J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'

Mkuu kwanza nakupongeza sana kwa uchambuzi wako uliokua mzuri kwa kweli nakupa ahsante sana kwa hilo.
Ila ukweli utabakia kua ndani ya CCM hakuna alie msafi hata huyo Kikwete sio msafi.
kwa kifupi tungeungana tu kuitoa ccm madarakani! aje mchawi mwingine kuturoga, huyu tuliyemzoea dawa zake zinadunda!
 
galiya wewe uko kundi gani? muda uliotumia kukusanya habazi zote hizi si bure lazima unajenga mazingira ya kupunguza upinzani kwa mtu wako
 
Last edited by a moderator:
POMPO,

Nashukuru mkuu. Pamoja sana. Nakuhakikishia mimi natumwa na UZALENDO. Mambo ya UVCCM hayanihusu.

Umeuliza ni kwanini JK aliweza kupita 2005 na ni vipi EL atashindwa kupita. Kama nilivyosema katika utangulizi wangu ni kua Nyerere alimkubali JK kwani hakuna na kashfa yoyote. Nyerere alimkataa EL kwakua alikua ananuka rushwa ingawa alikua bado kijana mdogo. NASISITIZA KAMATI KUU YA CCM 2015 haitakubali kumpitishwa EL.

Wale wote mnaoganga njaa gangeni jaa zenu lakini mjue kua at the end of the day EL atachinjiwa baharini. Habari ndio hiyo!
hakumkubali wala nini naye alionekana hafai tu ndo maana nyerere alikomaa na mkapa
 
Galiya,

Karibu JF.

Sie tumetumwa na Lowassa na tuna njaa. Pundit wa siasa asingesema hayo maneno. Unaponyosha kidole kimoja kwetu vinne vinakuelekea wewe. Safi. Umepewa shs ngapi na wewe?

Nyerere ni Malaika au Mungu mpaka asemalo lazima liwe?. Je kama faili alilopewa "mungu" wako Nyerere lilikua la chuki utajuaje? (remember 'mungu' wako alikua hayupo kwenye system wakati huo)

Je hata kama ni kweli, haijaandikwa kwenye vitabu vitakatifu UKITUBU unasamehewa?, je unajuaje kua Lowassa ameshajirekebisha?

Au ndio magazeti yanafikiria kwa niaba yako?

Karibu JF.
hawezi kujirekebisha! yule ni mchafu tu! alishaipaka nyeupe kuwa nyekundu kwa matendo yake! binafsi simtaki, simtaki ccm yeyote kuongoza tena nchi hii!
 
galiya wewe uko kundi gani? muda uliotumia kukusanya habazi zote hizi si bure lazima unajenga mazingira ya kupunguza upinzani kwa mtu wako
unataka kwenda ikulu una team work wewe.......bado sijaoteshwa ......nikioteshwa nitautangazia umma wa WATANZANIA.....BM
 
umechambua vema! Bt umekosea kwani umemsafsha JK..wakat nae aliingia ikulu kwa njia chafu kulio hata anavyo fanya Lowassa
 
Mimi siamini kwamba EL hajui anachofanya ndani ya ccm kwa sasa! Anajua fika kuna vikao vya cc, nec na mkutano mkuu. Anajua kuwa ili apitishwe na chama lazima apite kote huko. Siamini kama anao uwezo wa kupanga safu katika nec na mkutano mkuu ambako kote kuna wajumbe wengi zaidi ashindwe kupanga safu katika cc? EL anajua anachofanya na anajua kuwa with money in tz nothing impossible. My take: wapenda mabadiliko wote tufurahie kwa lowasa kupitishwa na ccm maana hawezi kuhonga wa tz 10m wamchague hivyo kazi itakuwa rahisi kuimaliza ccm.
 
FAIRPLAYER

Inaonekana una CHUKI KALI baada ya kusoma hii makala. Nisemacho mimi nikua sisi wote ni watanzania hivyo ninachotaka ni kua tubishane kwa hoja na sio kuleta chuki. Ukiona mtu analeta chuki ujue hana pointi au kazidiwa hoja. Ni hilo tu kaka!

Mkuu sio wewe una chuki na Lowassa kiasi cha kufanya maneno ya Nyerere kua msahafu au biblia?

Jibu maswali bana, acha kukimbia
 
hawezi kujirekebisha! yule ni mchafu tu! alishaipaka nyeupe kuwa nyekundu kwa matendo yake! binafsi simtaki, simtaki ccm yeyote kuongoza tena nchi hii!

Yule ni mchafu tuu, hawezi kujirekebisha! As if unamjua zaidi ya kumsoma magazetini!

Khaaa "miafrika ndivyo tulivyo" - Nyani ngabu
 
Jibu basi angalau hili jepesi:

Je kama faili alilopewa Nyerere lilikua la chuki utajuaje? (remember Nyerere alikua hayupo kwenye system wakati huo). Alipataje data za ndani raia wa kawaida?. Tena alipewa wakati wa kinyang'anyiro
 
Mkuu sio wewe una chuki na Lowassa kiasi cha kufanya maneno ya Nyerere kua msahafu au biblia?

Jibu maswali bana, acha kukimbia
Siasa za JF bruudani sana kuna watu akisemwa Lowassa hat kama wapo offline chini ya bahari wataibuka kuja kufight back.Kuna wengine akisema Membe aah wataibuka mara moja,akisema lowassa wa membe wata like vice versa is true.Mkuu safi sana
 
POMPO,

Nashukuru mkuu. Pamoja sana. Nakuhakikishia mimi natumwa na UZALENDO. Mambo ya UVCCM hayanihusu.

