Jairo asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.
Na mimi nashangaa sana. Mara tumsubiri raisi ndio mwenye mamlaka ya mwisho kuhusu hatima ya Jairo; mara anajitokeza Luhanjo kwamba hii ni kesi yake hivyo ataimaliza yeye. Lakini nawalaumu wote waliompa kura huyu mtu mwenye IQ ndogo kabisa kuwahi kutokea kuwa rais wa nchi yetu. Sijui aliwarubuni nini nyie mwaka 2005 hadi mnamwita chaguo la Mungu. Mimi sikuwahi kumpa kura hata ya mwaka 2005 sikumpa hiivyo sina hatia mie. Mtakaa kwenye giza mpaka akili ziwaingieni!!!!!!
 
Kama Jairo anao ushahidi wa kimaandishi kuwa alikuwa anatekeleza amri ya waziri wake, anaweza kuponyoka. Vinginevyo tusubiri huo uchunguzi ambao ukiwa huru unaweza kuigusa hata Ikulu yenyewe.
 
Kapewa likizo ya malipo na kazi hatofukuzwa,hao ndio wakubwa wanavyolindana hakuna jipya hapa.Kama Pm alisema ni mamlaka Hana angekuwa ameshamfukuza kazi vp mkuu wa Kaya kuja na hakuna kilichofanyika zaidi ya likizo ya malipo kupisha uchunguzi(danganya toto)hewa?Kama barua imekamatwa kwenda kwa taasisi zilizopo chini zichange ml50 kuipitisha bajeti hiyo hapo pana nini Kama sio wizi wizi wizi tu wa Serikali hii dhalimu ya ccm?Kwa nini mnakula kodi zetu bila huruma!?
 
Jairo, Jairo. Haya mambo yalishakuwa sera, utamaduni. Hata Luhanjo ana mgao wake humo. Ni usanii tu kwa kwenda mbele. Huyo CAG aliyetumwa kwenda kuchunguza kila mwaka anayaona mavocha haya tena mahala pengi tu.
 
Tanzania haiko kama unavyoifahamu wewe.
katika makosa aliyokua nayo yule kijana aliepata ajali na kupelekea kifo cha Marehemu Chacha Wangwe,
Andrew Chenge alikutwa na makosa yaleyale ukiongezea na lingine la gari kutokua na BIMA HALALI, pia kufoji hati ya bima FEKI.
Yule jamaa (Milya/Malya) alifungwa bila option ya kulipa faini, wakati mtu anaekuambia Tshs 1Bil. ni vijisenti kwake aliambiwa atoe laki 7 tu ili aachiwe.
 
Nawe acha fikra za utoto, kuna mambo ambayo yanatumia common sense kama msomi, sio lazima kuwa mtaalamu wa sheria!!!!!!! Kuna mambo ya wazi. Ile barua inajieleza haina utata -does not need interpretation nor interpolation!!!! quite express

Asante kwa hili,watu wengine sijui wakoje?
 
Kama Jairo anao ushahidi wa kimaandishi kuwa alikuwa anatekeleza amri ya waziri wake, anaweza kuponyoka. Vinginevyo tusubiri huo uchunguzi ambao ukiwa huru unaweza kuigusa hata Ikulu yenyewe.

Ukijaribu kufikiri kinadharia mlolongo wa matukio yaliyopelekea uchunguzi ufanyike utaona kwamba huu hauwezi kuwa uchunguzi huru. 1. Inasemekana hili jambo la kuonga wabunge ili budget zipite ni jambo la kawaida kwa wizara mbalimbali. Serikali imekuwa ikifanya hivyo miaka mingi, raisi anajua, waziri mkuu anajua,mawaziri wanajua, wabunge wanajua na hakukuwa na sababu ya kuhofu kwamba wakati huu wangekuwa exposed kwa wananchi. 2. Kwa kuwa hawakuwahi kuwaza kuwa wangekuwa exposed hivyo hawakuwa wamejiandaa kimkakati kukwepa masahibu ambayo yangeweza kuwapata hivyo kila mmoja anayeguswa katika hili anaanza kujikanyaga; kwa waziri mkuu, oh, tumsubiri raisi, raisi naye anapatwa na mstuko mkubwa huko Afrika Kusini; Katibu Mkuu mwenyewe anaaza kupayuka mara wabunge ni kama comedy; mara vitisho kwa Shelukindo; Ngeleja yeye yuko kimya kabisa. 3. Wote hawa sasa wanaanza kushauriana wafanye nini. Mara akili zinawajia kwamba hili jambo tumsukumizie Katibu Mkuu Kiongozi. Na deal inafanyika kwamba apewe likizo ya malipo halafu somehow, someway, watapata tu loophole ya kumchomoa huyu Jairo na watanzania watazugika. After all hii ni TZ na hakuna nchi rahisi kuongoza kama TZ.

