J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'

FAIRPLAYER

Sasa naona unakaribia kunifanya nikuite mpuuzi wakati mimi sitaki kukuita hivyo. Hivi kuna mtu hapa TZ asiyejua kua Teddy ni MLA RUSHWA NUMERO UNO?? Nyerere alipewa file la Teddy na watu wa usalama but sio kwamba alipoingia kwenye kikao ndo aliegemea file hilo tu. Ujue licha ya Nyetrere kustaafu 1985 lakini alikua akifuatilia SANA siasa za TZ kuliko hata Viongozi. Ndo maana pale kilimanjaro 1995 alisema tunataka Rais asiyetumwa na mkewe maana ilionekana Mwinyi alikua kifuata sana maagizo ya Siti. Aidha, Katika kitabu chake alichowasema Malecela na Kolimba aliwaeleza mabaya yao 1992 licha ya kua alikua Musoma

Achana na nyerere

Mimi najua WEWE SIO MPUUZI.

Nyerere raia kama wewe ilikuwaje USALAMA WA TAIFA umpelekee file la mtu?. Kaka/dada unaelewa maana ya usalama wa taifa?

Mkapa akitaka file kuhusu wewe usalama wanampelekea tu?. Ndivyo ujuavyo?.

Unaposema Lowassa ni mla rushwa nambari moja kila mtu anajua, hii inanikumbusha vijiwe vya kahawa kule Lindi. Kwani kuna asiyejua kuwa Nyerere alikua sahihi kila kitu na yet mkavunja Azimio la Arusha?

Kila mtu anasema kua RIZ1 ana mali kila kona ya nchi. Unaamini hilo kwa kua kila mtu anasema?

Sijauliza ya Kolimba na Malecela. Hapa ni Lowassa. Thibitisha kauli zako na acha kutumia FIKRA JUMUIYA.

Naamini bado sio mpuuzi wewe kuamini kila usikiacho.
 
Jamaa wanadai wewe ni Nape.

Mie siwaamini maana Mungu amenipa akili za kupembenua mambo. Akili toka kwa Mungu sio kutoka kwa baba wa Taifa Mwalimu JKN (RIP)
 
Siasa za JF bruudani sana kuna watu akisemwa Lowassa hat kama wapo offline chini ya bahari wataibuka kuja kufight back.Kuna wengine akisema Membe aah wataibuka mara moja,akisema lowassa wa membe wata like vice versa is true.Mkuu safi sana

Nokiatochi,

Kinachotukera ni kua watu wote wachafu lakini wanamnyoshea kidole mmoja wakati vinne vinaelekea kwao.

Iliandikwa aliye msafi aanze kurusha jiwe.

Afadhali Lowassa ana uthubutu kuliko hiyo mijizi mingine. Pia Kauli Jumuiya hatuzitaki hapa.

Hakuna asieweza kufikiri hapa. Eboo!
 
Hakuna jipya hapa. Just recycling old stories kwa kuzifanyia cosmetic changes ili zionekane kama ni mpya vile.

Nani asiyejua hayo yote uliyoandika? Unadhani Watanzania ni ignorant kiasi hicho?

Labda kwa vile Watanzania ni watu wa kuambiwa tuu utawakamata wengi tuu hapa.

Nyie wenyewe kama mna taarifa zote kuwa Lowassa ni fisadi mmefanya nini so far?

Kama Lowassa hafai kuwa rais basi ni kigezo kuwa aliyeko nyuma yako na unayejaaribu kumtetea anafaa?

Next time njoo na hoja kwa nini unayetetea anafaa kuwa rais, siyo kwa nini mpinzani wake hafai kuwa rais.

Acha kabisa kuwahadaa wananchi kwa kuwatumia kama toilet paper.

This bothers me a great deal, hawajagi na alternative hata siku moja, ni kuponda tuuuu.......
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kama kweli Lowassa amechafuka hivyo mnavyotaka tuamini mbona mapovu yanawatoka na kila kikucha ni kumponda?

