Jairo asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.
Yaani hili sakata linatufundisha kuwa tunapoteza muda wetu kumlaumu Ngeleja kuhusu tatizo la umeme, kwani inaonekana kwa serikali yetu maamuzi makubwa hufanywa na raisi tu!!!!!!!!!! hahaha ahahaha ahahah!!!! cry my beloved country!!!!!
 
Unaijua sheria ya kazi au unaongea kishabiki tu?
Katibu mkuu ni mtu wa kuteuliwa, yupo hapo alipo kwa mapenzi ya president(a presidential appointee) hivyo anaweza kutimuliwa muda wowote na bosi wake au yeye mwenyewe kuwajibika kwa heshima ya bosi wake. Sheria ya kazi ina nafasi ndogo sana au haina kabisa kwa nafasi za kuteuliwa kama hizi. Kumbuka yaliyompata Dr. Balali.
 
Katibu mkuu ni mtu wa kuteuliwa, yupo hapo alipo kwa mapenzi ya president(a presidential appointee) hivyo anaweza kutimuliwa muda wowote na bosi wake au yeye mwenyewe kuwajibika kwa heshima ya bosi wake. Sheria ya kazi ina nafasi ndogo sana au haina kabisa kwa nafasi za kuteuliwa kama hizi. Kumbuka yaliyompata Dr. Balali.
Yupo "kwa Mapenzi ya Rais?"Unachanganya mambo sasa. sheria ipi ya Kazi unayoizungumzia? Issue ya Dr. Balali na ya Jairo ni tofauti Mkuu.
 
Jairoing is the system of CCM government, MPs normally are jairoed, let us not vote for CCM MPs since they are addicted to jairoing. Yusuf Makamba said all CCM who vied for different leadership position practiced jairoing but the difference was the magnitude!!
 
Breaking news,hivi punde Katibu wa wizara ya nishati na madini Bwana,David Jairo amesimamishwa kazi,taarifa hiyo imetolewa na katibu mkuu kiongozi philemon Luhanjo ,amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma anazokabiriwa nazo.source ITV breaking news.

Kwa kawaida barua zote za wizara hutiwa sahihi na Katibu Mkuu (Accounting Officer). Kwa hali ya kawaida itakuwa aliletewa dokezo la kumtaka abariki hilo pendekezo. Kwahiyo bila shaka aliomba ushauri akaambiwa Mzee hiyo ni kawaida yetu, wabunge bila kitu kidogo bajeti haipiti. Lilivyopata baraka akatia sahihi, licha ya kwamba alikuwa na uwezo wa kukataa pia maana halazimishwi kutia sahihi. Hii ina maana pia kwa asilimia kubwa Waziri alijua na maafisa wengine wakuu. Uwezekano mkubwa kuwa wizara nyingi hufanya vitendo hivi vya kifisadi.

Kumwajibisha Jairo ni sawa lakini kama wanataka kutenda haki kwa watanzania, wang'oe visiki vyote na kwakweli wengi watatiwa kitanzini.
 
Duh!!!!!!!
"Nimeona niwaambie hili ili tusiendelee kuwaambia wananchi tunamsubiri Rais, wakati mimi mwenye dhamana ya kusimamia nidhamu nipo hapa, nimeshachukua hatua".

Kwa maneno haya anataka kutuambia kuwa bw. Pinda hajui nani anawajibika wa nani kwenye mambo ya nidhamu? Kweli hii ni ZeComedy!
Jairo nimekuvulia kofia. ... Ulitoa kauli hiyo ukiujua mchezo wote. Hata kama wabunge wamekasirika, ila huo ndo ukweli wenyewe kama ulivyodhihirika. Kusimamishwa kwako kwa kupewa likizo ya malipo ni ZeComedy tosha
 
Ikulu yagwaya kumtimua David Jairo
• Ushauri wa Pinda wawekwa pembeni

na Waandishi wetu
Tanzania Daima
OFISI ya Rais (Ikulu), imepata kigugumizi cha kutekeleza ushauri uliotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wa kumtimua kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayekabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili ya kazi, Tanzania Daima limebaini.

Badala yake, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Ikulu imeamua kumsimamisha kazi kwa siku 10 ili kumpa fursa, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kumchunguza.

