ITV yaanika kila kitu na ushahidi wa kutosha kuhusu mauaji ya mwandishi huko Iringa

Mkuu kauli zake huyu mwandishi ndio zinafahamika, huyu ni mwanachama mtiifu wa CDM na hilo linafahamika. Kwa hiyo uandishi ilikuwa just cover tu.

Poor reasoning capacity!! Hivi kuwa mwanachama wa CDM au chama kingine cha upinzani ni uhaini Hapa Tanzania? Ni nani aliyewapa polisi leseni ya kuua raia badala ya kuwalinda?? Mie nafikiri pamoja na mitizamo yetu tofauti kwa hili ni lazima tujue kwamba uhai wa binadamu umeondolewa kimakosa na hili jambi ni irrevesible!
 
Polisi na risasi, mabomu huku wanachama wanafungua matawi kuna tatizo gani au kwa kuwa unajua kusoma na kuandika ndo unaadika kama akili yako inavyo kutuma! jichunguze yaonekana we nimiongoni mwa wauwaji
 
Walianza na wapemba, wakaja migodini, Arusha, Mwanza, Songea, Morogoro na Leo Iringa kwa Daudi Mwangosi, Kesho ..................!?

Inawezekana kabisa ikawa kwangu au kwako! Fanya kitu kuzuia hii hali. Maana hapa ndipo tulipofikia. Vunja ukimya sema na MTANZANIA mwenzako!
 
nashindwa kuelewa nini umuhimu wa hii tume ya uchunguzi ... na kazi zake kwaajili ya nani,
maana tukio lipo waaazi kabisa na haliitaji uchunguzi wa muda mrefu saaana, maana ushahidi upo kwa baadhi ya watu.

pengine ikihitajika kupindisha ukweli inahitajika kuwa na jopo la watu wenye uwezo wa kutoa taarifa(kisheria) isiyoweza kupingwa.... pia yenye kutoa mapendekezo yatakayohitaji utekelezaji.
Swali ... kwa nini mauaji mengine yasiundiwe tume/ kamati.

Tusubiri taarifa yao(TUME) ....lakini kwa kuwa jambo hili bado halijafika mahakamani yaani lipo katika uchuguzi.. nilitegemea baadhi ya Watuhumiwa watakuwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi... (Conflct of Interest)
 
Leo imekuwa kijana, mwandishi asiye na hatia Daudi Mwangosi. Una hakika gani kwamba kesho haiwezi kuwa MIMI au WEWE? Umma unashinda. Hofu yao kuu ni kuamka kwa Watanzania. Mauaji ya raia wasio na hatia ni hofu ya wazi wazi! Tuungane, tusimame, tusitetereke, tunakaribia ukombozi!
 
shauri hili halina hadhi ya kwenda the hague, kosa hili halijadondokea kwenye any of the four crimes under the icc statute...can you say this is a widespread and systematic attack against civilian population within the meaning of the icc statute? ili tuseme hii ni crime against humanity? bado haijafikia hadhi hiyo, halafu hata hivyo, bado nchi yetu inayo room kupelekea watu mahakamani kwa at least mwaka mmoja ndio reasonable before the icc gets in...kuna principle kweney article 17 of the icc statute inaeleza principel ya complimentarity, na kama watu watapelekwa mahakamani kwa nia ya kuwashield tu au kama selikali itakuwa serious etc...kwa hili, hawa wataangukia kwenye mahakama zetu hizihizi tu bro.
Ubungoubungo Hivi kwa mahakama hizi zetu na serekali hii kuna haki itatendeka?
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu ukikutana nao wakiwa katika mavazi yao, unadhani ni binadamu waliokamilika, mpaka wanapoandika au kuongea, ndiyo tunapata uelewa kuwa punguani katika nchi hii ni wengi kuliko tunavyodhania. Aheri wajinga wanaweza kuelemishwa, lakini punguani wa namna hii wanaweza kusaidiwa kwa namna gani maana ni kweli kuwa upungufu huu hawakujitakia ila ndivyo walivyo.