Kama Lowassa hakubaliki kwanini msiwaachie wananchi waamue?.

Pigieni debe watu wenu, Tangazeni sera zenu.

Usiku kucha hamlali mnamuota Lowassa kisha mnasema hasafishiki.

Nashindwa kabisa kuelewa kwa nini hawawataji watu wao.Utaishia kuambiwa unalipwa na Lowasa.
 
Wakuu hawa wanaboa sana. Ndugu Kwame Nkurumah umenena vyema.

Mie nawaambiaga watatawaliwa milele hii mijitu. Hawana mpya kila siku Lowassa kafanya hivi mara Lowassa kaonekana akinywa chai. Inaboa.

It is time njooni mtueleze kwanini Samwel Sitta anafaa. Mwakyembe juzi kazindua treni... Mpigieni debe.

Mnavyozidi kulia lia na Lowassa mnamfanya maarufu enyi kizazi kisichoweza kufikiria!!
 
Mimi najua WEWE SIO MPUUZI.

Nyerere raia kama wewe ilikuwaje USALAMA WA TAIFA umpelekee file la mtu?. Kaka/dada unaelewa maana ya usalama wa taifa?

Mkapa akitaka file kuhusu wewe usalama wanampelekea tu?. Ndivyo ujuavyo?.

Unaposema Lowassa ni mla rushwa nambari moja kila mtu anajua, hii inanikumbusha vijiwe vya kahawa kule Lindi. Kwani kuna asiyejua kuwa Nyerere alikua sahihi kila kitu na yet mkavunja Azimio la Arusha?

Kila mtu anasema kua RIZ1 ana mali kila kona ya nchi. Unaamini hilo kwa kua kila mtu anasema?

Sijauliza ya Kolimba na Malecela. Hapa ni Lowassa. Thibitisha kauli zako na acha kutumia FIKRA JUMUIYA.

Naamini bado sio mpuuzi wewe kuamini kila usikiacho.
Fair Player,
Nyerere hakuwa raia wa kawaida. As a founding father and the first president he was entitled to intelligence briefing.
As far as I know former presidents are entitled to intelligence briefings.
 
Nokiatochi,

Kinachotukera ni kua watu wote wachafu lakini wanamnyoshea kidole mmoja wakati vinne vinaelekea kwao.

Iliandikwa aliye msafi aanze kurusha jiwe.

Afadhali Lowassa ana uthubutu kuliko hiyo mijizi mingine. Pia Kauli Jumuiya hatuzitaki hapa.

Hakuna asieweza kufikiri hapa. Eboo!

Watu wanapenda sana kutuchukulia for granted. Utafikiri Lowassa ndiye fisadi pekee humu nchini.

Wanaenda kuokota takataka zilizooza kwenye mashimo wanazileta hapa eti tuzijadili without any context.

Hivi Nyerere ndiye aliyekuwa na authority pekee ya kutupangia nani awe rais?

Kama ni hvyo then mbona Kikwete ni rais pamoja na kwamba Nyerere alimkataa?

Watasema nini tena kama Lowassa nae akiwa rais?
 
Fair Player,
Nyerere hakuwa raia wa kawaida. As a founding father and the first president he was entitled to intelligence briefing.
As far as I know former presidents are entitled to intelligence briefings.

Jasusi,

UWT wanawajibika kwa Rais wa jamhuri wa Muungano.

Mleta mada hayuko informed, ametumwa kuji register leo na kutuambia tunayojua.

Nilimuuliza ataje mmoja alie msafi CCM na pia atuambie kwanini hajamshambulia mwingine zaidi ya Lowassa. Why Lowassa?

Wanaanza kumtangaza bila wao kujua.

JKN (Rip) alimchagua Mkapa. Mr Clean. Je ilikua chaguo sahihi?. Nyerere yupo sahihi kila wakati? Jibu ni hapana coz ni binadamu.

It is time wawapigie wagombea wao debe.

Mbona CDM wanampigia debe Dr Slaa?.

Hawa vibaraka wanachosha mkuu.
 
labda nione kuwa kumjadili na kumtabiria mtu uraisi ni kazi ya watabiri,manabii na hata waganga wa ramli.
EL au SAM 6 au Dr.WS au ZZK au JAN KAMBA ni wanadamu tena waja wa Mwenyezi Mungu tu.Unapoumiza misuli kusema lazima EL achukue nchi ina maana umeshajihakikishia ataishi wakati uhakika wa wewe binafsi kuiona kesho haupo?
Suala ni kuwa na mfumo ambapo Rais hawezi kuwa juu ya sheria ili akileta ufisadiu tuweze kum BERLUSCONNI kama Waitaliano walivyofanya.
 
EL at work! Anyway unadhani kwanini tunamwita J.k. Nyerere baba wa taifa? Unadhani kwanini nyerere aliwakataa Samwel, Edward na Jakaya 1995 na kumpitisha benjamini na cc pamoja na nec zote zikaafiki bila kupinga.

Unadhani kwanini baada ya jkn kumkataa Edward ilifikia edward akatuma ujumbe kwa jkn ili asafishwe bila mafanikio? Unaamini kwamba jkn bado alikua na nguvu za maamuz CCM?
 
VIJANA WENZANGU MMENIANGUSHA BIG TIME!!

Mimi nikiwa Mzalendo wa nchi yangu niliteta mada hii baada ya kuambiwa na wenzangu kua humu kuna GREAT THINKERS..NASIKITIKA nilichoshuhudia humu ni tofauti kabisa na nilivyotegemea. Mimi nilieleza ni kwanini nadhani LOWASA HAFAI KABISA kua RASI wa nchi yangu niipendayo ya Tanzania. Sasa nilitegemea kwamba wale wote ambao wanaona anafaa basi wangejikita kueleza mazuri ya Lowasa ili baadae tuchambue kama pamoja na mabaya niliyoyataja lakini mambo mengine ya Lowasa ni mazuri.

Mimi sina kambi wala mtu yoyote ninayemuunga mkono. Nina uelewa na yale yaliyofanyika katika vikao vya CCM, NEC na Mkutano Mkuu maana kuna mmoja wa Vigogo ambae alihudhuria vikao vya 1995 na vya 2005 ingawa kwasasa hayumo tena. Mi naona ni vizuri kila mgombea anayetajwa kuutaka Urais basi AJADILIWE KWA MAPANA NA MAREFU ili hatimaye TUMPATE KIONGOZI BORA AJUAE MATATIZO YETU NA AMBAYE ANA UWEZO WA KUYATATUA NA SI YULE AMBAE NAPELEKA TUMBO LAKE MBELE.

Iwapo topic itamuhusu MIGIRO AU MEMBE AU SITA AU NCHIMBI AU MWAKYEMBE BASI WOTE TUJADILI UZURI NA UBAYA WA MTU HUYO BILA KUTAJA WENGINE .

TUSIKUBALI KUBURURWA NA WENYE MAKUNDI. NCHI HII INA WATU 45 000 000. JE HAKUNA WENGINE WANAOFAA ZAIDI YA HAWA TUNAOWASIKIA??? MAWAZIRI AU MABALOZI HAWAPO KWELI? KWELI? MKAPA ALIKUA HAJULIKANI 1995 LAKINI NDIYE ALIYEPATA..DID WE LEARN ANYTHING FROM THAT EXPERIENCE???

Mimi nina rafiki zangu kazini ambao wanampenda kwa dhati Lowasa na wanaamini ye ndio atawatia adabu waislamu, uamsho na wenye ukabila. Wao hawajalipwa chochote na wanachoongea kinatoka moyoni mwao na naheshimu mawazo yao. KINACHONIBOA NI MTU KUTUMIWA ILI AWE PUNDA WA KUMUINGIZA MWINGINE IKULU BAADA YA KUPEWA CHENJI!
 
Hii ni story ya kuuuunda unda sababu ya woga kwa mtu shupavu,mchapakazi,mkuulima,mfugaji,mwanasiasa,mjengahoja,mfanyabiashara na mwanadiplomasia, 1995 mwl alitua Dodoma na kuwaita MH, kawawa na MH Mwinyi, na kuwaambia hataki kuona jina la Malecela na Kolimba. na wala si EL.

kama ilivyoada MWL alikuwa na mgombea wake ambaye ni MH Mkapa lkn hakuwa maarufu hivyo MWL , ilibidi afanye kazi ya ziada kumuinua BEN, hivyo alikuwa akipangua vizuizi vyote.

Alipofika kwa EL kwani naye alikuwa na anayo nguvu mpaka leo hii, hakuwa na shida naye yoyote lkn ni kizuizi kwa mgombea wake ikabidi aseme huyu kijana ni tajiri saana[ MWL si muumuni wa utajiri, enzi zake za Azimio la Arusha zimepitwa viongozi kutojilimbikizia mali, kutokuwa na hisa ktk makampuni haziko teeeena ] hivyo muunda story atofautishe nyakati.

Baada ya EL kuenguliwa kampeni zake akaziamishia kwa JK kutokana na nguvu aliyonayo ktk kura round ya kwanza JK aliongoza akifuatiwa na BEN mwisho Msuya .

Ndipo mzee MWl alipoinuka na kusema JK hajavuka nusu ya kura , hivyo ikabidi BEN na JK warudie kura ndipo ktk kampeni MWl akamuelekeza BEN aseme kuwa atamteua DR OMARY ALLY JUMA kuwa mgombea mwenza akafanikiwa kushinda kwa kura za ZANZIBAR , muunda story usimlishe maneno MWL ambayo hakuyasema kwa woga wako na kutaka kuwatisha watu wengine hapo hajaonesha nia mnampima na wagombea wenu mnaweweseka , huyo anakuja.
 
kwa jinsi tu ulivyo elezea inaonekana wazi umetoswa UVccm,na ni wazi wewe ulikuwa mfuasi wa manywele,msalimie mama Regina Lowassa.:target:
 
naona una mawazo ya kitajiri sana wewe! maana walikuwepo wazalendo wakina nyerere na bado nchi ikawa masikini ......
 
VIJANA WENZANGU MMENIANGUSHA BIG TIME!!

Mimi nikiwa Mzalendo wa nchi yangu niliteta mada hii baada ya kuambiwa na wenzangu kua humu kuna GREAT THINKERS..NASIKITIKA nilichoshuhudia humu ni tofauti kabisa na nilivyotegemea. Mimi nilieleza ni kwanini nadhani LOWASA HAFAI KABISA kua RASI wa nchi yangu niipendayo ya Tanzania. Sasa nilitegemea kwamba wale wote ambao wanaona anafaa basi wangejikita kueleza mazuri ya Lowasa ili baadae tuchambue kama pamoja na mabaya niliyoyataja lakini mambo mengine ya Lowasa ni mazuri.

Mimi sina kambi wala mtu yoyote ninayemuunga mkono. Nina uelewa na yale yaliyofanyika katika vikao vya CCM, NEC na Mkutano Mkuu maana kuna mmoja wa Vigogo ambae alihudhuria vikao vya 1995 na vya 2005 ingawa kwasasa hayumo tena. Mi naona ni vizuri kila mgombea anayetajwa kuutaka Urais basi AJADILIWE KWA MAPANA NA MAREFU ili hatimaye TUMPATE KIONGOZI BORA AJUAE MATATIZO YETU NA AMBAYE ANA UWEZO WA KUYATATUA NA SI YULE AMBAE NAPELEKA TUMBO LAKE MBELE.

Iwapo topic itamuhusu MIGIRO AU MEMBE AU SITA AU NCHIMBI AU MWAKYEMBE BASI WOTE TUJADILI UZURI NA UBAYA WA MTU HUYO BILA KUTAJA WENGINE .

