Iringa kwachafuka: FFU watumia mabomu, waandishi wapigwa mawe

Ukimkubali Yesu Kristo Unakuwa Huru na huwezi tena kuhofia majini, wachawi wala misule, ikija Damu Ya Yesu itakufunika Nawe Utakuwa Salama. ACCEPT JESUS AND YOU'LL BE FREE.
 
Hapo anavuna alichokipanda hayo ndio matokeo ya kumtumikia shetani hata umnyenyekee vipi kuna siku ata kuacha uchi tu.
 
Serikali inaposhindwa kudhibiti ghasia na watu wanapozidi kujichukulia hatua ni dalili ya kuwa inacolapse
 
MONDAY, NOVEMBER 14, 2011


Askari wa kikosi cha askari wa kutuliza Ghasia (FFU) Iringa watumia mabumu kuwatawanya wananchi waliovamia nyumba ya mtumishi wa Mungu kwa madai kuwa kuna misukule.

Wananchi hao wenye hasira kali zaidi ya 200 walitumia mawe kuwashambulia FFU huku wao FFU wakitumia mabomu ya machozi kupambana Huku wanahabari wa vyombo mbali mbali na askari polisi na mchungaji mmoja wakinusurika kuuwawa wakishambuliwa kwa mawe na wengine kuvunjiwa kamera zao na wananchi hao ambao walionyesha kuwachukia askari polisi pamoja na wanahabari ambao waliteuliwa na wananchi wenyewe kuwawakilisha katika kukagua nyumba hiyo bila mafanikio .

Tukio hilo lilitokea eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa na kudumu zaidi ya masaa manne baada ya kuanza majira ya saa 8 mchana na kuendelea hadi saa 12.50 jioni .


Wakielezea juu ya tukio hilo wananchi hao walisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa mmoja kati ya wananchi wa eneo hilo kuwa katika nyumba hiyo ya mfanyabiashara wa maji kumeonekana misukule 15 ambayo ilionekana ndani ya uzio wa nyumba hiyo.


Kutokana na uvumi huo wananchi kutoka pande mbali mbali za mji wa Iringa walifika katika nyumba hiyo na kuizingira kwa lengo la kutaka kuichoma moto kabla ya askari polisi kufika na kuwaomba wananchi kutofanya hivyo na badala yake kuteuwa wawakilishi ili kuingia ndani ya nyumba hiyo kujikagua misukule hiyo bila mafanikio .


Hata hivyo baada ya askari hao walioambatana na wanahabari zaidi ya sita kutoka vyombo mbali mbali akiwemo mwandishi wa habari hizi kushindwa kuona misukule hao baadhi ya wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi waliamua kuruka ukuta baada ya kuona wananchi wakionyesha jazba zaidi.


Huku baadhi ya waandishi wakiongozwa na katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard ambaye ni mwandishi wa gazeti la Habari leo wakilazimika kujifungia ndani ya nyumba hiyo baada ya wananchi kuanza kuishambulia kwa mawe.


Hali hiyo iliwalazimu askari polisi zaidi ya 10 walikuwepo kuanza kutumia mabumu ya machozi kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiimba kuwa mmekela rushwa wote wanahabari,wachungaji na polisi hivyo lazima mchomwe moto.


Katika tukio hilo mabomu ya machozi zaidi ya 30 yalipigwa hewani huku wananchi wakizidi kuongezeka na kupelekea askari hao kuomba msaada zaidi wa askari wa FFU ambao walifika wakiongozwa na mkuu wa FFU mkoa wa Iringa Mnunka na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao.


Zaidi ya watu 10 walikamatwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na vurugu hizo huku watu wengine zaidi ya 20 wakiwemo wanahabari familia ya mfanyabiashara huyo ,mchungaji aliyefahamika kwa jina la Mang'uliso walijeruhiwa kwa mawe.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla hakuweza kupatikana kuzungumzia madhara yaliyojitokeza katika tukio hilo japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari matatu likiwemo la polisi yakiwa yameharibiwa vibaya kwa mawe.



4712530841850548562-4433966476443058166
Habari kwa Hisani ya Francis Godwin







Wananchi wakiishambulia nyumba inayotuhumiwa kuwa na misukule kwa mawe





Mwandishi wa ITV Iringa Laulian Mkumbata akionyesha kamera iliyovunjwa

DSCF1625.JPG


Wananchi wakiwa wameizunguka nyumba inayodaiwa kuwa na misukule ndani ,huku ndani ya nyumba hiyo kukiwa na wanahabari pia
Na Francis Godwin
 
Haya Sasa Iringa.... na FFU wako na kawaida yao Mabomu ya Machozi

Ni lini walianza kurushia Mabomu wananchi? Wakati wa Mwalimu hakukuwa na Mabomu ya kurushia wananchi?

** Rais wetu anataka nini na kukaa kimya?

Maeneo yote yaliyopelekewa FFU ni Mikoa ambayo ina Makabila Makubwa Nchini.... Mwanza, Arusha, Mbeya na Sasa Iringa

** CCM imeshindwa kuongoza??

Au KIKWETE APENDA AKIMBILIE NJE YA NCHI??
 
Hiyo ndiyo Tanzania yangu ninayokupenda kwa Moyo na hata ikibidi nikufie...ILOPOFIKIA!! Utu na Ubinadamu wako Utarejea vipi ... ONA .. aibu ya Ushirikina inavyo kudidimiza ...How low is the Low you can get!!
 
Watu wa Iringa nao hawana mpango, watanzania wanadai katiba nyie mnadai misukule?.
 
Haya Sasa Iringa.... na FFU wako na kawaida yao Mabomu ya Machozi

Ni lini walianza kurushia Mabomu wananchi? Wakati wa Mwalimu hakukuwa na Mabomu ya kurushia wananchi?

** Rais wetu anataka nini na kukaa kimya?

Maeneo yote yaliyopelekewa FFU ni Mikoa ambayo ina Makabila Makubwa Nchini.... Mwanza, Arusha, Mbeya na Sasa Iringa

** CCM imeshindwa kuongoza??

Au KIKWETE APENDA AKIMBILIE NJE YA NCHI??
kumbe iringa pia kuna makabila makubwa eh?? sikujua kabisa nilidhani wahehe ni kabila dogo kulinganisha na wahaya

haya
 
kumbe iringa pia kuna makabila makubwa eh?? sikujua kabisa nilidhani wahehe ni kabila dogo kulinganisha na wahaya

haya

Wewe unamatatizo -- regional wise Iringa ni kubwa na Wahehe ni kabila kubwa
 
Watanzania ndugu zetu wanatia huruma sana...Wwengi hawana elimu wala kazi,na maisha ni kiimani imani tu.Na hapo viongozi wanapapenda sana kwasababu wanakula na vipofu tu...Inasikitisha sana tu!

Naifahamu nchi yangu ndiyo maana nasema hivyo
 
Inaonekana wenzetu wa nchi ya Iringa mambo yao safi. Usawa huu wa kushabikia misukule! Mambo yote katiba mpya bwana.
 
Wangemtia kiberiti tuu atangulie mbele za haki huwezi weka wenzio kama misukule!
Huyu maana mambo ya giza ameanza kitambo sana na ndiko utajili wake unakotokea uko!

kama wewe huna dhambi na uwe wa kwanza kuchukua mafuta na kumtia kiberiti,usihukumu usije ukahukumiwa
 
DSCF1673.JPG
DSCF1667.JPG
DSCF1666.JPG
DSCF1681.JPG
DSCF1643.JPG
DSCF1652.JPG


VURUGU ZA WANANCHI IRINGA, ASKARI NA WAANDISHI WAJERUHIWA VIBAYA


Zaidi ya watu 10 wakiwemo askari wanne na wanahabari wamejeruhiwa huku baadhi yao wakitibiwa na kuruhusiwa na wengine kulazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kuibuka kwa mapigano hayo kati ya polisi na wananchi ,mapigano ambayo yametokana na imani potofu za wananchi katika kuamini ushirikina. Wananchi hao zaidi ya 200 walivamia nyumba ya mzee wa kanisa moja la kilokole katika mji wa Iringa eneo la Frelimo jina limehifadhiwa kwa sababu za kimaadili .

Hata hivyo pona ya wanahabari na polisi waliokuwa wamefungiwa ndani ya nyumba hiyo na kushambuliwa kwa mawe na kunusurika kuteketezwa kwa moto wakiwa ndani ya nyumba hiyo ilionekana baada ya askari polisi wa FFU kutumia mbinu kubwa ya kulazimika kutumia risasi ya moto kumshambulia mguuni mmoja kati ya watu wanaodaiwa kutaka kuongoza wengine kuichoma moto nyumba hiyo iliyokuwa na wahahabari ndani ,polisi na mchungaji mmoja . Baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa kuokoa maisha ya wanahabari hao na watu wengine zaidi ya 10 ambao walipaswa kuuwawa na wananchi hao .

Wananchi hao walionekana kuongezeka idadi baada ya FFU kuwatisha kwa mabomu ya machozi huku wakidai kuwa mabomu hayo hayaui na bila polisi kupata mbinu ya haraka ya kutumia risasi ya moto zaidi ya watu hao 10 wakiwemo wanahabari waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wangekuwa wameuwawa na wananchi hao ambao waliondoa imani na kikosi hicho kuwa wamehusika kuificha misukule hiyo.
 
mbombo ngafu! huyo mama aliwahi kuwa na kashfa ya kufanya 'matanga' baada ya lori lake lenye mzigo wa maji africa kupata ajali. inasemekana alidai kama alifanya sherehe aliponunua,why not sherehe lilipopata ajali,maake ni kama mtoto wake. ni mama maarufu mkoani iringa.
 
Haya Sasa Iringa.... na FFU wako na kawaida yao Mabomu ya Machozi

Ni lini walianza kurushia Mabomu wananchi? Wakati wa Mwalimu hakukuwa na Mabomu ya kurushia wananchi?

** Rais wetu anataka nini na kukaa kimya?

Maeneo yote yaliyopelekewa FFU ni Mikoa ambayo ina Makabila Makubwa Nchini.... Mwanza, Arusha, Mbeya na Sasa Iringa

** CCM imeshindwa kuongoza??

Au KIKWETE APENDA AKIMBILIE NJE YA NCHI??
wewe vp?.CCM na misikule wapi na wapi,kwani huyo mama ni CCM? ulitaka FFU wafanye nini?.sheria lazima ifatwe.huwezi kuunguza nyumba na kuua mtu bila ushahidi.na wapongeza FFU na viongozi walio husika.
 
Back
Top Bottom