Prediction: Kwa sababu hii kesi ni ngumu sana kwa Jairo kutoka safi kwa mazingira yaliyopo hasa ile barua iliyo very obvious kwa sahihi yake na malengo yake, lakini kwa sababu ili jambo kaachiwa Katibu Mkuu Kiongozi, most likely vitatafutwa vifungu vya sheria vya uongo na kweli, vitapindishwa, na jamaa ataonekana ana makosa lakini kwa sababu yeye si mwanasiasa ni mtendaji atachukuliwa hatua za kinidhamu za kiutendaji. Lakini si kufukuzwa kazi. Ngeleja, ah, haguswi hata kidogo. Tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele.
 
Pamoja na kwamba mimi si mtaalam wa sheria na taratiibu za mambo ya utumishi wa umma, la jana la Katibu Mkuu Kiongonzi Bw Philemon Luhanjo kumpa likizo yenye malipo Bw. David Jairo kupisha uchunguzi wa kashfa ya kukusanya fedha ili wizara itoe mlungula kwa wabunge huko Dodoma limenishangaza sana. Mtu anaonekana kuwa na kosa la wazi kabisa la kiutendaji/kiutumishi anapewa likizo badala ya kumfukuza mara moja?Ndio maana hata Waziri wa Ulinzi Mh.Hussein Mwinyi hakufanywa kitu kutokana na issue ya mabomu Mbagala na G/Mboto.Nchi hii ndio huwa nachoka kabisa nikiona haya.
Sishangai kusikia hayo ya Jairo kwa serikali ya ccm. Wao wanalindana lakini wanyonge tunaonewa na kuwindwa kama ndege na manati. Mwenye ile habari ya Ngeleja na yule askari wa benki aliyefukuzwa atuwekee ili tuone jinsi wanavyolindana na kumnyanyasa baba wa watu. Tunajua cheo ni cheo bana na masikini ni masikini. Imebakia kulamba viatu vyao tu kwa ajili ya upumbavu wetu. Kama tunataka serikali ithamini mawazo yetu na itende haki sasa tuchukue maamuzi magumu tuingie barabarani tuishinikize serikali nayo ifanye kazi kama serikali.
 
tunahitaji kuingia mtani kuandamana

kusubiri miaka minne ni mingi sana jamani
hebu amasisheni watu
uozo umezini
tunahitaji kiongozi sio kuchezena akili
Likizo ya mtuhumiwa na malipo?
au ndio Bosi wa pinda aliyoamua? bada ya kusuburiwa?
 
Hivi binti Kiroboto mjengoni baada ya barua kuwasilishwa mjengoni alitakiwa kuchukua hatua gani za kibunge? Wapinzani nao hawaoni kasoro hii ya serikali kutuhumiwa bungeni na kupewa fursa ya kujiamulia namna ya kusolve tatizo? Ama kweli laana ya kakobe imewapata ninyi nyote kuanzia serikali/wapinzani na hata sisi raia.

.
 
Wala msijidanganye, Luhanjo hawezi kumtosa Jairo. Hawa watu ni wazee, lazima walindane.
Just wait and see.
 
Jamani mlioangalia tv yetu ile na kusikiliza clouds fm mmh yaani
ni hatari kwa kweli jamani kusikia mwizi huyu eti anasubiri uchunguzi
na amepewa likizo ya malipo jamani kweliiiiiiiiiiiiiii wewe kikwete weewe ndio uamuzi uliomwambia pinda asubiri urudiiiiiiiii unatafuta laan kwa watanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaa

uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mwenye msaada wa kunipa permit ya kuishi sudan kuzini jamani naomba msaada
 
Jairo atakuwa kapewa likizo ili atafakari kati ya vyeo vingine wanavyotaka kumpa achague kipi, tusishangae kusikia kawa balozi.
 
Jairo ni mbuzi wa kafara wa siasa za kupakana matope za ccm. Kwa wale tuliozoea tunajua kabisa kila wizara " hutoa hongo" ili bajeti yake ipite. Hii ni kuendesha semina na warsha siku za jmosi na jpili wakati bunge liko kwenye mapumziko ya weekend. Hapo hutolewa posho kubwa kubwa zisizo na kichwa wala miguu kuwaeleza wabunge mambo mbalimbali hizo fedha huwa hutolewa na wizara husika. Biliono moja ilikuwa ni kwa kazi hiyo na David Jairo atarudi kwenye ulingo tu....yetu macho. Shelukindo yupo kwenye timu ya SS hivyo wanataka kuonyesha ccm haitaki ufisadi !!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom