ITV yaanika kila kitu na ushahidi wa kutosha kuhusu mauaji ya mwandishi huko Iringa

Mkuu Shark, huyu amaa ni mwanachama na mfuasi wa CDM, fuatilia kauli zake hivyo uandishi ilikuwa cover tu.

Hivi ukiwa mwanachama wa chama cha upinzani ndo uuwawe kama mnyama? Jana nilishangaa kusikia kamanda Kova akimjibu mwandishi mmoja kwa simu akisema yawezekana wewe siyo mwandishi labda wewe ni mwanachama wa CHADEMA. najiuliza, hivi mwanachama wa CHADEMA hastahili kupata habari au taarifa?
 
Kwa hiyo yule mwandishi alikua wa Chama kisichotii sheria za nchi??

Achana nae huyo mpumbavu anafikiri kwa kutumia makalio. Sheria za nchi ziko wazi kuwa kila chama cha siasa kina haki ya kufanya mikutano yake baada ya kutoa taarifa polisi na polisi sio wao wanaotoa kibali bali wao wanapaswa tu kutoa ulinzi.

Inashangaza polisi wao huwa wanawakuta watu wakiwa na amani ya kutosha isipokuwa wao ndio huwa wanaanzisha vurugu alafu wapumbavu kama huyo anakurupuka kishoga shoga huku hafahamu hata sheria ya vyama vya siasa zinasemaje.

Kisa kahongwa mlo mmoja na tisheti ya rangi ya kijani au njano tu unauza nchi.

Ni aibu sana.
 
Ndugu watanzania mapak lini tutanyanyaswa namna hii na utawala wa kidhalimu wa CCM. Je watanzania tumekosa thamani kiasi hichi, angalia RPC wa Iringa anavyohusika moja kwa moja katika mauaji haya ya Iringa.

Hiki ni kisa cha kawaida kwa polisi wa Tanzania katika ukiukaji wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na ubabe wa utawala wa kimabavu wa Tanzania ulivyotokea 2 Septemba, kwa kushambuliwa, kuteswa na kuuawa kwa mwandishi wa habari kama inavyoonekana.Haya yalishuhudiwa na mamia ya wanakijiji ambao machozi yaliwatoka baada ya mwandishi huyu kuuwa kwa unyama huu wa kutisha kwa bahati nzuri na msaada wa teknolojia dunia inashuhudia ukandamizaji huu wa serikali dhalimu ya CCM chini ya utawala wa Jakaya Kikwete. Damu hizi za watanzania hazitaishia hivi lazima wananchi wote tuungane na ifikapo 2015 CCM iwe historia na tuanze kujenga upya nchi yetu....Kinachouma zaidi na kuumiza roho ni pale polisi wanavyobeza unyama kwa kusema hawausiki, ingekuwa nchi zinajoli utawala wa sheria wairi wa mambo ya ndani angechukuwa jukumu la kujiuzulu pamoja na Said Mwema. Kwao wao unyama wa polisi ndiyo kulinda maslahi ya CCM ya Mafisadi. Si hilo tu ndiyo linaumiza roho bali pia unaposikia mtu aliyegawiwa madaraka kama January Makamba akisema CHADEMA ndiyo wamemuua mwandishi wakati ushahidi unaonekana wazi kwa polisi wakimwuua mwandishi huyu. Ulevi huu wa madaraka na kuukomesha kabisa kwa kuondoa hichi CHAMA CHA MAAUAJI (CCM)


Dunia nzima inatakiwa kutambua unyama huu

TANZANIAN POLICEMEN BRUTALITY TO A LOCAL JOURNALIST - CNN iReport
 
Kimsingi vyombo vya habari vinapaswa kuwa huru na wazi katika kazi yao sasa hawa TBC vp? Tido alikuwa mzalendo.
 
Bonyeza kusikiliza Mahojiano na Dw redio
AUDIO | DW.DE
Majeruhi%2Bpolisi%2Bna%2Bmarehemu.JPG

1346667662.jpg

Mwandishi Daudi Mwangosi auliwa kikadili na Jeshi la Polisi


Uongozi wa Africa Media, ambao ni wamiliki wa kituo cha televisheni "Channel 10" Tanzania umelaani vikali mauwaji ya mwandishi wake Daudi Mwangosi.
0,,1737246_4,00.jpg
Purukushani za polisi na chama cha upinzani Chadema

Mwangosi aliuwawa kutokana na mripuko wa bomu wakati wa purukushani za polisi na wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo CHADEMA zlizotokea katika ufunguzi wa matawi wa chama huko huko Mkoani Iringa. Kutoka Dar es salaam Sudi Mnette alizungumza na Mhariri Mkuu wa Habari, kituo cha Channel 10, Dina Chahali na kwanza alimuuliza kama mratibu wa habari, kifo cha mwandishi Mwangosi kimetokana na nini kwa ufahamu wake.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi:Sudi Mnette
Mhariri: Saumu Yusuf
 
sasa na wewe mbona umechelewa hivyoooooo? hii habari ina siku 2 hapa wewe ndio unaianzisha sasa?
 