Umeuliza ni kwanini JK aliweza kupita 2005 na ni vipi EL atashindwa kupita. Kama nilivyosema katika utangulizi wangu ni kua Nyerere alimkubali JK kwani hakuna na kashfa yoyote. Nyerere alimkataa EL kwakua alikua ananuka rushwa ingawa alikua bado kijana mdogo. NASISITIZA KAMATI KUU YA CCM 2015 haitakubali kumpitishwa EL.

Wale wote mnaoganga njaa gangeni jaa zenu lakini mjue kua at the end of the day EL atachinjiwa baharini. Habari ndio hiyo!

Huyo Nyerere alikuwa ni nani hasa hadi kila alichokisema tukiamini...
Kama alikuwa anajua Lowasa alikuwa ananuka rushwa kwa nini hakumpeleka kwenye vyombo vya sheria? Au kwa nini hakuwahi kutuambia rushwa au kashfa yoyote aliyofanya Lowasa kipindi hicho, kama haukuwa unafiki ni nini...!
 
Siasa za JF bruudani sana kuna watu akisemwa Lowassa hat kama wapo offline chini ya bahari wataibuka kuja kufight back.Kuna wengine akisema Membe aah wataibuka mara moja,akisema lowassa wa membe wata like vice versa is true.Mkuu safi sana
Kwani hao Lowassa na Membe unadhani hawamo humu?Wamekuwa nani wasiwemo?lol!

Wamo humu wamejaa tele,given the fact that they don't have to use their real names!
 
Huyo Nyerere alikuwa ni nani hasa hadi kila alichokisema tukiamini...
Kama alikuwa anajua Lowasa alikuwa ananuka rushwa kwa nini hakumpeleka kwenye vyombo vya sheria? Au kwa nini hakuwahi kutuambia rushwa au kashfa yoyote aliyofanya Lowasa kipindi hicho, kama haukuwa unafiki ni nini...!
Matatizo tuliyonayo Nyerere naye anahusika kwa kiasi kikubwa sana,waliokuwa na kashfa,hakuwachukulia hatua,bali aliwahamishia sehemu nyingine ambazo zilikuwa hazipendwi.Sasa sijui kwanini hakujiuliza kwamba why sehemu nyingine zilipendwa na nyingine hazikupendwa?Ukiangalia kwa undani,utagunduwa kuwa sehemu zilizochukiwa hazikuwa na ulaji.
 
Yule ni mchafu tuu, hawezi kujirekebisha! As if unamjua zaidi ya kumsoma magazetini!

Khaaa "miafrika ndivyo tulivyo" - Nyani ngabu
hata wewe nimekusoma hapa tu! ila nimeshakujua ulivyo, 'aogopwe yeyote anayeng'ang'ania ikulu, aogopwe kama ukoma'! RIP NYERERE, we r missing u!
 
JMUSHI1

Jamani nimeamini kweni NJAA MBAYA! Moshi na wenzako wengi hapa majuzi tu mlikua mnailaani CCM kwa kutomuenzi Mwalimu Nyerere na kudai Nyerere alikua ni mtu ambaye ana mapenzi mema kwa Taifa lake. Leo tunapozungumzia huyu ALIYECHAFUKA kwa kila hali ghafla mmebadilika na kumuona Mwalimu CHIZI! WALAI PESA SI MCHEZO. Nchii bado ina safari ndefu. Kumbe wapuuzi sio wazee wa vijijini tu wapo wengi tu!
 
FAIRPLAYER

Sasa naona unakaribia kunifanya nikuite mpuuzi wakati mimi sitaki kukuita hivyo. Hivi kuna mtu hapa TZ asiyejua kua Teddy ni MLA RUSHWA NUMERO UNO?? Nyerere alipewa file la Teddy na watu wa usalama but sio kwamba alipoingia kwenye kikao ndo aliegemea file hilo tu. Ujue licha ya Nyetrere kustaafu 1985 lakini alikua akifuatilia SANA siasa za TZ kuliko hata Viongozi. Ndo maana pale kilimanjaro 1995 alisema tunataka Rais asiyetumwa na mkewe maana ilionekana Mwinyi alikua kifuata sana maagizo ya Siti. Aidha, Katika kitabu chake alichowasema Malecela na Kolimba aliwaeleza mabaya yao 1992 licha ya kua alikua Musoma

Achana na nyerere
 
Hakuna jipya hapa. Just recycling old stories kwa kuzifanyia cosmetic changes ili zionekane kama ni mpya vile.

Nani asiyejua hayo yote uliyoandika? Unadhani Watanzania ni ignorant kiasi hicho?

Labda kwa vile Watanzania ni watu wa kuambiwa tuu utawakamata wengi tuu hapa.

Nyie wenyewe kama mna taarifa zote kuwa Lowassa ni fisadi mmefanya nini so far?

Kama Lowassa hafai kuwa rais basi ni kigezo kuwa aliyeko nyuma yako na unayejaaribu kumtetea anafaa?

Next time njoo na hoja kwa nini unayetetea anafaa kuwa rais, siyo kwa nini mpinzani wake hafai kuwa rais.

Acha kabisa kuwahadaa wananchi kwa kuwatumia kama toilet paper.
 
Back
Top Bottom