Jaji Mutungi ateuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, achukua nafasi ya John Tendwa

Kisa alikuwa msaidizi wake au kisa alimuwakilisha kwenye kipindi mpaka uamini kwamba ndo alikuwa mbadala!

Na si ni huyu ambaye kila mtu alikuwa anasema alipwaya kwenye hule mdahalo?wewe ndo ulimuona bora?
 
Magaidi wako Chadema, mnatumia nguvu kubwa na fedha nyingi kuwahonga Mahakama wawe upande wenu lakini wananchi wanajua kila kitu, nani alimwagia MUSA TESHA Tindikali huko Igunga?

Ngoja wakusikie mahakimu na majaji, sidhani kama utaweza hivi: To prove beyond reasonable doubt.
 
naam,kweli mkuu.wapo wengi ndani ya serikali wanaobanwa na mfumo.binafsi kuna mtu namfahamu kuwa mchapakazi mkubwa sana asiependa ujinga alipokuwa ngazi za chini huku mpaka wale mafisadi wa ofisini walikuwa hawampendi.alikuwa hapendi ujinga mzee huyu.lakini nae mfumo umembana tangu aingie kwenye cabinet anafurukuta lakini najua kabanwa!ni huyu mzee Christopher Kajoro Chiza!ni jembe kweli yule lakini mfumo...kama ulivyosema.ok,bwana naona mtandao unanisumbua kweli let me logout!nasubiri hizo makala mkuu!


nani Chiza??? Du, haya mdogo wangu.
 
Ni nani anaejiita mpigania uhuru wa wengine? Je unaweza kurudisha sura ya yule kijana MUSA TESHA kwa kusingizia kauli yako? naomba ikuguse na uwe na huruma, jaribu kuvaa viatu vya kijana huyo halafu watuhumiwa wako waachiwe huru.
Wewe unahitaji msaada kichwani,!
Ile kesi ya Mauaji ya Zombe, Mahakama Kuu ilimuachia kwa kusema Zombe hakuua,japo kuna watu waliuliwa. Hivyo Polisi wakamtafute muuaji. H
Hali kadhalika,Si "lazima" Kina Kileo (au makada wa Chadema) wawe ndo wamwagiaji tindikali kwa Tesha,wanaweza kuwa wengine,hivyo ni jukumu la Polisi kuwasaka.
 
Chadema kupitia mwenye kiti wao #SLAA Walikuwa wanamkana mara nyingi sana Tendwa na walisisitiza kutolewa kwake katika nafasi hiyo je yaweza kuwa nguvu yao? kwani wiki 2 vilizo pita walisema hawamtaki na leo kang'olewa na JK wadau hii imekaaje
 
Usiniambie Tendwa katemeshwa mzigo......haki ya nani......MUNGU MKUBWA
 
Nipo mbali na vyombo vya habari,naomba taarifa hii kwa kina.Kang'olewa au kastaafu maana na umri wake umeenda sana.
 
Taarifa nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika lakini kisicho rasmi ni kwamba Msajili wa vyama John Tendwa amestaafu rasmi leo na Jaji Mtungi (nimepata jina moja) ameteuliwa kuwa msajili wa vyama.

Nawasilisha.
Kaka Mikael pole sana, fuatilia huduma ya mobile sms alert kutoka j.f imeshaanza ungekuwa umepata habari hii mapema kutoka source ya kuaminika. Mimi niliipata mapema sana.
 
Japo watu wengi wamefurahia Taarifa hii kwangu mimi naona kama bado haisadii kwasababu naamin tatizo siyo Tendwa bali tatizo ni namna gani aliushika huo wadhifa alionao, mtakubaliana nami kuwa Tendwa aliteuliwa na Raisi ambaye pia ni mwenyeketi wa CCM, na Mutungi pia kateuliwa na na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, kitu cha msing nadhan ni kuangalia mfumo mzima wa namna msajili wa vyama vya siasa anavyopatikana kwasababu ni ukweli uliowazi kuwa Msajili wa vyama vya siasa lazima atakuwa mtii kwa mamlaka iliyompa wadhifa huo na mamlaka yenyewe ni Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala. So kwangu mimi naona ni muendelezo tu wa ofisi hii ya msajili wa vyama vya siasa kutokuwa huru.
 
Mungu ibariki Tanzania. Sitegemei jipya kwa uteuzi wa Kikwete! Nafasi nyingine ya matatizo!
 
Hakuna jaji mwenye akili timamu atakayeimba ngojera ya John Tendwa ya kuifuta Chadema. Hiyo ni sawa na ndoto ya alinacha.

Kama walishindwa kwa Lema Arusha kwenye kata nne wataweza kwenye kata zaidi ya 400, wabunge wa kutosha na vijiji/mitaa kibao iliyoko chini ya Chadema?? wasubutu, waone.

MKUU AMKA. Hujamsoma kaka Manyerere. TATIZO ZE SYSTEM. Ngoja uone vituko baadaye ndio utasema. INSHALLAH MWENYEZI MUNGU ATUPE MAISHA MAREFU.
 
Mutungi ni mtu mzuri,hope ataitumia vema taaluma yake.Dah!!Tendwa,pumzika kwa amani aise!

Wengi wanakuwa wazuri sana kabla ya kukabidhiwa hizo nyadhifa. Wakishakabidhiwa, na ukizingatia kuwa TOR wanakabidhiwa baadaye kwa njia ya vimemo kulingana na mahitaji, jumlisha na kaulevi ka madaraka; hapo utaona mambo yanaenda shaghalabaghala
 
rais ameshaona kuwa tendwa anakipa promo cdm wacha apumzike, bado wengine wa chamani. hivi ile picha inayoonyesha ubongo wa tendwa ipo wapi?
 
Back
Top Bottom