Jairo ajiuzulu wadhifa wake

Status
Not open for further replies.
Nimewataja TAKUKURU kwa kuwa jana wametamba kwamba wameanza uchunguzi na halafu ndiyo chombo pekee kilichopitishwa na bunge kufanya kazi kama hizi. Au washauri tumuombe DCI Manumba ashupalie hili suala, lakini looh nanongonezwa na kuwa kumbe Hosea wa TAKUKURU na Manumba wanatoka wilaya moja, sijui hiyo itaathiri utendaji wao!!! Kuhusu swali lako, miimi ni Mtanzania, naishi muda nusu kwa nusu Bongo na nje ya nchi katika kuhangaikia maisha. Kumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere alipokuwa anaongea kuhusu uchaguaji wa candidate mzuri wa uraisi: 'Mimi siyo kuku sitagi mayai, lakini ukinipa yai bovu nitaligundua!!', hivyo nchi yangu naifahamu, ondoa shaka.

Nimeipenda sana hili jibu, thankx very much, mwaka gani huu Nyerere aliyoa hii naomba ili niitumie kwenye signature yangu.
 
Hivi kwani mtu akijiuzulu hawezi fikishwa katika vyombo vya sheria kama step ya kwanza huku uchunguzi ukiwa unaendelea???

Hii ndiyo step ZERO ya kuwashughulikia wahusika na wakifika step TEN basi mawizara yote yatakuwa yameshikishwa adabu ila anahitajika mtu mwenye roho ngumu kuanzisha hii move kwani ni mawaziri, makatibu wakuu na wabunge wachache sana watakao salimika.

Najua mzee wangu ninayemuheshimu sana Peniel Lyimo hana huu uchafu wanaofanya hawa jamaa; huyu ni mtu namfahamu ni mwadilifu na anapenda kusimama katika haki most of time.
 
Naomba nirudie kitu ambacho niliwahi kuandika huko nyuma.
The mother of all cardinal rules in politics: Ukiona issue/potential scandal inaongelewa na umma including media for more than 24hrs basi ujue you are in big trouble na ACTS haraka. Yapata sasa masaa 36 tangu issue ya Jairo kuanza na hadi sasa barua ya ama kumfukuza au kujiuzulu kwake inasuasua. Hata kama watakuja kumfukuza Jairo jioni, kesho, kesho kutwa ccm wakae wakijua kuwa every minute kwa sasa ni 'inazidi kuwamaliza'

Kuendelea kukalia hii saga ni confirmation kuwa serikali yote imeoza na ndio maana wanaogopa kumtosa Jairo. Pinda na majigambo yake ya maamuzi magumu - porojo!
 
one side:Mheshimiwa huyu jamaa kaharibu mambo,kuna m-mbeya mmoja
kakamata barua yake na ameisoma bungeni imebidi nilazimike kuondoa bajeti ya ile wizara bungeni,...


other side:Dah sasa itakuaje bana?kwanini hamkumpa cash ya kutosha lakini
hadi akatoka kusema?


one side:naona umfukuze tu kazi bana au unasemaje maana waheshimiwa ndivo walivo komaa eti,
tena mbaya zaidi hadi wa upande wetu sijui wamekunywa juice nyekundu+nyeupe+nyeusi??!!!!


other side:aiseee,ntaweza kweli?au mwambie tu aandike baru ya kujiuzuru ili apate malupu lupu yake aondoke,
kafanya kosa mwenyewe hakua makini kama wengine!!


one side:eti eh?ila kweli ukimfukuza atatoa siri zetu nyingi maana naona kuna
mashushushu wengi kweli tusio wajua,kama vipi ngoja niongee nae fasta!!!
 
Mkuu..Ngeleja , na yule mdogo wake nanihiii ....yes Malima pamoja ma katibu wao...wote watoswe na mahakamani wafikishwe. It does not make sense that the katibu could have done by himself, there should be a chain of participants
 
Amesema ni kwa nini anajiuzulu? Yawezekana ni bangusilo na 'wakuu' wanataka kufunika kombe! Hii habari ya kulobby (kuhonga!) ili bajeti zipite imeanza kusikika muda mrefu tu.
Mkuu, unaamini kabisa Ngereja na naibu wake walikuwa hawajui habari hii....hahahaha
 
Atakuwa ameonyesha njia ila isiishie hapa lazima mtandao mzima uwe tracked ikiwemo list ya wabunge waliokula hizo hela. Ni rahisi kuwapata kwani benki wana jina la mtu aliye draw hizo hela na tarehe aliyochukua. Pia wizara nyingine zifuatiliwe maana najua huo ndio utamaduni wa serikali inayopinga rushwa lakini yenyewe inatoa rushwa kwa wabunge.