Akitangaza hekima hiyo mpya ya Ikulu ambayo haijawahi kutumiwa kwa viongozi wengine waliopata kukabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili ya kazi, Luhanjo alisema hatua atakazochukuliwa Jairo zitategemea matokeo ya uchunguzi huo.
"Nimeona niwaambie hili ili tusiendelee kuwaambia wananchi tunamsubiri Rais, wakati mimi mwenye dhamana ya kusimamia nidhamu nipo hapa, nimeshachukua hatua.

"Kutokana na uzito wa jambo hili, nimelazimika kumwamuru CAG, Ludovick Utuoh, kufanya uchunguzi ndani ya siku 10 na iwapo itabainika kuwa ana kosa, hatua nyingine za kisheria zitafuata," alisema Luhanjo.

Pasipo kusema kwamba alikuwa akitekeleza maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa karibu kikazi na Jairo kwa miaka mingi, Luhanjo alisema likizo hiyo itakuwa ni ya malipo.

Kauli hiyo ya Luhanjo inakuja ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu Waziri Mkuu Pinda akaririwe akisema kuwa alikuwa amepewa maelekezo tofauti na Rais Kikwete baada ya kuwasilisha kwake malalamiko ya wabunge dhidi ya Jairo.

Pinda alitoa kauli hiyo juzi ikiwa ni siku moja tu baada ya kulitangazia Bunge kwamba iwapo suala hilo lingekuwa katika mamlaka yake na si ya Rais, angeshakuwa amemtimua kazi Jairo.

Akizungumzia tuhuma ambazo Jairo anakabiliana nazo, Luhanjo alirejea hoja zilizotolewa na wabunge ambao walitaka afukuzwe kazi kwa kosa la kuandika barua yenye maelekezo ya kukusanya kiasi cha fedha kinachofikia shilingi milioni 50 kutoka kwa kila taasisi iliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

"Kama mnavyofahamu, Julai 18 mwaka huu wakati wa majadiliano ya hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, baadhi ya waheshimiwa wabunge wakati wakichangia hotuba hiyo walimtuhumu Jairo kuhusika na tuhuma mbalimbali.
"Baadhi ya tuhuma zinazomkazili ni kuzitaka taasisi, vitengo na idara zilizo chini ya wizara hiyo zichangie shilingi milioni 50 kila moja, ili fedha hizo zitumike kuwalipa masurufu ya safari watumishi walio chini ya wizara na taasisi zake ambao tayari walishalipwa na wizara na taasisi zao," alisema Luhanjo.

Alisema lengo la kufanya uchunguzi huo ni kutaka kumpa fursa ya kujitetea kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma.

"Katibu Mkuu alituhumiwa na wabunge, na yeye hana nafasi ya kujitetea ndani ya ukumbi wa Bunge, na ni lazima tuhuma zipate maelezo ya upande wa pili na hapa ndipo sheria hii ya utumishi wa umma inachukua nafasi yake," alisema.

Akieleza kuhusu sheria za utumishi wa umma, Luhanjo alisema wakati wa kipindi cha uchuguzi, mtumishi wa umma anayetuhumiwa anaweza kupewa likizo ya malipo, ili kupisha uchunguzi au akaruhusiwa kuendelea na kazi wakati uchunguzi ukifanywa.
Alisema baada ya uchunguzi huo kukamilika na kama utabaini makosa ya kinidhamu, mamlaka ya nidhamu itampa mtumishi taarifa za tuhuma ambayo itaambatana na hati ya mashtaka na kwamba wakati huo mtumishi atasimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara.

Mzimu wa Jairo wamtesa Pinda

Katika hatua nyingine mzimu wa Jairo jana uliendelea kumtesa Pinda bungeni baada ya kubanwa kutokana na kushindwa kumwajibisha.
Akiuliza swali la papo hapo, mbunge wa Tumbe, Rashid Ally Abdallah (CUF), alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais ana mamlaka ya kufanya kazi za Rais endapo Rais hayupo, hivyo Pinda aliposema alikuwa hana mamlaka ya kumwajibisha Jairo ni kwenda kinyume na Katiba hiyo.

Akijibu swali hilo, Pinda alikiri kupata mtihani ambao hakuwa akiutarajia na akasema ni ukweli kwamba wanapokuwa viongozi wajuu wawili, Rais na makamu wake hawapo, hata yeye angeweza kuchukua mamlaka ya kufanya kazi za Rais.

"Mheshimiwa Abdallah kanipa mtihani wala sikutegemea. Ni kweli Rais asipokuwapo na hata Makamu wa Rais, mimi naweza kukwaa mamlaka hayo, lakini kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo si kila jambo tuna mamlaka ya kuchukua hatua. Kwa mfano hatuwezi kutoa msamaha wa wafungwa. Tuna kikomo cha mamlaka," alisema Pinda.
Alisema kuwa hata Makamu wa Rais anaweza kuchukua majukumu mengine ya Rais, endapo tu atapata ushauri wake (Pinda) wakati Rais hayupo.
Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alisema kwa mtazamo wake suala la Jairo si zito, hivyo kushauri kufanyika marekebisho ya Katiba ili viongozi hao wawe na mamlaka hiyo.
Aliposimama kulijibu swali hilo, Pinda hakutaka kuingia kwa undani zaidi ya kusema, "Naheshimu mawazo yako, naomba majibu yake yabaki yale yale."
Mbunge wa kwanza kuibua tuhuma hizo dhidi ya Jairo alikuwa ni mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo (CCM), ambaye ndiye aliyeionyesha barua ambayo inadaiwa kuandikwa na Jairo kwenda kwa taasisi 21 zilizo chini ya wizara yake kuomba wachangie kufanikisha bajeji yake.

Baada ya taasisi hizo kupata kiwango hicho cha fedha, zilitakiwa kuingizwa katika akaunti ya Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye akaunti namba 5051000068 iliyopo benki ya NMB, tawi la Dodoma.

Sehemu ya barua hiyo inasomeka: "Kama ilivyo wakati wa kuwasilishwa hotuba ya bajeti, maofisa mbalimbali wa wizara na taasisi zilizo chini yake huambatana na viongozi waandamizi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala yanayojitokeza wakati wa mjadala wa hotuba hiyo.

"Ili kukamilisha mawasilisho ya hotuba hiyo, unaombwa kuchangia jumla ya sh 50,000,000. Fedha hizo zitumwe Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye akaunti namba 5051000068 iliyoko benki ya NMB, tawi la Dodoma. Baada ya kutuma fedha hizo, wizara ipewe taarifa kupitia ofisi ya DP," alisema.

Wakati CAG akimchunguza Jairo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) nayo ilitangaza kuanza uchunguzi kama huo dhidi ya Jairo sambamba na ule unaomgusa Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge.

Mkurugenzi wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini , (TAKUKURU), Dk. Edward Oseah, amesema kuwa ofisi yake imeanza kuchunguza tuhuma zilizoibuliwa bungeni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, alikusanya shilingi bilioni 1 kutoka idara mbalimbali za wizara hiyo kwa ajili ya kutoa rushwa kuwezesha bajeti ya wizara hiyo kupita .

Pia wanamchunguza mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge kutokana na kumiliki kiasi kikubwa cha fedha nje ya nchi ingawa alisema kuwa kwa suala la rada hawawezi kumhusisha nalo kwani suala hilo lilitendeka nchini Uingereza (mhhh! Mbona yule Mahalu aliiba akiwa Italy na bado alipandishwa Kizimbani!?)na wahusika walishakiri hilo hivyo kwa sasa kinachojadiliwa ni namna ya kurudisha fedha hizo nchini.

Aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Naural Spring ambapo TAKUKURU wameandaa semina ya siku mbili kwa wahihiri wa habari.

Dk. Oseah alisema kuwa masuala hayo wanayachunguza na anatarajia kutoa taarifa mapema mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.
"Suala la Chenge kuhusika kwenye rada naomba niungane na DPP imeonekana hakuhusika kwani suala hilo halikufanyika hapa nchini bali lilifanyikia nchini Uingereza na wahusika waligawana fedha hukohuko ndiyo maana kampuni ya BAE Systems imekubali kurudisha fedha hizo nchini na majadiliano yanendelea juu ya namna ya kuzirejesha.

"Hili la Chenge kuwa na vijisenti hilo tunalichunguza, kwa kuwa na vijisenti vingi kuliko inavyotarajiwa nje ya nchi hili tunalifanyia uchunguzi ukikamilika tutawapa taarifa," alisema mkurugenzi huyo wa TAKUKURU .

Hivi karibuni mbunge wa Kilindi , Beatrice Shellukindo alilipua bomu Bungeni akimtuhumu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Jairo, kwa kutumia zaidi ya sh bilioni moja kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge.

Tuhuma hizo nzito zinakuja kipindi ambacho tayari wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini wakiwa wameibua tuhuma kama hizo za baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa na maofisa wa wizara hiyo, ili kurahisisha upitishaji wa bajeti ndani ya kamati.

Ilidaiwa kuwa Jairo alisambaza barua kwenye idara mbalimbali za wizara hiyo akiagiza wachangie shilingi milioni 50 kila moja kwa ajili ya kusaidia bajeti ya wizara hiyo kupitishwa ambapo pamoja na suala la mgao mkali wa umeme unaoendelea nchini ulisababisha waziri mkuu, Mizengo Pinda kutoa hoja ya kuondoa bungeni hotuba ya makadirio ya matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa wiki tatu .

Waziri Mkuu alisema kuwa alikuwa akisubiri Rais Jakaya Kikwete afike Afrika ya Kusini alikokwenda katika ziara ya kiserikali ili aweze ‘kumshtaki' Katibu Mkuu huyo kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake kwani hawezi kuchukua hatua dhidi yake kwani kwa mujibu wa sheria, mamlaka ya uteuzi ndiyo inayoweza kuchukua hatua dhidi yake.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Mwanza , Aishieli Sumari, ambaye alikuwa kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari aliwataka wananchi kuacha kuwapelekea fedha mahakimu ambapo alishauri ni vema TAKUKURU wakatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waepukane na vitendo hivyo vinavyochochea kuendelea kwa rushwa .

Aidha aliishauri serikali iwape watumishi wa umma stahiki zao zinazoweza kukidhi mahitaji yao jambo litakalowawezesha kukataa kupokea rushwa kwani watakuwa wamekidhi mahitaji yao kutokana na mishahara yao .

Jaji Sumari aliwataka TAKUKURU kubadili utaratibu wa kushughulikia tatizo la rushwa kwenye idara ya mahakama badala ya kufanya kazi ya kuwakamata watumishi wa mahakama wakipokea rushwa wawaelimishe kuacha kupokea rushwa ambapo alisema kuwa kwa semina waliyowapa wameanza kujenga mshikamano katika kupambana na rushwa.
FemAct watoa tamko

Nao Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea usawa wa jinsia, haki za binadamu, demokrasia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) umemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuwachukulia hatua za kinidhamu wote waliohusika na tuhuma za kuchangisha fedha za kuwahonga wabunge.

Akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti ya Femact, Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Ussu Malya alisema mambo hayo yamefanyika kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

"Tunamtaka Rais Kikwete awafute kazi watendaji hao mara moja na kuwachukulia hatua za kisheria Katibu Mkuu,Waziri,Naibu wake kwa pamoja na watendaji wengine waliohusika ili iwe mfano kwa wahalifu wengine waliojificha katika ajira za serikali," alisema Mallya.

Alieleza kuwa sema katika marekebisho ya bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati Serikali ilete mikakati sahihi ya kulimaliza tatizo la umeme nchini.
Alisema kwao wao kama wanaharakati wanaona kuwa kitendo hicho ni ishara ya mambo makubwa zaidi yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu yanayosababisha kuendeleza ufukara na umaskini wa taifa letu na watu wake.

"Hali hii inatufanya tuzidi kuamini kuwa serikali inayoghubikwa na kuendeshwa kwa mfumo wa kuhongana miongoni mwa viongozi na watendaji wenye mamlaka ya kufanya maamuzi katika mihimili mikuu ya dola, ni serikali ya hatari na isiyostahili kuendelea kuwa madarakani," alisema Mallya.
Alieleza kuwa tatizo la umeme halikuanza leo kwani limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu, Serikali imekosa mbinu na mikakati sahihi hadi kufikia hatua ya kutaka kubinafsisha Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO).
Aliongeza kuwa mikataba mingi michafu imeingiwa na Serikali kwa kutumia makampuni makubwa ya nje kama IPTL, Agreco, Songas, Richmond, Dowans na NetGroup Solutions.
Alisema Muungano wao unaamini kuwa kuna sababu nyingine inayolazimisha Serikali kujaribu kutoa rushwa ili kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ni mfumo mzima wa mikataba, uwekezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli za madini na gesi asilia hapa nchini ambao hauna uwajibikaji; na uwazi wake una mashaka na hivyo kuhalalisha vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kauli ya January Makamba

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba (CCM) amewataka wanasiasa kujisafisha na kuacha kutumia muda mrefu kwa kurushiana maneno.
Akizungumza katika tamasha la vijana lililofanyika katika ukumbi wa Kanisa la ATN lililopo Mbezi Jogoo jijini Dar es Salaam, Makamba alisema kuwa hiyo ni moja ya changamoto inayowakabili viongozi kwa sasa ambapo hushindwa kufanya shughuli ngingine za maendeleo.
Alisema inawapasa viongozi kujitazama upya na kuhakikisha wanakuwa na roho safi ili kufikia malengo ya kimaendeleo kuliko kuendelea kurushiana maneno.
"Hata mkitazama magazeti mtagundua wazi kuwa viongozi wanatumia muda mrefu kurushiana maneno …huyu anagombana na yule vitendo ambavyo havimpendezi Mungu," alisema.
Makamba alisema kuwa jamii imejengwa katika misingi ya ustaarabu ndiyo maana imekuwa ikipuuza vitendo hivyo ambavyo vimekuwa havionekani ndani ya jamii.
"Viongozi wengi vijana kama mimi tunatazamiwa kuwa viongozi zaidi mbeleni kwa kuwatumikia wananchi hivyo inatupasa kuepuka majibizano na kuhakikisha tunapigania maendeleo ya nchi yetu kuliko kuendeleza malumbano," alisema.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na vijana hao likiwemo suala la umeme, Makamba alisema kuwa wanafahamu kuwa Watanzania wanahitaji umeme wa uhakika hivyo suala la visingizio vya kukosa mvua si vya msingi.
Alisema wataalam walipaswa kuelewa kuwa kuna kipindi cha kiangazi hivyo ni vyema wakatumia mipango iliyoandaliwa ili kuwapatia Watanzania Umeme.
Makamba alisema kuwa suala hilo limewafanya baadhi ya wananchi kuondoa imani walioijenga kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) lakini aliwahakikishia kuwa ataendelea kupigania bila kuchoka hadi umeme wa uhakika upatikane.
"Hapa lazima tukubali kuwa tatizo la kutoweka mipango thabiti ndiyo imetufikisha hapa na nakubaliana nanyi kuwa kuna watu wanatakiwa kuwajibika katika suala la umeme, alisema na kuongeza: "…Kama ningekuwa msimamizi mkuu katika Wizara hiyo ningehakikisha ifikapo Desemba 31 kila mwaka tungeweka utaratibu wa kukutana na yule anayeshughulikia umeme ambapo anatakiwa kufika na barua mbili moja ya kujiuzulu na nyingine ya kufungua miradi ya umeme," alisema.
Alisema iwapo msimamizi wa suala la umeme atashindwa kuonyesha mradi unaotakiwa kufunguliwa basi ile barua ya kujiuzulu anatakiwa kukabidhiwa pasipo maswali hasa kutokana na kushindwa kuwajibika.
Pamoja na hilo aliwahakikishia Watanzania kuwa hataacha kulipigania suala hilo na wala kuacha kuikosoa serikali katika masuala ya msingi yaliyo na maslai kwa Taifa.
"Mtakumbuka kama ninyi ni wafuatiliaji wa masuala ya Bunge jinsi Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe (CHADEMA) alivyohoji juu ya taarifa niliyoitoa kwa serikali na kushangazwa na kunitaka kujiunga nao,nawaahidi kusimamia ukweli," alisema.
Aidha Makamba aliwaasa vijana hao kujiepusha na tamaa ya kutaka mafanikio ya haraka kwa kupita njia ya mkato bali wanapaswa kumtumaini Mungu kwa kuwa mafanikio hayaji mara moja. Ataka Bunge kujiuzulu

Sakata la kutopitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini linazidi kutolewa maoni mapya kila siku baada ya mwaharakati katika masuala ya siasa, Kadawi Limbu, kulitaka Bunge la Jamhuri kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo.
Limbu ambaye uchaguzi uliopita aligombea kiti cha ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Temeke, alisema Bunge hilo halina haja ya kuendelea kutokana na barua ya Katibu wa Wizara hiyo, David Jairo, kuwagusa moja kwa moja na wao.
Akinukuu mojawapo ya sehemu ya barua iliyoandikwa na Katibu wa Wizara hiyo, David Jairo, na kusomwa na Mbunge wa Bumbuli, Beatrice Shelukindo, iliyotaka idara zote zilizo chini ya wizara hiyo kuchangia kila moja shilingi milioni 50 kama ilivyo kawaida, ili kufanikisha kupitishwa kwa bajeti hiyo…"
Limbu alisema nukuu ya barua hiyo inaonyesha wazi kuwa huo ndio utaratibu wa Bunge kupokea rushwa hiyo, hivyo haoni haja wabunge hao kuendelea kupoteza muda Dodoma na kufuja fedha za wananchi wakati Bunge lote linanuka rushwa na kuongeza kuwa limeoza.

Aidha mwanasiasa huyu alisema ni vyema wabunge hao wakaachia nyadhifa zao bila kujali vyama walivyotokea na kuitishwa uchaguzi mwingine na wao kukaa kando bila kugombea nafasi yoyote ile.
"Jamani ninavyoona mimi, Jairo anafanywa mbuzi wa shughuli katika sakata hili, kwani barua aliyoaindika inaonekana ni ya kikazi na hajakaa mwenyewe tu na kuielekeza katika idara hizo na ndio maana ikasisitiza kama ilivyo kawaida, yote hii inamaanisha hata katika wizara nyingine ndivyo inavyofanyika.
"Pia tumezoea kuona tuhuma zote zinazowasilishwa na wabunge, Spika kutaka kupelekwa kwa maandishi mezani kwake, mbona hii ya Shulukindo hakutaka apelekewe mezani hata pale mbunge huyo aliposema endapo itakanushwa ataipeleka mezani kwake, ina maana na yeye anajua utaratibu huo kuwa unafanyika ndani ya Bunge lake," alisema Limbu.
Alienda mbali zaidi kuwa mpaka sasa mihimili mikuu miwili ya nchi ikiwemo Serikali na Bunge wananchi wameshakosa imani nayo kwa kushindwa kuonyesha dhamira ya kweli ya kupambana na rushwa na barua hiyo ni ushahidi tosha na kutaka iwekwa wazi hata kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kuona kile kilichoandikwa humo.
Alisema barua hiyo inaonyesha dhairi kwamba Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikishawishi Bunge kwa fedha ili kupitisha mambo yasiyofaa na mhimili pekee uliobaki ambao bado vithibitisho havijapatikana ni mahakama peke yake. Hata hivyo alitahadharisha kuwa Raisi Jakaya Kikwete asije akadhani atakapomfukuza Jairo, nchi itakuwa salama, kwani serikali yake yote imeoza na dawa ni iliyopo ni kuivunja.


Sijawahi kuona Serikali jinga na pumbavu kama hii
 
Unaijua sheria ya kazi au unaongea kishabiki tu?

Sheria ipi? Sheria nyingi zina provision ya 'summary dismissal'. Kuna makosa ukifanya (gross misconduct) unafukuzwa kazi mara moja! Labda cha kujiuliza hilo alilofanya Jairo linaangukia katika aina gani ya makosa na katika sheria ipi (mind you yeye ni presidential appointee).
 
KATIBA mpya jamani. Wenzetu Kenya TEUZI hizi za Rais hazitawapa shida tena kwa katiba yao mpya ilivyo sasa.
 
Pamoja na kwamba mimi si mtaalam wa sheria na taratiibu za mambo ya utumishi wa umma, la jana la Katibu Mkuu Kiongonzi Bw Philemon Luhanjo kumpa likizo yenye malipo Bw. David Jairo kupisha uchunguzi wa kashfa ya kukusanya fedha ili wizara itoe mlungula kwa wabunge huko Dodoma limenishangaza sana. Mtu anaonekana kuwa na kosa la wazi kabisa la kiutendaji/kiutumishi anapewa likizo badala ya kumfukuza mara moja?Ndio maana hata Waziri wa Ulinzi Mh.Hussein Mwinyi hakufanywa kitu kutokana na issue ya mabomu Mbagala na G/Mboto.Nchi hii ndio huwa nachoka kabisa nikiona haya.
 
si mmesikia Malawi kimenuka? soon kinakuja bongo hawa maharamia lazima waswekwe ndani wooote saa ya ukombozi ni sasa!!!!
 