Hao mashahidi wamepandikizwa, na unaposema alipigwa bomu kwa nyuma utumbo ukatoka na akakatika vipande vipande,hilo ni bomu gani,la machozi au RPG. Mimi nashaka sana na hao mashahidi wako, lazima watakua wametumwa kudanganya umma. Sisi tunasubiri uchunguzi ufanyike kwanza.
 
Leo imekuwa kijana, mwandishi asiye na hatia Daudi Mwangosi. Una hakika gani kwamba kesho haiwezi kuwa MIMI au WEWE? Umma unashinda. Hofu yao kuu ni kuamka kwa Watanzania. Mauaji ya raia wasio na hatia ni hofu ya wazi wazi! Tuungane, tusimame, tusitetereke, tunakaribia ukombozi!
Acheni kutumika kwenye siasa, unaambiwa fanya fujo wakati ane kwambia ufanye fujo anapanda gari na kuondoka, unabaki wewe unakula kisago.
 
kuna mashahidi wawili ambao ni waandishi wa habari waliokuwa na marehemu MWANGOSI (JANA- KATIKA UVUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA-IRINGA, MUFINDI) wakati anakamatwa na mapolisi shahidi walikuwa wanaelezea tukio zima itv news usiku huu (sa 2 ) wa kwanza anasema
"marehemu alikamatwa na mapolisi 8, wakampiga sana na marungu kwa mda mrefu kila upande wa mwili wake, akatokea polisi wa nyota tatu akawasihi hao polisi 8 wamwachie marehemu lakini haikufaa kitu akatokea polisi mmoja akaja kwa nyuma ya yule aliyekuwa akiwazuia wasiendelee kumpiga marehe akamfyatulia risasi marehemu na kumtawanya utumbo na bomu hilo likamvunja mguu hata huyo polisi aliyekuwa akiwazuia wasimuue.

Shahidi wa pili anasema
Yeye (huyo shahidi-ambaye pia ni mwandishi wa habari)alipoona marehemu anapigwa alikimbilia kutoa taarifa kwa mkuu wa mapolisi waliokuwa katika eneo hilo la tukio huyo mkuu wao alikuwa katika gari akiwa kafunga viooo huyo shuhuda ambaye naye ni mwandishi alipofika hapo akagonga kioo cha gari ili huyo afisa wa polisi afungue, alipofungua huyo mwandishi akamweleza tafadhali naomba msaada wako mkuu yule anayepigwa pale ni mwandishi wa habari, tafadhali naomba msaaada wako huyo afisa hakumsikiliza akarock kiooo.

Ndio maaana nawahuliza hao (Majebere, mwiba na wengineo) wapenda uozo na mauaji ya polisi wameyasikia haya (Ushahidi toka kwa watu wailiokuwa eneo la tukio)? na kuangalia tv... maana wao sijui wanamioyo gani hawa watu ni zaidi ya wanyama kila wakati wao ni kuwatetea polisi hata uweke ushahidi wazi kiasi gani.

Imeniuma sana wakuu SORRY KWA ALIYEKWAZIKA JINSI NILIVYOLIPOTI NI HASIRA JUU YA HAO WATU

Haya maelezo yanashabihiana na taswira hii

Tanzanian%2BJournalist.jpg
 
Ili kupata impact ya kutosha susieni shughuli zote za wizara ya mambo ya ndani (kama mlivyomfanya Mapuri enzi zile) au hata za serekali nzima.

Na ndivyo inavyotakiwa na sio wizara hii serekali nzima kabisa !
 
Hawa waandishi inatakiwa wawe na msimamo wao wenyewe. Wasiwe kama kina Ulimboka.

Ulitaka Ulimboka afanyeje? vipi familia yake? unaifikiriaje? ulitaka aseme nini? kwanini wewe kama unaujua ukweli husemi kwa niaba yake?

NA hawa CHADEMA , ndio nimeamini walivosema watahakikisha nchi haitawaliki! wao ndio waanzilishi wa haya mauaji! na mwisho wanaonekana police,! sheria za nchi zipo kwanini wanazivunja? je wangetii haya yote yangekuwepo? kweli hiki CHAMA CHA WENZAWAZIMU MADISCO JOKA , WAZINIFU NA HAKIFAI HATA KUONGOZA MTAA!
 
ITV imetoa habari iliyokamilika kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari, waandishi wa habari walioshuhudia tukio hilo wameeleza bayana tukio hilo kwa kubainisha chazo cha mauaji hayo, na huku wakitoa ushahidi kuhusu jinsi gani marehemu alivyouawa kikatili na jeshi la polisi.

Mwandishi wa pili aliyeshudia amesema kuwa aliona marehemu akipigwa na polisi na baada ya hapo alienda kwa RPC kuomba amsaidie kumnusuru yule marehemu na kumuambia yule anayepigwa ni mwandishi wa habari, RPC hakmjibu ila alifungua kioo cha gari na kukifunga tena.
Siku inakuja watu wa aina hii watakapokuwa gerezani ambako hawatapata kioo cha kufunga wala kufungua. Ole wenu!
 
Mkuu kauli zake huyu mwandishi ndio zinafahamika, huyu ni mwanachama mtiifu wa CDM na hilo linafahamika. Kwa hiyo uandishi ilikuwa just cover tu.

Hivyo unataka kutuambia kuwa walimuua kwa sababu alikuwa mwanachama wa CDM?kwani polisi wanaruhusiwa
kuua wanachama wa CDM?
 
Acheni kutumika kwenye siasa, unaambiwa fanya fujo wakati ane kwambia ufanye fujo anapanda gari na kuondoka, unabaki wewe unakula kisago.

Hii haitawafanya watanzania wasijue ukweli,hata kama itatumika nguvu kiasi gani bado ukweli
unajulikana na utabaki kuwa hivyo.Pia elewa Mungu anasimama upande wa haki.
 
kuna mashahidi wawili ambao ni waandishi wa habari waliokuwa na marehemu MWANGOSI (JANA- KATIKA UVUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA-IRINGA, MUFINDI) wakati anakamatwa na mapolisi shahidi walikuwa wanaelezea tukio zima itv news usiku huu (sa 2 ) wa kwanza anasema
"marehemu alikamatwa na mapolisi 8, wakampiga sana na marungu kwa mda mrefu kila upande wa mwili wake, akatokea polisi wa nyota tatu akawasihi hao polisi 8 wamwachie marehemu lakini haikufaa kitu akatokea polisi mmoja akaja kwa nyuma ya yule aliyekuwa akiwazuia wasiendelee kumpiga marehe akamfyatulia risasi marehemu na kumtawanya utumbo na bomu hilo likamvunja mguu hata huyo polisi aliyekuwa akiwazuia wasimuue.

Shahidi wa pili anasema
Yeye (huyo shahidi-ambaye pia ni mwandishi wa habari)alipoona marehemu anapigwa alikimbilia kutoa taarifa kwa mkuu wa mapolisi waliokuwa katika eneo hilo la tukio huyo mkuu wao alikuwa katika gari akiwa kafunga viooo huyo shuhuda ambaye naye ni mwandishi alipofika hapo akagonga kioo cha gari ili huyo afisa wa polisi afungue, alipofungua huyo mwandishi akamweleza tafadhali naomba msaada wako mkuu yule anayepigwa pale ni mwandishi wa habari, tafadhali naomba msaaada wako huyo afisa hakumsikiliza akarock kiooo.

Ndio maaana nawahuliza hao (Majebere, mwiba na wengineo) wapenda uozo na mauaji ya polisi wameyasikia haya (Ushahidi toka kwa watu wailiokuwa eneo la tukio)? na kuangalia tv... maana wao sijui wanamioyo gani hawa watu ni zaidi ya wanyama kila wakati wao ni kuwatetea polisi hata uweke ushahidi wazi kiasi gani.

Imeniuma sana wakuu SORRY KWA ALIYEKWAZIKA JINSI NILIVYOLIPOTI NI HASIRA JUU YA HAO WATU
ITV wamefanya investigative journalism,wamewaonyesha watanzania nini kinaendelea baina ya watawala na watawaliwa. Mioyo ya watanzania inayo majibu tayari,Mungu ilinde nchi yetu,
 
Back
Top Bottom