Hapa ndo napata picha kwamba siyo rahisi TAKUKURU ifanikiwe kufanya kazi kama autonomous institution kwani nao pia kama idara kuna jinsi nao walitakiwa watoe mchango wa rushwa kwa wabunge ili bajeti YA WIZARA yao ipite na kwa kufanya hivyo wataweza kupambana na rushwa vizuri zaidi. "WHAT A JOKE"

Hivi TAKUKURU iko chini ya Wizara ipi, Wizara ya Sheria na Katiba au Ofisi ya Rais? Kama iko Ofisi ya Rais nachelea kushauri kwamba na wao wachunguzwe akaunti yao hapo Ofisi za TAKUKURU Dodoma kama inapitisha fedha za kulaininsha wabunge ili bajeti ya Ofisi ya Rais ipite. Halafu kila mara huwa tunasikia kuwa kila bajeti ikipitishwa, Wizara husika hjuangusha bonge la party (millions of sdhillings) kusherehekea bajeti yao kupitishwa. Kuna mwaka Wizara ya Mali Asili ilitayarisha party kubwa pale Dodoma baada ya bajeti yao kupita, na wanyama pori kibao walichinjwa na kuliwa. Hii ni dalili ya kitu gani?
 
Kama TAKUKURU wako serious, waongeze wigo wa uchunguzi, wapitie akaunti zote za Idara za serikali zilizoko hapo Dodoma yaani hiyo Geological Survey (Madini), Msalato na Bihawana Secondary (Elimu), Isanga Prisons (Mambo ya Ndani), Mirembe Nursing School (Afya), Makutupora JKT (Ulinzi) nk; hizi zote inawezekana ziunatumiwa kupitisha mafungu ili zitumike kuhonga wabunge. Na hasa wachunguze zile transfer kubwa kubwa za funds katika kipindi cha March hadi August. Naamini kwa kuwa wao ni wataalamu, basi watajua technic nzuri zaidi ya mapendekezo yangu. Lakini nikikumbuka uchakachuaji wa uchunguzi wa awali wa Richmond, basi na-reserve my comments kama hawa TAKUKURU wanaweza chukua maamuzi magumu!!!
maadam chenge ni safi machoni mwa takukuru, jueni ya kuwa imeshafeli kabla haijaanza takukuru-puka, mimi binafsi sina imani na serikali hii ya ccm-jk.
 
Naona Jairo ni mbuzi wa kafara. Kwa kifupi nimjuavyo Jairo ni kipenzi na zao la Kikwete kamwe sikutegemea angeweza kufukuzwa. jamaa alikuwa TIS miaka ya nyuma na ni chapombe kupindukia ni jeuri wa kutupwa. Aliwahi kuwa wizara moja na JMK na kila Jmk alipotaka kumchukua kwenye wizara nyingine alipopita jamaa wa wizara hizo nyingine walimkataa.
Anajulikana wizara zote kwa ukorofi na ujjueuri alioupata kupitia kwa Kikwete. JK alimteua kuwa katibu wake akafuja pesa kama kawaida yake akaondolewa Ikulu pamoja na kina Sisqo na Chabaka Kilumanga.

JK kama kawaida yake akampa shavu Nishati na madini na sasa ameboronga. Ikumbukwe akiwa nishati na madini before alikuwa Project Manager na alipata kashfa ya kupiga pesa akahamishwa wizara so u can see the chap has gut to squander with Pesa ya Umma atakavyo.

Nasema ni mbuzi wa kafara kwa sababu huu unaonekana ni utaratibu ambao wizara zimejiwekea ili bajeti zipite lakini hili limemnkuta Jairo baada ya kuonekana hawaheshimu wabunge wala mawaziri wake.Wahusika watafute njia ya kuona kwa jinsi gani wizara nyingine zimekuwa zikifanya na miaka mingine nyuma.
 
source kwanza ndo nachangia, isije ikawa tunakumbushana ya tarehe 1 kila mwezi wa 4 maana ndo siku ya wapumbavu na si wajinga maana siku yawajinga ni kila siku
 
huyu Jairo kuondoka haitoshi, Ngeleja anangoja nini huko bungeniiiiiiii??????
 
Hivi TAKUKURU iko chini ya Wizara ipi, Wizara ya Sheria na Katiba au Ofisi ya Rais? Kama iko Ofisi ya Rais nachelea kushauri kwamba na wao wachunguzwe akaunti yao hapo Ofisi za TAKUKURU Dodoma kama inapitisha fedha za kulaininsha wabunge ili bajeti ya Ofisi ya Rais ipite. Halafu kila mara huwa tunasikia kuwa kila bajeti ikipitishwa, Wizara husika hjuangusha bonge la party (millions of sdhillings) kusherehekea bajeti yao kupitishwa. Kuna mwaka Wizara ya Mali Asili ilitayarisha party kubwa pale Dodoma baada ya bajeti yao kupita, na wanyama pori kibao walichinjwa na kuliwa. Hii ni dalili ya kitu gani?

Ipo ofisi ya rais

Kwahiyo hizi bajeti siyo kwa ajili ya maendeleo? Kweli waafrika wanahitaji kutawaliwa bado hawajaweza kujitawala.
 
Jairo na viongozi wa juu yake wanatufanya sisi watanzania mabwege siyo...... Jamaa anajiuzulu ili apate Mafao yake! Huyu angefukuzwa asingepata kitu,Hapa kuna kamchezo kanaendelea
 
When will our presdaa be responsible and take things seriously ???????
Kuchukua hatua anasubiri mpaka yeye mwenyewe ahusishwe kwenye rushwa waziwazi?
 
hata kijihuzuru hasara ngapi ameshasababisha? apelekwe court ili apate zawadi yake na haki isimamiwe moja kwa moja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom