Jaji Mutungi ateuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, achukua nafasi ya John Tendwa

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.
 
Mutungi ni mtu mzuri,hope ataitumia vema taaluma yake.Dah!!Tendwa,pumzika kwa amani aise!
 
Rais JK amemteuwa jaji Francisi Mutungi kuwa msajili wa vyama vya siasa kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Tendwa
source kurugenzi ya mwasiliano Ikulu

My take
Huyu bwana ni mchapa kazi ingawa alikumbwa na kashfa nyingi za kutowatendea haki wafanyakazi wa mahakama akiwa masajili wa mahakama ya rufani tanzania..Msajili wa mahakama kuu katika kashifa | Gazeti la MwanaHalisi
je kwa upande wa vyama atatenda haki?
bado tumwachie rais kazi ya kuchagua msajili wa vyama badala ya kuchaguliwa na tume maalumu inayoundwa na wawakilishi va vyama vyote?
 
Vielelezi muhimu mkuu.......huyu hapa!

ushindi.jpg
 
Back
Top Bottom