Pamoja na kwamba mimi si mtaalam wa sheria na taratiibu za mambo ya utumishi wa umma, la jana la Katibu Mkuu Kiongonzi Bw Philemon Luhanjo kumpa likizo yenye malipo kupisha uchunguzi wa kashfa ya kukusanya fedha ili wizara itoe mlungula kwa wabunge huko Dodoma limenishangaza sana.Mtu anaonekana kuwa na kosa la wazi kabisa la kiutendaji/kiutumishi anapewa likizo badala ya kumfukuza mara moja?Ndio maana hata Waziri wa Ulinzi Mh.Hussein Mwinyi hakufanywa kitu kutokana na issue ya mabomu Mbagala na G/Mboto.Nchi hii ndio huwa nachoka kabisa nikiona haya.

What do you expect from the magambas. This is what it means when they say "Collective responsibility". This is not Jairo's issue. It is the government's issue. Such corruption has been happening over the years. This time ni sawa na mtu aliyejivisha mabomu na kujilipua mwenyewe. You know how?? baada ya kubainishwa kwa rushwa katika kamati ya madini na nishati ambayo spika ameizugazuga ikaishia baadae waligundua kwamba rushwa kubwa inayowahusisha wabunge wengi wa magamba imeshavuja kwa wapinzani. Kilichoendelea ni kwamba walikuwa hawana jinsi ila kujilipua wenyewe kabla wapinzania hawajaishusha bungeni serikali ikapata aibu. Sasa mkakati uliopo ni kutafuta kondoo wa kafara na jinsi ya kulishughulikia na kulizima jambo lenyewe kwa style ya kimagamba. Wait and see..
 
kama si mtaalam wa masuala ya sheria unapaswa uuliza na siyo kuhoji/kuzoza. Soma vizuri kauli ya luhanjo labda utaelewa.
 
"amani amani amani, wimbo wetu tuupendao sana na umekaririwa na kila mtz kama waja wakaririvyo Haya Takatifu!"
Ngoja tuhesabu ni siku ngapi zimebakia kuuimba wimbo huo mzuri.
si mmesikia Malawi kimenuka? soon kinakuja bongo hawa maharamia lazima waswekwe ndani wooote saa ya ukombozi ni sasa!!!!
 
kama si mtaalam wa masuala ya sheria unapaswa uuliza na siyo kuhoji/kuzoza. Soma vizuri kauli ya luhanjo labda utaelewa.

Nawe acha fikra za utoto, kuna mambo ambayo yanatumia common sense kama msomi, sio lazima kuwa mtaalamu wa sheria!!!!!!! Kuna mambo ya wazi. Ile barua inajieleza haina utata -does not need interpretation nor interpolation!!!! quite express
 
Jamani za mbayuwayu, tieni na zenu. Kwanza kuna connection gani kati ya mkuu wa nchi na jairo asichokifahamu Pm? Angalieni kauli ya pinda ya kumsubiria mkuu arudi nchini kutoa hatma ya jairo, na baada ya kurudi ndio jamaa anapewa likizo. Ni nini Jk alikuwa anataka atete kwanza na Jairo? Ni maslahi gani jk anataka kulinda kwa jairo? Kwanini katibu mkuu hakutoa uamuzi alioutoa jana kabla hadi mkuu wa kaya arudi?
Hili li nchi limegeuzwa kijue cha gahawa, wallah miaka minne ya jamaa iliyobaki hakuna rangi tutaacha kuona.
Habari ya jairo katika blog ya mwananchi wameblock maoni maana raia wenye hasira kali walikuwa wanaiharishia serikali kwa jinsi isivyoweza kuadisiwa.

.
 
Lowasa, mtuhumiwa mkubwa kabisa wa Richmond ni WM mstaafu, ni mwenyekiti kamati nzito kabisa ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na ni "rais mtarajiwa" come 2015! Tanzania zaidi ya unavyoifahamu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom