Upi msimamo wa Serikali kuhusu mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel huko Gaza

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri.

Nchi yetu ina mahusiano ya kibalozi na Israel na Palestina pia. Je ni upi msimamo wa serikali kuhusu mauaji haya ya watu wasiokuwa na hatia wakiwemo wanawake, watoto, wanaume na waandishi wa habari yanayoendelea kila siku huko Gaza.

Na je mbona BAKWATA wapo kimya kabisa kana kwamba hakuna masaibu yanayowapata waislamu wenzao huko Gaza?

Wenzetu Afrika ya kusini wameshajipambanua kwa kupinga mauaji hayo kwa kupeleka kesi ICJ kutaka Israel ichukuliwe hatua kwa mauaji inayofanya kwa raia huko Gaza. Mbona sisi tupo kimya?
 
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri...
Wewe kwako kila siku umeme unakatika,sukari imepanda bei na vitu vingine,unashindwa kuwaonea huruma Watanzania unasumbukia Waisrael na Wapalestina ambao hata siku moja hamtakula ugali pamoja.
 
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri. Nchi yetu ina mahusiano...
Israel wana haki ya kujilinda dhidi ya magaidi wa Hamas walioanzisha hayo mauaji na utekaji wa raia wasio na hatia. Wanachofanya sasa ni kusafisha maficho ya magaidi. Tulia
 
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri....
Jamani nimeangalia ramani yote ya Dunia bara na visiwa vyake sijaona taifa la "Islaeri".
 
Mbona mmetuambia wanajeshi wa Israel wanapigwa na Hamas na vifaru vyao vinateketezwa helicopter za Israel zinarudisha maiti ya wanajeshi za wanajeshi wa Israel sasahivi mbona mnalalamika mauaji ya halaiki kwa wapalestina tena?
 
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri...
Kwani aliyeanzisha mauaji ni nani? October 7 Hamas waliwavamia Waisraeli na kuuawa watu 1,200 na wakasherehekea kwa kuimba Allahu Akbar, Allahu Akbar, hivi walitegemea Nini? Nchi za Kiarabu walikaa na kujadili Cha kufanya, mmoja wao alitoa maoni kwa kutulia swali, "ikitokea Taiwan ikaivamia China, litakuwa ni wazo la busara, ikiwa matokeo ya kitendo hicho yanajulikana ni kama kijinyonga?

Hamas kuivamia Israel tarehe 7 huku walisherehekea kwa Allahu Akbar, Allahu Akbar, walikuwa wanajua matokeo yake ni Nini. Kwani wao mauaji ya watu 1,200 siyo KIMBARI? au KIMBARI inaanzia watu wangapi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Maelfu ya wapalestina wengi wao wakiwa waislam na waandishi wa habari wameuawa na wanaendelea kuawa kila siku huko Gaza na majeshi ya Islaeri...
Nchi Yetu haifungamani na upande wowote kwenye mzozo huu huko mashariki ya kati na kwingineko duniani...

Wito wa Serikali ya Tanzania siku zote umekua wazi kwamba pande zote mbili zinazozozana kuketi chini meza moja kutafuta suluhu ya mazungumzo na kuridhiana namna bora ya kutatua mzozo baina yao.....
 
Wapi watakua na time na waislamu, viongozi hawa hawa tulionao wanasherehekea kupata uhuru wa kumwaga damu za waislamu!! Tena wanasema ni "Mapinduzi Matakatifu"!!

Hii dunia tunapita tu.
 
Sasa sisi hayo mapigano yao yanatuhusu nini? Waache waendelee na mishe zao. Sisi tuna mgao wa umeme huku tunakimbizana nao.

Hao masela wengine wana enjoy kupigana na hawataacha mpaka mwisho wa dunia. Alafu acha kiherehere cha kuweka udini eti BAKWATA....sasa wanaingiaje hapo?

Usipende kuingilia vitu ambazo hazikuhusu. Pambana na mamigao yenu ya umeme na matozo!
 
Back
Top Bottom