ITV ingieni kwenye king'amuzi cha Dstv!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
ITV ni kituo kikongwe na kikubwa hapa nchini ambacho hutegemewa na watazamaji wengi kwa habari na burudani. Mimi ni mmoja wa watu wanaokiamini sana kituo hicho hasa kwa taarifa za habari kwakuwa huwa wanajitahidi kuwa neautral na kufanya coverage kubwa. Ushauri wangu kwao ni kuwa wafanye kila jitihada kuhakikisha kuwa wanaingiza channel yao katika king'amuzi cha Dstv ili kujitanua zaidi kwani king'amuzi hicho ni cha kimataifa. Sidhani kama ITV wanaweza kushindwa na TBC, Channel 10 na Star tv ambavyo vinapatikana katika Dstv. Uongozi harakisheni hilo.
 
dstv ndo wafanye mpango wa kuweka itv lkn sio itv wajipeleke dstv. lazima uangalie maslahi
 
dstv ndo wafanye mpango wa kuweka itv lkn sio itv wajipeleke dstv. lazima uangalie maslahi
Sijui kama ni wenye king'amuzi ndio wanaotafuta channel za kuzisajili au ni wenye channel ndio wanaotafuta ving'amuzi vya kujisajili. Lakini nafikiri wenye channel ndio wanaopaswa kuwa wa kwanza kutafuta ving'amuzi vitakavyorusha matangazo yao kulingana na soko. Soko la ITV naamini ni kubwa sana hivyo wakiingia Dstv watakuwa wanapanua uwigo wa matangazo yao na kukua kibiashara kimataifa. Mimi naona ITV wanavutavuta miguu na hivyo kupigwa bao na vituo vilivyokuja nyuma yao. Hata matangazo ya BBC kwa kiswahili ungetegemea ITV ndio wangekuwa wanarusha lakini yanarushwa na Star tv ambao wako Dstv. Usharp nao unasaidia katika biashara
 
Back
Top Bottom