Jaji Frederick Mwita Werema ateuliwa Mwanasheria Mkuu wa serikali

Kwa ninavyofahamu heshima ya majaji katika mkondo wa sheria bado ni kubwa hivyo nategemea kuwa huyu mheshimiwa atakuwa ni uchaguzi sahihi.

Ni nadara sana kusikia kashfa kwa majaji ukilinganisha na wanasheria na mahakimu, angalau kwa mara ya kwanza tumefikiria nje ya boksi na kumteua jaji kushika nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali, napongeza sana jambo hili...
 
Lakini AG ni mshauri mkuu wa serikali kuhusu sheria, na hana nguvu ya kupinga mambo yanayofanywa na serikali. kwahiyo nafikiri hatutegemei makubwa saaana kutoka kwa new AG. Akakae pale aangalie tu asipate kashfa za kijinga kwa kutotumia taaluma yake vizuri.
 
Something is very wrong or right with this picture. Aidha baraza la mawaziri litavunjwa na Membe kuukwaa U-PM au bungeni kuna mtikisiko unakuja.

Uwezekano wa tatu unanitisha. Ill give it 14 days

Heshima mbele Mzee Mwanakijiji.

Uwezekano wa baraza la mawaziri kuvunjwa kwa sasa ni mkubwa sana.
Mheshimiwa waziri mkuu pinda alishindwa kwa kiwango cha kutisha kusimamia utekelezwaji wa maazimio ya bunge kuhusiana na Richmond.

Muungwana anatafuta njia ya kuinasua serekali yake baada ya kulemewa na kashfa kubwa kubwa kula kukicha,lakini sidhani Mheshimiwa Membe ndiyo jawabu la matatizo.Nadhani mfumo wa uendeshaji serekali kwa ujumla unapaswa kurekebishwa.
 
Ni among few surprises kutoka kwenye hii administration. Naona leakages za habari za uteuzi zimepungua kidogo - siyo kama enzi za uteuzi wa akina Membe, Lowassa, nk.
 
JK ataendelea kubadili watendaji waje. hivi ameishajiuliza ni kwanini kila mtu anayemweka kwenye kazi anapaya? Yawezekana kuna ubovu katika uteuzi au system yote iliyopo ni mbovu sana.
 
kujua sheria za mikataba si kigezo pekee cha mtu kuwa mwanasheria mkuu. Kuna mambo mengi sana zaidi ya hilo
Cheki kwanza cv ya mwanaidi maajar sinare mwanasheria aliyebobea.huyu jaji wako mpya hana cv hadi sasa mmeshindwa kuileta.

Mtu mwingine ni professor Abdallah Jumbe safari alifaa sana kwenye nafasi hii.
 
Asante Mods kwa kutoa takataka katika thread hii. Inafaa sana hata zile threads zingine zenye mwelekeo wa kugawa watanzania ambazo bado zinaonekana ziondolewe.
 
cheki kwanza cv ya mwanaidi maajar sinare mwanasheria aliyebobea.huyu jaji wako mpya hana cv hadi sasa mmeshindwa kuileta.
Mtu mwingine ni professor abdallah jumbe safari alifaa sana kwenye nafasi hii.
Chenge nae mbona alikuwa kabobea tena kamaliza Havard,mbona alituua tu
 
Something is very wrong or right with this picture. Aidha baraza la mawaziri litavunjwa na Membe kuukwaa U-PM au bungeni kuna mtikisiko unakuja.

Uwezekano wa tatu unanitisha. Ill give it 14 days


on your side;
Guess something strong is smelling
 
Ni among few surprises kutoka kwenye hii administration. Naona leakages za habari za uteuzi zimepungua kidogo - siyo kama enzi za uteuzi wa akina Membe, Lowassa, nk.
Nafikiri kuna kila sababu ya kuingiza sura mpya kwenye idara nyeti za umma maana mambo yanaenda kwa mazoea tu siku hizi. Kikubwa ni uadilifu wa hawa viongozi wapya wanaoteuliwa. Wasituangushe.
 
Rais anapangua wasaidizi wake kutoka Ikulu na kuwaweka katika mawizara. Kuna nini? Maana Jairo, Husu anayekuwa DAG. Kabla ya hapo kamuhanda, Dr. Mpango nk. Kuna nini?