Inasikitisha sana; tena mno. Ila naona kwenye hiyo video CNN wameweka lebo "NOT VETTED BY CNN". Kiingereza kidogo kimepinda; 2TH SEPT, ... FEW PEOPLE MANAGED TO CAPTURE AND RECORDING THE WHOLE ..., n.k. All in all, ukweli ni kwamba tukio limetokea na watuhumiwa namba moja ni waliopaswa kuwa walinzi wa uhai. Habari yenyewe hiyo hapo chini.


THIS IS A SHOCKING STORY,ABUSE OF HUMAN RIGHTS,FREEDOM OF SPEECH AND AN ACT OF AUTHORITARIAN REGIME IN TANZANIA.
ON 2TH SEPTEMBER,ARMED POLICEMEN ATTACKED A JOURNALIST,TORTURED AND KILLED HIM ON SPOT.THIS ACT WAS WITNESSED BY HUNDREDS OF VILLAGERS AND CITIZENS WHOSE TEARS CAME DOWN AS THEY WITNESSED AN INNOCENT MAN AT WORK BEING KILLED VIOLENTLY. FORTUNATELY WITH THE SUPPORT OF TECHNOLOGY,FEW PEOPLE MANAGED TO CAPTURE AND RECORDING THE WHOLE DEVASTATING ACTIONS.
FOR MANY YEARS,THE GOVERNMENT OF TANZANIA THROUGH ITS POLICE HAS VIOLATED HUMAN RIGHTS OF CITIZENS PARTICULARLY JOURNALISTS WHO FOR YEARS HAVE BEEN DENIED OF FREEDOM OF SPEECH,THREATS AND EVEN DEATHS ATTEMPTS TO SOME JOURNALISTS (THERE IS EVIDENCE)
INTERNATIONAL MEDIAS AND INSTITUTIONS HAVE NOT BEEN LUCK ENOUGH TO UNDERSTAND HOW THE BUREAUCRATIC STATE FUNCTIONS TO AVOID ITS SCANDAL.
 
hao mashahidi wamepandikizwa, na unaposema alipigwa bomu kwa nyuma utumbo ukatoka na akakatika vipande vipande,hilo ni bomu gani,la machozi au rpg. Mimi nashaka sana na hao mashahidi wako, lazima watakua wametumwa kudanganya umma. Sisi tunasubiri uchunguzi ufanyike kwanza.

kesho ni wewe maana huishi na marafiki tu unao maadui ambao ni opposite na mtazamo wako wa sasa.
 
Ubungoubungo Hivi kwa mahakama hizi zetu na serekali hii kuna haki itatendeka?
hakuna haki itatendeka hapo aisee, ndio maana tunasema icc statute inatakiwa iwe domesticated ili yale makosa yaliyoko mle yawepo kwenye penal code, na kama selikali haitafanya juhudi kuwafikisha mahakamani, basi n i rahisi kwa icc kuingilia kati....sheria na mahakama za tz ni usanii tu...sisi wengine wanasheria tunajua kinachoendelea huko mahakamani hasa serikali ikiwa na interest.
 
Wale waandishi mashahidi wasipo angalia nao watapotelea "mwebepande" maana wanaushahidi wakutosha
 
Mtu mmoja asiyekuwa na silaha kwa askari polisi NANE, haihitaji akili za ziada kufikiria. Mnaosema ni kosa la CDM kukaidi kufanya mkutano, je huyu mwandishi anahusikaje mpaka auwawe wakati yeye alikuwa anachukua habari. Kama mwandishi alikuwa na kosa lolote askari mmoja (maximum wawili) walikuwa wanatosha kumkamata na kumfunga pingu na kumfikisha polisi kwa mahojiano. Watanzania wenzangu tuwe na UTU hivi mtu anauwawa kinyama hivi unasema ni CDM??!! Wewe unayesema ni CDM pia wewe ni muuaji kwa sababu mtu mwenye akili TIMAMU, kwa kilichotokea na picha zinavyoonyesha hawezi kusema unyoyasema. TUBADILIKE, NA SIDHANI MAUAJI NI NJIA MUAFAKA ZAIDI INAONGEZA CHUKI.
 
sijui watasema ni chadema tena!!!! kazi ya police ni nin?? kuua wananchi au kuwalinda wananchi?? kweli kazi tunayo!!!
 
Hii ni dharau kubwa sana iliyooneshwa na jeshi la polisi nchini. Bila shaka Mkulu atalikemea hili. Nini wasiwasi hapa wahisika wa tukio hili wataenda na maji, ngoja arudi.
 
...mkuu hii tume uchwara inayoongozwa na mwema kamwe haitawaita hao jamaa wawili watoe ushahidi na si ajabu wanaweza kabisa kunyamazishwa ili kuficha ukweli wa kile kilichojiri katika mauaji ya mwangosi.

kwani ile tume inayoshugulikia sakata la ulimboka ilishafunguka?
 
My sources are telling me mitaani kuna vijana wasomi kabisa wanaotumiwa na CCM, bado wanabisha kwenye hili!!

Naelewa kwa nini, si wanfaidika na mfumo huu!!!
 
Back
Top Bottom