ITV/RADIO One na Viporo vya Habari

Mpaka sasa ITV ndio inaongoza kwa viewership kwenye local channel ikifiatiwa na TBC. ITV inaongoza kwa viewership sio kwa sababu ndio inapendwa sana, bali kwa sababu ya mazoweya. ITV inaitumia supremacy hii kutoza ngarama kubwa kwa vipindi na matangazo yake huku wakifanya kazi kwa mazoea kwa kujiaminisha wakwanza ni wakwanza tuu. Wanapaswa kuwaangalia TVZ ambao ndio wakwanza kweli, hivi sasa wako wapi.

Ukweli ni kuwa kuendesha TV Station profitably hapa nchini ni ngumu ndio maana vituo vina unganisha nguvu ili kushare cost. Ukiritimba wa vituo vya TV unamalizika rasmi 2014 wakati nchi imehama toka analogy ya sasa kwenda digital, hivyo kazi za Vituo itakuwa ni kuprovide contents tuu hali itakayopelekea hata JF kuzindua channel yake, makanisa na channel zao hata vi production houses vidogo kama PPR vitarusha matangazo yao hali itakayoilazimisha ITV kuingana na Star na kupunguza ngarama za matangazo yake or face extinction.

Kituo pekee ambacho ndio most promising ku survive bila jasho ni TBC tuu, kwa kuwa kiko spoon fed na hazina at the same time upendeleo kwa matangazo ya serikali.

Nawaombeni sana tusiwalaumu watangazaji, ni watu wa kuhurumiwa tuu kwa sababu hawapati malipo kulingana na jasho lao. They are simply over exploited, underpaid, overworked na demoralized with no any sort of incentives, unategemea nini kwa watu wa aina hii!.
 
Mimi ni SAMU MAHELA WA ITV!

Mkuu wata ku fire si unaona walichofanyiwa akina Misanya Bingi, Julius Nyaisanga, Nevile Meena na wengi kibao. Wao wanajua wakifukuza leo kesho wana application 100 kwani vijana wengi masharobaro na wale ambao hawapendi shida ya kutesa vichwa vyao kusoma vitu vigumu wamekimbilia uandishi wa habari. Badala ya kuheshimika wamekuwa readly available CHEAP LABOUR.

Kumbuka pia Zembwela ni mtangazaji!!!!!!!???????????
 
Kwa kweli wana bore sana,kwenye michezo ndo usiseme.Na ikitokea mmiliki ametembelea ka shule ka chekechea sehemu,ndo 20 min zitaishia hapo
 
hivi itv pamoja na makampuni yote ya media,tbc,star tv hawawezi kuonyesha movie on weekends??wanafikiri sisi tunataka kuona siasa zao mondya to sunday??/badilikeni wakuu
 
Mkuu wata ku fire si unaona walichofanyiwa akina Misanya Bingi, Julius Nyaisanga, Nevile Meena na wengi kibao. Wao wanajua wakifukuza leo kesho wana application 100 kwani vijana wengi masharobaro na wale ambao hawapendi shida ya kutesa vichwa vyao kusoma vitu vigumu wamekimbilia uandishi wa habari. Badala ya kuheshimika wamekuwa readly available CHEAP LABOUR.

Kumbuka pia Zembwela ni mtangazaji!!!!!!!???????????

mkuu una uhakika walipigwa fired au unatania?
 
kuna mtu mmoja anaitwa ndamalya,yule hawezi kuhama itv utafikiri ni ya baba yake
 
hivi itv pamoja na makampuni yote ya media,tbc,star tv hawawezi kuonyesha movie on weekends??wanafikiri sisi tunataka kuona siasa zao mondya to sunday??/badilikeni wakuu

ITV zamani siku za siku kuu walikuwa wanoyesha movies nzuri sana ila siku hizi sijui nani amewaloga wanaweka mambo ya ajabu na imetubidi wengi wetu tujiunge na cables ili tupate movies. Ila nilichogundua ITV inataka kutumia gharama kiduchu kupata mihela mingi na huu ubahili ndo una i cost.
 
mkuu una uhakika walipigwa fired au unatania?

Nina uhakika Misanya Bingi alifukuzwa, J Nyaisanga, Meena na wengine wengi ila majority wa watangazaji nguli waliondoka kutokana na mshiko mdogo. Rafiki yangu aliyewahi fanya kazi ITV/Radio one aliwahi niambia jinsi mshiko wa waandishi ulivyo finyu na mtu kuamu a kufanya tu kwa sababu hana namna.
 
Radio one na ITV zina maisha mafupi sana,kwa ubunifu huu mbuzi tutawasahau digital ikianza!
 
Back
Top Bottom