hata mzee wa kanisa,
 
Mh Tendwa John ukapumzike salama baada ya utumishi wako kwa jamii.
Nimesikia RC wa Arusha Mh Magesa Mulongo naye ametolewa/hamishwa kutoka Arusha kwenda Mtwara(tetesi).
 
Hata shehe yahaya alisema slaa atakufa akafa yeye

Hata yule babu aliyesema atashuhudia kifo cha CCM ikageuka CCM ndio ikashuhudia kifo chake... Japo kwa ajali haikujulikana kama ilipangwa au lah!
 
Njia pekee ya kujua mwelekeo wa kiitikadi wa huyu jaji ni kuangalia hukumu zake na maandishi yake; je ametoa hukumu ngapi zinazohusiana na haki za raia, siasa, haki za binadamu na usawa? Je ameandika nini kuhusiana na masuala hayo?
 
Kauli hii inayotolewa kuwa John Tendwa Kastaafu kwa mujibu wa sheria sina uhakika nayo kwani kuna maswali najiuliza ambayo sina majibu yake maswali yenyewe ni haya hapa

1. Mpaka John Tendwa anastaafu alikuwa na umri wa miaka mingapi?
2. Kisheria Msajili wa vyama vya siasa ukomo wake anatakiwa awe na miaka mingapi?

Naomba mwenye ufahamu wa maswali yangu anijuze ili niondokane na hii sintofahamu kwani nahisi kauli hii inayotumika kuwa amestaafu kwa mujibu wa sheria ni kama kumlinda lakini kiuhalisia ni kuwa kaondolewa kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa weredi na alikuwa analipeleka Taifa kwenye machafuko hususani kauli zake zenye utata juu ya CHADEMA.
 
Mutungi ni mtu mzuri,hope ataitumia vema taaluma yake.Dah!!Tendwa,pumzika kwa amani aise!

Mimi nimesikitika sana maana kile kibabu kilikuwa kinasaidia kuiua Ccm japo kolikuwa kinakera sana....kwa hiyo mafaili ya kuifuta cdm kitamkabidhi huyu mccm mpya (mtungi)?
 
Back
Top Bottom