TUSIKUBALI KUBURURWA NA WENYE MAKUNDI. NCHI HII INA WATU 45 000 000. JE HAKUNA WENGINE WANAOFAA ZAIDI YA HAWA TUNAOWASIKIA??? MAWAZIRI AU MABALOZI HAWAPO KWELI? KWELI? MKAPA ALIKUA HAJULIKANI 1995 LAKINI NDIYE ALIYEPATA..DID WE LEARN ANYTHING FROM THAT EXPERIENCE???

Mimi nina rafiki zangu kazini ambao wanampenda kwa dhati Lowasa na wanaamini ye ndio atawatia adabu waislamu, uamsho na wenye ukabila. Wao hawajalipwa chochote na wanachoongea kinatoka moyoni mwao na naheshimu mawazo yao. KINACHONIBOA NI MTU KUTUMIWA ILI AWE PUNDA WA KUMUINGIZA MWINGINE IKULU BAADA YA KUPEWA CHENJI!

Acha unafiki na kutuzuga hapa. Hakuna mzalendo nchi hii. Kungekuwa na wazalendo nchi isingeliwa kihivi. Mpaka wafagiaji wamekuwa mafisadi ndiyo sembuse Lowassa? Pia usidhani wote hapa ni vijana. Kuna vibabu humu pia. So, heshima mbele tafadhali.

Yes, humu kuna great thinkers. Lakini kwa taarifa yako, kama ulikuwa hujui, great thinkers huwa wanajadili hoja, siyo watu. Great thinkers huwa wana-argue objectively, siyo subjectively. Great thinkers use their brains and analyse issues critically, siyo kuokota habari za zamani na kuziweka hapa.

Great thinkers provide solutions to the issues being addressed, siyo kama wewe uliyesema Lowasa hafai bila kutoa alternative. Kama Lowassa hafai unampendekeza nani then and why? Great thinkers hawaandiki kwa hasira kama wewe inavyoandika kwa herufi kubwa. Calm down.

Unasema eti wewe huna kambi wala mtu yoyote unayemuunga mkono. Unatuchukulia for granted kuwa sisi tuna kambi na tunamuunga mkono Lowassa simply because tunapinga your recycled thread?

Unasema eti una uelewa na yale yaliyofanyika katika vikao vya CCM, NEC na Mkutano Mkuu. Hivi ni Mtanzania gani ambaye hayajui hayo? Kwa nini mnapenda kuwadharau Watanzania kiasi hiki? Yaani bado unadhani tuko dunia ya 47 ambapo mnaweza ku-hold information na kuzi-release pale mnapojisikia?

Kwako umeona umetoa inside information ya maana, kumbe ume-recycle tuu. Tena hata hiyo recycling uliyofanya ni hearsay maana unadai "kuna mmoja wa Vigogo ambae alihudhuria vikao vya 1995 na vya 2005." Ndiyo maana kwenye thread yako umeweka quotations za Nyerere ambazo hata hakuzisema kwenye hiyo mikutano. Watu watakuletea minutes zote za vile vikao hapa utashangaa na roho yako.

We don't believe on hearsay hapa. Kajipange upya.
 
EMT unaongoza KWA PUMBA. kiukweli kabisa kwa namna hii TZ ITAENDELEA KUJENGWA NA WENYE NCHI NA KULIWA NA WENYE MENO NA MITUMBO MIKUBWA. I REST MY CASE
 
Galilaya(kada) umetulia na umeweza kuchota mawazo ya watu wote tujadili majina ya wana ccm, kitu ambacho Mwalimu alikikataa...ccm hakuna msafi:Sofia Simba(waziri officini kwa RAIS) hakuna aliyekana/kubisha, ndiyo tusemeje hakuna afaaye ktk hiki chama? (acheni wafu wazikane?)...purukushani za el (el vs membe) ni mbinu zile zile (sumaye vs jk) yaani kura za huruma/kishindo...2015 haijalishi ccm atapita nani, yatakuwa ni mpambano ya vijana wa ktz wanaotumiwa (waiba kura/vyombo vya dola) dhidi ya vijana wazalendo... Hoja yangu kujadili majina ni KUTUPOFUSHA..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom