ITV yaanika kila kitu na ushahidi wa kutosha kuhusu mauaji ya mwandishi huko Iringa

Hata hivyo waandishi wa habari wametangaza kusususia shughui zote za polisi kuanzia ile NENDA KWA USALAMA.

Nimeipenda hii.....Hizi ndio hatua za kuchukua kwa jeshi dhalili Kama hili tulilonalo la Polisi. It's a shame kwa uongozi mzima WA Polisi, Shame kwa Wizara husika na Serikali kwa ujumla wake. Aibu na kwa dhambi Hizi hakika 2015 Magamba lazima mng'oke tu.......hamvumiliki. Shame on you peoples.
 
kuna mashahidi wawili ambao ni waandishi wa habari waliokuwa na marehemu MWANGOSI (JANA- KATIKA UVUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA-IRINGA, MUFINDI) wakati anakamatwa na mapolisi shahidi walikuwa wanaelezea tukio zima itv news usiku huu (sa 2 ) wa kwanza anasema
"marehemu alikamatwa na mapolisi 8, wakampiga sana na marungu kwa mda mrefu kila upande wa mwili wake, akatokea polisi wa nyota tatu akawasihi hao polisi 8 wamwachie marehemu lakini haikufaa kitu akatokea polisi mmoja akaja kwa nyuma ya yule aliyekuwa akiwazuia wasiendelee kumpiga marehe akamfyatulia risasi marehemu na kumtawanya utumbo na bomu hilo likamvunja mguu hata huyo polisi aliyekuwa akiwazuia wasimuue.

Shahidi wa pili anasema
Yeye (huyo shahidi-ambaye pia ni mwandishi wa habari)alipoona marehemu anapigwa alikimbilia kutoa taarifa kwa mkuu wa mapolisi waliokuwa katika eneo hilo la tukio huyo mkuu wao alikuwa katika gari akiwa kafunga viooo huyo shuhuda ambaye naye ni mwandishi alipofika hapo akagonga kioo cha gari ili huyo afisa wa polisi afungue, alipofungua huyo mwandishi akamweleza tafadhali naomba msaada wako mkuu yule anayepigwa pale ni mwandishi wa habari, tafadhali naomba msaaada wako huyo afisa hakumsikiliza akarock kiooo.

Ndio maaana nawahuliza hao (Majebere, mwiba na wengineo) wapenda uozo na mauaji ya polisi wameyasikia haya (Ushahidi toka kwa watu wailiokuwa eneo la tukio)? na kuangalia tv... maana wao sijui wanamioyo gani hawa watu ni zaidi ya wanyama kila wakati wao ni kuwatetea polisi hata uweke ushahidi wazi kiasi gani.

Imeniuma sana wakuu SORRY KWA ALIYEKWAZIKA JINSI NILIVYOLIPOTI NI HASIRA JUU YA HAO WATU


Kila mwenye uchungu na nchi hii na raia kwa ujumla ameumizwa sana na hiki kitendo, na ikumbukwe kuwa marehemu alikuwa pale kikazi, akijitafutia riziki and not otherwise...you can call them any name, they are animals, i hate to say that i feel like a stranger in my own country... If the Police, who are supposed to make sure that there is peace and harmony within the citizens are the ones who are becoming brutal, then there are more questions than answers, i believe in time. Time is the best healer!!!!!!!!! Only Time will tell!!!
 
Waliua mabwepande wakaachiwa huru, wameua Morogoro na Iringa wanaunda kufanikisha uovu wao pia.
"Nachukia kazi inayowafanya watu wasitende kwa akili bali nguvu na mabavu"..
 
hakizabinadamu na jumuia ya waandish wa habari unganeni kuwashitaki RPC wa Iringa, IGP na Mr. presedent mahakama ya kimataifa The hauge, Direct evedence ipo picha zipo naushaid mwingine mwingi, Plz dont delay, hawa jamaa wasije waka zima hii issue kama ya DR. ulimboka.
 
Kuna waandishi wengine nimeona kama wameonyesha RPC hakuwepo pale alikuwa kwenye gari, na picha zinaonyesha alikuwa amekumbatiwa na marehemu...sasa unajua baadi ya waandishi tena waliowengi ni walarushwa na mara nyingi huwa wanatumiwa na selikali, unaweza kuona hata kwenye hii habari hadi mwisho itatetewa sana na waandishi ili kuwasafisha polisi hasa RPC aliyekuwa anatoa command pale kwenye tukio... Mapandikizi mmejaa kwenye hiyo taaluma yenu, wala rushwa kama kina muro mmejaa vilevile...mfano mdogo tu huo...sasa mwandishi mwenzenu ameuawa lakini wenyewe mtashuhudia kabisa baadhi ye waandishi wenzenu wakiwa kinyume na marehemu wakitetea serikali na polisi ili at the end of the day wasafishike.....si ajabu ukasikia bom hilo lilirushwa na chadema hapo...wakati tumeona kila kitu, nimesikia RPC huyo alisema bom lilirushwa na waandamanaji na sio kwamba lilitoka kwa polisi.. Pamoja na kusema kuwa bom hilo lilikuwa ni lile la kutoa machozi, bado tu wanajichanganya kuwa bom lilitoka kwa wananch....nafikiri mabom ya machozi siku hizi wananchi wanaenda kuyachukua kule kwenye boma la silaha la field force unit kule kihesa iringa...hahaha.ajabu kweli... Polisi kama mlikuwa mnaongea uongo mara nyingi..kwa hili itabidi watu waajibike au waadibishwe haraka kwasababu wananchi wamejua ukweli kabla ninyi hamjaunda uongo mlioutangaza.
Hata kama polisi aliona ni Chadema waliorusha bomu na kumwua mwandishi wa habari wa Channel Ten kwa kutumia taarifa za kiintelejinsia si wanajua ni nani aliyetupa na alikuwa ameficha wapi hilo bomu? Otherwise, atawezaje kusema kuwa ni Chadema kama hakuona aliyetupa na alipokuwa amelihifadhi? Hii ngoma nzito! Ngoja tusibiri tuone.
 
yaani hawa jamaa ninawatamini ile mbaya hata mitaani ni afadhari tuanze kuwapa kichapo moja baada ya mwingine
 
ITV imetoa habari iliyokamilika kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari, waandishi wa habari walioshuhudia tukio hilo wameeleza bayana tukio hilo kwa kubainisha chazo cha mauaji hayo, na huku wakitoa ushahidi kuhusu jinsi gani marehemu alivyouawa kikatili na jeshi la polisi.

Mwandishi wa kwanza aliyeshuhudia amesema aliona marehemu akipigwa na askari kama nane, na baada ya hapo alioneakana askari mwenye nyota tatu akamkumbatia mwandishi wa habari ili kumnusuru lakini askari Mwingine alimrushia bomu tumboni na kusambatisha tumbo la mwandishi.

Mwandishi wa pili aliyeshudia amesema kuwa aliona marehemu akipigwa na polisi na baada ya hapo alienda kwa RPC kuomba amsaidie kumnusuru yule marehemu na kumuambia yule anayepigwa ni mwandishi wa habari, RPC hakmjibu ila alifungua kioo cha gari na kukifunga tena.

Hata hivyo moja wa ndugu wa marehemu amesema kuwa ni vizuri kila chama kikawa huru kujieleza kwa Wananchi ili Wanainchi wapate fursa ya kuchagua chama wanachokitaka.

Hata hivyo waandishi wa habari wametangaza kusususia shughui zote za polisi kuanzia ile NENDA KWA USALAMA.

Hivi kulikuwa na tukio gani maalum la kiserikali ktk ufunguzi wa tawi hilo la CHADEMA lililopelekea jeshi lote la polisi mkoa wa Iringa akiwemo RPC kuwepo eneo la tukio?
 
Back
Top Bottom