Utabiri wangu;
  1. Wale wote waliokuwa karibu sana na EL wataondolewa. Hii inatokana na shutuma nyingi za ufisadi ambazo hivi sasa zinaelekezwa moja kwa moja na waziwazi kwa EL ambaye ndiye aliyeijenga serikali ya JK kwa kiasi kikubwa.
  2. JK anajaribu kujisafisha ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa upinzani kwake kuteuliwa mgombea uraisi wa CCM hasa baada ya kushindwa kuwang'oa wanaopiga vita ufisadi hivi majuzi. Kauli ya hivi karibuni ya Mzee Butiku inawezekana imemshitua.
 
kama ni kubadili baraza la mawaziri jioni hii, ningemshauri JK aache tu,hakuna faida. Kwanza sioni yeyote anayefaa kuwa waziri mkuu katika timu aliyonayo. Labda avunjilie mbali tu hilo jibaraza, wizara ziendeshwe na makatibu wakuu kama wanavyofanya siku zote.
 
Hivi kwa nini aliteua mtu anayekaribia retirement??? Huyu naye ana miaka mingapi?? asije akawa anastaafu next year hivyo amepewa post ili amalizie kibanda chake!!!!
 
MIMI nasema NAFASI ilipaswa apewe Mwanaidi Maajar ana uwezo wa sheria za mikataba ya madini n.k huko ndiko tunakolizwa. Huyu mheshimiwa hana kiwango kizuri.
kama alikata unajuaje, maana yeye yupo kwenye biashara zake, inawezekana kaona zinalipa zaidi ya kuingia kwenye mambo ya serikali. au kutokana na shughuli zake za uwakili kuna uwezekano kwamba aliwahi fanya kitu ambacho kitakuwa na conflict of interest na kazi ya AG
 
..huyu naye kama Mwanyika ni mzoefu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali.

..aliwahi kuwa Mkurugenzi wa masuala ya Katiba, hakimu ktk mahakama ya SADC.

..nafasi ya mwisho aliyoshika ni Jaji wa Mahakama Kuu kitengo cha Biashara.

..sasa ukiangalia utaona kwamba yuko well rounded na hicho ndicho kinachotakiwa kwa nafasi hiyo.

NB:

..binafsi sidhani kama kutakuwa na mabadiliko yoyote makubwa.

..mikataba yetu ni mibovu kwasababu hatujui jinsi ya kupatana bei, na sidhani kama AG anaweza kutusaidia kutatua tatizo hilo.
 
Mzee Mwanakijiji na wana bodi.

Within 14 days Mkuu wa Nchi atabadilisha wakurugenzi wa Halmashauri na majiji ili kurahisisha utendaji.

Kimsingi alikuwa anapaswa kuanza na hili bali kutokana na bunge kuanza Nov na kuna baadhi ya mapendekezo yanatakiwa yaendane na mabdiliko haya ndiyo maana aliamua kuanza na la mwanasheria mkuu.

Mtagundua hata jana kijana wake Ngeleja hakutokea kwenye kamati ya Nishati na Madini kupeleka Mapendekezo na hii ni maelekezo toka ngome kuu.

Wale wote ambao wana kashfa wataondolewa, Baraza la mawaziri litabaki hivyo hivyo.

Ila kuelekea 2010 kuna mke wa rais atagombea ubunge kama mme wake akikubali jambo moja la kiushauri na probably Membe could appear somewhere..

Ni mapema sana kuzungumza ila ni maneno tu ya kutoka jikoni. Na kuhusiana na tatizo la Mgao, hili linamalizika kabla ya Ijumaa ili lisiharibu uchaguzi wa serikali za mitaa na Mkulu keshaagiza watu wasifanye kazi yoyote ile mpaka tatizo hili limalizike kabla ya Ijumaa.

Gembe.
 
tatizo Pinda maneno mengi...alizania uwaziri mkuu unahitaji tu maneno yenye busara na matamu kwa wananchi na watendaji which is very wrong, uwazi mkuu ni vitendo na vinavyoonekana wazi wazi...natamani angeiga style ya Lowasa hata punje tu.
 
Back
Top Bottom